2010–2019
“Mwonaji Mteule Nitamwinua Juu”
Oktoba 2016


“Mwonaji Mteule Nitamwinua Juu”

Kwa sababu Joseph alikuwa nabii, tuna zaidi ya dirisha kuingia mbinguni—mlango wa kuingia umilele uko wazi kwa ajili yetu.

Wakati Moroni alipokuja kwa mara ya kwanza kwa Joseph Smith, yeye alimwonya kwamba jina la Joseph “litasikika kwa mema na mabaya miongoni mwa mataifa yote.”1 Tumeona utimizo wa unabii huo. Katika vita kati ya mema na mabaya, Urejesho wa injili kupitia Nabii Joseph Smith umewainua wafuasi wanaomfuata na pia maadui wenye hasira ambao wanapingana na kuanzishwa kwa Sayuni na dhidi ya Joseph Smith mwenyewe. Mapigano haya si mapya. Yalianza mara baada ya Joseph alipokwenda kwenye Kichaka Kitakatifu na kuendelea leo kwa muonekano wa ziada kwenye tovuti.

Bwana mwenyewe aliatangaza kwa Joseph Smith.

“Miisho ya dunia italiulizia jina lako, na wapumbavu watakudhihaki, na jahanamu itapigana nawe kwa hasira;

“Wakati walio safi moyoni, na wenye hekima, na walio maarufu, na walio wema watautafuta ushauri, na mamlaka, na baraka kutoka chini ya mkono wako daima.”2

Leo ninatoa ushuhuda wangu kwa wote wanaotaka kuelewa kazi takatifu ya Joseph Smith Mdogo, Nabii wa Urejesho.

Hatutakiwi kuwa waoga kushuhudia juu ya kazi ya Joseph kama nabii, mwonaji na mfunuzi, kwani Bwana kila mara amefanyakazi na manabii.3 Kwa sababu ukweli umerejeshwa kupitia Joseph Smith, tunajua zaidi kuhusu Baba wa Mbinguni na Mwokozi Yesu Kristo. Tunajua sifa Zao takatifu, uhusiano Wao kwa kila mmoja wao na kwetu, na mpango mzuri wa ukombozi ambao unatuwezesha kurudi kwenye uwepo Wao.

Kuhusu Joseph, Rais Brigham Yound alitangaza: “Ilitangazwa katika baraza la milele, muda mrefu kabla ya misingi ya dunia kuwekwa, kwamba yeye, anapaswa kuwa ndiye mtu, katika kipindi cha mwisho cha dunia hii, wa kuleta neno la Mungu kwa watu, na kupokea utimilifu wa funguo na nguvu ya Ukuhani wa Mwana wa Mungu. Jicho la Bwana lilikuwa juu yake … [kwani yeye] aliteuliwa na Mungu katika milele ili aongoze katika kipindi hiki cha mwisho.”4

Katika maandalizi ya kazi hii kubwa, Joseph Smith alizaliwa katika familia yenye upendo iliyokumbana na matatizo ya kila siku na majaribu ya maisha. Wakati Joseph alipoanza kuwa mtu mzima, hisia zake kuhusu Mungu “zilikuwa nzito na daima kali,”5 hata hivyo alichanganyikiwa na mchafuko wa mawazo ya kidini yaliyofundishwa na wachungaji wa siku zake. Kwa bahati nzuri, kijana Joseph hakuacha maswali yake kupoozesha imani yake. Alitafuta majibu kwenye Biblia na alipata ushauri huu: “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekina, basi, anapaswa amwombe Mungu ambaye atampatia, kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu.”6

Joseph Alikumbuka: “Kamwe kifungu chochote cha maandiko hakijawahi kumwingia mtu moyoni kwa nguvu nyingi kuliko hiki kilivyofanya kwangu wakati huu. Kilionekana kuniingia kwa nguvu nyingi katika kila hisia za moyo wangu. Nilitafakari tena na tena.” Nilitafakari tena na tena.”7

Akiwa na imani rahisi, Joseph alitenda kulingana na hisia hizi za kiroho. Alitafuta sehemu nzuri, akapiga magoti, na “akaanza kutoa hisia za moyo wake kwa Mungu.”8 Kuna nguvu nyingi katika maelezo ya Joseph juu ya kile kilichotokea:

“Niliona nguzo ya mwanga juu ya kichwa changu, ambao ulikuwa ni mng’aro uliozidi mwangaza wa jua, ambao ulishuka taratibu hadi ukashuka juu yangu.

