2010–2019
Kwenda Kuokoa: Tunaweza Kufanya Hivyo.
Aprili 2016


Kwenda Kuokoa: Tunaweza Kufanya Hivyo.

Bwana ametoa nyenzo zote zinazohitajika kwetu ili kwenda kuokoa marafiki wasiohudhuria kikamilifu na wasio waumini.

Mwokozi alielewa vizuri kazi Yake ya kuwaokoa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni, kwani alisema:

“Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea. …

[Kwani] haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni, kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.”1

Malaika mama yangu, Jasmine Bennion Arnold, alielewa vizuri majukumu yake ya kusaidia kuwaokoa kondoo wa Baba wa Mbinguni waliojeruhiwa au potea, wakiwemo watoto wake na wajukuu zake mwenyewe. Ni jukumu zuri kiasi gani kwa babu na bibi wanaloweza kulifanya katika maisha ya wajukuu zao.

Mama mara nyingi alipangwa kuwatembelea na kuwafundisha wale waliokuwa wakisumbuka na imani zao, wasio washiriki kamili na baadhi ya familia; hata hivyo, kundi lake lilijumuisha na wale ambao hawakupangiwa mtu wa kuwatembelea. Kwa kawaida utembeleaji wake ilikuwa sio tu mara moja kwa mwezi, akiwa akihudumia wagonjwa kimya kimya na kuwapa faraja ya upendo. Miezi kadhaa ya mwisho ya maisha yake, alibaki nyumbani, hivyo alitumia masaa mengi kuandika barua, akielezea upendo wake, akitoa ushuhuda wake, na kuwainua wale waliokuja kumtembelea.

Tunapokwenda kwenye uokoaji, Mungu hutupa nguvu, faraja, na baraka. Alipomwamuru Musa kuwaokoa wana wa Israeli, Musa aliogopa, kama wengi wetu tunavyoogopa. Musa alijitetea mwenyewe, akisema, “Mimi siyo mshawishi, … bali sina ufasaha wa kuongea, na ulimi wangu ni mzito .”2

Bwana akamhakikishia Musa:

“Ni nani aliyeumba kinywa cha mtu? … je siyo mimi Mwenyezi Mungu?

“Basi nenda, mimi nitakiongoza kinywa chako, na kukufundisha nini cha kusema.”3

Kwa matokeo, Bwana alimwambia Musa, “Unaweza kufanya hivyo!” Unajua nini, nasi tunaweza!

Acha nishiriki kanuni nne ambazo zitawasaidia katika juhudi zenu za uokoaji.

Kanuni ya 1: Hatutakiwi Kuchelewa kwenda Kuokoa

Mzee Alejandro Patania, aliyekuwa Sabini wa Eneo, anasimulia habari ya kaka mdogo wake, Daniel, ambaye alienda kwa chombo baharini kuvua na wafanyakazi wake. Baada ya muda, Daniel alipokea onyo kali kwamba dhoruba kali ilikuwa inakaribia. Kwa haraka, Daniel na wafanyakazi wake walianza safari ya kurudi bandarini.

Picha
Kuenda baharini kwa mashua

Dhoruba ilipozidi, injini ya boti la uvuvi nyuma yao iliacha kufanyakazi. Wafanyakazi wa Daniel walifunga kamba kwenye boti lililoharibika na kuanza kulivuta. Waliongea na redio kwa ajili ya msaada, wakijua kwamba, kuongezeka kwa dhoruba, walihitaji msaada wa haraka.

Picha
Dhoruba ikipamba moto

Wapendwa wao wakiwasubiri kwa hamu, wawakilishi wa ulinzi wa mwambao, chama cha wavuvi, na wanamaji walikutana kuamua mikakati ya uokoaji. Baadhi walitaka kuondoka muda huo huo lakini waliambiwa wasubiri. Wakati wale waliokuwa kwenye dhoruba waliendelea kuomba msaada, wawakilishi waliendelea kukutana, wakijaribu kukubaliana njia nzuri na mpango wa kuwaokoa.

