2010–2019
Ninaamini?
Aprili 2016


Ninaamini?

Kama mambo haya ni ya kweli, basi tuna ujumbe mkubwa wa tumaini na msaada ambao dunia haijawahi kuona.

Mnamo Marchi 30, mwaka mmoja tu uliopita, mtoto mdogo wa miaka miwili Ethan Carnesecca, kutoka American Folk, Utah, alilazwa hospitalini na matatizo ya pneumonia na kuwa na maji kwenye mapafu. Siku mbili baadaye, hali yake ikawa mbaya ambayo ilimhitaji kupelekwa kwa helikopta mpaka Primary Children’s Hospital Salt Lake City Michelle, mama yake akiwa na hofu, aliruhusiwa kwenda naye akiwa kiti cha mbele na kuambatana na mwanawe. Alipewa vipaaza sauti vya masikio ili aweze kuwasiliana na wengine kwenye helikopta. Aliweza kuwasikia wataalamu wa afya wakimhudumia mwanawe, na yeye akiwa nesi wa watoto mwenyewe, Michele alijua vya kutosha kuelewa kuwa Ethan alikuwa kwenye hali mbaya sana.

Picha
Ethan Carnesecca akiwa mgonjwa

Katika hali hiyo mahututi, Michele aligundua kuwa walikuwa wanaruka juu ya hekalu la Draper Utah. Kutoka hewani, alitazama nje kwenye bonde na aliweza kuona hekalu la Jordan River, hekalu la Oquirrh Mountain, na hata hekalu la Salt Lake kwa mbali. Wazo lilimjia kichwani: “Je unaamini au siyo?”

Alisema kuhusu uzoefu huu:

“Nimegundua kuhusu baraka za hekaluni na kwamba ‘familia ni za milele’ katika madarasa ya Msingi na ya Wasichana.” Nilishiriki ujumbe kuhusu familia kwa watu wema wa Mexico katika misheni yangu. Nilifunganishwa na mwenza wangu wa milele kwa wakati na milele yote hekaluni. Nilifundisha masomo kuhusu familia kama kiongozi wa wasichana, na kushiriki nao hadithi kuhusu umilele wa familia na watoto katika jioni ya familia nyumbani. MIMI NILIJUA, lakini NILIAMINI? Majibu yangu yalikuja kwa haraka kama maswali yalivyotoka katika kichwa changu: Roho ilinihakikishia kwenye moyo wangu jibu ambalo nilishalijua—NILIIAMINI!

“Kwa wakati huo niliumwaga moyo wangu katika maombi kwa Baba yangu wa Mbinguni, nikimshukuru kwa ajili ya ufahamu na amini niliyokuwa nayo kwamba familia kwa kweli ni za milele. Namshukuru kwa ajili ya Mwanawe, Yesu Kristo, ambaye aliwezesha yote. Nilimshukuru kwa ajili ya mwanangu, na nikamwambia Baba yangu wa Mbinguni kama akihitaji kumchukua mwanangu Ethan kwenye nyumba yake mbinguni, ni SAWA. Nilimwamini Baba yangu wa Mbinguni kabisa, na nilijua kuwa ningemuona Ethan tena. Nilikuwa na shukrani sana katika kipindi hiki kigumu, nilikuwa na uelewa NA imani kwamba injili ilikuwa ni ya kweli. Nilikuwa na amani.”1

Ethan alikaa wiki nyingi sana hospitalini, akipata matibabu kutoka kwa wataalam. Maombi, kufunga, na imani ya wapendwa, ikijumuishwa na kujali, ilimfanya atoke hospitalini na kurudi nyumbani kuwa na familia yake. Ni mwenye afya njema na yuko sawa hivi leo.

Picha
Familia ya Carnesecca
Picha
Ethan Carnesecca akiwa amepata nafuu

Wakati huu wa kutafakari kwa Michele ilidhihirisha kwamba kile alichokisema kilikuwa kimefundishwa maisha yake yote zaidi ya maneno tu; ni kweli.

