2010–2019
Kwa nini Kanisa
Oktoba 2015


Kwa nini Kanisa

Inastahili kutulia ili kufikiria kwa nini Yesu Kristo anachagua kutumia kanisa, Kanisa Lake, kufanikisha kazi Yake na ya Baba Yake.

Katika maisha yangu yote, mikutano mikuu ya Kanisa imekuwa na matukio ya kiroho ya kufurahisha sana, na Kanisa lenyewe limekuwa sehemu ya kuja kumjua Bwana. Ninaelewa kwamba kuna baadhi ya watu ambao wanajifikiria ni washika dini au watu wa kiroho na bado wamekataa kushiriki kwenye Kanisa au hata taasisi kama hiyo. Desturi ya kidini kwao ni ya binafsi hasa. Bado Kanisa ni uumbaji wa Yule ambaye kiini cha mambo yetu ya Kiroho—Yesu Kristo. Inastahili kutulia ili kufikiria kwa nini anachagua kanisa, Kanisa Lake, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kufanikisha kazi Yake na ya Baba Yake “Kuleta kutokufa na uzima wa milele.”1

Kuanzia na Adamu, injili ya Yesu Kristo ilihubiriwa, na ibada muhimu za wokovu, kama vile ubatizo, ziliendeshwa kupitia utaratibu wa ukuhani wa kifamilia.2 Wakati jamii zilipokuwa zilikua na kuwa changamano badala ya jamaa, Mungu pia aliwaita wengine manabii, wajumbe, na waalimu. Wakati wa Musa tunasoma kuhusu muundo wa utaratibu rasmi ukijumuisha wazee, makuhani, na waamuzi. Katika historia ya Kitabu cha Mormoni, Alma alianzisha kanisa likiwa na makuhani na walimu.

Kisha, katika wakati wa meridiani, Yesu alipanga kazi Yake katika njia ambayo injili ingeweza kuanzishwa kwa wakati mmoja katika mataifa mengi na miongoni mwa watu mbali mbali. Hii taasisis, Kanisa la Yesu Kristo, lilianzishwa juu ya “mitume na manabii, Yesu Kristo mwenyewe akiwa jiwe kuu la pembeni.”3 Lilijumuisha maofisa wa ziada kama sabini, wazee, maaskofu, makuhani, waalimu, na mashemasi. Yesu vilevile alianzisha Kanisa katika Nusu tufe ya Magharibi baada ya Ufufuko Wake.

Kufuatia ukengeufu na uchakachuaji wa Kanisa ambalo Yeye alikuwa ameanzisha alipokuwa ulimwenguni, Bwana alianzisha tena Kanisa la Yesu Kristo kupitia Nabii Joseph Smith. Azma ya zamani inabaki kuhubiri habari njema za injili ya Yesu Kristo na kusimamia ibada za wokovu---kwa maneno mengine, kuwaleta watu kwa Kristo.4 Na sasa kupitia muundo wa hili Kanisa la urejesho, ahadi ya wokovu imewezekana hata kwa roho za wafu ambao katika maisha yao hapa duniani walijua kidogo au hawakujua chochote kuhusu neema ya Mwokozi.

Ni kwa jinsi gani Kanisa Lake linaweza kutimiza azma za Bwana? Ni muhimu kutambua kwamba hatima ya azma ya Mungu ni maendeleo yetu. Nia Yake ni kwamba tuendelea “kutoka neema hadi neema, mpaka [sisi tupokee] utimilifu”5 wa yale yote anayoweza kutoa. Hiyo inahitaji zaidi kuliko kuwa wema au kujihisi kiroho. Hii inahitaji imani katika Yesu Kristo, toba, kuzaliwa kwa maji na kwa Roho, na kuvumilia hadi mwisho kwa imani.6 Mtu hawezi kupata haya kikamilifu peke yake, hiyo ndiyo sababu kubwa ya Bwana kuwa na kanisa ili kujenga jumuia ya Watakatifu ambayo itasaidiana katika “njia hii nyembamba iliyosonga ambayo inaelekea uzima wa milele.”7

