2010–2019
Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!
Oktoba 2016


Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!

Tumezungukwa na utajiri wa nuru na ukweli wa ajabu na maongozi na nashangaa kama kwa kweli tunathamini kile tulichonacho.

Ni jinsi gani tumebarikiwa kukusanyika tena katika mkutano huu mkuu wa ulimwenguni kote chini maelekezo na uongozi wa nabii wetu mpendwa na Rais, ThomasnbS. Monson. Rais, sisi tunakupenda na tunakukubali!

Wakati wa maisha yangu ya kazi yangu kama rubani nilitegemea kwa kiasi kikubwa usahihi na uwezo wa mfumo wa kompyuta lakini nilifanya kazi na kompyuta yangu binafsi mara chache sana. Katika ofisi yangu kama mtendaji, nilikuwa na wasaidizi na makatibu ambao kwa ukarimu walinisaidia kazi.

Haya yote yalibadilika mwaka 1994 nilipoitwa kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka. Wito wangu ulikuwa nafasi nyingi za ajabu kutumikia, lakini pia ulijumuisha kiasi kikubwa cha kazi za ofisini—zaidi ya hata nilivyofikiria kuwa inawezekana.

Kwa mshangao wangu, chombo kikuu cha kufanya kazi yangu vizuri kilikuwa ni kompyuta binafsi.

Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, ilibidi ni nichunguze sana ulimwengu mgeni, wa ajabu, usiyoeleweka.

Hapo mwanzo, kompyuta na Mimi hatukuwa marafiki sana.

Watu wenye ufundi walijaribu kunifundisha jinsi ya kutumia kompyuta. Kwa kawaida walisimama nyuma yangu, wakati mwingine wakiwa juu ya mabega yangu, vidole vyao vikienda waa na vikigonga kwa mshindo wa simfoni dhidi ya kibao cha kompyuta.

“ Ona?”wangesema kwa kujivunia. “Hivi ndivyo unavyofanya.”

Sikuona. Yalikuwa mabadiliko ya kuyumbisha.

Kizingo changu cha kujifunza kilikuwa zaidi kama ukuta wa matofali.

Ilichukuwa kiasi kikubwa cha muda wangu, marudio, subira, hamna kiasi kidogo cha tumaini na imani, uthibitisho kutoka kwa mke wangu, na lita nyingi za soda lishe ambazo zitabaki bila jina.

Sasa, miaka 22 baadae, nimezungukwa na tekinolojia ya kompyuta. Nina anwani ya barua pepe, akaunti ya Twitter, na ukurasa wa Facebook. Ninamiliki smart phone, tableti, kompyuta mpakato, na kamera ya digitali. Na, wakati utaalamu wangu wa ufundi unaweza usiwe sawa na ule wa watoto wa miaka saba, kwa mzee wa umri kati ya sabini na sabini na tisa, ninafanya vizuri.

Lakini nimeona kitu fulani cha kufurahisha. Ninapozidi kuwa hodari katika tekinolojia, na zaidi naona kuwa ni vya kawaida.

Takribani historia yote ya binadamu, mawasiliano yalifanyika kwa mwendo wa farasi. Kupeleka ujumbe na kupata jibu kuliweza kuchukua siku nyingi au hata miezi. Leo ujumbe wetu unasafiri maelfu ya maili katika anga au maelfu ya mita chini ya bahari kumfikia mtu fulani upande mwingine wa ulimwengu, na kama kuna ucheleweshaji wa hata sekunde chache, tunahudhika na kukosa subira.

Inaelekea kuwa ni asili ya binadamu: tunapozoea zaidi kitu fulani, hata kitu cha kimiujiza na cha kustahiwa, tunapoteza fahamu zetu za staha na tunaichukulia kama kitu cha kawaida.

Je, Tunachukuwa Kweli za Kiroho Kama Kitu Cha Kawaida?