Je, wakati mwingine tunakuwa na mazoea ya baraka tulizopewa kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kufikia kushindwa kuelewa miujiza na ukubwa wa kazi ya ufuasi katika Kanisa la Bwana? Je, tuna hatia ya kuwa watu walegevu kuhusu karama kuu tunayoweza kupewa katika maisha haya? Mwokozi mwenyewe alifundisha, “Kama utatii amri zangu na kuvumilia mpaka mwisho utaupata uzima wa milele, karama iliyo juu kuliko karama zozote za Mungu.”2

Tunaamini kwamba kanisa hili ni zaidi ya pahali pazuri pa kwenda siku za jumapili na kujifunza kuwa mtu mwema. Ni zaidi ya kilabu ya wapendwa Wakristo ambapo tunaweza kujumuika na watu wengine wenye tabia na mienendo miema. Siyo tu mfumo wa mawazo kwamba wazazi wanaweza kufundisha watoto wao nyumbani ili wawe wawajibikaji,watu wazuri. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho haina mwisho na zaidi ya vitu hivi vyote.

Fikiria kwa dakika moja kuhusu madai mazito tunayotoa kama dini. Tunaamini kwa kanisa lile lile Yesu Kristo aliloanzisha alipokuwa duniani limerejeshwa tena na Nabii aliyeitwa na Mungu katika wakati wetu na kwamba viongozi wetu wana nguvu zile zile na mamlaka kutenda katika jina la Mungu ambayo manabii wa kale walikuwanazo. Huitwa ukuhani wa Mungu. Tunadai kwamba, kupitia kwenye mamlaka haya yaliyorejeshwa, tunaweza kupokea ibada za wokovu kama vile ubatizo na kufurahia karama ya kutakasa na kusafisha ya Roho Mtakatifu kuwa nasi wakati wote. Tuna mitume na manabii wanaotuongoza na kulielekeza Kanisa hili kupitia funguo za ukuhani, na tunaamini kwamba Mungu hunena na watoto Wake kupitia manabii.

Vile vile tunaamini kwamba nguvu hizi za ukuhani zinatuwezesha kufanya maagano na kupokea ibada katika mahekalu matakatifu kwamba siku moja zituwezeshe kurudi katika uwepo wa Mungu na kuishi Naye milele. Vile vile tunadai kwamba, kupitia nguvu hiyo, familia zinaweza kuunganishwa pamoja milele yote pale wanandoa wanapoingia katika agano jipya na la milele la ndoa katika majengo matakatifu ambayo tunaamini ni nyumba halisi za Mungu. Tunaamini kwamba tunaweza kupokea ibada hizi za wokovu siyo tu kwa ajili yetu lakini pia kwa ajili ya mababu zetu ambao waliishi ulimwenguni bila fursa ya kushiriki katika ibada hizi muhimu za kuokoa. Tunaamini kuwa tunaweza kufanya ibada kwa ajili ya mababu zetu kwa niaba yao katika mahekalu hayo hayo.

Tunaamini kwamba, kupitia kwa nabii na nguvu ya Mungu, tumepokea maandiko ya ziada, yakiongeza kwenye ushuhuda ambao upo katika Biblia kutangaza kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu.

Tunadai kwamba Kanisa La Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni ufalme wa Mungu na Kanisa la pekee la kweli duniani. Linaitwa Kanisa la Yesu Kristo kwa sababu anasimamia kichwani; ni Kanisa Lake, na vitu hivi vyote vinawezekana kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho Wake.

Tunaamini kwamba vigezo hivi bainifu haviwezi kupatikana katika sehemu nyingine au shirika lingine katika dunia hii. Kwa uzuri na upendo kama vile dini zingine na makanisa yalivyo, hakuna aliye na mamlaka ya kutoa ibada za wokovu ambazo zipo katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Tuna uelewa wa vitu hivi, lakini tunaviamina? Kama mambo haya ni ya kweli, basi tuna ujumbe mkubwa wa tumaini na msaada ambao dunia haijawahi kuona. Kuyaamini ni jambo la umuhimu wa milele kwetu sisi na kwa wale tunaowapenda.