“Naye [Kristo] alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na walimu;

“… hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe:

“Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.”8

Yesu Kristo ni “mwanzilishi na mtimizaji wa imani [yetu].”9 Kutuunganisha sisi wenyewe kwenye mwili wa Kristo---Kanisa---ni sehemu muhimu ya kujichukulia jina lake juu yetu.10 Tunaambiwa kuwa Kanisa la kale “lilikutana pamoja mara kwa mara, kufunga na kuomba, na kuzungumza mmoja na mwingine kuhusu ustawi wa roho zao,”11 “na kusikia neno la Bwana.”12 Hii ni kweli katika Kanisa leo. Kuunganishwa katika imani, tunafundisha na kuadilishana na kujitahidi kufikia kipimo kamili cha ufuasi, “cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.” Tunajitahidi kusaidiana mmoja na mwingine ”kupata elimu ya Mwana wa Mungu,”13 mpaka ile siku ambayo “hawatamfundisha kila mtu jirani yake, ... wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana.”14

Katika Kanisa hatujifunzi tuu mafundisho matakatifu; tunapata uzoefu wa matumizi yake. Kama mwili wa Kristo, waumini wa Kanisa wanahudumiana wao kwa wao katika uhalisi wa maisha ya kila siku. Sisi sote hatujakamilika; tunaweza kukosa na tunakosewa. Tunafanyiana majaribu mmoja na mwingine kwa ubinafsi wetu mara kwa mara. Katika mwili wa Kristo, hatuna budi kutenda zaidi ya mawazo na maneno ya kuinua na kuwa na uzoefu wetu binafsi tunapojifunza kuishi “pamoja kwa upendo.”15

Dini hii haihusiki tu na nafsi; bali wote tumeitwa kuhudumia. Sisi ni macho, mikono, kichwa, miguu, na sehemu zingine za mwili wa Kristo, na hata “viungo vile … vidhaniwavyo vinyonge, ni muhimu.”16 Tunahitaji hii miito, na tunahitaji kuhudumu.

Mmoja wa wanaume katika kata yangu alikua akiwa sio tu bila msaada wa wazazi lakini pamoja na pingamizi za wazazi kwenye shughuli zake katika Kanisa. Alisema hivi katika mkutano wa sakramenti: “Baba yangu hawezi kuelewa kwa nini mtu yeyote angeweza kwenda kanisani wakati wangekwenda kuteleza kwenye theluji, lakini kwa kweli napenda kwenda kanisani. Katika Kanisa, sisi wote tupo kwenye safari moja, na napata maongozi hiyo safari na vijana wenye nguvu, watoto halisi, na kile ninachokiona na kujifunza kutoka watu wazima wengine. Nimeimarishwa na ushirikiano, na kupendezwa na furaha ya kuishi injili.”

Katika wakati huu, kata na matawi ya Kanisa yana mkusanyiko wa kila wiki ya kupumua na kufanywa upya, muda na mahali pa kuacha ulimwengu kando—Sabato. Ni siku ya “kufurahi binafsi katika Bwana,”17 kupata uzoefu wa uponyaji wa kiroho ambao unaoletwa na sakramenti, na kupokea ahadi iliyofanya upya ya Roho Wake kuwa pamoja nasi.18

Moja ya baraka kuu ya kuwa sehemu ya mwili wa Kristo, ingawa inaweza isionekane kama baraka kwa wakati huu, ni kuonywa kwa ajili ya dhambi na makosa. Sisi ni wepesi kutoa sababu na kutazama makosa yetu kimaantiki, na wakati mwingine kirahisi hatujui wapi tunabidi kufanya vizuri au jinsi ya kufanya. Bila wale ambao wanaweza kutuonya “kwa ukali kwa wakati wake, watakapokuwa wameongozwa na Roho Mtakatifu,”19 tunaweza kukosa ujasiri wa kubadilika na kwa ukamilifu zaidi kumfuata Bwana. Toba ni ya binafsi, lakini ushirika katika njia ile ambayo wakati mwingine ni ya maumivu ni katika Kanisa.20

