2010–2019
Kwa Sifa za Wale Wanaookoa
Aprili 2016


Kwa Sifa za Wale Wanaookoa

Na mnapoigiza upendo wa Mwokozi, kwa hakika Yeye atabariki na kufanikisha juhudi zenu za haki kuokoa ndoa zenu na kuimarisha familia zenu.

Miaka kadha iliyopita, nilikuwa katika Hekalu la Frankfrurt Ujerumani wakati nilipoona wanandoa wawili wazee wameshikana mikono. Kutunzana kwa upendo na huba walioonyeshana kulifurahisha moyo wangu.

Sina hakika kikamilifu kwa nini mandhari haya yalinigusa kwa ndani sana. Pengine ilikuwa kuvutiwa na upendo watu hawa wawili walishiriki kati yao—ishara ya kuvutia sana ya uvumilivu na msimamo. Ilikuwa wazi kwamba wanandoa hawa wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na upendo kati yao umekuwa wa kina kwa miaka mingi.

Jamii ya Kutupa

Nafikiri sababu ingine mandhari haya ororo yamekaa nami kwa muda mrefu ni tofauti inayoleta kwa baadhi ya fikra za siku hizi. Katika jamii nyingi ulimwenguni kote, kila kitu chaonekana cha kutupwa. Mara kitu fulani kinapoanza kuharibika au kuchakaa—au hata wakati kwa kawaida tumekichoka—tunakitupa nje na kukibadilisha na cha kisasa, kitu fulani kipya, chenye mg’aro, kizuri zaidi.

Tunafanya hivi na simu za vigajani, nguo, magari, kazi—na, kwa huzuni, hata mahusiano.

Wakati kunaweza kuwa na manufaa katika kutokuparaganyika kwa maisha yetu kwa vitu vya kutengenezwa tusivyovihitaji tena, inapokuja kwa vitu vya umuhimu wa milele—ndoa zetu, familia zetu, na dhamani yetu—mawazo tuliyopanga ya kubadilisha vya kale kwa kupendelea vipya inaweza kuleta majuto makubwa.

Ninashukuru kwamba mimi ni wa kanisa ambalo linadhamini ndoa na familia. Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanajulikana ulimwenguni kote kwa kudumumisha baadhi ya ndoa na familia mzuri sana mnazoweza kuzipata. Naamini hii ni kwa sababu, kwa kiasi fulani, kwa ajili ya kweli ya thamani iliyorejeshwa kupitia Joseph Smith kwamba ndoa ilikusudiwa kuwa ya milele. Familia hazipo tu kama mipango ya kuishi kiurashisi kufanya mambo kwenda kiulaini hapa dunuani, kutupwa wakati tutapokwenda mbinguni. Bali, ni utaratibu wa mbinguni. Ni mwangwi wa mpangilio wa selestia na muigo wa familia ya milele ya Mungu.

Lakini ndoa imara na mahusiano ya kifamilia hayatokei, kwa sababu tu sisi ni waumini wa Kanisa. Inahitaji siku zote, kazi za makusudi. Kanuni za familia za milele lazima zitupatie maongozi tutoe juhudi zetu za dhati kuokoa na kustawisha ndoa zetu na familia zetu. Ninapendezwa na kuwashangilia hao waliolinda na kurutubisha haya mahusiano muhimu ya milele.

Leo, nataka kuzungumza kwa kuwasifia wale wanaookoa.

Kuokoa Ndoa Zetu

Kwa miaka nimefanya ibada za kufunganisha kwa wengi wenye matumaini na wana ndoa vijana wanaopendana. Sijakutana asilani na yoyote ambaye, wakati walipotazamana kwenye madhabahu, walifikiri wataishia kuachana au kuvunjika moyo.

Kwa bahati mbaya, zingine huvunjika.

