2010–2019
Akina Baba
Aprili 2016


Akina Baba

Ninalenga leo hii kwa yale mazuri ambayo wanaume wanaweza kuyafanya katika kazi kubwa za uanaume—waume na baba.

Ninazungumzia leo hii kuhusu akina baba. Akina baba ni muhimu katika mpango mtukufu wa furaha na ninataka nipaze sauti yangu kuwatia moyo wale ambao wanapata shida kutimiza vyema wito huo. Kuwasifia na kuutia moyo ubaba na baba siyo kuwaaibisha wala kumshusha yeyote. Kwa urahisi leo hii nalenga mazuri ambayo wanaume wanaweza kuyafanya katika kazi kubwa ya uanaume—waume na kina baba.

David Blankenhorn, mtunzi Fatherless America, ametambua: “Leo, Jamii ya Kimarekani kimsingi imegawanyika kutokuwa na uhakika kuhusu dhana ya ubaba Baadhi ya watu hawaukumbuki. Wengine wanakasirishwa nao. Wengine ikijumuisha zaidi ya wanafamilia waliosoma, huukataa au kuubeza. Wengi wao hawaupingi, wala hawajajitolea kikamilifu kwa ajili yake. Watu wengi wana matamanio kwamba wangeweza kuufanyia kazi, lakini wanaamini kwamba jamii yetu haiwezi na haitaweza tena.”1

Picha
Tunaamini katika kina baba.
Picha
Kina baba wanaongoza kwa upendo na haki.

Kama Kanisa, tunaamini katika akina baba. Tunaamini katika “ubora wa mwanaume anayeiweka familia yake kwanza.”2 Tunaamini kwamba kwa uundaji wa kiungu kina baba wanatakiwa kuongoza familia katika upendo na haki na wana wajibu wa kukidhi mahitaji muhimu katika maisha na kulinda familia zao.”3 Tunaamini kwamba katika kazi zao zinazorandana za kifamilia, “kina baba na kina mama wana wajibu wa kusaidiana kama wenza wenye usawa.”4 Tunaamini kwamba kamwe si wasiohitajika bali, kina baba ni wa kipekee na hamna ka wao.

Picha
Wazazi wana majukumu ya kusaidiana.
Picha
Kina baba hamna kama wao.

Wengine wanaona uzuri wa ubaba katika suala la kijamii, kama kitu kinachowalazimu wanaume kwa uzao wao, ikiwalazimisha kuwa raia wazuri na kufikiria kuhusu mahitaji ya wengine, ikituongezea uwekezaji wa umama kwa watoto. … Kwa kifupi, muhimu kwa wanaume ni kuwa kina baba. Muhimu kwa watoto ni kuwa na kina baba. Cha muhimu kwa jamii ni kuunda akina kina baba.”5 Ilhali zingatio hili ni la kweli na muhimu, tunajua kwamba ubaba ni bora zaidi ya dhana la jamii au hatima ya kuibuka. Jukumu la baba ni la umuhimu wa mwanzo wa kiungu kuanzia kwa Baba wa Mbinguni na, katika maisha haya duniani, kukiwa na baba Adamu.

Mfano wa kiungu kamillifu wa ubaba ni Baba yetu wa Mbinguni. Tabia yake na sifa zinajumuisha wingi wa uzuri na upendo mkamilifu. Kazi na utukufu Wake ni maendeleo, furaha, maisha ya milele ya watoto Wake.6 Akina baba katika dunia iliyoanguka hawawezi kudai kitu kwa Mwenyezi aliye juu, lakini kwa ubora, wanajaribu kumuiga, na kwa hakika wanafanya kazi Yake. Wanatukuzwa kwa uaminifu mkubwa na busara.

Kwa wanaume, ubaba hutuonyesha mapungufu yetu wenyewe na haja yetu ya kukua. Ubaba unahitaji dhabihu, lakini ni chanzo cha kuridhisha kisicho kuwa na kifani, hata ni furaha. Tena, mfano wetu ni Baba wa Mbinguni ambaye ametupenda sana, na akamtoa mwanawe wa pekee kwa ajili ya wokovu na kuinuliwa kwetu.7 Yesu alisema, “hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.”8 Akina baba hudhihirisha upendo huo wanavyojitolea maisha yao kila siku, wakijitolea katika hudumu na kuzitumikia familia zao.