Kuchukuwa tekinologia za kisasa kama kitu cha kawaida na hali zisizo na taabu zinaweza kuwa jambo dogo sana. Lakini, kwa huzuni, sisi wakati mwingine tunachukuwa msimamo huo huo kwa mafundisho ya milele na yanayopanua roho ya injili ya Yesu Kristo. Katika Kanisa la Yesu Kristo, tumepewa kwa wingi. Tumezungukwa na utajiri wa nuru na ukweli wa ajabu na maongozi na nashangaa kama kwa kweli tunathamini kile tulichonacho.

Fikiria wale wafuasi wa mwanzo waliotembea na kuzungumza na Mwokozi wakati wa huduma Yake duniani. Fikiria shukrani na staha ambayo ilijaza mioyo yao na akili zao walipomwona amefufuka kutoka kaburini, wakati walipogusa majeraha katika mikono yake na ubavuni. Maisha yao kamwe hayatakuwa vile vile tena!

Wafikirie Watakatifu wa mwanzo wa kipindi hiki waliomfahamu Nabii Joseph na kumsikia akihubiri injili ya urejesho. Fikiria jinsi walivyojisikia kujua kwamba pazia kati ya dunia na mbingu limefunguliwa tena, kumwaga nuru na elimu juu ya ulimwengu kutoka nyumba yetu ya selestia huko juu.

Zaidi ya yote, fikiria jinsi ulivyojisikia wakati kwa mara ya kwanza ulipoamini na kuelewa kwamba wewe kwa kweli ni mtoto wa Mungu; kwamba Yesu Kristo kwa hiari yake aliteseka kwa ajili ya dhambi zako ili kwamba uweze kuwa safi tena; uwezo ule wa ukuhani ni wa kweli na unaweza kukuunganisha wewe kwa wapendwa wako kwa wakati na milelel yote; kwamba kuna nabii aliye hai duniani leo. Si hayo ni maajabu na yanashangaza?

Ukifikiria haya yote, inawezekanaje daima kuwa sisi kati ya watu wote tusiweze kufurahia kuhusu kuhudhuria ibada za Kanisa letu? Au kuchoka kusoma maandiko matakatifu? Nadhani inawezekana tu kama mioyo yetu ingekuwa haina hisia kuwa na uzoefu wa shukrani na hofu kwa zawadi adimu ambayo Mungu ameturidhia. Kweli zinazobadilisha maisha zipo mbele ya macho yetu na ncha ya vidole vyetu, lakini wakati mwingine tunakuwa wavivu kwenye njia ya ufuasi. Mara nyingi tunajiachia tuchanganyikiwe na mapungufu ya waumini wenzetu badala ya kufuata mfano wa Bwana wetu. Tunatembea katika njia iliyomwagwa almasi, lakini ni nadra tunaweza kuzitofautisha kutokana na changarawe za kawaida.

Ujumbe Uliozoeleka

Nilipokuwa kijana, marafiki zangu waliniuliza kuhusu dini yangu. Mara nyingi nilianza kwa kuwaeleza tofauti, kama vile neno la hekima. Wakati mwingine nilisisitiza kufanana na dini zingine za Kikristo. Hamna katika hivi kilichowavutia. Lakini wakati nilipowazungumzia kuhusu mpango mkuu wa furaha Baba yetu wa Mbinguni anao kwa ajili yetu kama watoto Wake, nilipata usikivu wao.

Nakumbuka kujaribu kuchora mpango wa wokovu kwenye ubao katika darasa la kanisa letu katika Franfurt, Germany. Nilitengeneza duara ambazo ziliwakilisha maisha kabla ya kuja duniani, maisha duniani, na kurudi kwa Wazazi wetu wa Mbinguni baada ya maisha haya.

Kama mvulana, nilipenda sana kishiriki ujumbe huu wa kusisimua. Wakati nilipoelezea kanuni hizi katika maneno yangu yaliyo rahisi, moyo wangu ulijawa na shukrani kwa Mungu ambae anawapenda watoto Wake, na Mwokozi aliyetukomboa sisi wote kutokana na mauti na jehanamu. Nilijivunia sana ujumbe huu wa upendo, furaha, na matumaini.

