2010–2019
Weka Imani Yako Katika Roho Yule Ambaye Huongoza Kufanya Mema
Aprili 2016


Weka Imani Yako Katika Roho Yule Ambaye Huongoza Kufanya Mema

Tunamkaribia Mwokozi, kutokana na upendo msafi, tunapowahudumia wengine kwa niaba Yake.

Ninashukuru kuwa nanyi jioni hii ya kuabudu, kutafakari, na kujitolea. Tumeomba pamoja. Baba yetu wa Mbinguni mpendwa ametusikia. Tumemkumbuka Mwokozi wetu, Bwana Yesu Kristo, kama tulivyoguswa na nyimbo za kutoa sifa kwake. Tumehamasishwa kufanya zaidi kumsaidia Bwana katika kazi yake kuwainua na kuwasaidia watoto wa Baba yetu wa Mbinguni.

Hamu yetu kuwahudumia wengine inapanuliwa na shukrani yetu kwa yale Mwokozi ametutendea. Hii ndiyo sababu mioyo yetu huvimba tunaposikia maneno haya yakiimbwa “Kwa sababu nimepewa zaidi, nami pia ni lazima nipeane.”1 Mfalme Benjamin, katika mahubiri yake yaliyorekodiwa katika Kitabu cha Mormoni, aliahidi hisia hiyo ya shukrani itakuja (ona Mosia 2:17–19).

Wakati imani yetu katika Yesu Kristo inatuongoza kuhitimu kupokea furaha ya msamaha wake, tunahisi hamu ya kuwahudumia wengine kwa niaba Yake. Mfalme Benjamin alifundisha kwamba msamaha hauwezi kukamilika mara moja.

Alisema hivi: “Na sasa kwa sababu ya vitu hivi ambavyo nimewazungumzia—kwamba, ili mhifadhi msamaha wa dhambi zenu siku kwa siku, ili mtembee bila hatia mbele ya Mungu—ningetaka kwamba muwapatie maskini mali yenu, kila mtu kulingana na ile aliyo nayo, kwa mfano kulisha wenye njaa, kuvisha walio uchi, kuwatembelea wagonjwa na kuwahudumia katika haja zao, kiroho na kimwili, kulingana na matakwa yao” (Mosia 4:26).

Mwenza mkuu wa Alma, Amuleki, pia alifundisha ukweli kwamba ni lazima tuendelee katika huduma yetu Kwake ndipo tuweze kuhifadhi msamaha: “Na sasa tazama, ndugu zangu wapendwa, ninawaambia, msidhani kwamba haya ni yote; kwani baada ya kufanya hivi vitu vyote, ikiwa mtawafukuza maskini, na walio uchi, na msiwatembelee wagonjwa na walioteseka, na kuwagawia mali yenu, ikiwa mnayo, wale ambao wanahitaji—Ninawaambia, ikiwa hamfanyi vitu hivi, tazama, sala yenu ni ya bure, kwani hayatakupatia chochote, na wewe ni kama wanafiki ambao wanakana imani” (Alma 34:28).

Nimefikiria usiku huu kuwahusu wanawake walio maishani mwangu. Kunao wanawake na wasichana 31 katika familia yetu, kuanzia bibi yangu na kuendelea ikiwa ni pamoja na vitukuu wetu wasichana wapya watatu. Wengine wako nasi hapa jioni hii. Watano wako chini ya umri wa miaka 12. Huu unaweza kuwa mkutano wao wa kwanza katika Kituo cha Mikutano pamoja na kina dada zao katika Kanisa la Mwokozi. Kila mmoja atapata kumbukumbu tofauti na kufanya ahadi zake kutokana na tukio hili usiku wa leo.

Kunazo kumbukumbu tatu na masharti matatu ambayo ninaomba yasalie nao maishani mwao na hata kupita hapo. Kumbukumbu hizi ni za hisia. Na masharti ni ya mambo ya kufanya.

Hisia muhimu zaidi ni ya upendo. Mmehisi upendo wa kina dada viongozi wakuu ambao wamekwishazungumza. Na mmehisi kwa Roho kwamba waliwapenda bila hata ya kuwajua kwa sababu walihisi upendo wa Baba wa Mbinguni na Mwokozi kwenu. Hii ndiyo sababu wanataka sana kuwahudumia na kuona kwamba mnapokea baraka ambazo Mungu anawatakia.

