2010–2019
Roho Mtakatifu
Aprili 2016


Roho Mtakatifu

Ninadhihirisha upendo wangu na shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa karama ya Roho Mtakatifu, kupitia kwake anaonyesha mapenzi Yake na kutuhimili.

Wapendwa ndugu na dada zangu, nazungumza leo kama mtumishi wa Bwana na pia kama babu mkuu. Kwenu ninyi na watoto wangu wapendwa, ninafundisha na kutoa ushuhuda usio kifani wa karama za Roho Mtakatifu.

Ninaanza na kutambua nuru ya Kristo, ambayo inatolewa kwa “kila mwanaume [na mwanamke] ambaye anakuja ulimwenguni.”1 Sisi wote tunanufaika kutoka nuru hii takatifu. Ipo “katika vyote na kupitia vitu vyote,”2 na inaturuhusu sisi kubaini jema na baya3

Lakini Roho Mtakatifu ni tofauti na Nuru ya Kristo. Yeye ni mshiriki wa tatu wa Uungu, mtu tofauti wa kiroho mwenye madaraka matakatifu, na mmoja katika azma pamoja na Baba na Mwana.4

Kama waumini wa Kanisa, tunaweza kupata uzoefu wa uenzi wa kuendelea wa Roho Mtakatifu. Kupitia ukuhani wa Mungu iliorejeshwa, tumebatizwa kwa kuzamishwa kwa ondoleo la dhambi zetu na kisha kuthibitishwa kama waumini wa Kanisa. Katika ibada hii tunapatiwa karama za Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono na wenye ukuhani.5 Baada ya hapo, tunaweza kupokea na kubakiza uenzi wa Roho Mtakatifu daima kwa kumkumbuka Mwokozi, kutii amri Zake, kutubu dhambi zetu, na kwa kustahili kupokea sakramenti siku ya Sabato.

Roho Mtakatifu anatoa ufunuo binafsi kutusaidia kufanya maamuzi makubwa ya maisha kuhusu mambo kama elimu, misheni, kazi, ndoa, watoto, wapi tutaishi na familia zetu, na kadhalika. Katika mambo haya, Baba wa Mbinguni anatutegemea sisi kutumia uhuru wetu wa kujiamulia, tuichunguze hali ilivyo katika mawazo yetu kufuatana na kanuni za injili, na kulete uamuzi Kwake katika sala.

Ufunuo binafsi ni muhimu, lakini ni sehemu moja tu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kama maandiko yanavyoshuhudia, Roho Mtakatifu pia anashuhudia juu ya Mwokozi.6 Anatufundisha “utulivu wa mambo ya ufalme”7 na kutusababishia sisi “kujawa na matumaini.”8 Yeye “anatuelekeza [sisi] kufanya mema … [Na] kuhukumu kwa haki.”9 Yeye hutoa “Kwa kila mwanaume [na mwanamke]… Karama [ya kiroho] … ili wote waweze kufaidika nayo.”10 Yeye “anatupa [sisi] elimu”11 na “kuvileta … vitu vyote kwenye kumbukumbu [zetu].”12 Kupitia Roho Mtakatifu, sisi “tunaweza kutakaswa”13 na kupokea “msamaha wa dhambi [zetu].14 Yeye ni “Mfariji,” yule yule ambaye “alihaidiwa kwa wanafunzi wa [Mwokozi] .”15

Nawakumbusha sisi wote kwamba Roho Mtakatifu hatolewi kutudhibiti. Baadhi yetu bila busara hutafuta maelekezo ya Roho Mtakatifu kwa maamuzi madogo sana katika maisha yetu. Hii inapuuza jukumu Lake takatifu. Roho Mtakatifu anaheshimu kanuni ya uhuru wa kujiamulia. Huzungumza kwenye akili zetu na mioyo yetu kwa upole kuhusu mambo muhimu.16

Kila mmoja wetu anaweza kuhisi mvuto wa Roho Mtakatifu kitofauti. Msukumo wake utahisiwa katika kiasi tofauti cha ongezeko kufuatia mahitaji na hali zetu.