Labda kazi ya kimsingi zaidi ya akina baba ni kugeuza mioyo ya watoto wao kwa Baba Yetu wa Mbinguni. Kama kwa mfano wake na kwa maneno yake baba anaweza kuonyesha jinsi uaminifu kwa Mungu unavyoonekana katika maisha yetu ya kila siku, kwamba baba atakuwa amewapa watoto wake ufunguo wa amani na uzima wa milele katika maisha yajayo.9 Baba anayesoma maandiko kwa watoto wake na pamoja nao anawajulisha kwa sauti ya Bwana.10

Picha
Baba akisoma maandiko

Tunaona katika maandiko mkazo unaojirudia rudia katika wajibu wa uzazi wa kuwafundisha watoto wake:

“Na tena, ilmradi wazazi wanao watoto katika sayuni au katika kigingi chake chochote ambacho kimeundwa, ambao hawawafundishi wao kuelewa mafundisho ya toba, imani katika Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, na ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono, wafikapo miaka minane, dhambi zao zitakuwa juu ya vichwa vya wazazi …

“Na pia wawafundishe watoto wao kuomba, na kusimama wima mbele za Bwana.”11

Mnamo mwaka 1833, Bwana aliwakanya washiriki wa Urais wa Kwanza, kwa kutokuwa makini katika kazi za kuwafundisha watoto wao: Kwa mmoja Yeye alisema hasusani “Hujawafundisha watoto wako nuru na kweli, kulingana na amri; na yule mwovu bado anazo nguvu juu yako, na hii ndiyo chanzo cha mateso yako.”12

Akina baba wanatakiwa kufundisha upya sheria ya Mungu na kazi kwa kila kizazi. Kama Mtunga Zaburi Alivyotamka:

“Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu wawajulishe wana wao:

“Ili kizazi kingine wawe na habari, ndio hao wana watakaozaliwa, wasimame na kuwaambia wana wao:

“Wamwekee Mungu tumaini lao, wala wasiyasahau matendo ya Mungu.”13

Picha
Baba na binti wakichenza densi

Hakika kufundisha injili ni kazi shirikishi kati ya baba na mama, lakini Bwana ameweka bayana kwamba anawategemea akina baba kuongoza na kuipa kipaumbele cha juu. (Na acha tukumbuke kwamba mazungumzo yasiyo rasmi, kufanya kazi na kucheza pamoja, na kusikiliza ni vitu muhimu katika kufundisha.) Bwana anawategemea akina baba kusaidia kuwaweka sawa watoto wao, na wanataka na kuhitaji mfano.

Picha
Baba na mwana wakifanya kazi pamoja

Mimi mwenyewe nilibarikiwa na baba wa kuigwa. Ninakumbuka kwamba nilipokuwa mvulana mwenye miaka 12, baba yangu alikuwa mgombea kiti katika halmashauri ya mji katika jamii yetu ndogo. Hakuweka kampeni kubwa ya uchaguzi—yote ninayokumbuka ni kwamba baba aliniomba mimi na kaka yangu tugawe vipeperushi mlango kwa mlango, tukiwaomba watu kumpigia kura Paul Christofferson. Kulikuwa na idadi ya watu wazima ambao niliwagawia vipeperushi ambao walisema kwamba Paul alikuwa mtu mwaminifu na kwamba wasingekuwa na shida kumpigia kura. Moyo wa wangu wa ujana ulijawa na imani katika baba yangu. Ilinipa ujasiri na shauku ya kufuata nyayo zake. Hakuwa mkamilifu—hakuna aliye—lakini alikuwa mtu wa haki na mwema na mwenye mfano mzuri kwa mtoto wake.

Nidhamu na kurekebisha ni sehemu ya mafundisho. Paulo alisema, “Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi.”14 Lakini katika kumrudi, baba ni lazima kutahadhari pasiwe jambo linalokaribia mateso ambayo kamwe hayakubaliki. Baba anapofanya marekebisho, msukumo wake lazima uwe ni upendo na ukiongozwa na Roho Mtakatifu:

“Kukemea kwa ukali kwa wakati wake, utakapokuwa umeongozwa na Roho mtakatifu, na halafu baadaye kuonyesha ongezeko la upendo kwa yule uliyemkemea, asije akakudhania wewe kuwa ni adui yake;

“Ili apate kujua kwamba uaminifu wako ni imara zaidi kuliko kamba za mauti.”15

Nidhamu ni mpangilio wa kiungu siyo tu kuhusu kuadhibu kwani ni zaidi kuhusu kumsaidia mpendwa katika njia ya kujimudu.

