2010–2019
Kipawa Elekezi cha Mtoto
Aprili 2016


Kipawa Elekezi cha Mtoto

Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafundisha watoto kuupiga teke ushawishi wa kilimwengu na kuiamini Roho?

Baba kijana alikuwa akizama. Yeye, na watoto wake wawili, na baba mkwe wake walikuwa wamekwenda kutembea ziwani. Walikuwa wamezingirwa na milima iliyofunikwa na misonobari, na anga za bluu, iliojawa na mawingu laini meupe, vikionyesha uzuri na utulivu. Wakati watoto walipopata joto na kuwa wachovu, wanaume hawa wawili waliamua kuweka watoto mgongoni mwao na kuogelea umbali mfupi kuvuka ziwa.

Ilionekana kuwa rahisi—mpaka wakati baba alipoanza kujisikia kuvutwa chini, kila kitu kikiwa kizito sana. Maji yalimsukuma chini ya ziwa, na hisia ya hofu ikaja juu yake. Angeeleaje—na kufanya hivyo akiwa na bintiye wa thamani juu ya mgongo wake?

Sauti yake ilitoweka umbali alipoitana; baba mkwe wake alikuwa mbali sana kujibu ombi la dharura kwa msaada. Alijisikia peke yake na mnyonge.

Je, unaweza kufikiria kuhisi peke yako kama alivyojisikia, kushindwa kufikia kitu chochote cha kushikilia na kujitahidi katika hali ya kukata tamaa kwa maisha yako na mtoto wako? Kwa bahati mbaya, sisi sote hupitia kiwango fulani cha hisia hii wakati tuko katika hali ambapo tunahitaji kupata msaada ili kuweza kuishi na kuokoa wale tunaowapenda.

Kakaribia kuingia hofu, aligundua kuwa viatu vyake vilivyolowa maji-vilikimfanya awe mzito. Wakati akijitahidi kuelea, alianza kujaribu kutoa viatu vyake vizito kutoka kwa miguu yake. Lakini ilikuwa ni kama vilikuwa vinanyonywa. Kamba zilifura kwa maji, zikikazika hata zaidi.

Katika kile kingekuwa wakati wake wa mwisho wa kukata tamaa, aliweza kufungua viatu kutoka miguuni mwake, na hatimaye viatu vikiondoa mvuto wake, kuanguka kwa haraka ndani ya ziwa. Akiwa huru kutokana na uzito mkubwa ambao ulikuwa ukimvuta chini, mara moja alijirusha juu na bintiye. Sasa angeweza kuogelea mbele, akielekea usalama katika upande ule mwingine wa ziwa.

Nyakati nyingine tunaweza kujisikia ni kama tunazama. Maisha yanaweza kuwa mazito. “Tunaishi katika ulimwengu wenye kelele na shughuli nyingi. … Ikiwa sisi si makini, mambo ya dunia hii yanaweza kuzamisha mambo ya roho.”1

Tutafuata vipi mfano wa baba huyu na kutimua baadhi ya uzito wa dunia tunaobeba, ili tuweze kuweka vichwa vya watoto wetu na akili zetu zenye wasiwasi juu ya maji? Tunawezaje, kama Paulo alivyoshauri, “kuweka kando kila mzigo mzito”?2 Tunawezaje kuwaandaa watoto wetu kwa ile siku ambapo hawawezi tena kuning’inia kwetu na shuhuda zetu—wakati wao ndio watakuwa wakiogelea?

Jibu huja tunapotambua chanzo hiki kitakatifu cha nguvu. Ni chanzo kinachopuuzwa kila mara, ilhali kinaweza kutumika kila siku kupunguza uzito wa mzigo wetu na kuongoza watoto wetu wenye thamani. Chanzo hilo ni kipawa elekezi cha Roho Mtakatifu.

Katika umri wa miaka nane, watoto wanaweza kupokea ubatizo. Wanajifunza kuhusu na kufanya maagano na Mungu. Wale wanaowapenda huwazingira wanapozamishwa na kuinuliwa nje ya maji kwa hisia ya furaha kuu. Kisha wanapokea kipawa kisicho na kifani cha Roho Mtakatifu, kipawa ambacho kinaweza kuwaongoza daima kama wataishi kwa ajili ya baraka hiyo.

Mzee David A. Bednar alisema: “Urahisi wa [uthibitisho] unaweza kutufanya kupuuza umuhimu wake. Haya maneno manne—‘Pokea Roho Mtakatifu’—si tangazo baridi tu; badala yake, yana matamshi ya ukuhani—amri yenye mamlaka ya kutenda na si tu kutendewa.”3

Watoto wana hamu ya asili ya kutenda mema na kuwa wema. Tunaweza kuhisi uzuri wao, usafi wao. Pia wana usikivu mkubwa kwa sauti ndogo tulivu.

Picha
Akiwahudumia watoto Wanefi

Katika 3 Nefi 26, Mwokozi alituonyesha uwezo wa kiroho wa watoto:

“Aliwapatia uwezo wa kuongea, na waliwazungumzia baba zao vitu vikubwa na vya ajabu, hata vikubwa kuliko alivyokuwa amewatambulia watu. …

“… Waliona na kusikia watoto hawa; ndio, hata watoto wachanga walifungua vinywa vyao, na kuongea vitu vya kustaajabisha.”4

Sisi kama wazazi tunaongezaje uwezo wa kiroho wa watoto wetu? Tutawafundishaje kutimua vishawishi vya ulimwengu na kutumaini Roho tusipokuwa nao, na wako peke yao katika maji ya kina kirefu cha maisha yao?