Katika mazungumzo haya ya Kanisa kama mwili wa Kristo, sharti siku zote tukumbuke vitu viwili. Kimoja, hatupambani dhidi ya kuongolewa katika Kanisa bali katika Kristo na injili Yake, uongofu ambao unatekelezwa na Kanisa.21 Kitabu cha Mormoni kinaelezea vizuri sana wakati kinaposema kwamba watu walimgeukia Bwana, na waliunganishwa katika Kanisa la Kristo.22 Pili, sisi sharti tukumbuke kwamba hapo mwanzoni, Kanisa lilikuwa familia, na hata leo kama vitengo tofauti, familia na Kanisa vinahudumiana na kuimarishana. Wala hakuna kinachoondoa kingine, na hasa Kanisa, hata likiwa nzuri vipi, haziwezi kuchukua nafasi ya wazazi. Jambo muhimu la kufundisha injili na ibada za ukuhani zitolewazo na Kanisa ni kwamba familia ziweze kuhitimu kwa uzima wa milele.

Kuna sababu kubwa ya pili Mwokozi hufanya kazi kupitia kanisa, Kanisa Lake, ni kufanikisha mahitaji yanayohitajika ambayo hayawezi kufanikishwa na watu binafsi au makundi madogo. Mfano mmoja wa wazi ni kushughulikia umaskini. Ni kweli kwamba kama watu binafsi na familia tunakidhi mahitaji ya kimwili ya wengine, “tukitoa kwa kila mmoja wetu kimwili na kiroho kufuatana na mahitaji yao na matakwa yao.”23 Lakini kwa pamoja katika Kanisa, uwezo wa kuwatunza maskini na wenye shida umeongezeka kukidhi haja aina aina, kujitegemea kunatumainiwa kuwa halisi kwa wengi.24 Zaidi ya hivyo, Kanisa, Miungano ya Usaidizi wa Kina Mama, na akidi zake za ukuhani wana uwezo wa kutoa ahueni kwa watu wengi katika sehemu nyingi zilizopatwa na maafa ya asili, vita, na mateso.

Bila uwezo wa Kanisa Lake kuwepo, agizo la Mwokozi la kuipeleka injili kote ulimwenguni haliwezi kutmizika.25 Hakungekuwa na funguo za kitume, utaratibu, nyenzo za tekinolojia, uwezo wa kifedha, na kujitolea na dhabihu ya mamia ya maefu ya wamisionari wanahitajika kufanya kazi. Kumbuka, “Injili hii ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote, kwa ajili ya ushahidi kwa mataifa yote, na ndipo mwisho utakuja, au maangamizo ya waovu.”26

Kanisa linaweza kujenga na kuendesha mahekalu, nyumba za Bwana, ibada na maagano yanaweza kufanywa. Joseph Smith alitamka kwamba kusudi la Mungu katika kuwakusanya watu Wake katika kipindi hiki ni “kumjengea Bwana nyumba ambapo Yeye [anaweza] kufunua kwa watu Wake ibada za nyumba Yake na utukufu wa ufalme Wake, kuwafundisha watu njia ya wokovu; kwani kuna ibada na kanuni fulani ambazo, zinapofunzwa na kutumiwa, sharti kuwe na mahali ama nyumba iliyojengwa kwa kusudi hilo.”27

Kama mtu anaamini kwamba barabara zote zinaelekea mbinguni au kwamba hakuna mahitaji mahususi ya wokovu, ataona hakuna haja ya kutangaza injili au ibada na maagano ya kukomboa wala walio hai au wafu. Lakini hatuzungumzi tu kuhusu kutokufa bali pia juu ya maisha ya milele, na kwamba njia ya injili na maagano ya injili ni muhimu. Na Mwokozi anahitaji kanisa kuyafanya yapatikane kwa watoto wote wa Mungu—wote walio hai na wafu.

