2010–2019
Kuridhia Mioyo yetu kwa Mungu
Oktoba 2015


Kuridhia Mioyo yetu kwa Mungu

Tunapojiridhia  wenyewe kwa Roho, tunajifunza njia ya Mungu na kuhisi mapenzi Yake.

Mzee Dallin H. Oaks, katika mkutano mkuu wa Aprili, alizungumza juu ya haja “ya kerekebisha maisha yetu binafsi.”1 Ninapendekeza kwamba marekebisho binafsi yanaanza na mabadiliko ya moyo—bila kujali uzoefu wa maisha yako au sehemu uliyozaliwa.

Ninatokea Kusini kabisa ya Marekani, na katika ujana wangu maneno ya nyimbo za kale za kiprotestanti zilinifunza mimi moyo wa kweli wa mfuasi—ule ambao umebadilishwa. Fikiria maneno ya wimbo, ambayo nayapenda sana:

Ni Njia Yako,Bwana!

Ni Njia Yako!

Wewe ni Mfinyanzi:

Mimi ni udongo

Nifinyange na nifanye mimi

Kufuatia mapenzi yako

Niko

radhi na tuli nikingojea.2

Tunawezaje, sisi watu wa kisasa, wenye shughuli nyingi, wenye ushindani, kuwa wa kuridhia na tuli? Tutafanyaje njia za Bwana kuwa njia zetu? Ninaamini kwamba tunaanza tunafanya hivyo kwa kujifunza kumhusu Yeye na kusali kwa uelewa. Wakati imani yetu katika Yeye inakuwa, tunafungua mioyo yetu, kutafuta kufanya mapenzi yake, na kungoja majibu ambayo yatatusaidia kuelewa.

Mabadiliko yangu ya kibinafsi ya moyo yalianza wakati nilipokuwa na umri wa miaka 12, nilianza kumtafuta Mungu. Mbali na kuomba sala ya Bwana,3 sikujua kwa kweli jinsi ya kuomba. Nakumbuka nikipiga magoti, nikitumaini kuhisi upendo Wake, na kuuliza, “Uko wapi Baba wa Mbinguni? Najua ni lazima uko nje sehemu fulani, lakini wapi?” Miaka yote ya ujana wangu, niliuliza. Niliweza kuwa na muda mfupi wa uzoefu wa uhalisi wa Yesu Kristo, lakini Baba wa Mbinguni aliniacha nitafute na kungoja kwa miaka 10.

Mnamo mwaka wa 1970, wakati wamisionari waliponifundisha kuhusu mpango wa Baba wa wokovu na Upatanisho wa Mwokozi, kungoja kwangu kukaisha. Nilipokea kwa moyo kweli hizi na nilibatizwa.

Kwa msingi wa uelewa huu wa huruma ya Bwana na uwezo, mume wangu, watoto, nami tulichagua wito huu wa familia: “Kila kitu hatimaye kitakuwa sawa.” Ila tutasemaje maneno hayo kati yetu wakati usumbufu unakuja na majibu hayapatikani kwa urahisi?

Wakati binti yetu Georgia wa miaka 21, mwenye furaha, mstahiki, alipolazwa hospitalini akiwa katika hali mahututi kufuatia ajali ya baiskeli, familia yetu ilisema, “Kila kitu hatimaye kitakuwa sawa.” Niliporuka kwa ndege mara moja kutoka misheni yetu katika Brazil mpaka Indianapolis, Indiana ili kuwa pamoja naye, nilishikilia wito wa familia yetu. Hata hivyo, binti yetu mpendwa alifariki masaa machache tu kabla ya ndege yangu kutua. Nikiwa na huzuni na mshituko vikiathiri familia yetu kama umeme, tungewezaje kuangaliana na bado tukasema “Kila kitu hatimaye kitakuwa sawa”?