Katika siku hiza za mwisho, tunakiri kwamba ni nabii peke yake anaweza kupokea ufunuo kupitia Roho Mtakatifu kwa Kanisa zima. Baadhi wanasahau hili, kama Haruni na Miriamu walijaribu kumshawishi Musa akubaliane nao. Lakini Bwana aliwafundisha wao na sisi. Alisema:

“Kama kuna nabii miongoni mwenu, Mimi Bwana nitajifanya mwenyewe kujulikana kwake. …

“Pamoja naye nitazungumza mdomo kwa mdomo. “17

Wakati mwingine adui anatujaribu na mawazo ya uongo kwamba tunaweza kumchanganya na Roho Mtakatifu. Ninashuhudia kwamba uaminifu katika kutii amri na kuweka maagano yetu kutatulinda kutokana na kudanganywa. Kupitia Roho Mtakatifu, tutakuwa na uwezo wa kutambua manabii hao wa uongo wanaofundisha kwa kanuni za amri za watu.18

Tunapopokea maongozi ya Roho Mtakatifu kwa ajili yetu wenyewe, ni busara kukumbuka kwamba hatuwezi kupokea ufunuo kwa ajili ya wengine. Namjua kijana ambaye aliyemwambia msichana, “Niliota ndoto kwamba wewe utakuwa mke wangu.” Msichana alitafakari taarifa ile na kisha akajibu, “Wakati nitakapokuwa na ndoto sawa na yako, nitarudi na kuongea nawe.”

Sisi wote tunaweza kujaribiwa kuacha matamanio yetu binafsi kushinda maelekezo ya Roho Mtakatifu. Nabii Joseph Smith alimsihi Baba wa Mbinguni amruhusu kuazimisha kurasa 116 za kwanza za Kitabu cha Mormoni kwa Martin Harris. Joseph alifikiri ilikuwa wazo jema. Hapo mwanzo Roho Mtakatifu hakumpa hisia za kuthibitisha. Hatimaye Bwana alimruhusu Joseph hata hivyo kuhazima kurasa hizo. Martin Harris alizipoteza. Kwa muda, Bwana alichukuwa karama ya nabii ya kutafsiri, na Joseph alijifunza somo chungu lakini lenye thamani ambalo lilitengeneza huduma yake iliyosalia.

Roho Mtakatifu ni kitovu cha Urejesho. Kuhusu usomaji wake wa ujanani wa Yakobo1:5, Nabii Joseph Smith alisimulia, “Kamwe kifungu chochote cha maandiko hakijawahi kumwingia mtu moyoni kwa nguvu nyingi kuliko hiki kilivyofanya kwangu wakati huu.”19 Nguvu iliyoelezwa na Joseph Smith ilikuwa ni mvuto wa Roho Mtakatifu. Matokeo yake, Joseph alienda kwenye kijisitu cha miti karibu na nyumbani kwake na alipiga magoti kumwomba Mungu. Ono la kwanza ambayo lililofuata lilikuwa kwa kweli la maana sana na tukufu. Lakini njia ya kule kutembelewa ana kwa ana na Baba na Mwana kulianza na ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Ukweli uliotolewa wa injili ya urejesho ulikuja kupitia mpangilio wa kutafuta katika sala na kisha kupokea na kufuata ushawishi wa Roho Mtakatifu. Fikiria mifano hii: kutafsiri Kitabu cha Mormoni; urejesho wa ukuhani na ibada zake—kuanzia na ubatizo; na mpangilio wa Kanisa—kutaja vichache. Ninashuhudia kwamba leo, maono kutoka kwa Bwana kwenda kwa Urais wa Kwanza na wale Kumi na wawili yanakuja kulingana na mfumo mtakatifu huu huu. Huu ndiyo ule ule mfumo mtakatifu ambao huruhusu ufunuo binafsi.

Tunatoa shukrani kwa wote ambao wamemfuata Roho Mtakatifu kupokea injili ya urejesho, kuanzia na wanafamilia wake Joseph Smith. Wakati kijana Joseph Smith alipomwambia baba yake kuhusu matembezi ya Moroni, baba yake alipokea ushahidi wa uthibitisho yeye mwenyewe. Mara moja, Joseph alipumzishwa kutoka majukumu yake ya shambani na alitiwa moyo kufuata maelekezo ya malaika.

