2010–2019
“Nilikuwa Mgeni”
Aprili 2016


“Nilikuwa Mgeni”

Kwa maombi amua kile utafanya—kulingana na wakati wako na hali yako mwenyewe—kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji katika jamii yako.

Katika ile siku ambayo Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ulianzishwa, Emma Smith alitamka: “Sisi tutafanya kitu cha ajabu sana. … Sisi tunatarajia nafasi zisizo za kawaida na miito mizito.”1 Hiyo miito mizito na nafasi zisizo za kawaida zilijitokeza mara kwa mara wakati huo—kama inavyofanyika sasa.

Moja ilijitokeza wakati wa Mkutano Mkuu wa 1856 Rais Brigham Young alipoutangazia mkutano kwamba waasisi wakiwa na mikokoteni walikuwa wamekwama huko umbali wa mamia ya maili. Alitangaza: “Imani yenu, dini, kazi yenu ya dini, katu haitaokoa hata nafsi moja kati yenu katika ufalme wa selestia wa Mungu wetu, pasipo ninyi kutekeleza kanuni kama hizi ninazokufundisheni hivi sasa. Enendeni mkawaleteni wale watu walio nyandani sasa, na mkavishughulikie vitu ambayo tunaviita vya muda, … kinyume na hivyo imani yenu itakuwa bure.”2

Tunawakumbuka kwa shukrani za ajabu wanaume ambao walifanya safari kwenda kuwaokoa wale Watakatifu waliokuwa wanateseka. Basi kina dada walifanya nini?

“Dada [Lucy Meserve] Smith aliandika … kwamba baada ya kushawishiwa na Rais Young, wale walikuwepo walichukua hatua. … Wanawake ‘[walitoa] gagulo [kamisi kubwa ambazo zilikuwa sehemu ya mtindo wa siku hizo na ambazo zilipasa joto], stokingi, na kila kitu ambacho wangetoa, hapo hapo katika tabanekulo la zamani, na wakaviweka kwenye magari ya kukokotwa hadi kwa Watakatifu huko milimani.’”3

Wiki kadhaa baadaye. Rais Brigham Young aliwakusanya Watakatifu tena kwenye Tabanekulo wakati waokoaji na makundi ya mikokoteni walipokuwa wanakaribia kufika Jijini Salt Lake. Kwa msisitizo mkubwa, aliwasihi Watakatifu—hasa kina dada—kuwauguza waathiriwa, na kuwalisha, na kuwapokea, akisema: “Baadhi mtakuta miguu yao imeganda hata kwenye visigino vyao; baadhi wameganda hadi kwenye magoti na wengine wameganda katika mikono yao. … Tunataka mwapokee wao kama watoto wenu wenyewe, na muwe na hisia hizo kwao.”4

Lucy Meserve Smith pia aliandika:

“Tulifanya yote tuliyoweza, kwa msaada wa ndugu na akina dada wema, tuliwafariji wenye shida. … Walikuwa wameganda vibaya miguu na mikono yao. … Hatukusita katika juhudi zetu mpaka wote walipopata faraja. …

“Kamwe sijawahi kuridhika sana, na, naweza kusema, sijawahi kujisikia mwenye furaha katika kazi yoyote niliyopata kufanya katika maisha yangu, kama hisia za umoja zilizokuwepo wakati huo. …

Ni kitu gani kinachoweza kishinda mikono yenye hiari?”5

Dada zangu wapendwa, tukio hili linaweza kulinganishwa na siku zetu na wale wanaoteseka ulimwenguni kote. Jingine ni ”tukio lisilo la kawaida” ambalo hugusa mioyo yetu.

Picha
Mahema katika kambi ya wakimbizi
Picha
Watoto katika kambi ya wakimbizi
Picha
Mwanamke katika kambi ya wakimbizi
Picha
Familia katika kambi ya wakimbizi
Picha
Mfanyikazi wa msaada akizungukwa na watoto katika kambi ya wakimbizi
Picha
Kuisalimu familia ya wakimbizi
Picha
Mfanyikazi wa msaada akimkumbatia mkimbizi

“Kuna zaidi ya wakimbizi milioni 60 ikijumuisha watu waliofurushwa ulimwenguni kote. Nusu yao ni watoto6 “Hawa watu wamepitia shida kubwa mno na wanaanza maisha upya katika … nchi na tamaduni mpya. Hali kuna mashirika [wakati mwigine] ambayo uwasaidia na sehemu za kuishi na mahitaji ya msingi, kile wanachohitaji ni rafiki na mwandani ambaye anaweza kuwasaidia kujifunza lugha, kuelewa mifumo, na kuhisi kukubalika.”7

Picha
Yvette Bugingo

Majira ya joto yaliyopita nilikutana na Dada Yvette Bugingo, ambaye akiwa wa umri wa miaka 11, alitoroka kutoka sehemu moja hadi nyingine baada ya baba yake kuuawa na kaka zake watatu kupotea katika sehemu fulani ya vita hapa duniani. Yvette na wanafamilia waliobakia hatimaye waliishi kwa miaka sita na nusu kama wakimbizi katika nchi jirani mpaka walipoweza kuhamia katika nyumba ya kudumu ambapo walibarikiwa kuwa na wenzi ambao waliwasaidia kwa usafiri, shule, na vitu vingine. Yeye alisema, walikuwa kimsingi jibu la maombi yetu.”8 Mama yake mrembo na kipenzi dada mdogo wapo hapa pamoja nasi katika kwaya. Nimeshangaa mara nyingi tangu nikutane wanawake hawa warembo, “Kama hadithi yao ingekuwa hadithi yangu?

