2010–2019
Jukumu Takatifu
Aprili 2016


Jukumu Takatifu

Tunu hii ya thamani ya nguvu za ukuhani huleta si tu majukumu matakatifu bali pia baraka maalumu kwa ajili yetu wenyewe na watu wengine.

Ndugu zangu wapendwa, ninaomba Roho aiongoze hotuba yangu jioni hii. Mkanda mmoja unatuunganisha. Tumeaminiwa kuwa ukuhani wa Mungu na kutenda katika jina Lake. Sisi ni wapokeaji wa jukumu takatifu. Mengi yanatarajiwa kutoka kwetu.

Tunasoma katika Mafundisho na Maagano, sehemu ya 121, mstari wa 36, “Haki ya ukuhani zimeungana na hazitenganishiwi na nguvu za mbinguni.” Ni tunu nzuri kiasi gani ambayo tumepewa. Letu ni jukumu la kulinda huo ukuhani na kustahili baraka zote takatifu za Baba wa Mbinguni alizotuwekea sisi—na wengine kupitia kwetu sisi.

Kokote uendako, ukuhani utakwenda pamoja nawe. Unasimama mahali patakatifu? Kabla ya kujiweka mwenyewe na ukuhani wako hatarini kwa kwenda katika sehemu au kushiriki katika shughuli ambazo si njema kwako au kwa ule ukuhani, tulia ufikirie madhara yake. Kumbuka kuwa wewe ni nani na Mungu anatarajia uwe nani. Wewe ni mtoto wa ahadi. Wewe ni mtu wa nguvu. Wewe ni Mwana wa Mungu.

Tunu hii ya thamani ya nguvu za ukuhani huleta si tu majukumu matakatifu bali pia baraka maalumu kwa ajili yetu wenyewe na watu wengine. Ninaomba, mahali popote tutakapokuwepo, kustahili daima ili kuziita nguvu zake, kwani kamwe hatujui lini mahitaji na fursa zetu za kufanya hivyo zanavyoweza kuja.

Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, rafiki yangu alikuwa akihudumu katika Pasifiki ya Kusini wakati ndege yake ilipotunguliwa kwenye maeneo ya baharini. Yeye na wafanyakazi wenzake waliruka kwa parachuti kutoka kwenye ndege iliyokuwa ikiungua, walijaza upepo maboya yao ya kujiokoa, na kuyashikilia maboya kwa siku tatu.

Siku ya tatu waliona kile walichojua kuwa ni chombo cha uokoaji. Kiliwapita. Asubuhi iliyofuata kiliwapita tena. Walianza kufa moyo walipogundua kwamba hii ilikuwa siku ya mwisho chombo cha uokoaji kitakuwa kwenye eneo.

Ndipo Roho Mtakatifu alinena na rafiki yangu: “Una ukuhani. Waamuru waokoaji waje kuwachukueni.”

Alifanya kama alivyoongozwa: “Katika jina la Yesu Kristo na kwa nguvu za ukuhani, geukeni mje mtuchukue.”

Baada ya dakika chache chombo cha uwokoaji kikaja, kikawapeleka kwenye nchi kavu. Mwenye ukuhani mwaminifu na anayestahili, katika mwisho wa mateso, alitumia ukuhani, kubariki maisha yake na maisha ya wengine.

Naomba tuamue, hapa na sasa, tujiandae kwa ajili ya wakati wa shida, wakati wa utumishi, wakati wa baraka.

Tunapofikia mwisho wa kikao hiki cha ukuhani, ninawaambieni kwamba ninyi “ninyi ni ukoo mteule, makuhani wa mfalme” (1 Petro 2:9). Naomba tuwe wema katika sifa hizi takatifu, ninaomba kwa moyo wangu wote katika jina la Yesu Krsto, Mwokozi wetu, amina.