Baadhi ya marafiki zangu walisema kwamba ujumbe huu ulionekana wa kawaida, ingawa vitu kama hivi kamwe havikufundishwa katika malezi ya dini zao. Ilikuwa kama vile siku zote wamekuwa wakijua vitu hivi kuwa ni vya kweli, kama vile nilikuwa narusha tu mwanga kwenye kitu fulani ambacho kilikuwa tayari kimeota mizizi katika mioyo yao.

Tuna Majibu!

Ninaamini kila binadamu anabeba katika moyo wake kiasi fulani cha maswali ya msingi kuhusu maisha yenyewe. Nilitoka wapi? Kwa nini nipo hapa? Nini kitatokea baada ya kufa?

Aina hii ya maswali yamekuwa yakiulizwa na binadamu tangu mwanzo wa ulimwengu. Wanafilsofia,wasomi na wabukuzi wametunia maisha yao na utajiri wao kutafuta majibu.

Ninashukuru kwamba injili ya urejesho ya Yesu Kristo ina majibu ya maswali magumu kabisa katika maisha. Majibu haya yanafundishwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ni ya kweli, dhahiri, na wazi, na rahisi kueleweka. Yana maongozi, na tunayafundisha kwa watoto wa miaka mitatu katika darasa la Sanbim.

Kina kaka na kina dada, sisi ni viumbe vya milele, tusio na mwanzo na tusio na mwisho. Tumeishi siku zote.1 Sisi ni watoto halisi wa kiroho wenye utukufu, wenye kudra ya Wazazi wa Mbinguni!

Tunatoka kwenye mabaraza ya mbinguni ya Bwana Mungu wetu. Sisi ni wa nyumba ya kifalme ya Elohimu, Mungu Aliye juu sana. Tulitembea pamoja naye katika maisha yetu kabla ya kuja duniani. Tulimsikia akisema, kushuhudia utukufu Wake, tulijifunza njia Zake.

Wewe nami tulishiriki katika Baraza Kuu ambako Baba yetu mpendwa aliwasilisha mpango Wake kwa ajili yetu—kwamba tungekuja duniani, kupokea miili inayokufa, kujifunza kuchagua kati ya mema na maovu, na kuendelea katika njia ambazo vinginevyo isingewezekana.

Wakati tulipita pazia na kuingia maisha haya ya mwili wenye kufa, tulijua kwamba hatungekumbuka tena maisha ya hapo nyuma. Kungekuwa na upinzani na matatizo na majaribu. Lakini vilevile tulijua kwamba kupata umbo la mwili ilikuwa na umuhimu sana kwetu. Ee,Jinsi gani tulitegemea kwamba tungejifunza kufanya chaguzi sahihi upesi, kushinda majaribu ya Shetani, na hatimaye kurudi kwa wapendwa Wazazi wetu Mbinguni.

Tulijua tungefanya dhambi na kufanya makosa—labda hata yale makubwa. Lakini pia tulijua kwamba Mwokozi wetu,Yesu Kristo, aliahidi kuja duniani, kuishi maisha yasio na dhambi, na kwa kujitolea kuweka maisha Yake chini katika dhabihu ya milele. Tulijua kwamba kama tungeitoa mioyo yetu Kwake, kumwamini Yeye, na kujitahidi kwa nguvu zote za roho zetu kutembea katika njia ya ufuasi, tungeweza kuoshwa safi na mara nyingine tena kuingia katika uwepo wa mpendwa Baba yetu wa Mbinguni.

Kwa hiyo, kwa imani katika dhabihu ya Yesu Kristo, wewe na mimi tuliukubali, kwa hiari yetu wenyewe, mpango wa Baba wa Mbinguni.

Ndio maana tupo hapa kwenye hii sayari dunia maridadi—kwa sababu Mungu alitupa nafasi, na tulichagua kuikubali. Maisha yetu ya mwili wa kufa, hata hivyo, ni ya muda mfupi tu na tutamaliza na kifo cha mwili wetu. Lakini asili ya wewe na mimi ni kina nani haitaweza kuharibiwa. Roho zetu zitaendelea kuishi na kungoja Ufufuo—zawadi ya bure kwetu sisi wote kutoka kwa Baba yetu na Mwanae Yesu, wenye upendo.2 Wakati wa Ufufuko, roho zetu na miili yetu vitaunganika tena, na kuwa huru kutokana na maumivu na kasoro za kimwili.

