2010–2019
Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2015
Aprili 2016


Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2015

Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Ndugu Wapendwa: Kama ilivyoagizwa kwenye sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Utumiaji wa Zaka—linajumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi—huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Mashirika ya Kanisa hugawa fedha kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa, sera, na taratibu.

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, ambayo inajumuisha wataalamu wenye sifa na ni huru kutoka kwa idara nyingine zote za Kanisa, ina jukumu la kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango inayopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na kulinda mali ya Kanisa.

Kulingana na ukaguzi uliofanywa, Idara ya Ukaguzi ya Kanisa inatoa maoni kwamba, katika mambo yote muhimu, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na mali ya Kanisa kwa mwaka 2015 vimerekodiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa na Kanisa, sera, na utendaji wa uhasibu. Kanisa linafuata utendaji uliofundishwa kwa waumini wake wa kuishi katika mipaka ya bajeti, kuepuka madeni, na kuweka hifadhi kwa ajili ya wakati wa shida.

Kwa heshima imewasilishwa,

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa

Kevin R. Jergensen

Mkurugenzi Mkuu