2010–2019
Sehemu Takatifu ya Urejesho
Aprili 2016


Sehemu Takatifu ya Urejesho

Palmyra lilikuwa jukwaa la Urejesho, ambapo sauti ya Baba ingesikika baada ya karibu milenia mbili.

Rafiki yangu mzuri ambaye alikuwa muumini wa Kanisa alijaribu, kwa miaka mingi, kunifundisha injili ya familia za milele. Haikuwa hadi nilipohudhuria kufunguliwa kwa Hekalu la Sao Pauol mnamo Oktoba 1978, na nilipoingia katika chumba cha kuunganisha, ndipo mafundisho ya familia za milele yalipokuja moyoni mwangu, na kwa siku kadha niliomba nijue kama hili lilikuwa Kanisa la kweli.

Sikuwa mshika dini lakini nilikuwa nimelewa na wazazi ambao walikuwa washika dini na ambao walikuwa wameona kilichokuwa kizuri katika dini zingine. Wakati huo wa maisha yangu, nilifikiri dini zote zilikubalika kwa Mungu.

Baada ya ziara yangu ya ufunguaji wa hekalu, nilitafuta jibu, nikiwa na imani na uhakika wa matumaini kwamba Mungu angenijibu, ni lipi lilikuwa Kanisa Lake duniani.

Baada ya mfadhaiko mkuu wa kiroho, mwishowe nilipokea jibu wazi. Nilialikwa kubatizwa. Ubatizo wangu ulikuwa tarehe 31 Oktoba 1978, usiku kabla ya kikao cha kuwekwa wakfu kwa hekalu la São Paulo.

Niligundua kwamba Bwana alinijua na alinijali Yeye alipojibu maombi yangu.

Asubuhi iliyofuata, mke wangu na Mimi tulikwenda Sao Paul kuhudhuria kikao cha kuweka wakfu hekalu.

Tulikuwa pale, lakini sikujua bado kwa kweli jinsi ya kufurahia nafasi ile ya ajabu. Siku iliyofuata, tulihudhuria mkutano mkuu wa eneo.

Tulikuwa tumeanza safari yetu katika Kanisa, na tulipata marafiki wazuri ambao walitukaribisha wakati huu wa mabadiliko wa maisha.

Masomo ya waumini wapya tuliohudhuria katika mikutano yetu ya Jumapili kila wiki yalikuwa mazuri ajabu. Yalitujaza na maarifa na kutufanya tutamani kwa wiki kupita haraka ili jumapili tuweze kupata zaidi ya marutubisho ya kiroho.

Mke wangu nami kwa hamu tulitazamia kuingia hekaluni ili familia yetu iweze kuunganishwa milele. Hiyo ilifanyika mwaka mmoja na siku saba baadaye, ambao ulikuwa muda mfupi baada ya ubatizo wangu, ambao ulikuwa wakati mzuri ajabu. Nilihisi kama kwamba maisha ya milele yamegawanywa pale madhabahuni kati kile kilichotokea kabla na kile kilichotokea baada ya kuunganishwa.

Nikiwa nimeishi kihalali katika Pwani ya Mashariki ya Merikani kwa miaka michache, nilikuwa kwa kiasi fulani nimezoea baadhi ya miji, na ilikuwa kwa kawaida midogo sana.

Mara nyingi wakati niliposoma au kusikia kuhusu matukio yaliyofuatwa na Ono la Kwanza, makundi ya watu yalitajwa, ambayo hayakuwa na maana kwangu.

Maswali yalianza kuibuka akilini mwangu. Kwa nini Kanisa lilikuwa lirejeshwe nchini Merikani na sio nchini Brazil au Italia, nchi ya mababu zangu?

Makundi hayo yaliyotajwa na watu yalikuwa wapi, hao waliohusika katika msisimko na katika makanganyiko wa dini—yote hayo ambayo yalikuwa yametokea katika sehemu yenye amani na iliyotulia?

Niliwauliza watu wengi kuhusu hii lakini sikupata jibu. Nilisoma kila kitu nilichoweza kwa Kireno na kisha katika Kiingereza lakini sikupata chochote ambacho kingetuliza moyo wangu. Lakini niliendelea kutafuta.

Mnamo Oktoba 1984, nilihudhuria mkutano mkuu kama mshauri katika urais wa kigingi. Baadaye, nilikwenda Palmyra, New York nikiwa na hamu ya kupata jibu.

Kufika hapo, nilijaribu kuelewa: Kwa nini urejesho ulitakiwa uwe hapa, na kwa nini vurumai ya kiroho jinsi hii? Hawa watu waliotajwa katika usimilizi wa Joseph walitokea wapi? Kwa nini hapa?

Wakati huo, jibu la maana kwangu lilikuwa kwa sababu ya Katiba ya Marekani ilihakikisha uhuru.

Asubuhi hiyo nilitembelea jengo la Grandin, ambako toleo la kwanza la Kitabu cha Mormoni lilipigwa chapa. Kisha nilikwenda kwenye Msitu Mtakatifu, ambako nilisali sana.

Hapakuwa na mtu yeyote kwenye mitaa ya ule mji mdogo wa Palmyra. Yalikuwa wapi yale makundi ya watu ambayo Joseph alikuwa ameyataja?