Baada ya Ufufuko, kutakuwa na Siku ya Hukumu. Hali wote hatimaye wataokolewa na kurithi ufalme wa utukufu, wale wanaomwamini Mungu na kutafuta kufuata sheria na ibada zake watarithi maisha katika milele ambayo hayafikiriki katika utukufu wake na yaliyojaa fahari.

Siku ya Hukumu itakuwa siku ya huruma na upendo—siku ambayo mioyo iliyovunjika inaponywa, wakati machozi ya huzuni yanabadilishwa na machozi ya shukrani, wakati vyote vitafanywa sawa.3

Ndiyo, kutakuwa na huzuni kubwa kwa sababu ya dhambi. Ndiyo, kutakuwa na majuto na hata uchungu moyoni kwa sababu ya makosa yetu, ujinga wetu, na ukaidi wetu ambao ulitusababishia kukosa nafasi ya maisha makuu ya baadae.

Lakini nina imani kwamba hatutatosheka tu na hukumu ya Mungu; pia tutastaajabishwa na kuzidiwa na hisani Yake isiyo na mwisho, huruma ukarimu na upendo kwetu sisi, watoto Wake. Kama matamanio na matendo yetu ni mazuri, kama tuna imani katika Mungu aliye hai, basi tunaweza kungojea kile Moroni alichokiita “uwakili unaofurahisha wa Jehova mkuu, Mwamuzi wa milele.”4

Pro Tanto Quid Retribuamus

Ndugu zangu na dada zangu wapendwa, marafiki zangu wapendwa, haijazi mioyo na akili zetu na mshangao na woga kutafakari mpango mkuu wa furaha ambao Baba yetu mpendwa ameutayarisha kwa ajili yetu? Haitujazi na furaha isiyosemeka kujua utukufu ujao ambao umetayarishwa kwa wote wanaomsubiri Bwana?

Kama kamwe hamjahisi mshangao na furaha, ninawaalika mtafute, mjifunze, na mtafakari kweli rahisi za injili ya urejesho bali zilizo muhimu. “Wacha sherehe za ibada za milele zikae juu ya akili zenu.”5 Hata zishuhudie kwenu mpango mtakatifu wa wokovu.

Kama mmehisi vitu hivi kabla, nawauliza nyinyi leo, “Mnaweza [nyinyi] kuhisi hivyo sasa?”6

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kusafiri kwenda Belfast, Northern Ireland. Wakati nikiwa kule, niliona nembo ya Belfast, ambayo inajumuisha wito “Pro tanto quid retribuamus, au “Tutatoa nini kama malipo kwa hayo mengi?”7

Ninawaalika kila mmoja wetu kufikiria swali hili. Nini tutakachotoa kama malipo kwa wingi wa nuru na kweli ambazo Mungu amemwaga juu yetu?

Baba yetu mpendwa kiurahisi anatutaka tuishi kilingana na ukweli tulioupokea, na kwamba tufuate njia aliyotoa. Kwa hiyo, acha tuwe na ujasiri na kuamini katika mwongozo wa Roho. Acha sisi kwa neno na kwa kitendo tushiriki na watu wenzetu ujumbe wa kushangaza na staha wa mapango wa wakovu wa Mungu. Na motisha yetu iwe ni upendo kwa Mungu na kwa wtoto Wake, kwani wao ni kaka na dada zetu. Huu ni mwanzo wa kile tunaweza kufanya kama malipo kwa mengi mno.

Siku moja “kila goti litapiga na kila ulimi utaungama” kwamba njia za Mungu ni za haki na mpango Wake ni thabiti.8 Kwa nyinyi na mimi, wacha siku hiyo iwe leo. Wacha tutangaze, na Yakobo wa kale, “Ee jinsi gani ulivyo mkuu mpango wa Mungu wetu!”9

Juu ya haya nashuhudia kwa shukrani za dhati kwa Baba yangu wa Milele, ninapowaachia baraka zangu, katika jina la Yesu Kristo, amina.