2010–2019
Daima Mmkumbuke Yeye
Aprili 2016


Daima Mmkumbuke Yeye

Kwa unyenyekevu nashuhudia, na kuomba, kwamba daima tutamkumbuka Yeye—katika wakati wote, vitu vyote, na sehemu zote ambazo tutakuwepo.

Wapendwa ndugu na akina dada, wakati nilipokuwa nahudumia kimataifa, watu wakati mwingine waliuliza, “Mzee Gong, ni watu wangapi wanaishi katika Eneo la Asia la Kanisa?”

Nilisema, “Nusu ya idadi ya watu ulimwenguni—watu bilioni 3.6.”

Mtu fulani akauliza, “Je ni vigumu kukumbuka majina yao wote?”

Kukumbuka—na kusahau—ni sehemu ya maisha ya kila siku. Kwa mfano, wakati fulani, baada ya kutafuta simu yake mpya ya kiganjani kila mahali, mke wangu hatimaye aliamua kuiita kutoka simu ingine. Wakati aliposikia simu yake ikiita, mke wangu alifikiri, “Nani angekuwa ananiita ? Sijampa namba hii mtu yoyote!”

Kukumbuka—na kusahau—pia ni sehemu ya safari yetu ya milele. Muda, uhuru wa kujiamulia, na kumbukumbu vinatusaidia kujifunza, kukua, na kuongezeka katika imani.

Katika maneno ya wimbo ninaoupenda:

Tunaimba sifa zote katika jina la Yesu,

Na sifa zote na heshima twatoa. …

Ninyi Watakatifu, mnapokea na kushuhudia

Mnamkumbuka Yeye.1

Kila wiki, katika kupokea sakramenti, tunaweka agano daima kumkumbuka Yeye. Kuvuta chache ya zaidi ya marejeo 400 ya maandiko kwa neno kumbuka, hapa kuna njia sita daima tunazoweza kumkumbuka Yeye.

Kwanza, tunaweza daima kumkumbuka Yeye kwa kuwa na matumaini katika maagano, ahadi, na uhakikisho Wake.

Bwana anakumbuka maagano Yake ya milele—kutoka muda wa Adamu mpaka siku watoto wa Adamu “watakapokumbatia ukweli, na kutazama kuelekea juu kisha ndipo Sayuni itaangalia chini, na mbingu zote zitatikisika kwa furaha, na dunia itatetemeka kwa furaha.“2

Bwana anakumbuka ahadi Zake, ikijumuisha kuikusanya Israeli iliyotawanyika kupitia Kitabu cha Mormoni. Ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo na ahadi zilizotolewa kwa kila muumini na mmisionari anayekumbuka thamani ya nafsi.3

Bwana anakumbuka na anaahidi mataifa na watu. Katika siku hizi za mwendo na vurugu,4 “baadhi wanaamini katika magari, na baadhi katika farasi: lakini tutakumbuka jina la Bwana Mungu wetu, “5 anayeongoza “ya baadaye kama alivyoongoza yaliyopita.6 Katika “nyakati zenye hatari,”7 “tunakumbuka kwamba sio kazi ya Mungu ambayo inapingwa bali kazi ya binadamu.”8

Pili, tunaweza daima kumkumbuka kwa kutambua kwa shukrani mkono Wake katika maisha yetu yote.

Mkono wa Bwana katika maisha yetu ni wazi sana kila mara katika utambuzi. Kama mwanafalsafa Mkristo Soren Kierkegaard alivyosema: “Maisha lazima yaeleweke kuelekea nyuma. Lakini … lazima kuishi kwa kuangalia mbele.“9

Mama yangu mpendwa hivi karibuni atasherekea mwaka wake wa 90 wa kuzaliwa. Kwa shukrani alishuhudia baraka za Bwana katika kila jambo kubwa katika maisha yake. Historia za familia, mila za famila, na mahusiano ya familia yanatusaidia kufurahia kukumbuka mambo yaliyopita, hali yakitupatia mpangilio wa siku zijazo na matumaini. Safu za mamlaka ya Ukuhani na baraka za baba mkuu zinashuhudia mkono wa Mungu kuvuka vizazi.

Kamwe umewahi kujifikiria wewe mwenyewe kama kitabu hai chako mwenyewe cha kumbukumbu—kukumbuka nini na jinsi gani unachagua kukumbuka?

Kwa mfano, wakati nilipokuwa kijana, kwa kweli nilipenda kucheza mpira wa kikapu shuleni. Nilifanya mazoezi na nikafanya mazoezi. Siku moja kocha alinionesha wachezaji wetu mwenye urefu wa futi-6 inchi-4 (mita 1,93) kiungo wa kati wa taifa na futi- 6 inchi-2(1.88) mshambulizi na akaniambia, “Naweza kukuweka wewe kwenye timu, lakini huenda kamwe usicheze.” Kisha nakumbuka jinsi kwa huruma alivyonitia moyo, “Kwa nini usijaribu kandanda? Utakuwa mzuri.” Familia yangu ilishangilia wakati nilipofunga goli langu la kwanza.