“… Wakati mwanga ulipotua juu yangu niliwaona Viumbe wawili, ambao mng’aro na utukufu wao unapita maelezo yote, wakiwa wamesimama juu yangu angani. Mmoja wao akaniambia, akiniita mimi kwa jina na kusema, huku akimwonyesha yule mwingine—Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!9

Joseph Smith alimwona Mungu, Baba wa Milele, na Yesu Kristo, Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu. Hili lilikuwa ni Ono la Kwanza la Joseph Smith. Miaka iliyofuata, Joseph alitafsiri Kitabu cha Mormoni kwa uwezo na nguvu za Mungu. Idadi kubwa ya viumbe wa mbinguni walimtembelea, wakirejesha ukweli na mamlaka ambayo yalikuwa yamepotea kwa karne nyingi. Mawasiliano haya matakatifu kwa Joseph Smith yanafungua madirisha ya mbinguni na utukufu wa milele mbele ya macho yetu. Maisha ya Joseph yanasimama kama ushuhuda kwamba kama mmoja wetu anakosa hekima, tunaweza kumwuliza Mungu katika imani na kupata majibu—wakati mwingine kutoka viumbe wa mbinguni lakini mara nyingi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ambaye anaongea nasi kupitia mawazo na hisia takatifu.10 Ni kupitia kwa Roho Mtakatifu kwamba tunaweza “kujua ukweli wa mambo yote.”11

Kwa wengi wetu, ushuhuda wa Nabii Joseph Smith huanza tunaposoma Kitabu cha Mormoni. Niniposoma Kitabu cha Mormoni kutoka jalada hadi jalada kama mwanafunzi kijana wa semianri ya asubuhi. Kwa fikra wazi za kivulana, niliamua kusoma kana vile mimi ni Joseph Smith, nikavumbua kweli katika Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza kabisa. Ikawa na msukumo wa ajabu katika maisha yangu kwamba niliendelea kusoma Kitabu cha Mormoni katika njia ile. Mara nyingi niliipata hiyo kuwa na uzito kwa shukrani zangu kwa Nabii Joseph na kwa kweli zilizorejeshwa zilizomo katika kitabu hiki chenye thamani.

Kwa mfano, fikiria hisia za Joseph akiwa anatafsiri vifungu kuhusu ubatizo kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Joseph, aliyeambiwa hasijiunge na kanisa lolote, kihalisia alikuwa na maswali kuhusu ibada hii ya kuokoa. Maswali yake yalimpelekea, kwa mara nyingine, kuomba, na maombi yale yalimpelekea kutembelewa na Yohana Mbatizaji, aliye urejesha Ukuhani wa Haruni na mamlaka ya kubatiza.12

Au fikiria jinsi Joseph alivyojisikia pale alipojifunza kwa mara ya kwanza kwamba Yesu Kristo aliwatembelea watu wa Ulimwengu wa Magharibi—kwamba aliwafundisha, aliwaombea, aliwaponya wagonjwa wao, aliwabariki watoto, alitoa mamlaka ya ukuhani, na aliwalisha sakramenti.13 Joseph huenda hakutambua wakati ule, lakini alichojifunza kuhusu ibada na muundo wa Kanisa la Kristo la kale kulimwandaa yeye baadaye kumsaidia Bwana katika kulirejesha Kanisa kama lile hapa duniani.

Wakati wa kutafsiri Kitabu cha Mormoni, Joseph na mke wake Emma waliomboleza kifo cha mwana wao mchanga. Katika siku hizo wahubiri walifundisha kwamba watoto ambao walikufa bila ya kubatizwa watahukumiwa milele. . Akiwa na haya akilini, fikiria jinsi Joseph alivyojisikia akiwa akitafsiri maneno haya kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni: “Na watoto wachanga hawahitaji toba, wala ubatizo. … [Kwani] watoto wachanga ni wazima katika Kristo, hata kutokea mwanzo wa dunia.”14

