2010–2019
Mpango Mkuu wa Ukombozi
Oktoba 2016


Mpango Mkuu wa Ukombozi

Mimi najua kwamba tunapotubu dhambi kwa uaminifu, kweli zinaondoshwa—hakutakuwa na alama!

Miezi michache kabla ya Rais Boyd K. Packer kufariki, viongozi wakuu wa ukuhani na viongozi makundi saidizi walikuwa na fursa ya thamani ya yeye kunena nasi. Sijaweza kukoma kufikiria juu ya kile alichosema. Alisema kwamba alichunguza nyuma katika maisha yake yote, akitafuta ushahidi wa dhambi alizotenda na kutubu na hakuweza kupata alama zake. Kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi, Yesu Kristo, na kupitia kwa toba ya kweli, dhambi zake zilikuwa zimefutwa kabisa, kana kamwe hazikuwa zimefanyika. Rais Packer kisha alitupa sisi jukumu kama viongozi siku hiyo tushuhudie ukweli huu kwa kila mmoja wetu ambaye atatubu kwa uaminifu.

Nafahamu mtu ambaye alihusika katika makosa ya kimaadili miaka kadhaa iliyopita. Kwa muda fulani, mtu huyu aliona aibu mno na kuwa na wasiwasi sana kumkaribia mke wake na viongozi wake wa ukuhani. Alitaka kutubu kikamilifu lakini alielezea kwa kikweli kwamba alikuwa tayari kusalimisha wokovu wake mwenyewe wa milele badala ya kumleta mkewe au watoto wake kwa huzuni, aibu, na matokeo mengine ambayo yangesababishwa na kuungama kwake.

Tunapofanya dhambi, Shetani mara nyingi hujaribu kutushawishi kwamba jambo bora la kufanya ni kulinda wengine kutokana na uharibifu wa ufahamu wa dhambi zetu, ikijumuisha kukwepa kukiri kwa askofu wetu, ambaye anaweza kubariki maisha yetu kupitia kwa funguo zake za ukuhani kama mwamuzi wa wote katika Israeli. Ukweli, hata hivyo, ni kwamba jambo la upendo na la Kikristo la kufanya ni kukiri na kutubu. Huu ni mpango mkuu wa Baba wa Mbinguni wa ukombozi.

Hatimaye, mtu huyu mpendwa alikiri kwa mke wake mwaminifu na viongozi wake wa Kanisa, akielezea kwa majuto makuu. Ingawa ilikuwa ni jambo gumu zaidi alilowahi kufanya, hisia za msamaha, amani, shukrani, upendo kwa Mwokozi wetu, na ufahamu wa kwamba Bwana alikuwa akiinua mzigo wake mzito na kumbeba ilimletea shangwe isiyoeleweka, bila kujali matokeo yake na siku zake zijazo.

Picha
Mwokozi akifariji

Alikuwa na uhakika kwamba mke na watoto wake watahudhika—na waliudhika; na kwamba kutakuwa na hatua za kinidhamu na kuachiliwa kutoka kwa mwito wake—na hatua zilichukuliwa. Alikuwa na uhakika kwamba mke wake atavunjika moyo, kuumia, na kuwa na hasira—na alikuwa hivyo. Na alikuwa na hakika kuwa mkewe ataondoka, pamoja na watoto—lakini hakufanya hivyo.

Wakati mwingine dhambi mbaya hupelekea talaka, ambayo inaweza kuhitajika. Lakini kwa mshangao wa mtu huyu, mkewe alimkumbatia na kujitolea mwenyewe kumsaidia kwa njia yoyote ambayo angeweza. Baada ya muda, aliweza kumsamehe kikamilifu. Alihisi uwezo wa uponyaji wa Upatanisho wa Mwokozi kwake. Miaka baadaye, wanandoa hawa na watoto wao watano wako imara na ni waaminifu. Mume na mke wanahudumu hekaluni na wana ndoa ya ajabu, upendo. Kina cha ushuhuda wa mtu huyu na upendo wake na shukrani kwa Mwokozi ni dhahiri katika maisha yake.

Amuleki alishuhudia, “Ndio, ningependa kwamba mje mbele na msishupaze mioyo yenu mara nyingine … ikiwa mtatubu … , mara moja mpango mkuu wa ukombozi utatimizwa kwenu.”1

Nilipokuwa nikihudumu pamoja na mume wangu alipokuwa akisimamia misheni, tulienda kwenye uwanja wa ndege ili kuchukua kundi kubwa la wamisionari asubuhi moja. Kijana fulani alivutia macho yetu. Alionekana mwenye huzuni, kuzidiwa, karibu kufadhaika. Tulimwangalia kwa makini mchana huo. Kufikia jioni, kijana huyu alikuwa ameungama akiwa amechelewa, na viongozi wake waliamua kwamba alihitaji kurudi nyumbani Ingawa tulihuzunika sana kuwa kwamba hakuwa mwaminifu na hakuwa ametubu kabla ya kuja katika misheni yake, njiani kuelekea kwenye uwanja wa ndege kwa dhati na upendo tulimsifu kwa kuwa na ujasiri wa kujitokeza, na tuliahidi kumweka katika mawasiliano ya karibu na yeye.