Mmehisi upendo kwa wengine usiku huu—kwa marafiki, wanashule, majirani, na hata mtu ambaye ameingia tu kwa maisha yako, mgeni. Hisia hiyo ya upendo ni zawadi kutoka kwa Mungu. Maandiko yanaiita “hisani” na “upendo msafi wa Kristo” (Moroni 7:47). Mmehisi upendo huo usiku wa leo, na mnaweza kuupokea mara nyingi mkiutafuta.

Hisia ya pili mmekuwa nayo usiku wa leo ni ushawishi wa Roho Mtakatifu. Kina dada wamewaahidi leo hii kwamba Roho Mtakatifu atawaongoza kupata huduma ambayo Bwana angetaka mtoe kwa wengine kwa niaba Yake. Mmehisi kupitia kwa Roho kwamba ahadi yao ilitoka kwa Bwana na kwamba ni ya kweli.

Bwana alisema, “Na sasa, amini, amini, ninakuambia wewe, weka imani yako katika yule Roho ambaye huongoza kufanya mema—ndiyo, kufanya haki, kutembea kwa unyenyekevu, kuhukumu kwa haki; na huyu ndiyo Roho wangu” (M&M 11:12).

Unaweza kuwa umekwishapokea baraka hiyo usiku wa leo. Kwa mfano, jina au sura ya mtu aliye na mahitaji inaweza kuwa imekujia akilini mwako. Wakati wa mkutano huu. Inaaweza kuwa lilikuwa wazo la kupita, lakini kwa sababu ya yale uliyosikia usiku wa leo, utasali juu yake, ukiwa na imani kwamba Mungu atakuongoza kufanya mema Yeye anayowatakia. Hivyo basi sala huwa muundo maishani mwako, wewe na wengine mtabadilika na kuwa bora.

Hisia ya tatu mmekuwa nayo usiku wa leo ni kwamba unataka kuwa karibu na Mwokozi. Hata msichana mwenye umri mdogo zaidi hapa atakuwa amehisi ukweli wa mwaliko ulioko katika wimbo: “‘Njooni, mnifuate, Mwokozi alisema. Basi acheni tufuate nyayo zake.”2

Kwa hiyo, na hisia hizo, jambo la kwanza ambalo ni lazima uweke sharti kufanya ni kwenda kuhudumu ukifahamu ya kwamba hauko pekee yako. Wakati unapoenda kumfariji au kumhudumia mtu yeyote kwa niaba ya Mwokozi, Yeye huandaa njia yako. Sasa, kama vile wamisionari waliorejea walio hapa usiku wa leo watakwambia, hiyo haimanishi kwamba kila mtu yuko tayari kukukaribisha au kila mtu unayejaribu kuhudumia atakushukuru. Lakini Bwana ataenda mbele zako kutayarisha njia.

Mara kwa mara Rais Thomas S. Monson amesema kwamba anajua ukweli wa ahadi ya Bwana. “ Na yeyote awapokeaye ninyi, hapo nitakuwepo pia, kwani nitakwenda mbele ya uso wenu. Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu” (M&M 84:88).

Moja kati ya njia ambazo anaenda mbele ya uso wako ni kutayarisha moyo wa mtu ambaye amekuuliza umhudumie. Atatayarisha moyo wako pia.

Utakuja kugundua ya kwamba Bwana huweka wasaidizi kando yako—kuume kwako, kushoto kwako, na kando yako. Hauendi pekee yako kuwahudumia wengine kwa niaba Yake.

Alifanya hivyo kwangu usiku wa leo. Bwana alipanga “mashahidi wengi” (Waebrania 12:1), katika maneno na muziki, kuchanganya na kuzidisha nguvu ya yale alitaka niseme. Nilitaka tu kuwa na hakika kwamba ningeweza kuweka sehemu yangu katika utunzi Wake. Ninatumaini na kusali kwamba mtahisi shukrani na furaha Bwana anapowaweka pamoja na wengine kuhudumu kwa niaba Yake.

Wakati mnapopitia tukio hilo mara nyingi, na mtapitia, mtatabasamu kwa kutambua, kama ninavyo tu, wakati tunapoimba, “Kazi Ilivyo Tamu.”3

Mtatabasamu pia mnapokumbuka aya hii: “Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mathayo 25:40).