Tunaweza kuwakumbuka wale wanaotupa nafasi, na nafasi ya pili, kwa uaminifu, upole, uvumilivu, na kututia moyo. Na tunaweza kuwa mtu fulani wengine hukumbuka wakati wanapohitaji msaada sana. Kwa shukrani kukumbuka msaada wa wengine na ushawishi wa mwongozo wa Roho ni njia tunamkumbuka Yeye. Ni njia tunahesabu baraka zetu nyingi na kuona kile Mungu amefanya.10

Tatu, tunaweza daima kumkumbuka Yeye kwa kuamini wakati Bwana anatuhakikishia “Yeye ambaye ametubu dhambi zake, huyu atasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena.“11

Wakati tunapotubu kikamilifu, ikijumuisha kuungama na kuziacha dhambi zetu, tunauliza pamoja na Enoshi, wakati hatia zetu zinapoondolewa, “Bwana, inafanyika vipi?” na sikiliza jibu “Kwa sababu ya imani yako katika Kristo”12 na mwaliko Wake “kuniweka katika kumbukumbu.”13

Mara tunapotubu na viongozi wa ukuhani wanatutangaza kuwa tunastahili, hatuhitaji kuendelea kuungama na kuungama dhambi za hapo awali. Kustahili hakumaanishi kuwa mkamilifu. Mpango Wake wa furaha hutualika tuwe wanyenyekevu kwa amani kwenye safari ya maisha yetu ili siku moja tuwe wakamilifu katika Kristo,14 sio siku zote kuwa na wasiwasi, kukatishwa tamaa, au kuto kuwa na furaha katika kutokamilika kwetu leo. Kumbuka, Yeye anajua vitu vyote ambavyo hatutaki mtu mwingine yoyote kujua kutuhusu sisi—na bado anatupenda sisi.

Wakati mwingine maisha hujaribu imani yetu katika huruma ya Mungu, haki, na hukumu na mwaliko wa ukombozi Wake kuruhusu Upatanisho Wake kutuponya tunapowasamehe wengine na sisi wenyewe.

Msichana katika nchi nyingine aliomba kufanya kazi kama mwandishi wa habari, lakini ofisa aliyekuwa anagawa kazi hakuwa na huruma. Alimwambia, “Kwa saini yangu, ninakuhakikishia hautaweza kuwa mwandishi wa habari bali utachimba mifereji ya uchafu.” Alikuwa mwanamke pekee aliyekuwa akichimba mifereji ya uchafu katika genge la wanaume

Miaka mingi baadae, mwanamke huyu alikuwa ofisa. Siku moja mwanaume alikuja akihitaji saini yake kwa ajili ya kazi.

Aliuliza,”Unanikumbuka mimi?” Hakumkumbuka.

Alisema, “Hunikumbuki mimi, lakini nakukumbuka wewe. Kwa saini yako, ulinihakikishia nisingeweza kuwa mwandishi wa habari. Kwa saini yako, ulinipeleka kuchimba mifereji ya uchafu, mwanamke pekee katika genge la wanaume.”

Aliniambia, ”Ninahisi nilipaswa kumtendea mtu yule vizuri zaidi kuliko alivyonitendea mimi—lakini sina nguvu hiyo.” Wakati mwingine nguvu ile haipo pamoja nasi, lakini inaweza kupatikana katika Upatanisho wa Yesu Kristo.

Wakati imani inaposalitiwa, ndoto zimevunjika, mioyo imevunjika, na kuvunjika tena, wakati tunataka haki na kuhitaji huruma, wakati ngumi zetu tumezikunja na machozi yetu yanatiririka, wakati tunahitaji kujua nini cha kushikilia na nini cha kuachia kiende, tunaweza daima kumkumbuka Yeye. Maisha sio katili kama yanavyoweza kuonekana wakati mwingine. Huruma Yake isiyo na mwisho inaweza kutusaidia kuona njia yetu, ukweli, na maisha.15

Wakati tunakumbuka maneno na mfano Wake, hatutatoa au kuona maudhi.

