2010–2019
Hatua Yako Inayofuata
Oktoba 2015


Hatua Yako Inayofuata

Baba yako Mbinguni mwenye upendo na Mwanawe, Yesu Kristo, wanakualika uchukue hatua yako inayofuata kwenda Kwao. Usisubiri. Ichukue sasa.

Moyo wangu ulilemewa hivi karibuni wakati wa mkutano na Watakatifu wa Siku za Mwisho wazuri. Swali liliulizwa, “Ni nani anatamani kuishi tena na Baba wa Mbinguni?” Kila mkono ulinyooshwa. Swali lililofuata lilikuwa “Nani ana uhakika atafanikiwa?” Kwa huzuni na mshangao, mikono mingi iliteremshwa chini.

Wakati tunapoona pengo kati ya sisi tulivyo sasa na wale tunataka kuwa, wengi wetu tunashawishika kuchagua kupoteza imani na tumaini.1

Kwa sababu “hakuna kitu kichafu kinaweza kukaa na Mungu, ”2 ili kuishi Naye tena tutahitaji kusafishwa dhambi3 na kutakaswa.4 Kama tunahitaji kufanya hili peke yetu, hakuna kati yetu anaweza kufanikiwa. Lakini hatupo peke yetu. Hakika, hatupo peke yetu kamwe.

Tuna msaada wa mbinguni kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake.5 Mwokozi alisema, “Kama mtakuwa na imani na mimi mtakuwa na uwezo wa kufanya kitu kinachotarajiwa na mimi.”6 Imani inapofanyiwa kazi, imani huongezeka.

Acha tufikirie kwa pamoja kanuni tatu ambazo zitatusaidia sisi katika safari yetu kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni.

Kuwa kama Mtoto

Mjukuu wetu wa mwisho wa kiume anaelezea kanuni ya kwanza. Baada ya kujifunza kutambaa na kisha kusimama, alikuwa tayari kujaribu kutembea. Wakati wa majaribio yake ya kwanza, alianguka, alilia, na alionyesha sura ambayo ilisema, “Kamwe siwezi—tena—kujaribu tena mara nyingine! Nitakwenda kuendelea kutambaa.”

Wakati anapojikwaa na kuanguka, wazazi wake wapendwa hawakufikiria kwamba alikuwa hana maana au kwamba asingetembea tena. Badala yake walinyoosha mikono yao wakati wakimwita, na macho yake akiwaangalia, alijaribu tena kwenda kuelekea kwenye kumbatio la upendo.

Wazazi wapendwa mara zote wapo tayari na mikono iliyonyoshwa kukaribisha hata hatua ndogo katika mwelekeo sahihi. Wanajua kwamba kutaka kwetu kujaribu na kujaribu tena kutatuongoza kuendelea na kufanikiwa.

Mwokozi alifundisha kwamba kuurithi ufalme wa Mungu, lazima tuwe kama watoto wadogo.7 Hivyo, kuongea kiroho, kanuni ya kwanza ni kwamba tunahitaji kufanya tuliyoyafanya kama watoto.8

Kama watoto wadogo unyenyekevu na matamanio ya kulenga kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, tunapiga hatua kuwaelekea Wao, bila kukata tamaa ya matumaini, hata kama tunaanguka. Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo anafurahi katika kila hatua ya wema, na kama tunaanguka, Anafurahia kila juhudi ya kusimama na kujaribu tena.

Tenda kwa Imani

Kanuni ya pili imeelezewa na Watakatifu waaminifu wawili, kila moja akitamani kumtafuta mwenza wa milele. Wote kwa maombi walichukua hatua zilizojaa imani.

Yuri, Mtakatifu wa Siku za Mwisho Mrusi, alitoa dhabihu na aliwekeza ili kusafiri kwenda hekaluni. Katika gari la moshi alimwona mwanamke mzuri mwenye uso angavu, na alihisi kwamba ashiriki naye injili. Bila kujua kitu kingine cha kufanya, alianza kusoma Kitabu cha Mormoni, akitarajia kwamba angeweza kumwona.

Yuri hakugundua kwamba yule mwanamke, Mariya, tayari alikuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho. Bila kujua kwamba Yuri pia alikuwa muumini, na akifuata mwongozo wa kutaka kushiriki naye injili, Mariya alianza kusoma Kitabu cha Mormoni chake pia, akitarajia kwamba angeweza kumwona.

Vizuri, wakati kwa pamoja walitazamana, Yuri na Mariya walishangazwa kuona Kitabu cha Mormoni kwenye mikono ya kila mmoja wao—na ndiyo, baada ya kupendana, waliunganishwa hekaluni. Leo, Yuri na Mariya Kutepov wa Voronezh, Urusi, kama wenza wa milele, wanachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Kanisa huko Urusi.

Msisitizo hapa siyo tu kwa hawa wanandoa kukubali kutenda katika imani. Lakini pia kuhusu kanuni ya pili—ni zaidi ya Bwana kuambatanisha kukubali kwetu kutenda katika imani. Kukubali kwetu kuchukua hatua hakujaisha, kuliendelezwa na baraka zilizoahidiwa na Bwana.