Acha nishiriki nanyi baadhi ya mawazo.

Kwanza, tunaweza kuwajulisha watoto wetu wanaposikia na kuhisia Roho. Hebu turudi nyuma katika muda wa Agano la Kale ili kuona ni kwa jinsi gani Eli alifanya hivi kwa Samweli.

Kijana Samweli alisikia sauti mara mbili Eli, akisema, “Mimi hapa”

“Sikukuita,” alijibu Eli.

Lakini “Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.”

Kwa mara ya tatu, Eli alijua kwamba Mungu alimwita Samweli na akamwambia Samweli aseme, “Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.”5

Samweli alikuwa ameanza kuhisi, kutambua, na kuisikiliza sauti ya Bwana. Lakini kijana huyu hakuanza kuelewa mpaka Eli alipowezesha utambuzi huu. Na baada ya kufundishwa, Samweli angeweza kutambua zaidi sauti ndogo tulivu.

Pili, tunaweza kuandaa nyumbani mwetu na watoto wetu kuhisi sauti ndogo tulivu. “Waalimu wengi wa lugha za kigeni huamini kwamba watoto hujifunza lugha bora katika ’mipango ya kuhusisha,’ ambako wanazungukwa na wasemaji wengine wa lugha na kuitwa kuongea wenyewe. Wanajifunza si tu kusema maneno, lakini kusema kikamilifu na hata kufikiri katika lugha mpya. Mipangilio bora wa ‘uhusishaji’ kwa elimu ya kiroho ni katika nyumba, ambapo kanuni za kiroho zinaweza kujenga msingi kwa maisha ya kila siku.”6

“Nawe uwafundishe [maneno ya Bwana] watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.”7 Kuzihusisha familia zetu katika Roho kutaweka wazi mioyo ya watoto wetu kwa ushawishi Wake.

Tatu, tunaweza kuwasaidia watoto wetu kuelewa jinsi Roho anavyoongea nao. Joseph Smith alifundisha, “Akimjia kwa mtoto mdogo, Yeye atajiweka mwenyewe kwa lugha na uwezo wa mtoto mchanga.”8 Mama mmoja aligundua kwamba kwa vile watoto hujifunza kwa namna tofauti—baadhi hujifunza kuona, kusikia, kugusa, au mwendo—kadri alivyowaangalia watoto wake, ndivyo alivyogundua kuwa Roho Mtakatifu anafundisha watoto wake kwa njia waliyojifunza vyema.9

Mama mwingine alishiriki uzoefu wa kuwasaidia watoto wake kujifunza kutambua Roho. “Wakati mwingine,” aliandika, “[watoto] hawatambui kwamba mawazo yajayo mara kwa mara, hisia ya faraja baada ya kulia, au kukumbuka kitu kwa wakati ufaao zote ni njia ambayo Roho Mtakatifu huwasiliana [nao].” Akaendelea, “Nawafundisha watoto wangu kuzingatia kile wanahisi [na kutenda juu yake].”10

Kuhisi na kutambua Roho kutaleta uwezo wa kiroho katika maisha ya watoto wetu, na sauti watakayo kuja kujua itakuwa wazi kwao. Itakuwa kama vile Mzee Richard G. Scott alivyosema: “Unapopata uzoefu na mafanikio katika kuongozwa na Roho, ujasiri wako katika misikumo unayohisi inaweza kuwa dhahiri zaidi kuliko utegemezi wako juu kile unaona au kusikia.”11

Hatuhitaji kuogopa kama tunapoona watoto wetu wakiingia kwenye bahari ya maisha, kwa kuwa tumewasaidia kujiondolea uzito wa kilimwengu. Tumewafundisha kuishi wakitegemea kipawa elekezi cha Roho. Kipawa hiki kitaendelea kupunguza uzito wanaobeba na kuwaongoza nyumbani kwao mbinguni, ikiwa wataishi kuitegemea na kufuata misukumo yake. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Joseph B. Wirthlin, “The Unspeakable Gift,” Liahona, May 2003.

  2. Waebrania 12:1.

  3. David A. Bednar, “Receive the Holy Ghost,” Liahona, Nov. 2010.

  4. 3 Nefi 26:1416.

  5. Ona 1 Samweli 3:4–10.

  6. C. Terry and Susan L. Warner, “Helping Children Hear the Still, Small Voice,” Liahona, Aug. 1994

  7. Kumbukumbu la Torati 6:7.

  8. Joseph Smith, katika History of the Church, 3:392.

  9. Ona Merrilee Browne Boyack, “Helping Children Recognize the Holy Ghost,” Liahona, Dec. 2013.

  10. Irinna Danielson, “How to Answer the Toughest ‘Whys’ of Life,” Oct. 30, 2015, lds.org/blog.

  11. Richard G. Scott, “To Acquire Spiritual Guidance,” Liahona, Nov. 2009.