Picha
Baba kazini
Picha
Kujipatia kipato

Bwana alisema kwamba “watoto wote wanayo haki juu ya wazazi wao kwa ajili ya matunzo hadi wafikiapo umri wa kujitegemea.”16 kazi ya kukimu mahitaji ya kila siku ni kazi iliyotakaswa. Kuisaidia familia yako, ingawa inahitaji muda mbali na familia yako, ni sambamba na ubaba—ni sehemu ya kuwa baba mwema. “Kazi na familia ni maeneo yanayorandana.”17 Hili, kwa hakika, haitetei mtu anayeitupa familia yake kwa ajili ya kazi yake, kwa wakati mwingine, mtu ambaye hatajitolea anapenda kuhamisha majukumu yake kwa wengine. Katika maneno ya Mfalme Benjamini:

“Na hamtukubali watoto wenu kupatwa na njaa, au kukaa uchi; wala hatakubali kwamba wavunje sheria za Mungu, na kupigana na kutetanisha moja kwa mwingine, …

“Lakini nyinyi mtawafunza kutembea katika njia za kweli na za kiasi; mtawafunza kupendana na kutumikiana.”18

Tunatambua maumivu ya wanaume ambao hawawezi kupata njia na namna ya kuzitunza familia zao kikamilifu. Hakuna aibu kwa wale ambao katika kipindi fulani mbali na juhudi zao za nguvu hawawezi kutimiza wajibu wao na shughuli zao kama baba. “Ulemavu, kifo, au namna nyingine yoyote inaweza kulazimisha mabadiliko binafsi. Familia za mbali lazima zitoe msaada zinapohitajika.”19

Picha
Wazazi wenye upendo
Picha
Wazazi wakicheza densi

Kupenda mama wa watoto wake—na kuonyesha upendo huo—ni kati ya mambo mawili baba anaweza afanya kwa ajili ya watoto wake. Hii inatoa msisitizo na kutia nguvu ndoa kwamba ni msingi wa maisha ya familia zao na usalama wao.

Picha
Baba wana matineja

Baadhi ya wanaume ni kina baba pekee, baba walezi au kina baba wa kambo. Wengi wao wanajitahidi kufanya kadri wawezavyo kujitahidi katika jukumu ambalo wakati mwingine ni gumu. Tunaheshimu wale wote wanaojitahidi kufanya yote yanayowezekana kufanyika katika upendo, subira, na kujitolea kukimu mahitaji binafsi na ya kifamilia. Itambulike kwamba Mungu Mwenyewe alimwamini Mwanawe wa Pekee kwa Baba mlezi. Kweli baadhi ya sifa zinamwendea Yusufu kwa kweli jinsi Yesu alivyokua, “Alizidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na mwanadamu.”20

Cha kusikitisha, kutokana na kifo, kutengwa, au talaka, baadhi ya watoto hawana kina baba wanaoishi nao. Wengine wanaweza kuwa na kina baba ambao wapo tu kimwili lakini kimawazo hawapo au kwa namna nyingine hawako karibu na hawatoi msaada. Tunawaambia akina baba wote kufanya vyema na kuwa wema zaidi. Tunawaambia vyombo vyote vya habari na burudani, vionyeshe akina baba wanaojitolea na wenye uwezo ambao kwa kweli wanawapenda wake zao na kwa akili kuwaongoza watoto wao, badala ya waropokaji na wakorofi, au “watu wanaosababisha matatizo,” kama kina baba wanavyoonyeshwa kila wakati.

Kwa watoto ambao hali ya familia ina matatizo, tunawaambia, ninyi wenyewe hamjapungukiwa kwa sababu ya hilo. Changamoto mara nyingi ni ishara ya uaminifu wa Bwana ndani yenu. Anaweza kukusaidia, moja kwa moja kupitia kwa wengine, kushughulika na kile unachokumbana nacho. Unaweza kuwa kizazi, labda cha kwanza katika familia, ambapo mpangilio wa kiungu ambao Mungu ametawaza kwa ajili ya familia zetu hasa hupata muundo mzuri na kubariki vizazi vingine baada yako.