Kwa namna fulani, baada ya muda, wakati siku zinapozidi na rangi ya njozi za mapenzi na upendo zinabadilika, wako baadhi ambao polepole wanaacha kufikiria furaha ya mwenzie na kuanza kuona nyufa ndogo ndogo. Katika mazingira kama haya, baadhi wanashawishika na majonzi ya huzuni kwamba wake zao sio watanashati vya kutosha, wazuri vya kutosha, wacheshi vya kutosha, au vijana vya kutosha. Na kwa namna fulani wanapata wazo kwamba hii inawapa kujisadikisha kuanza kutazama kungine.

Ndugu, kama hii inakaribia kukuelezea wewe kwa vyovyote, ninakuonya kwamba uko kwenye barabara ambayo inaelekea kwenye kuvunjika ndoa, kuvunjika nyumba, na mioyo iliyovunjika. Ninawasihi muache sasa hivi, mgeuke, na kurudi kwenye njia salama ya uadilifu na uaminifu kwa maagano. Na, kwa vyovyote, kanuni hizi hizi zinahusu dada zetu wapendwa.

Sasa, wacha niseme kwa wale ndugu zetu maseja ambao wanafuata udanganyifu kwamba kwanza budi watafute “mwanamke mkamilifu” kabla hawajaanza kuingia katika mazungumzo ya dhati ya miadi au ndoa

Ndugu zangu wapendwa, naomba niwakumbusheni, kama pangekuwa na mwanamke mkamilifu, kwa kweli unafikiri angevutiwa na wewe kiasi hicho?

Katika mpango wa Mungu wa furaha, kwa kiasi kikubwa hatuangalii mtu fulani mkamilifu, lakini mtu ambaye, kupitia maisha yote, tunaweza kuunganisha juhudi kutengeneza, mahusiano kamili zaidi ya upendo, na ya kudumu. Hilo ndilo lengo.

Wale wanaookoa ndoa zao wanaelewa kwamba shughuli hizi huchukua muda, uvumilivu, na zaidi ya yote, baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo. Huhitaji wewe uwe mkarimu, bila wivu, usitafute vyako mwenyewe, usikasirike upesi, usifikirie uovu, na ufurahie katika kweli. Kwa maneno mengine, huhitaji upendo, upendo wa kweli wa Kristo.1

Haya yote hayatatokea tu mara moja. Ndoa kubwa zimejengwa tofali kwa tofali, siku baada ya siku, maisha yote.

Na hiyo ndiyo habari mzuri.

Kwa sababu haijalishi jinsi gani ni tambarare (au hata iliyobonyea) mahusiano yetu yanaweza kuwa kwa sasa, kama tutaendelea kuongeza changarawe za upole, huruma, kusikiliza, dhabihu, kuelewa, na kutojijali, hatimaye piramidi yenye nguvu itaanza kukua.

Inaonekana kuchukua milele, kumbuka: ndoa zenye furaha zinakusidiwa kudumu milele! Kwa hiyo “msiwe na wasiwasi katika kufanya mema, kwani mnaweka msingi wa [ndoa] kubwa. Na kutoka kwenye vitu vidogo hutokea kile kilicho kikubwa,”2

Inaweza kuwa kazi ya polepole, lakini haihitaji kuwa ya kuchosha. Kwa kweli, katika udhubutu wa kuanzisha yaliyodhahiri, naomba kufuatilia kwamba talaka inatokea kwa nadra wakati mume na mke wana furaha?

Kwa hiyo furahia!

Na kisha, mshangaze mkeo kwa kufanya vitu ambavyo vitamfanya afurahi.

Wale ambao wanaokoa ndoa zao walichagua furaha. Wakati ni kweli kwamba baadhi ya aina ya mfadhaiko wa kudumu unahitaji matibabu ya kipekee, ninapenda sehemu hii ya busara, inayofikiriwa ni ya Abraham Lincon. “Karibu watu wote wako ilmradi kama wenye furaha wanapofanya akili zao ziwe hivyo.” Inaendana na mwenzi wake kimaandiko: “Tafuta, na utapata.”3

Kama tunatafuta mapungufu katika wake zetu au usumbufu katika ndoa yetu, kwa hakika tutavipata, kwa sababu kila mmoja ana kiasi. Kwa upande mwingine, kama tunatafuta kilicho kizuri, kwa hakika, tutakipata, kwa sababu kila mmoja ana sifa mzuri nyingi.