Kufuatia kifo cha kimwili cha Georgia, hisia zetu zilikuwa na maumivu makali, tulipambana, na mpaka leo tuna wakati wa huzuni kubwa, lakini tunashikilia kwa kuamini kwamba hakuna yoyote anayekufa kwa kweli. Licha ya uchungu wetu wakati mwili wa Georgia ulipoacha kufanya kazi, tulikuwa na imani kwamba alikwenda moja kwa moja kuishi hali ya kiroho, na tunaamini tutaishi pamoja naye milele kama tutakuwa waaminifu kwa maagano yetu ya hekaluni. Imani katika Mkombozi wetu na Ufufuko Wake, Imani katika nguvu za ukuhani Wake, na Imani katika kufunganishwa milele hutuwezesha sisi kusema wito wetu kwa uthabiti.

Rais Gordon  B. Hinckley alifundisha: ”Ukifanya bidii kwa uwezo wako, utafanikiwa. Weka imani yako katika Mungu. … Bwana hatatuacha sisi.”4

Wito wa familia yetu hausemi, “Kila kitu kitakuwa sawa sasa.” Unahusu imani yetu katika matokeo ya milele—si lazima kwa matokeo ya wakati huu. Maandiko yanasema, “Tafuteni kwa bidii, ombeni daima, na muwe wenye kuamini, na mambo yote yatafanyika kwa pamoja kwa faida yenu.”5Hii haimaanishi mambo yote ni sawa sawa, lakini kwa wanyenyekevu na wenye imani— vitu vyote chanya na hasi—vinafanya kazi pamoja kwa faida, na uwekaji muda ni wa Bwana. Tunamngojea, wakati mwingine kama Ayubu katika mateso yake, akijua kwamba Mungu ”hutia jeraha, lakini pia huyafunga, huumiza, lakini mikono yake pia huponya.”6 Moyo mnyenyekevu unakubali majaribu na kungoja kwa wakati wa kupona na uzima uje.

Tunapojiridhia  wenyewe kwa Roho, tunajifunza njia ya Mungu na kuhisi mapenzi Yake. Wakati wa sakramenti, ambao ninaita kiini cha Sabato, nimegundua kwamba baada ya kuomba msamaha wa dhambi, ni vyema kujifundisha kumwomba Baba wa Mbinguni, “Kuna kitu zaidi naweza kufanya?” Wakati tunapokuwa wanyenyekevu na watulivu, akili zetu zinaweza kuelekezwa kwenye kitu zaidi tunahitaji kubadilisha—kitu fulani kinachopunguza uwezo wetu wa kupokea mwongozo wa kiroho au hata uponyaji na msaada.

Kwa mfano labda kwa uangalifu nimeficha kwa makini chuki juu ya mtu fulani. Wakati nikiuliza kama kuna zaidi cha kuungama, ile “siri” inanijia wazi katika mawazo yangu. Kwa dhati, Roho Mtakatifu ananong’ona, “Uliuliza kwa dhati kama  kulikuwa na zaidi, na hiki hapa. Udhia wako hupunguza maendeleo yako na huharibu uwezo wako wa kuwa na uhusiano mzuri. Unaweza kusamehe hii.” Eh, ni kazi ngumu—tunaweza kuhisi kabisa tumehalalishwa katika uadui wetu—lakini kujiridhia kwa njia ya Bwana ni njia pekee kwa furaha ya milele.

Katika muda na kwa kiwango, tunapokea uwezo na mwelekeo Wake wa neema—labda kutuongoza sisi kila mara hekaluni au kujifunza zaidi kwa kina Upatanisho wa Mwokozi au kushauriana na rafiki, askofu, mshauri stadi au hata daktari. Uponyaji wa mioyo yetu unaanza wakati tunajitoa kwa na kumwabudu Mungu.