Acha sisi, kama wazazi na viongozi, tufanye viyvo hivyo. Na tuwatie moyo watoto wetu na wengine wafuate maelekezo ya Roho Mtakatifu. Kwa kufanya hivyo, na tufuate mfano wa Roho Mtakatifu sisi wenyewe, kuongoza kwa upole, unyenyekevu, huruma, uvumilivu, na upendo wa kweli.20

Roho Mtakatifu ni chombo kwa kazi ya Mungu, katika familia na Kanisa zima. Pamoja na uelewa huo, naomba nishiriki mifano michache binafsi ya Roho Mtakatifu katika maisha yangu na huduma ya Kanisa? Ninatoa kama shahidi binafsi kwamba Roho Mtakatifu anatubariki sisi wote.

Miaka mingi iliyopita, Dada Hales nami tulipanga kuwa wenyeji wa baadhi ya washirika wangu wa kazini katika chakula cha jioni maalumu nyumbani mwetu. Nilipokuwa nikirudi nyumbani kutoka ofisini, nilikuwa na wazo la kusimama nyumbani kwa mjane ambaye nilikuwa mwalimu wake wa nyumbani. Nilipogonga mlango wa dada, alisema, “Nimekuwa ninaomba kwamba wewe uje.” Wazo lile lilitoka wapi? Roho Mtakatifu.

Hapo nyuma, baada ya ugonjwa mkali, nilisimamia mkutano mkuu wa kigingi. Kulinda nguvu yangu, nilipanga kuondoka kanisani mara tu baada ya kikao cha uongozi wa ukuhani. Hata hivyo, baada ya maombi ya kufunga, Roho Mtakatifu aliniambia, “Unaenda wapi?” Nilivutiwa kusalimiana kwa mikono na kila mtu walipokuwa wanatoka chumbani. Wakati mzee kijana mmoja alipojitokeza, nilishawishiwa kumpa ujumbe maalumu: Yeye alikuwa anatazama chini, na nikangojea macho yaje juu kukutana na yangu, na niliweza kusema, “Omba kwa Baba wa Mbinguni, msikilize Roho Mtakatifu, fuata misikumo utakayopatiwa, na mambo yote yatakuwa shwari katika maisha yako.” Baadaye rais wa kigingi aliniambia kwamba kijana huyu alikuwa karudi mapema kutoka misheni yake. Rais wa kigingi akitenda kwa msukumo wa wazi alikuwa amemwahidi baba wa kijana kwamba kama angemleta mwanae kwenye mkutano wa ukuhani, Mzee Hales atazungumza naye. Kwa nini nilisimama na kusalimiana kwa mkono na kila mtu? Kwa nini nilisimama kuongea na huyu kijana maalum. Nini kilikuwa chanzo cha ushauri wangu? Ni wazi: Roho Mtakatifu.

Mapema mwaka 2005 niliongozwa kutayarisha ujumbe wa mkutano mkuu kuhusu wamisionari wenza wazee. Kufuatia mkutano mkuu, ndugu alisimulia: “Wakati tulipokuwa tunasikiliza mkutano mkuu, … mara moja Roho wa Bwana aligusa moyo wangu kwelikweli. … Ilikuwa hamna kukosea ujumbe huu kwangu na kipenzi changu. Tulikuwa twende tukahudumu misheni, na wakati ulikuwa sasa. Wakati nilipo … mwangalia mke wangu, nilitambua kwamba amepokea ushawishi ule ule kutoka kwa Roho. “21 Ni nini kilileta jibu hili kwa nguvu wakati ule ule? Roho Mtakatifu.

Kwa watoto wangu mwenyewe na wote wanaonisikiliza, ninatoa ushuhuda wangu wa ufunuo binafsi na mtiririko wa kudumu wa mwongozo wa kila silu, onyo, kutia moyo, nguvu, usafi wa roho, kufariji, na amani ambayo imekuja kwenye familia yetu kupitia Roho Mtakatifu. Kupitia Roho Mtakatifu, tulipitia “wingi wa upendo wa huruma wa [Kristo] ororo”22 na miujiza ambayo haiishi.23

Ninatoa ushuhuda wangu maalumu kwamba Mwokozi yu hai. Ninadhihirisha upendo wangu na shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa karama ya Roho Mtakatifu, kupitia kwake anaonyesha mapenzi Yake na kutuhimili. Katika jina la Yesu Kristo, amina.