Mchana ule mzuri niliamua kwenda kwenye shamba la Peter Whitmer na nilipofika kule nilimkuta mtu akiwa kwenye dirisha la kibanda. Alikuwa na jazba kali katika macho yake. Nilimwamkia kisha nikaanza kumwuliza maswali yayo hayo.

Aliniuliza,”Je, una muda?” Nikasema ndiyo.

Alielezea kwamba maziwa Erie na Ontario na, chini mashariki, Mto Hudson vilikuwa katika eneo lile.

Mapema miaka ya 1800 waliamua kujenga mfereji kwa ajili ya eundeshaji wa vyombo majini, ambavyo vingepita eneo lile, lililokuwa zaidi ya maili 300 (km 480) kufika mto wa Hudson. Ilikuwa mradi mkubwa kwa wakati ule, na wangeweza kutegemea nguvu za watu na nguvu za wanyama.

Palmyra ilikuwa kitovu cha baadhi ya ujenzi ule. Wajenzi walihitaji watu wenye ujuzi, mafundi, familia, na marafiki zao. Watu wengi walianza kuingia kutoka miji yote jirani, sehemu za mbali sana, kama vile Ireland, kuja kufanya kazi kwenye mfereji.

Huo ulikuwa wakati mfupi mtakatifu na wa kiroho kwa sababu hatimaye nimeyapata makundi. Walileta tamaduni zao na imani zao. Wakati mtu alipotaja imani yao, akili zangu ziliangazwa na macho yangu ya kiroho yalifunguliwa na Mungu.

Wakati ule mfupi, nilielewa jinsi mkono wa Mungu Baba yetu, katika busara Yake kuu, alikuwa ametayarisha katika mpango Wake kumleta kijana Joseph Smith, kumweka katikati ya vurugu zile za kidini, kwa sababu pale, katika Kilima Kumora, mabamba ya thamani ya Kitabu cha Mormoni yalifichwa.

Hili lilikuwa jukwaa la Urejesho, ambako sauti ya Baba ingesikika baada ya takribani milenia mbili, katika ono la ajabu, akizungumza na mvulana Joseph Smith, wakati alipokwenda kwenye Msitu Mtakatifu kusali na kusikia: “Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!”1

Pale aliona Viumbe wawili, ambao mng’aro na utukufu wao wapita maelezo yote. Ndio, Mungu alijionyesha Mwenyewe kwa binadamu tena. Giza lililofunika dunia likaanza kutawanyika.

Manabii ya Urejesho yalianza kutimizwa. “Na nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awahubirie hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa.”2

Katika miaka michache mifupi Joseph alielekezwa kwenye kumbukumbu za manabii, maagano, na ibada zilizoachwa na manabii wa kale, Kitabu cha Mormoni chetu kipendwa.

Kanisa la Yesu Kristo lisingeweza kurejeshwa bila injili ya milele, iliyofunuliwa katika Kitabu cha Mormoni kama ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo, hata Mwana wa Mungu, Mwana Kondoo wa Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu.

Kristo aliwaambia watu Wake huko Yerusalemu:

“Kondoo wengine ninao ambao si wa zizi hili”3

“Mimi ni mchugaji mwema, na nawajua kondoo wangu, na wao wanijua.”4

Wakati nikiondoka kutoka kwa shamba la Whitmer, sikumbuki nikisema kwaheri. Nakumbuka tu machozi yakitiririka yasiyozuilika usoni mwangu. Jua lilikuwa linazama katika wingu zuri sana.

Katika moyo wangu furaha tele na amani vilituliza nafsi yangu. Nilijawa na shukrani.

Sasa ninajua kwa uwazi kwa nini. Mara ingine tena Bwana amenipa uelewa na nuru.

Katika safari yangu kurudi nyumbani, maandiko yaliendelea kutiririka akilini mwangu: ahadi iliyofanywa kwa Baba Ibrahimu kwamba katika uzao wake familia zote za ulimwengu zitabarikiwa.5

Na kwa hili, mahekalu yatajengwa ili kwamba nguvu takatifu ziweze kutunikiwa binadamu mara nyingine tena duniani ili kwamba familia ziweze kuunganishwa, sio mpaka kifo kiwatenganishe bali kwa milele yote.

“Na itakuwa katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.”6

Kama wewe unayenisikia una maswali yoyote katika moyo wako, usikate tamaa!

Mimi nawaalika mfuate mfano wa Nabii Joseph Smith wakati aliposoma katika Yakobo 1:5, “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Kile kilichotokea Kumora kilikuwa sehemu muhimu ya Urejesho, Joseph Smith alipopokea mabamba ambayo yalikuwa na Kitabu cha Mormoni. Kitabu hiki kinatusaidia sisi kujongea karibu na Kristo kuliko kitabu kingine chochote ulimwenguni.7

Ninatoa ushuhuda wangu kwamba Bwana aliwainua manabii, waonaji, na wafunuaji kuongoza ufalme Wake katika hizi siku za mwisho na katika mpango Wake wa milele familia zinatakiwa kuwa pamoja milele. Yeye huwajali watoto Wake. Yeye hujibu maombi yao.

Kwa sababu ya upendo Wake mkuu, Yesu Kristo alipatanisha kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Juu ya haya ninashuhudia katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.