Ibada ya kweli inaanza wakati mioyo yetu imenyooka mbele za Baba na Mwana. Nini hali ya mioyo yetu leo? Kimafumbo, ili tuwe na moyo ulioponywa na wenye imani, ni lazima kwanza tuuruhusu uvunjike mbele za Bwana. “Mtatoa dhabihu kwangu ya moyo uliovunjika na roho iliyopondeka,”7 Bwana anatangaza. Matokeo ya kutoa dhabihu mioyo yetu, au mapenzi, kwa Bwana ni kwamba tupokee mwongozo wa kiroho tunaohitaji.

Pamoja na uelewa unaokuwa wa neema ya Bwana na huruma, tunapata kwamba mioyo yenye hiari inaanza kupata ufa na kuvunjika kwa shukrani. Kisha tunamfikia Yeye, tukitamani kujitia nira sisi wenyewe kwa Mwana Mzaliwa Pekee wa Mungu. Katika mioyo yetu iliyovunjika kufika na kutia nira, tunapokea matumaini mapya na mwongozo wenye nguvu kupitia Roho Mtakatifu.

Nimepambana kuondoa hamu ya kibinadamu kufanya mambao kwa njia yangu, hatimaye kutambua kwamba njia yenyewe ina upungufu, ina kikomo, na ni duni kwenye njia ya Yesu Kristo. ”NjiaYake ni njia ambayo inaelekeza kwenye furaha katika maisha haya na maisha ya milele katika ulimwengu ujao.”8 Tunaweza kumpenda Yesu Kristo na njia Yake zaidi kuliko tunavyojipenda sisi wenyewe na ajenda yetu?

Baadhi wanaweza kufikiri wameshindwa mara nyingi mno na kuhisi wadhaifu sana kubadili vitendo vya dhambi au tamaa za ulimwengu za moyoni. Hata hivyo, kwa vile sisi ni sehemu ya Israeli tuliofanya maagano na Baba wa Mbinguni, hatujaribu tu na kujaribu sisi wenyewe kubadilika. Kama tukimsihi Mungu, anatukubali kama tulivyo—na kutufanya zaidi ya hata tulivyojifikiria. Mtaalamu na mwalimu wa dini maarufu Robert  L. Millet anaandika kuhusu matamanio mema ya kuboresha, uliyowiana na uhakika wa kiroho kwamba katika na kupitia kwa Yesu Kristo, tutakwenda kufanikiwa.”9 Kwa uelewa kama huu, tunaweza kwa uwaminifu kusema kwa Baba wa Mbinguni:

Kwa hivo nitayaachilia yote kwa ulinzi wako,

Na kujua unanipenda mimi,

Nitafanya mapenzi yako kwa moyo wa kweli:

Nitakuwa kile wewe unataka mimi niwe.10

Wakati tunapotoa mioyo yetu iliyovunjika kwa Yesu Kristo, anakubali matoleo yetu. Anatuchukua tena. Bila kujali hasara, vidonda, na kukataliwa tulikoteseka, neema Yake na uponyaji ni vyenye uwezo mkubwa kuliko vitu vyote. Kwa kutiwa nira na Mwokozi kwa kweli, tunaweza kusema kwa uhakika,”Kila kitu hatimaye kitakuwa sawa.” Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Dallin H. Oaks, “The Parable of the Sower,” Liahona, May 2015, 32.

  2. “Have Thine Own Way, Lord,” The Cokesbury Worship Hymnal, no. 72.

  3. Ona Mathayo 6:9–13.

  4. Gordon  B. Hinckley, Jordan Utah South regional conference, priesthood session, Mar.  1, 1997; see also “Excerpts from Addresses of President Gordon B. Hinckley,” Ensign, Oct. 2000, 73.

  5. Mafundisho na Maagano 90:24.

  6. Ayubu 5:18.

  7. 3 Nefi 9:20 AM.

  8. “The Living Christ: The Testimony of the Apostles,” Liahona, Apr. 2000, 3; emphasis added.

  9. Robert L. Millet, After All We Can Do: Grace Works (2003), 133.

  10. “I’ll Go Where You Want Me to Go,” Hymns, no. 270.