Kama kina dada, sisi tunajumuisha karibu nusu ya ghala la Bwana la kusaidia watoto wa Baba wa Mbinguni. Ghala Lake halijumuishi tu bidhaa bali pia muda, talanta, maarifa, na asili yetu takatifu. Dada Rosemary M. Wixom amefundisha, “Uhalisi wa uungu upo ndani yetu kuwasha hamu yetu ya kuwafikia wengine na kutusukuma tutende.”9

Akitambua uhasili wa uungu wetu, Rais Russell M. Nelson alielezea:

“Tunahitaji wanawake ambao wanajua jinsi ya kufanya vitu muhimu vitendeke kwa imani yao na ambao ni watetezi jasiri wa maadili na familia katika dunia iliyozangaa dhambi … ; wanawake ambao wanajua jinsi ya kuita nguvu za mbinguni ili kulinda na kuimarisha watoto na familia. …

“… Walioolewa na wasioolewa, nyinyi akina dada mna uwezo tofauti na uwezo wa kipekee kuhisi kitu haraka ambao mmepokea kama zawadi kutoka kwa Mungu. Sisi ndugu hatuwezi kunakili ushawishi wenu wa ajabu.”10

Barua ya Urais wa Kwanza aliyotumwa kwa Kanisa mnamo Oktoba 27, 2015, inaelezea wasi wasi mkubwa na huruma kwa mamilioni ya watu ambao wanatoroka nyumba zao kutafuta faraja kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na dhiki zingine. Urais wa Kwanza unamwalika kila mtu, familia, na vitengo vya Kanisa kushiriki katika huduma ya kama Kristo katika miradi ya kuwasaidia wakimbizi, na kuchangia katika mfuko wa fadhila wa Kanisa, inapowezekana.

Urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Wasichana, na Msingi umezingatia jinsi ya kujibu mwito wa Urais wa Kwanza. Tunajua kwamba ninyi, dada zetu wapendwa wa rika zote, mnatoka katika matabaka yote na huishi katika hali mbali mbali. Kila mshiriki wa huu udada wa Watakatifu wa ulimwenguni kote alifanya agano katika ubatizo la “kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa.”11 Hali sharti tukumbuke hakuna yeyote kati yetu anayepaswa kukimbia kushinda nguvu tulizonazo.12

Tukiwa na kweli hizi akilini, tumeanzisha juhudi za msaada zinazoitwa “I Was a Stranger.” Kwa maombi amua kile utafanya—kulingana na wakati wako na hali yako mwenyewe—kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji katika jamii yako. Hii ni fursa ya kumhudumia mtu mmoja mmoja, katika familia, na kwa kikundi ili kufanya urafiki, unasihi, na huduma zingine za kama Kristo na ni mojawapo ya njia nyingi ambazo kwazo kina dada wanaweza kuhudumu.

Katika juhudi zetu zote za maombi, tunapaswa kutumia ushauri wa hekima wa Mfalme Benyamini, uliotolewa kwa watu wake baada ya kuwasihi wao wawatunze wale walio na shida: “Na mhakikishe kwamba vitu hivi vyote vinafanywa kwa hekima na mpango.”13

Kina dada, tunajua kwamba kuwafikia wengine kwa upendo ni muhimu kwa Bwana. Fikiria maonyo ya kimaandiko:

“Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako.”14

“Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”15

Na Mwokozi Mwenyewe alisema:

“Kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; Nalikuwa na kiu, mkaninywesha; Nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

“Nalikuwa uchi, mkanivika: Nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama.”16

Picha
Sarafu za Mjane

Mwokozi kwa upendo alimtambua mjane ambaye alikuwa amechanga senti mbili tu kwa sababu alifanya kile ambacho angeweza kufanya.17 Yeye pia aliwaambia methali ya Msamaria Mwema—ambayo Yeye alihitimisha kwa kauli “Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.”18 Wakati mwingine kufikia watu si jambo rahisi. Lakini tunapofanya kazi pamoja kwa upendo na umoja, tunaweza kutarajia msaada wa mbinguni.