Huenda kifungu kizuri kabisa kwenye Kitabu cha Mormoni kwa kijana Joseph kinaweza kuwa aya ya tatu 2 Nefi. Aya hii inajumuisha unabii wa kale kuhusu “mwonaji mteule” ambaye Bwana angemwinua katika siku za mwisho—mwonaji aitwaye Joseph, aliyepewa jina la baba yake. Nabii huyu wa baadaye angekuwa “mwenye utukufu” na angefanya kazi “ya thamani kubwa” kwa watu wake. Angekuwa “mkuu kama Musa” na angepewa uwezo kulileta neno la Mungu.15 Fikiria jinsi Joseph Smith alivyojisikia alipogundua kwamba unabii huu ulikuwa kwa ajili yake! Hakuwa anatafsiri historia; alikuwa akitafsiri ono la siku za mwisho, la Urejesho wa ajabu wa injili ya Yesu Kristo—na Joseph mwenyewe angesaidia kutimiza!

Leo, takribani miaka 200 baadaye, ni rahisi kuona jinsi unabii huu ulivyotimia. Tunajua kuhusu vitu vikubwa ambavyo Joseph alivikamilisha kama nabii wa Bwana. Lakini kumbuka kwamba wakati Joseph alipotafsiri unabii huu, alikuwa tayari amefanya machache ya vitu walivyotabiri manabii. Alikuwa bado kijana wa umri wa miaka ya 20. Kanisa lilikuwa bado halijaanzishwa. Hapakuwa na kata na matawi, hakuna wamisionari, na wala mahekalu. Ni vigumu kujua kama watu walimsikia Joseph Smith, na baadhi ya wale waliompinga. Sasa hebu angalia kazi kubwa ambayo Bwana anaifanya kwa mkono wa mtumishi Wake Joseph, bila kujali upinzani dhidi yake. Je, huku siyo kutimizwa kwa unabii huu ushahidi thabiti wa wito wa kinabii wa Joseph Smith?

Kwa yeyote anayeweza kuwa anatilia shaka ushuhuda wake juu wa Joseph Smith au kusumbuka na makosa, kupotosha, au juu habari kuhusu maisha yake na huduma, ninamwalika afikirie matunda—baraka nyingi ambazo zimekuja kwetu kwa njia ya ujumbe wa ajabu wa Joseph Smith, Nabii wa Urejesho.

Kwa sababu Joseph alikuwa nabii, ufunuo na unabii siyo vitu vya kale. “Siku ya miujiza”—ya maono, uponyaji, na utumishi wa malaika—haijakoma.16

Kwa sababu Joseph alikuwa nabii, kila mmoja wetu ana nafasi ya uwezo na baraka za ukuhani mtukufu, zikiwemo ubatizo, kipawa cha Roho Mtakatifu, na sakramenti.

Kwa sababu Joseph alikuwa nabii, tuna baraka na ibada za hekalu ambazo zinatuunganishwa na Mungu, kutufanya tuwe watu Wake, na kudhihirisha kwetu “nguvu ya utauwa,” kufanya iwezekane siku moja“ kuona sura ya Mungu, hata Baba, na kuishi.”17

Kwa sababu Joseph alikuwa nabii, tunajua kwamba ndoa na familia ni sehemu muhimu ya mpango wa Mungu kwa ajili ya furaha yetu. Tunajua kwamba kupitia ibada na maagano ya hekalu, uhusiano wetu wa kifamilia unaweza kudumu milele

Kwa sababu Joseph alikuwa nabii, tuna zaidi ya dirisha kuingia mbinguni—mlango wa kuingia umilele uko wazi kwa ajili yetu. Tunaweza kumjua “Mungu pekee wa kweli, na Yesu Kristo, ambaye [Amemtuma].”18 Uzima wa milele unaweza kuwa wetu.

Zaidi ya yote, kwa sababu Joseph alikuwa nabii, tuna shahidi juu ya shahidi, ushuhuda juu ya ushuhuda, kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa ulimwengu. Tuna mnyororo usiokatika wa mashahidi maalumu wa Yesu Kristo, akiwemo nabii wetu leo, Rais Thomas S. Monson; washauri katika Urais wa Kwanza, na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Kwa ushahidi wao, nami bado naongeza ushuhuda wangu wa hakika: Yesu Kristo yu hai na analiongoza Kanisa Lake. Joseph Smith alikuwa na ni Nabii wa Urejesho. Ukuhani na mamlaka ya Mungu yapo tena duniani. Naomba bila woga tutangaze ushahidi wetu na furaha yetu kwa nabii huyu, mwonaji, na mfunuzi wa Bwana ni maombi yangu katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.