Baba ya rafiki yangu alifanya kazi kama mekanika. Kazi yake ya uaminifu ilionekana hata katika mikono yake iliyooshwa kwa makini. Siku moja, mtu fulani hekaluni alimwambia baba ya rafiki yangu anatakiwa kuosha mkono yake kabla ya kuhudumia pale. Badala ya kuudhika, mtu huyu mwema alianza kusugua vyombo vya familia kwa mkono kwa maji yenye sabuni zaidi kabla ya kuhudhuria hekaluni. Alitoa mfano wa wale ambao “wanaopanda kwenye mlima wa Bwana” na “kusimama katika sehemu yake takatifu” wakiwa na mikono iliyo safi sana na mioyo iliyo safi sana.16

Kama tuna hisia mbaya, vinyongo, au chuki au kama tuna sababu ya kuomba msamaha wa wengine, sasa ndiyo wakati wa kufanya hivyo.

Nne. Yeye anatualika kukumbuka kwamba daima anatukaribisha nyumbani.

Tunajifunza kwa kuuliza na kutafuta. Lakini tafadhali msiache upelelezi mpaka mnapofika—katika maneno ya T. S. Eliot— “kule ulikoanza na kujua sehemu kwa mara ya kwanza.”17 Unapokuwa tayari, tafadhali fungua moyo wako kwa Kitabu cha Mormoni, tena, kwa mara ya kwanza. Tafadhali sali na dhamira ya kweli, tena, kwa mara ya kwanza.

Amini hiyo mapema na usiwe na hofu. Iache ikuze imani yako. Kwa Mungu, hakuna sehemu ya kutoweza kurudi nyuma tena.

Manabii wa zamani na wa sasa wanatusihi tusiruhusu hitilafu ndogo ndogo za kibinadamu, makosa, au udhaifu—wa wengine au wetu—hutusababishie sisi kukosa kweli, maagano, na nguvu ya wokovu katika injili Yake ya urejesho.18 Hii hususani ni muhimu katika kanisa ambako kila mmoja wetu anakua kupitia kushiriki kwetu kusiko kamilifu. Nabii Joseph alisema, “Kamwe sikuwaambia nilikuwa mkamilifu; lakini hakuna kosa katika maono ambayo nimewafundisha.”19

Tano, tunaweza daima kumkumbuka Yeye kwenye Sabato kupitia sakramenti. Mwishoni mwa huduma Yake duniani na mwanzo wa huduma Yake baada ya kufufuka,—nyakati zote mbili—Mwokozi wetu alichukuwa mkate na mvinyo na aliomba kwamba tukumbuke mwili na damu Yake,20 “na mara nyingi mtakapofanya hivi mtakumbuka saa hii kwamba nilikuwa pamoja nanyi.”21

Katika ibada ya sakramenti, tunashuhudia kwa Mungu Baba kwamba tupo tayari kuchukua juu yetu jina la Mwanae ili daima kumkumbuka Yeye, na kutii amri Zake, ambazo ametupa sisi, ili daima Roho Wake apate kuwa pamoja nasi.22

Kama Amuleki anavyofundisha, tunamkumbuka Yeye wakati tunaposali juu ya mashamba yetu, mifugo yetu, na kaya zetu na wakati tunapokumbuka maskini, walio uchi, wagonjwa na wanaoteseka.23

Mwishowe, ya sita, Mwokozi wetu anatualika sisi daima kumkumbuka Yeye jinsi daima anavyotukumbuka sisi.

Katika ulimwengu mpya, Mwokozi wetu aliyefufuka aliwaalika wale waliokuwepo kuja mmoja mmoja, kukumba mikono yao kwenye ubavu wake na kuhisi alama za misumari katika mikono Yake na katika miguu Yake.24

Maandiko yanaelezea ufufuko kama “kila mkono na kiungo kitarudishwa kwenye—framu yake stahiki na kamilifu,” na “hata unywele wa kichwani hautapotea.”25 Hiyo kuwa hivyo, tafadhali fikiria jinsi inakuwa kwamba mwili kamili, uliofufuka wa Mwokozi wetu bado una vidonda katika ubavu Wake na alama za misumari katika mikono na miguu Yake.26

Mara nyingi katika historia, watu wamekuwa wakiuawa kwa kusulibiwa. Lakini Mwokozi wetu pekee, Yesu Kristo, anatukumbatia bado akiwa na alama za upendo Wake safi. Pekee anatimiza unabii wa kuinuliwa juu ya msalaba ili aweze kuvuta kila mmoja wetu, kwa jina, Kwake.27

Mwokozi wetu anatangaza:

“Naam, wanaweza kusahau, bado sitakusahau wewe.

“Tazama, Nimewachora kwenye viganja vya mikono yangu.”28

Yeye hushuhudia: “Mimi ni yule aliyeinuliwa. Mimi ni Yesu ambaye alisulibiwa. Mimi ni Mwana wa Mungu.”29

Kwa unyenyekevu nashuhudia, na kuomba, kwamba daima tutamkumbuka Yeye—katika wakati wote, vitu vyote, na sehemu zote ambazo tutakuwepo.30 Katika jina la Yesu Kristo, amina.