Wale wanaookoa ndoa wanang’oa magugu na kunyunyiza maua maji. Wanasherehekea vitendo vidogo vya huruma ambavyo vinaanzisha cheche laini za upendo. Wale wanaookoa ndoa wanaokoa vizazi vijavyo.

Kumbuka kwa nini ulimpenda.

Fanya kazi kila siku kufanya ndoa yako kuwa imara na ya furaha.

Rafiki zangu wapendwa, wacha tufanye kila kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wetu tuhesabiwe miongoni mwa wale walio wekwa wakfu na nafsi zenye furaha wanaookoa ndoa zao.

Kuokoa Familia Zetu

Leo pia napenda kuzungumza kwa kusifia wale wanaookoa mahusiano yao pamoja na familia zao. Kila familia inahitaji kuokolewa.

Kwa maajabu kama ilivyo kwamba Kanisa hili linajulikana kwa familia zake imara, tunaweza kila mara kuhisi hii inahusu kila familia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho isipokuwa yetu. Lakini ukweli ni kwamba hakuna familia kamilifu.

Kila familia ina wakati wake mgumu.

Kama, wakati wazazi wako wanakuomba kuchukuwa “selfii” yao, au wakati shangazi yako mkubwa anasisitiza kwamba wewe bado mseja kwa sababu wewe ni mchaguzi sana, au wakati shemeji yako mwenye kushikilia maoni yake anafikiria wazo lake la kisiasa ni wazo la injili, au wakati baba yako anapanga picha ya familia pamoja na kila mmoja amevaa kama waigizaji katika sinema yake anayoipenda.

Na unapata vazi la Chewbacca.

Familia ziko hivyo.

Tunaweza kuwa na jenimoja, lakini hatuko sawa. Sisi ni roho za kipekee. Tumeathiriwa katika njia tofauti na uzoefu wetu. Na kila mmoja wetu matokeo yake huishia tofauti.

Badala ya kujaribu kulazimisha kila mtu kwenye umbile letu tuliloliumba wenyewe, tunaweza kuchagua kusherehekea tofauti hizi na kuzifurahia kwa kuongeza utajiri na mshangao daima kwa maisha yetu.

Wakati mwingine, hata hivyo, wanafamilia zetu hufanya chaguo au vitu ambavyo ni bure, vinahudhi, au viovu. Tufanye nini katika hali kama hizi?

Hakuna suluhisho moja ambalo linatosheleza kila hali. Hao wanaookoa familia zao wamefanikiwa kwa sababu wanashauriana na wake zao, hutafuta mapenzi ya Bwana, na kusikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu. Wanajua kile kilicho sawa kwa familia moja kinaweza kisiwe sawa kwa ingine.

Kuna kitu kimoja tunaweza kufanya, hata hivyo, hicho ni sawa katika kila jambo.

Katika Kitabu cha Mormoni tunajifunza juu ya watu waliogundua siri ya furaha. Kwa vizazi, “hapakuwa na mabishano. … Na kwa hakika pasingekuwa na watu wasio na furaha miongoni mwa watu wote walioumbwa na mkono wa Mungu.” Walifanyaje? “Kwa sababu ya upendo wa Mungu ambao ulikuwa ndani ya mioyo ya watu.”4

Matatizo yoyote familia yako inakabiliana nayo, chochote ambacho huna budi ufanye kutafutia jibu, mwanzo na mwisho wa jibu ni upendo, upendo safi wa Kristo. Bila upendo huu, hata familia zinazoonekana kwa nje ni kamili zina shida. Kwa upendo huu, hata familia zenye changamoto kubwa zinafanikiwa.