Picha
Wapendwa wakisubiri kwa wasiwasi

Wakati kikundi cha waokoaji kilipojiandaa, simu ya mwisho ya dharura ikaja. Dhoruba kali ilikata kamba kati ya boti mbili, na wafanyakazi wa Daniel walikuwa wanaenda nyuma kuona kama wangeweza kuwaokoa wavuvi wenzao. Mwishowe, maboti yote mawili yalizama pamoja na wafanyakazi wake, akiwemo Daniel kaka ya Mzee Patania walipotea.

Picha
Mashua zote mbili zilizama

Mzee Patania alilinganisha janga hili na onyo la Bwana wakati Yeye alisema “[Hamkuwapatia] nguvu, … [au] waliotangatanga hamkuwarudisha, … [au] waliopotea hamkuwatafuta; … na nitawaondoa kondoo wangu makuchani [mwenu].”4

Mzee Patania alielezea kwamba, wakati tunapotakiwa kuratibu katika mabaraza, akidi, usaidizi, na hata kama watu binafsi, hatutakiwi kuchelewa kwenda kuokoa. Wakati mwingine wiki nyingi zinapita tunapoongea kuhusu kuzisaidia familia au watu binafsi ambao wanahitaji msaada maalumu. Tujadili kuhusu nani atawatembelea na mbinu ya kuchukua. Hali, ndugu na dada zetu wanaendelea kuhitaji na wakati mwingine hata kuita na kulilia msaada. Hatutakiwi kuchelewa.

Kanuni ya 2: Hatutakiwi Kukata Tamaa

Rais Monson, ambaye amepiga parapanda la kwenda kuokoa, alisema, “Waumini wetu wanahitaji kukumbushwa kwamba hawajachelewa sana inapokuja kwa … Waumini wasiohudhuria … ambao wangefikiriwa hawafai.”5

Kama ilivyo kwa wengi wenu, wengine ambao nimeshiriki nao injili karibu watabatizwa au kurudishwa kundini, na wengine—kama vile rafiki yangu asiye muumini Tim na mke wake asiyeshiriki, Charlene, wanachukua muda mwingi.

Kwa zaidi ya miaka 25 niliyomhusisha Tim katika maongezi ya injili na kumchukua Tim na Charlene kwenda kwenye ufunguzi wa hekalu. Wengine walijiunga kwenye uokoajii, lakini Tim alikataa kila mwaliko wa kukutana na wamisionari.

Wikiendi moja nilipangwa kusimamia kwenye mkutano wa kigingi. Nilimwomba rais wa kigingi kufunga na kusali juu ya nani tumtembelee. Nilishtuka wakati akinipa jina la rafiki yangu Tim. Wakati askofu wa Tim, rais wa kigingi, na mimi tulipogonga mlango, Tim alifungua, akaniangalia, akamwangalia askofu, na akasema, “Askofu, nilifikiri uliniambia utamleta mtu maalum!”

Kisha Tim akacheka na kusema, “Ingia ndani, Merv.” Muujiza ukatokea siku ile. Tim sasa amebatizwa, na yeye na Charlene wameunganishwa hekaluni. Hatutakiwi Kukata Tamaa

Picha
Tim na Charlene hekaluni

Kanuni ya 3: Shangwe yako itakuwa kubwa jinsi gani kama utazileta nafsi nyingi kwa Kristo.

Miaka mingi iliyopita niliongea jinsi José de Souza Marques alivyoelewa maneno ya Mwokozi kwamba “Na kama mtu yeyote miongoni mwenu akiwa imara katika Roho, na amchukue yule dhaifu pamoja naye, ili aweze … kuwa imara pia.”6

Kaka Marques aliyajua majina ya kila kondoo katika akidi ya makuhani na aligundua kwamba Fernando hakuwepo. Alimtafuta Fernando nyumbani kwake, kisha nyumbani kwa rafiki yake, na hata alikwenda ufukoni.