Kwa vijana, tukitambua sehemu mtakayokuwa nayo kama watoaji na walinzi, tunawaambia mjiandae sasa muwe watiifu shuleni na katika kujiandaa na mafunzo baada ya masomo baada ya shule ya upili. Elimu, iwe chuo kikuu, vyuo vya ufundi, kujifunza kwa ukufunzi, au mipango inayofanana, ni ufunguo katika kukuza ujuzi na uwezo utakaouhitaji. Tumia nafasi ya fursa ya kujihusisha na watu wa rika zote, ukijimuisha watoto, na jifunze jinsi ya kuanzisha mahusiano mema na yenye thamani. Hiyo inamaanisha kuongea uso kwa uso na watu na wakati mwingine kufanya mambo pamoja, siyo tu kupevusha ujuzi wako wa kutuma ujumbe mfupi. Ishi maisha yako ili kwamba kama mwanaume utaleta usafi katika ndoa yako na kwa watoto wako.

Kwa vizazi vyote vinavyoinukia, tunawaambia, unapompima baba yako katika kipimo cha mzuri—bora—bora zaidi (na ninatumaini kuwa kipimo chako kitapanda kadri unavyokua na kuwa na hekima), weka msimamo wa kumheshimu yeye na mama yako kwa maisha yako mwenyewe. Kumbuka tamanio la matumaini ya baba limeelezewa na Yohana, “Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika ukweli.”21 Haki yako ni heshima kubwa baba yeyote anaweza kupokea.

Kwa kaka zangu, kina baba wa Kanisa hili, ninasema, ninajua mnatamani kuwa mgekuwa kina baba wakamilifu zaidi. Ninajua ninatamani ningekuwa. Hata hivyo, mbali na udhaifu wetu tuendelee mbele. Na tuweke pembeni wazo lililokuzwa la ubinafsi na utawala wa tamaduni ya leo na kufikiria kwanza upendo na maisha mema ya wengine. Hakika mbali na mapungufu yetu, baba yetu wa Mbinguni atatukuza na kusababisha juhudi zetu kuzaa matunda. Ninafurahishwa na hadithi iliyotokea katika gazeti la New Era miaka michache iliyopita. Mwandishi alinukuu yafuatayo:

“Nilipokuwa mdogo, familia yetu ndogo iliishi katika nyumba ya chumba kimoja katika ghorofa ya pili. Nililala kwenye kochi sebuleni. …

“Baba yangu, mfuaji wa vyuma, aliondoka nyumbani asubuhi na mapema kwenda kazini kila siku. Kila asubuhi alikuwa … akinifunika blangeti na kusimama kwa dakika. Nilikuwa nusu kuota nilipohisi baba yangu amesimama pembeni ya kochi langu, akinitazama. Nilipoamka taratibu, nilijawa na aibu kumuona pale. Nilijaribu kujifanya kama bado nimelala. … nikatambua kwamba alipokuwa amesimama pembeni mwa kitanda changu alikuwa anasali kwa mkazo wote, nguvu, na mtazamo—kwa ajili yangu.

“Kila asubuhi baba yangu aliniombea. Aliniombea kwamba niweze kuwa na siku nzuri, kwamba niwe salama, kwamba niweze kujifunza na kujiandaa kwa ajili ya maisha ya baadaye. Na kwa sababu hakuweza kuwa na mimi mpaka jioni, aliwaombea walimu wangu na marafiki zangu ambao ningekuwa nao siku hiyo. …

“Mwanzoni, sikuelewa hata kile baba alikuwa akikifanya asubuhi hizo aliponiombea. Lakini kila nilipokuwa mkubwa, nikitambua upendo na shauku aliyokuwa nayo kwangu katika kila kitu nilichokuwa nikifanya. Hiyo ni moja kati ya kumbukumbu zangu nzuri. Haikuwa mpaka miaka michache baadaye, baada ya kuoa, kuwa na watoto wangu mwenyewe, na ningeingia kwenye chumba chao walipokuwa wamelala na kuwaombea kwamba ninaelewa vipi baba alivyokuwa ananiwazia.”22

Alma alishuhudia kwa mtoto wake wa kiume:

“Tazama, nakwambia, kwamba ni yeye kwa kweli atakayekuja … ; ndio, anakuja kutangaza habari njema ya wokovu kwa watu wake.

“Na sasa, mwana wangu, hii ndio huduma ambayo uliitiwa, kutangaza hizi habari njema kwa watu hawa, kutayarisha akili zao; kwa usahihi zaidi afadhali kwamba wokovu uwajie, kwamba watayarishe akili za watoto wao kusikiliza neno wakati wa kuja kwake.”23

Hiyo ndio kazi ya akina baba leo hii. Mungu awabariki na kuwawezesha, katika jina la Yesu Kristo, amina.