Katika ibada ya mazishi ya binti ya Mungu wa ajabu, mtu fulani alisimulia kwamba dada huyu, kama rais wa kigingi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alifanya kazi na wengine katika kigingi chao ili kuchanga mafarishi ya kuwapa joto watu waliokuwa wanateseka huko Kosovo miaka ya 1990. Kama Msamaria mwema, alifanya juu chini wakati yeye na binti yake walipoendesha gari ya mizigo lililojaa mafarishi hayo kutoka London hadi Kosovo. Njiani akirudi nyumbani, alipokea mnong’ono wa kiroho ambao ulizama kwa kina katika moyo wake. Mnong’ono ulikuwa namna hii: “Kile ulichofanya ni kitu kizuri sana. Sasa nenda nyumbani, tembea mtaani, na ukamhudumie jirani yako!”19

Mazishi haya yalijawa na matukio zaidi ya kuvutia ya jinsi huyu mwanamke mwaminifu alivyotambua na kujibu miito isiyo ya kawaida na mizito—na pia matukio ya kawaida—ya yale yaliyo chini ya usimamizi wake. Kwa mfano, alifungua nyumba yake na moyo wake ili kuwasaidia vijana wakati wowote—mchana ama usiku.

Dada zangu wapendwa, tunaweza kuwa na uhakika wa msaada wa Baba wa Mbinguni tunapopiga magoti na kuomba mwongozo wa kiungu kwa ajili ya kuwabariki watoto Wake. Baba wa Mbinguni, Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu wako tayari kusaidia.

Rais Henry B. Eyring alitoa ushuhuda huu wenye nguvu kwa wanawake wa Kanisa.

“Baba wa Mbinguni husikia na hujibu maombi yenu ya imani kwa mwongozo na kwa msaada wa kuvumilia katika huduma yenu Kwake.

“Roho Mtakatifu hutumwa kwenu na kwa wale mnaowatunza. Mtaimarishwa na kupata maongozi kujua ufinyu na kiwango cha uwezo wenu wa kuhudumu. Roho atawafariji wakati ninyi mnaposhangaa, ‘Je, nimefanya vya kutosha?’”20

Tunapofikiria hii “miito mizito” ya wale tunaohitaji kusaidia, acha tujiulize, “Kama hadithi yao ingekuwa hadithi yangu? Basi na tutafute maongozi, tukitenda juu ya misukumo tunayopokea, na kufikia kwa umoja ili kuwasaidia wale walio na shida kadiri tunavyoweza na kupata maongozi kufanya hivyo. Labda basi inaweza kusemwa juu yetu, kama Mwokozi alivyosema kuhusu dada mwenye upendo aliyemhudumia: “Ametenda kazi njema. … Ametenda alivyoweza.”21 Mimi nasema hayo ni maajabu! Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Emma Smith, in Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 14.

  2. Brigham Young, in Daughters in My Kingdom, 36.

  3. Daughters in My Kingdom, 36–37.

  4. Brigham Young, katika James E. Faust, “Go Bring Them in from the Plains,” Liahona, Nov. 1997, 7; ona pia LeRoy R. and Ann W. Hafen, Handcarts to Zion: The Story of a Unique Western Migration 1856–1860 (1960), 139.

  5. Lucy Meserve Smith, katika Jill Mulvay Derr and others, eds., The First Fifty Years of Relief Society: Key Documents in Latter-day Saint Women’s History (2016), 217, 218, herufi na vituo vimesawazishwa; ona pia Daughters in My Kingdom, 37.

  6. Ona “Facts and Figures about Refugees,” unhcr.org.uk/about-us/key-facts-and-figures.html.

  7. 40 Ways to Help Refugees in Your Community,” Sept. 9, 2015, mormonchannel.org.

  8. Barua e- kutoka kwa Yvette Bugingo, Mar. 12, 2016.

  9. Rosemary M. Wixom, “Discovering the Divinity Within,”Liahona, Nov. 2015, 8. Emily Woodmansee, mmoja wa wale waliookolewa katika mwaka wa 1856 katika kundi la mkokoteni la Willie, alielezea asili takatifu kwa njia hii (kwa mabadiliko kidogo katika upande wangu):

    Kazi ya malaika huaptiwa wanawake;

    Na hii ni karama ambayo, kama kina dada, tunaweza kudai:

    Kufanya kile tunaweza kufanya ni upole na [Kama Kristo],

    Kufariji na kubariki katika jina la [Mwokozi],. (“As Sisters in Zion,” Hymns, no. 309)

  10. Russell M. Nelson, “A Plea to My Sisters,”Liahona, Nov. 2015, 96, 97.

  11. Mosia 18:9.

  12. Ona Mosia 4:27.

  13. Mosia 4:27.

  14. Mambo ya Walawi 19:34.

  15. Waebrania 13:2.

  16. Mathayo 25:35–36.

  17. Ona Luka 21:1–4.

  18. Luka 10:37.

  19. Ibada ya mazishi ya Rosemary Curtis Neider, Jan. 2015.

  20. Henry B. Eyring, “The Caregiver,”Liahona, Nov. 2012, 124.

  21. Marko 14:6, 8.