Sababu ya mwisho nitakayoitaja ya Bwana kuanzisha Kanisa Lake ni ya kipekee sana—Kanisa ni, hata hivyo, ufalme wa Mungu duniani.

Wakati Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lilipokuwa linaanzishwa katika miaka ya 1830, Bwana alimwambia Nabii Joseph Smith, “Inueni mioyo yenu na mfurahi, kwani kwenu ufalme, au kwa maneno mengine, funguo za kanisa zimetolewa.”28 Katika mamlaka ya funguo hizi, maofisa wa ukuhani wa Kanisa wanalinda usafi wa mafundisho ya Mwokozi na uadilifu wa ibada Zake za kuokoa.29 Wanasaidia kuwatayarisha wale wanaotaka kupokea, kuamua sifa na ustahiki wa wale wanaoomba, na kisha kuyafanya.

Kwa funguo za ufalme, watumishi wa Bwana wanaweza kutambua vyote ukweli na uongo, na mara nyingine kimamlaka asema, “Bwana asema hivi.” Kwa kujutia, baadhi huchukia Kanisa kwa sababu wanataka kufafanua ukweli wao wenyewe, lakini kihalisi ni baraka kubwa zaidi kupokea “maarifa ya mambo kama yalivyo [hasa], na kama yalivyokuwa, na kama yatavyokuwa”30 kwa kiasi ambacho Bwana yu tayari kufunua. Kanisa linalinda na kuchapisha mafunuo—kanuni za maandiko.

Wakati Danieli alipotafsiri ndoto ya Mfalme Mbabeli Nebukadreza, akifanya ijulikane kwa mfalme “mambo yatakayokuwa siku za mwisho,”31 alitangaza kwamba “Mungu wa Mbinguni [angeweka] ufalme, ambao kamwe hautaharibiwa: na ufalme huo hautaachwa kwa watu wengine, bali utavunjika katika vipande vipande na kuteketeza falme zote [zingine], na utasimama milele.”32 Kanisa ni ufalme ule ambao ulitabiriwa katika siku za mwisho usio umbwa na binadamu, bali uliowekwa na Mungu wa Mbinguni na unasonga mbele kama jiwe lililochongwa kutoka mlimani bila mikono kujaza dunia.33

Majaliwa yake ni kuanzisha Sayuni katika matayarisho ya kurudi na utawala wa milenia wa Yesu Kristo. Kabla ya siku ile, hautakuwa ufalme kwa maana ya kisiasa---kama Mwokozi alivyosema, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu34 Bali, ni mwanzo wa mamlaka Yake katika dunia, Mtawala wa maagano Yake matakatifu, mlinzi wa mahekalu Yake, mhifadhi na mtangazaji wa ukweli Wake, sehemu ya kukutania kwa Waisraeli waliotawanyika, na “ulinzi, na … kimbilio kutoka kwa dhoruba, na kutoka kwa ghadhabu wakati itakapo mwagwa bila mchanganyiko juu ya dunia yote.”35

Namalizia na ombi la Nabii na sala:

“Mwite Bwana, ili ufalme wake uweze kusonga mbele juu ya dunia, ili wakazi wake waweze kuupokea, na wawe wamejitayarisha kwa siku zijazo, kwa kuwa Mwana wa Mtu atakuja chini kutoka mbinguni, amevikwa mg’aro wa utukufu wake, kukutana na ufalme wa Mungu ambao umewekwa juu ya dunia.

“Kwa hiyo, na ufalme wa Mungu uenee, ili ufalme wa mbinguni uweze kuja, ili wewe, Ee Mungu uweze kutukuzwa mbinguni hata na duniani, ili adui zako waweze kushindwa; kwa kuwa ukuu ni wako, uweza na utukufu, milele na milele.”36

Katika jina la Yesu Kristo, amina.