Picha
Kumwokoa Fernando

​Hatimaye alimpata Fernando akiwa akitereza baharini. Hakusita hadi boti lizame, kama ilivyokuwa kwenye simulizi ya Daniel. Kwa haraka akajitosa majini kumwokoa kondoo wake aliyepotea, akimleta nyumbani kwa furaha.7

Picha
Kuhakikisha kwamba Fernando ataondoka kutoka kwenye zizi

Kisha akahakikisha mwendelezo wa huduma ili Fernando asiondoke tena kundini.8

Naomba niwarejeshe juu ya nini kilichotokea tangu Fernando alipookolewa na kushiriki furaha hiyo kutokana na uokoaji wa kondoo mmoja aliyepotea. Fernando alimwoa kipenzi cha moyo wake, Maria, katika hekalu. Sasa wana watoto 5 na vijukuu 13, ambao wote wanahudhuria Kanisani. Ndugu zao wengine na familia zao nao pia wamejiunga na Kanisa. Kwa pamoja wamewakilisha maelfu ya majina ya mababu zao ili kufanyiwa ibada za hekalu, na baraka bado zinamiminika.

Picha
Familia ya Fernando

Fernando sasa anahudumu kama askofu kwa mara ya tatu, na anaendelea kuokoa. Hivi karibuni alishiriki maneno haya, “Katika kata yetu, tuna vijana 32 wanaohudhuria kikamilifu wenye Ukuhani wa Haruni, kati yao 21 waliokolewa miezi 18 iliyopita.” Kama mtu binafsi, familia, akidi, makundi saidizi, madarasa, na walimu wa nyumbani na walimu watembeleaji, tunaweza kufanya hivyo!

Picha
Wavulana wa Fernando

Kanuni ya 4: Bila Kujali Umri Wetu, Sisi Wote Tumeitwa Kwenda Kuokoa

Rais Henry B. Eyring alitangaza, “Bila kuangalia umri wetu, uwezo, wito wa Kanisani, au mahala, sisi tumeitwa kufanya kazi ya kumsaidia [Mwokozi] kwenye mavuno Yake ya nafsi hadi pale atakapokuja tena.”9

Kila siku zaidi na zaidi sana watoto wetu, vijana wetu, vijana wazima, na waumini watu wazima wa kila umri wanasikia mwito wa Mwokozi wa kuenda kuokoa. Asanteni kwa juhudi zenu! Acheni nishiriki mifano fulani.

Amy, miaka 7, alimwalika rafiki yake Arianna na familia yake kwenye programu yake ya sakramenti ya Msingi ya mwisho wa mwaka. Miezi michache baadaye, Arianna na familia yake walibatizwa.

Allan, kijana ambaye hajaoa, alihisi kushiriki video za Kanisa, Ujumbe wa Mormoni, na mistari ya maandiko na marafiki zake wote akitumia mtandao wa kijamii.

Dada Reeves alianza kushiriki injili na kila muuzaji wa kutumia simu aliyepiga simu.

James alimwalika rafiki yake Shane ambaye siyo muumini kwenye ubatizo wa binti yake.

Spencer alimtumia dada yake ambaye hakuwa mhudhuriaji kamili kiungo cha ripoti ya mkutano ya Rais Russell M. Nelson na akatoa ripoti, “Alisoma maongezi na dirisha likafunguka.”

Bwana ametoa nyenzo zote zinazohitajika kwetu ili kwenda kuokoa marafiki wasiohudhuria kikamilifu na wasio waumini. Wote tunaweza kufanya hivi!

Ninawaalika kila mmoja wenu kusikiliza wito wa Mwokozi wa kwenda kuokoa. Tunaweza kufanya hivi!

Ninashuhudia kwa dhati kwamba ninajua Yesu ni Mchungaji Mwema, kwamba Anatupenda na kutubariki tunapokwenda kuokoa. Ninajua yu hai; ninajua hivyo. Katika jina la Yesu Kristo, amina