2010–2019
Hakuna Furaha Kubwa Zaidi ya Kujua Kuwa Wanajua
Oktoba 2016


Hakuna Furaha Kubwa Zaidi ya Kujua Kuwa Wanajua

Sijui kama kila kitu katika dunia hii kinaweza kuleta furaha kubwa na shangwe zaidi ya kujua kwamba watoto wetu wanamjua Mwokozi.

Akina kaka na kina dada, hivi majuzi nimekuwa nikitafakari swali hili: “Kama kila kitu ambacho watoto wako wanakijua kuhusu injili kingetoka kwako—kama chanzo chao pekee—je, wangejua kwa kiasi gani?” Swali hili ni kwa wale wote wanaopenda, kufundisha na kuwashawishi watoto.

Je, kuna zawadi kubwa yoyote ambayo tunaweza kuweka kwa watoto wetu kuliko kumbukumbu iliochomelewa ndani zaidi katika mioyo yao kwamba tunajua kwamba Mkombozi wetu yu hai ? Je, wanajjua kwamba tunajua? Na cha muhimu zaidi, wamekuja kujua wenyewe kwamba Yeye yu hai?

Nilipokuwa mvulana mdogo, nilikuwa kijana mgumu sana kwa mama yangu kulea. Nilikuwa na nguvu za ajabu. Mama yangu huniambia kuwa hofu yake kubwa ilikuwa kwamba nisingekua nikauona utu uzima. Nilikuwa na nguvu nyingi sana.

Nakumbuka kama kijana mdogo nikiwa nimekaa kwenye mkutano mmoja wa sakramenti na familia yetu. Mama yangu alikuwa tu amepokea seti ya aandiko mapya. Maandiko haya mapya yalijumuisha vitabu vyote vya msingi kanisani katika toleo jipya, na katikati yake kulikuwa na karatasi ya kuandika vidokezo

Wakati mkutano ukiendelea, nilimuomba kama ningeweza kubeba maandiko yake. Kwa tumaini la kunituliza na kuwa mkimya, alinipatia Nilipokuwa nadurusu maandiko yake, niligundua kuwa alikuwa ameandika malengo yake binafsi katika sehemu ya kikaratasi. Ili nikupe muktadha wa lengo lake, lazima nikwambie kwamba mimi ni mtoto wa pili katika watoto sita na jina langu ni Brett. Mama yangu alikuwa ameandika, katika maandishi mekundu, lengo moja tu: “Uvumilivu na Brett!”

Kama ushahidi zaidi kukusaidia kuelewa changamoto ambazo wazazi wangu walikumbana nazo wakati wa kuilea familia yetu, ngoja niwaambie kuhusu kusoma kwetu maandiko kama familia. Kila asubuhi, mama yangu alisoma Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya familia wakati wa kifungua kinywa. Kwa wakati huu, kaka yangu, Dave, na mimi hukaa kimya lakini bila staha. Kuwa mkweli kabisa, tulikuwa hatusikilizi. Tulikuwa tunasoma maandishi katika maboksi ya nafaka.

Mwishowe, asubuhi moja, niliamua kuwa sambamba na mama yangu Nikasema, “Mama, kwa nini unatufanyia hivi? Kwa nini unatusomea Kitabu cha Mormoni kila asubuhi? Baadaye nikanena kauli ambayo inaniabisha kuikiri. Kwa kweli, siamini kama kweli nilikisema. Nilimwambia, “Mama, mimi sisikilizi!

Jibu lake lenye upendo lilikuwa kielelezo muhimu katika maisha yangu Alisema,”Mwanangu, nilikuwa kwenye mkutano ambapo Rais Marion G. Romney alifundisha kuhusu baraka za kusoma maandiko. Wakati wa mkutano huo, nilipokea ahadi kwamba kama ningewasomea Kitabu cha Mormoni wanangu kila siku, nisingewapoteza.” Baadaye akanitazama moja kwa moja machoni, na kwa uamuzi dhabiti, akasema “Na sitakupoteza!”

Maneno yake yalichoma moyo wangu. Bila kujali upungufu wangu, nilikuwa na thamani kiasi cha kuokolewa! Alinifundisha ukweli wa milele kwamba mimi ni mtoto wa Baba yetu Mpendwa wa Mbinguni. Niligundua kwamba haijalishi namna yoyote, nilistahili. Huu ulikuwa ni wakati mkamilifu kwa ajili ya mvulana huyu mpungufu.

Nina shukrani za milele kwa mama yangu malaika na kwa malaika wote ambao wanawapenda watoto kikamilifu, bila ya kujali mapungufu yao. Ninaamini kwa nguvu zote kwamba akina dada wote—nitawaita “malaika”—ni akina mama katika Sayuni, wawe wameolewa au la au wawe wana watoto katika maisha haya au la.

Miaka michache iliyopita Urais wa Kwanza ulitangaza: “Umama ni karibu na uungu. Ni huduma ya juu zaidi, takatifu ambayo inafanywa na mwanadamu. Inamuweka yule anayeheshimu mwito wake mtakatifu na huduma karibu na malaika.”1.

Ninashukuru kwa ajili ya malaika kote Kanisani ambao kwa ujasiri na upendo hutangaza ukweli wa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni.