“Upendo Haupungui Neno.”5

Ni kweli juu ya kuokoa ndoa! Ni kweli juu ya kuokoa familia!

Weka Kiburi Pembeni

Adui mkubwa wa upendo ni kiburi. Kiburi ni moja wapo ya sababu kubwa ndoa na familia kuhangaika. Kiburi kina hasira za haraka, hakina huruma, na kina wivu. Kiburi kinakuza nguvu zake na hakijali wema wa wengine. Kiburi ni uchoyo na rahisi kukasirishwa. Kiburi kinasadiki kudhamiria maovu ambapo hayapo na kinaficha udhaifu wake nyuma visingizio vya kijanja. Kiburi ni beuzi, hakina rajua, kina hasira, na hakina subira. Hakika, hisani ni upendo safi wa Kristo, kwa hiyo kiburi ni ufafanuzi wa tabia ya Shetani.

Kiburi kinaweza kuwa ushinde wa kawaida wa binadamu. Lakini sio sehemu ya urithi wetu wa kiroho, na hakina mahali miongoni mwa wenye ukuhani wa Mungu.

Ndugu maisha ni mafupi. Majuto yanaweza kudumu muda mrefu—baadhi yatakuwa na athari ambazo zinapiga mwangwi milele yote.

Jinsi unayomtendea mkeo au watoto wako, au wazazi au ndugu inaweza kushawishi vizazi vijavyo. Unataka kuacha uridhi gani kwa vizazi vijavyo? Wa ukali, kisasi, hasira, hofu, au kubaguliwa? Au wa upendo, unyenyekevu, msamaha, huruma, na ukuaji wa kiroho na umoja?

Sisi wote tunahitaji kukumbuka kwamba “Hukumu ni bila huruma kwa yule asiyeonesha huruma.”6

Tafadhali, kwa ajili ya mahusiano yenu, kwa ajili ya roho zenu, muwe wenye huruma, kwani “huruma hushinda hukumu.” 7

Weka kiburi pembeni.

Kuomba msamaha kwa watoto wako, mkeo, familia yako, au marafiki zako sio ishara ya udhaifu bali ni nguvu. Je, kuwa mwadilifu ni muhimu zaidi kuliko kulea mazingira ya malezi, kuponya, na upendo?

Jenga madaraja, usiyaharibu.

Hata wakati hauna makosa—pengine hususani wakati huna makosa—wacha upendo ushinde kiburi.

Kama utafanya hivi, matatizo yoyote unayokabiliana nayo, yatapita, kwa sababu ya upendo wa Mungu katika mioyo yenu, mabishano yatafifia. Kanuni hizi za kuokoa familia zinatuhusu sisi wote, bila kujali kama tumeoa, tumetalakiana, wajane, au mseja. Sisi wote tunaweza kuwa waokoaji wa familia imara.

Upendo Mkubwa Sana

Ndugu, katika juhudi zetu za kuokoa ndoa zetu na familia zetu, kama ilivyo katika vitu vyote, na tufuate mfano wa Yule aliyetuokoa. Mwokozi wetu alishinda “roho zetu kwa upendo.”8 Yesu Kristo ni Bwana wetu. Kazi yake ni Kazi yetu Ni kazi ya wokovu, na inaanzia majumbani mwetu.

Upendo mkuu zaidi katika mfumo wa wokovu ni kutokuwa na choyo na hutafuta hali mzuri kwa wengine. Huo ndio upendo wa Baba wa mbinguni alionao juu yetu.

Na mnapoigiza upendo wa Mwokozi, kwa hakika atabariki na kufanikisha juhudi zenu za haki kuokoa ndoa zenu na kuimarisha familia zenu.

Na Bwana awabariki katika juhudi zenu bila kuchoka na za haki mjumuishwe miongoni mwa wale wanaookoa. Haya ndiyo maombi yangu katika jina la Yesu Kristo, amina.