Ili kuamini, tunahitaji kupata injili kutoka kwenye vichwa vyetu kwenda kwenye mioyo yetu! Inawezekana kwetu sisi kupitia kwenye mienendo ya injili iliyo hai kwa sababu tunatarajiwa kufanya hivyo au kwa sababu ni tamaduni ambamo tumekulia au kwa sababu ya tabia. Labda wengine hawajapata uzoefu wa watu wa Mfalme Benjamini walivyohisi kufuatia mahubiri yake ya kuvutia: “Na wote wakalia kwa sauti moja wakisema: Ndio, tunaamini maneno yote ambayo umetuzungumzia, na pia tunajua uhakika na ukweli wake, kwa sababu Roho wa Bwana Mwenyezi, ambaye ameleta mabadiliko makuu ndani yetu, au mioyoni yetu, hata kwamba hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima”3

Tunahitaji kutafuta kuwa na mioyo na hali zetu zibadilishwe ili kwamba tusiwe na hamu ya kufuata njia za ulimwengu lakini tumtii Mungu. Uongofu wa kweli ni hatua ambayo inafanyika kwa muda mrefu na inajumuisha shauku ya kuifanyia kazi imani. Unakuja tunapoyapekua maandiko badala ya mtandao. Unakuja tunapokuwa watiifu kwa amri za Mungu. Uongofu unakuja tunapowatumikia wale wanaotuzunguka. Unakuja kutoka kwa maombi ya dhati, kuhudhuria hekalu kila mara, na kutimiza kwa uaminifu majukumu tuliyopewa na Mungu. Inachukua msimamo na juhudi za kila siku.

Mara nyingi ninaulizwa, “Je, ni changamoto gani kuu vijana wetu wanakumbana nayo siku hizi?” Mimi najibu kwamba ninaamini ni ushawishi ambao upo kila mara wa lile “jengo kubwa na pana” katika maisha yetu.4 Kama Kitabu cha Mormoni kiliandikwa kwa ajili ya siku zetu, basi hakika hatuwezi kukosa uhusiano wa ujumbe kwa sisi wote kwenye ono la Lehi la mti wa uzima na madhara kwa wale walionyooshea vidole na kuwadhihaki kutoka kwenye jengo kuu.

Kile kinachohuzunisha sana ni yale maelezo ya wale ambao tayari wamejitahidi kupitia kwenye kiza kinene katika njia nyoofu na nyembamba, wameshikilia kwenye fimbo ya chuma, wametimiza malengo yao, na wameanza kuonja matunda matamu na mazuri ya mti wa uzima. Baadaye maandiko yanasema kwamba wale watu waliokuwa wamevaa vizuri katika jumba kuu na zuri “walikuwa katika hali ya kudhihaki na kunyoosha vidole kuelekwa kwa wale ambao walitoka walikuwa wakifungasha matunda.

“Na baada ya kuonja matunda waliaibika kwa sababu ya wale waliokuwa wakiwadharau na wakaingia katika njia zilizokataliwa na wakapotea.”5

Mistari hii inatuelezea sisi ambao tayari tuna injili ya Yesu Kristo katika maisha yetu. Iwe tunalizaliwa nayo au ilitubidi tunga’ang’ane katika ukungu wa giza ili kuipata, tumeshaonja tunda hili, ambalo “ni la thamani na la kutamanika sana”6 na uwezekano wa kutuletea uzima wa milele, “kipawa kikuu kati ya vipawa vya Mungu.” Tunahitaji tu kuendelea kusherekea na kutowasilikiza wale ambao wangetukejeli kwa ajili ya imani yetu au wale ambao wanafurahia kuzua shaka au wale wanaotafuta makosa katika viongozi na mafundisho ya Kanisa. Ni maamuzi tuyafanyayo kila siku—kuchagua imani juu ya shaka. Mzee M. Russell Ballard ametuhimiza “tubaki kwenye boti, kutumia koti la uokozi, na kushikilia kwa mikono miwili.”7

Kama waumini wa Kanisa la kweli la Bwana, tayari tumo ndani ya boti. Hatuhitaji kwenda na kitafuta kupitia kwenye filosofia za ulimwengu kwa ajili ya ukweli ambao utatupa faraja, msaada, na mwongozo wa kutupeleka kwa usalama kupitia kwenye majaribu ya maisha—sisi tayari tunao! Kama vile mama wa Ethan alivyoweza kuchunguza imani yake ya muda na kutangaza kwa ujasiri wakati wa shida, “Ninaamini,” nasi tunaweza!

Ninatoa ushuhuda wangu kwamba uumini katika ufalme wa Bwana ni karama isiyokuwa na kipimo. Ninashuhudia kwamba baraka na amani Bwana ameziweka kwa ajili ya wale ambao ni watiifu na wenye imani inayoshinda kila kitu ambacho akili za wanadamu zinaweza kufahamu. Ninawaachieni ushuhuda huu katika jina la Yesu Kristo, amina.