Ninashukuru kwa ajili ya Kitabu cha Mormoni Ninajua ni cha kweli! Kinajumuisha utimilifu wa injili ya Yesu Kristo. Sina taarifa ya yeyote ambaye anasoma Kitabu cha Mormoni kwa uadilifu kila siku kwa madhumuni ya haki na imani katika Kristo ambaye amepoteza ushuhuda na kuanguka. Ahadi za kinabii za Moroni zinabeba funguo za kujua ukweli wa mambo yote—ikijumuisha kuwa na uwezo wa kutambua na kuepuka vishawishi vya adui. (Ona Moroni 10:4–5.)

Ninashukuru pia kwa Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo na Mwanawe, Yesu Kristo. Mwokozi ametoa mfano kamilifu wa jinsi ya kuishi katika dunia isiyo kamilifu na isiyo na usawa. “Tunampenda, kwa sababu alitupenda kwanza” (1 Yohana 4:19). Upendo wake kwetu haupimiki. Ni rafiki yetu wa kweli. Anatokwa na jasho “kama ville ingekuwa tone kubwa la damu” kwa ajili yako na yangu (Luka 22:44). Aliwasamehe walioonekana hawasameheki. Aliwapenda wasiopendeka. Alifanya kile ambacho mwanadamu wa kawaida hawezi kukifanya. Alitupa Upatanisho kuyashinda majaribu, maumivu, na ugonjwa wa wanadamu wote.

Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kuishi na ahadi kwamba haijalishi shida zetu zaweza kuwa za namna gani, daima tunaweza kuwa na mtumaini kwake, “ambaye ni mkuu katika kuokoa” (2 Nefi 31:19). Kwa sababu ya Upatanisho Wake, tunaweza kuwa na furaha, amani, na shangwe, na uzima wa milele.

Rais Boyd K. Packer alisema: “Isipokuwa kwa wachache sana ambao wanakwenda kwa njia ya kupotea, hakuna tabia, au mazoea mabaya, au ukaidi, au dhambi, hakuna ukengeufu, hakuna jinai ambayo imeondolewa kutoka katika ahadi ya msamahama kamilif. Hii ni ahadi ya upatanisho wa Kristo.”2

Moja ya matukio ya maajabu katika historia ya binadamu ni huduma ya Mwokozi alipotembelea wakazi wa zamani wa Marekani. Weka taswira katika akili yako ingekuwaje kama ungekuwepo. Kama nilivyotafakari upendo na kujali kwake kwa kundi la Watakatifu waliokusanyika katika hekalu, nimewafikiria watoto ambao ninawapenda zaidi ya maisha yangu yenyewe. Nimejaribu kufikiria jinsi gani ningehisi kuona hawa wadogo wetu, kushuhudia binafsi Mwokozi akialika kila mtoto kuja kwake, kushuhudia Mwokozi akinyoosha mkono, kusimama karibu na kila mtoto, mmoja baada ya mwingine, kwa utaratibu akigusa alama mikononi mwake na miguuni mwake, na baadaye kuona kila mmoja akisimama na kushuhudia kwamba Yeye yu hai! (Ona 3 Nefi 11:14–17; ona pia 17:21; 18:25.) Kuwa na watoto wetu kutugeukia na kusema, “Mama, Baba, ni Yeye!”

Picha
Mwokozi na Watoto

Sijui kama chochote katika dunia hii kinaweza leta furaha na shangwe zaidi ya kujua kwamba watoto wetu wanamjua Mwokozi, kujua kwamba wanajua “asili ya kutegemea msamaha wa dhambi zao.” Hiyo ndiyo kwa nini, kama waumini wa Kanisa, “tunahubiri Kristo” na tunashuhudia Kristo (2 Nefi 25:26).

  • Ndio sababu tunasali na watoto wetu kila siku.

  • Ndio sababu tunasoma nao maandiko kila siku.

  • Ndio maana tunawafundisha kutumikiana, ili kwamba waweze kudai baraka ya kujipata wanapotumikia wanadamu wengine (Ona Marko 8:35; Mosia 2:17).

Tunapojitolea kwenye mifano hii rahisi ya ufuasi, tunawezesha watoto wetu kwa upendo wa Mwokozi na mwelekeo uliotukuka na ulinzi wanapokumbana na upepo mzito wa majaribu.

Injili kwa kweli inahusu yule mmoja. Ni kuhusu yule kondoo mmoja aliyepotea(ona Luka 15:3–7); ni kuhusu mwanamke msamaria mmoja kwenye kisima (ona Yohana 4:5–30); ni kuhusu mwana mpotevu ( Luka 15:11–32).

Ni kuhusu mvulana mdogo anayeweza kudai kwamba hasikilizi.

Ni kuhusu kila mmoja wetu—hata tulivyo wapungufu—kuwa kitu kimoja na Mwokozi kama alivyo kitu kimoja na Baba Yake (ona Yohana 17:21).

Ninashuhudia kwamba tuna Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo, anayetujua kwa majina! Ninashuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu anayeishi Ni Mwana wa Pekee na Mtetezi wetu kwa Baba Ninashuhudia zaidi kwamba wokovu huja kwa kupitia katika jina lake—na si kwa njia nyingine yeyote.

Ni maombi yangu kwamba tutajitolea mioyo yetu na mikono yetu kuwasaidia watoto wote wa Baba yetu wa Mbinguni kumjua Yeye na kuhisi upendo Wake. Tufanyavyo hivyo, Yeye anatuahidi furaha na shangwe ya mielel katika dunia hii na katika dunia ijayo. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “Message of the First Presidency,” katika Conference Report, Oct. 1942, 12–13; iliyosomwa na Rais J. Reuben Clark Jr.

  2. Boyd K. Packer, “The Brilliant Morning of Forgiveness,” Ensign, Nov. 1995, 20.