Jambo la pili ambalo ni lazima ufanye ni kumkumbuka Bwana unapoenda kwenye huduma kwa niaba Yake. Bwana haendi tu mbele ya nyuso zetu na kuwatuma malaika kuhudumu nasi, bali pia Yeye huhisi faraja tunayowapa wengine kana vile kwamba ni Yeye tulimpa.

Kila binti wa Mungu ambaye atasikia na kuamini jumbe za mkutano huu atauliza, “Ni nini Bwana angenitaka nifanye kumsaidia Yeye kutoa msaada kwa wale walio na mahitaji?” Hali ya kila dada ni ya kipekee. Hiyo ni kweli kwa mabinti zangu, mabinti wakwe, mabinti wajukuu, na mabinti vitukuu. Kwao, na kwa mabinti wote wa Baba wa Mbinguni, ninarudia ushauri wa busara wa Dada Linda K. Burton.

Amewaomba msali kwa imani ili mjue kile ambacho Bwana angewataka mfanye katika hali zenu. Na kisha akasema juu ya ahadi ya faraja tamu ambayo Bwana mwenyewe alimpa mwanamke ambaye alikosolewa kwa kumpaka mafuta kichwani na mafuta yaliyokuwa ya thamani kubwa wakati ambapo yangeliuzwa kuwasaidia maskini.

“Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema.

“Maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema: lakini mimi hamnami siku zote.

“Ametenda alivyoweza: ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.

“Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo injili katika ulimwengu wote, na hili alilolitenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu yake” (Marko 14:6–9).

Maandiko haya mafupi ni ushauri mtamu na wenye hekima kwa kina dada waaminifu katika ufalme wa Bwana katika nyakati za kutatanisha. Utasali ili ujue ni nani Baba angetaka umhudumie kutokana na upendo Kwake na kwa Mwokozi wetu. Na hautatarajia kumbukumbu ya umma, kufuatia mfano wa yule mwanamke katika simulizi ya Marko ya maandiko, ambaye tendo lake takatifu la heshima kwa Mwokozi wa ulimwengu linakumbukwa lakini sio jina lake.

Matumaini yangu ni kuwa kina dada katika familia yetu watafanya kadiri ya uwezo wao kutokana na upendo wao kwa Mungu kuwahudunia wale walio na mahitaji. Na kitu cha tatu ninatumaini watafanya ni kibinafsi kuwa na maadili kuhusu kazi zao njema. Na bado maomba kwamba wataukubali ushuari wa Bwana, wakati aliposema—ambao mimi ni imani sisi sote tunahitaji kusikia:

“Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.

Na kisha Yeye akasema:

“Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume:

“Sadaka yako iwe kwa siri: na Baba yako aonaye sirini atakujazi” (Mathayo 6:1–4).

Sala yangu kwa kina dada katika ufalme, mahali popote walipo au katika hali zozote walizonazo, ni kwamba imani yao katika Mwokozi na shukrani kwa ajili ya Upatanisho Wake itawaongoza kufanya yote wanayoweza kwa wale ambao Mungu anawataka wawahudumie. Wakati wanapofanya hivyo, ninaahidi kwamba watasonga mbele katika njia ya kuwa wanawake watakatifu, ambao Mwokozi na Baba wa Mbinguni watawakaribisha kwa furaha na kuwazawadi hadharani.

Ninashuhudia kwamba hili ni Kanisa la Yesu Kristo aliyefufuka. Amefufuka. Yeye amelipia fidia ya dhambi zetu zote. Mimi najua kwamba kwa sababu Yake sisi tutafufuliwa na tunaweza kuwa uzima wa milele. Rais Thomas S. Monson ni nabii Wake aliye hai. Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zetu. Ninashuhudia kwamba tunamkaribia Mwokozi, kutokana na upendo msafi, tunapowahudumia wengine kwa niaba Yake. Kwa hivyo mimi nawaachieni huo ushahidi wa hakika katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “Because I Have Been Given Much,” Hymns, no. 219.

  2. “Come, Follow Me,” Hymns, no. 116.

  3. “Sweet Is the Work,” Hymns, no. 147.