Baba wa Mbinguni na Mwokozi wetu wanatamani kutubariki. Zaidi ya yote, Wanahitaji moja ya kumi ya kile walichotubariki nacho na basi ile ahadi kwamba madirisha ya mbinguni yatafunguliwa!9

Wakati kwa hiari tukitenda kwa imani katika Yesu Kristo na kuchukua hatua nyingine, hususani hatua ya wasiwasi inahitaji badiliko, toba, tunabarikiwa kwa nguvu.10

Ninashuhudia kwamba Bwana anatuongoza kwenda—na kupitia—hatua zetu zinazofuata. Atatuongezea zaidi juhudi zetu pamoja na uwezo Wake kama tunakubali kuendelea kujaribu, kutubu, na kusonga mbele kwa imani katika Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae, Yesu Kristo.

Karama za kiroho hazijaahidiwa tu kwa wale wampendao Mungu na kutii amri Zake zote bali pia, kwa shukrani, kwa wale akina sisi ambao “[tunatamani] kufanya hivyo.”11

Vibao viwili muhimu vya kila wiki ambavyo vinahitimisha safari yetu ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni ni agano la ibada ya sakramenti na kuitii siku ya Sabato. Rais Russell M. Nelson alitufundisha kwenye mkutano mkuu uliopita kwamba Sabato ni zawadi ya Bwana kwetu. Kujitoa kwetu kila wiki kuitii Sabato ni ishara yetu kwa Bwana kwamba tunampenda Yeye.12

Kila siku ya Sabato tunashuhudia kwamba tupo “tayari [kujichukulia jina Lake],  na kumkumbuka yeye, na kutii amri zake.”13 kama malipo ya moyo wa toba na dhamira, Bwana anarejesha ahadi ya kusamehe dhambi na kutuwezesha “wakati wote Roho wake kuwa pamoja [nasi].”14 Ushawishi wa Roho Mtakatifu huboreshwa, huimarika, hufundisha, na hutuongoza.

Kama, katika kumkumbuka Yeye kila Sabato, tunaigeuza mioyo yetu kwa Mwokozi kupitia alama hizi mbili muhimu, juhudi zetu kwa mara nyingine zaidi zinaambatanishwa na Bwana kwa baraka Zake za ahadi. Tumeahidiwa kwamba, kwa kujitoa kuishika siku ya Sabato, ukamilifu wa dunia utakuwa wetu15

Njia ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni inatuongoza kwenye nyumba ya Bwana, ambako tumebarikiwa kupokea ibada za kuokoa kwa ajili yetu na kwa ajili ya wapendwa wetu waliofariki. Rais Boyd K. Packer alifundisha kwamba ibada na maagano yanakuwa ni sifa zetu kwa ajili ya kukubaliwa kwenye uwepo wa [Mungu].”16 Ninaomba kwamba kila mmoja wetu awe mwenye kustahili na kutumia sifu ya hekalu ili kutumikia mara kwa mara.

Kumshinda Mwanadamu wa Asili

Kanuni ya tatu ni hii: hatuna budi kukabiliana na tabia ya kuahirisha, kuweka mbali, au kushindwa.17

Tunapoendelea katika njia ya agano, tutafanya makosa, baadhi mara nyingi. Baadhi yetu tunaopambana na tabia au utawaliwa tunahisi hatuna nguvu za kuushinda. Lakini imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni kanuni ya matendo na uwezo.18 Kama tupo tayari kutenda, tutabarikiwa na nguvu za kutubu na nguvu za kubadilika.

Tunashindwa pale tu tunaposhindwa kuchukua hatua nyingine ya imani kusonga mbele. Hatutaweza, hatuwezi, kushindwa kama tumetiwa nira kwa uaminifu wa Bwana—Yeye ambaye hajawahi kushindwa na hawezi kutuangusha sisi!

Baraka Zilizoahidiwa

Nina ahidi kwamba kila hatua iliyojaa imani itakutana na msaada kutoka mbinguni. Mwongozo utakuja pale tunapoomba kwa Baba yetu wa Mbinguni, tukimtegemea Mwokozi na kumfuata Yeye, na kumsikiliza Roho Mtakatifu. Nguvu zitakuja kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Yesu Kristo.19 Uponyaji na msamaha utakuja kwa sababu ya neema ya Mungu.20 Hekima na uvumilivu utakuja kwa kuamini katika muda wa Bwana kwa ajili yetu. Ulinzi utakuja kwa kumfuata nabii aliye hai wa Mungu, Rais Thomas S. Monson.

Uliumbwa “ili kwamba uweze kuwa na furaha,”21 furaha utakayohisi wakati ukiwa mwema kurudi kwa Baba yako wa Mbinguni na Mwokozi wako na kukanyaga kwenye kumbatio Lao la joto.

Ninatoa ushuhuda wa hizo kweli halisi. Baba yako wa Mbinguni mwenye upendo na Mwana Wake, Yesu Kristo, wanaishi. Wanakujua wewe. Wanakupenda. Kwa upendo wanakualika kuchukua hatua yako inayofuata kwenda Kwao. Usisubiri. Ichukue sasa. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.