Kijana huyu wa ajabu alibarikiwa kuwa na wazazi wa ajabu, viongozi wa ajabu wa ukuhani, kata saidizi na yenye upendo. Baada ya mwaka ya kufanya kazi kwa bidii ili kutubu kikamilifu na kushiriki Upatanisho wa Mwokozi, aliweza kurudi kwenye misheni yetu. Ni vigumu kwangu kueleza hisia za furaha tulizohisi wakati tulipomchukua kijana huyu kutoka uwanja wa ndege. Alijawa na Roho, furaha, mjasiri mbele za Bwana, na tayari kutimiza misheni kwa uaminifu. Yeye akawa misionari hodari, na baadaye mume wangu na mimi tulikuwa na furaha ya kuhudhuria hekalu kwa ajili ya kufungishwa kwake.

Kwa upande mwingine, nafahamu mmisionari mwingine, ambaye akijua kwamba dhambi kabla ya misheni yake ingemrudisha nyumbani mapema, alifanya mpango wake mwenyewe wa kufanya kazi kwa bidii wakati wa misheni yake na kukiri kwa rais wa misheni siku chache tu kabla kukamilisha misheni yake. Alikosa neema ya Mungu na kujaribu kukwepa mpango ambao Mwokozi wetu mpendwa ametoa kwa kila mmoja wetu.

Wakati wa misheni yetu, niliwahi kuambatana na mume wangu alipokwenda kuhoji mtu kwa ubatizo. Wakati mume wangu alipokuwa akifanya mahojiano, nilisubiri nje pamoja na wamisionari kina dada ambao walifundisha mtu huyu. Wakati wa mahojiano yalipomalizika, mume wangu aliwaambia wamisionari kwamba mtu huyo angeweza kubatizwa. Mtu huyu mpendwa alilia na kulia alipoeleza kuwa alikuwa na hakika kwamba dhambi alizotenda katika maisha yake zingemzuia kuweza kubatizwa. Mara chache nimeshuhudia shangwe na furaha ya mtu aliyetoka gizani na kuingia katika mwanga sawa na kile nilichoshuhudiwa siku hiyo.

Picha
Mwokozi hutoa tumaini

Mzee D. Todd Christofferson alishuhudia:

“Na imani katika Mkombozi [wetu] mwenye rehema na uwezo wake, uwezekano wa kukata tamaa unageuka kuwa matumaini. Moyo na hamu za mtu hubadilika, na dhambi iliyovutia wakati fulani inazidi kuchukiza sana. …

“… Gharama yoyote ya toba, inamezwa na furaha ya msamaha.”{2

Uzoefu huu unanikumbusha juu ya Enoshi katika Kitabu cha Mormoni, ambaye “alimlilia [Bwana] kwa sala kuu,” kisha akasikia sauti ikisema, “Enoshi, umesamehewa dhambi zako. …

“Na mimi, Enoshi, nilijua kwamba Mungu hawezi kusema uwongo; kwa hivyo, hatia yangu iliondolewa mbali.

“Na nikasema: Bwana, je, inafanywa vipi?

Na akaniambia: Kwa sababu ya imani yako katika Kristo,  … nenda, imani yako imekufanya mkamilifu.”3

Katika kuandaa hotuba hii, nilitaka kujua jinsi wajukuu wetu wanavyoelewa toba na jinsi wanavyojisikia kuhusu Mwokozi, hivyo niliuliza watoto wetu kuwauliza maswali yafuatayo. Niliguswa na majibu ya wajukuu wetu.

Toba ni nini? “Wakati unapomgonga mtu fulani, unasema ‘pole’ na kumsaidia kuinuka.”

Ulihisi vipi unapotubu? “Unaweza kumhisi Yeye; unaweza kuhisi ukujufu Wake, na hisia mbaya zinaondoshwa.”

Unajisikiaje kuhusu Yesu na Baba wa Mbinguni unapotubu? “Najisikia kwamba Yesu anahisi ilistahili kufanya Upatanisho, na ana furaha kwamba tunaweza kuishi pamoja Naye tena.”

Ni kwa nini Yesu na Baba wa Mbinguni wananitaka nitubu? Katika maneno ya mjukuu wangu msichana. “Kwa sababu Wananipenda! Ili niweze kuendelea na kuwa kama Wao, ninahitaji kutubu. Tunataka pia Roho awe nami sikuzote, kwa hivyo ninahitaji kutubu kila siku ili niwe na wandani Wake wa ajabu. Kamwe sitaweza kuwashukuru vya kutosha.”

Wakati Brynlee mwenye umri wa miaka minne aliposikia maswali haya, alisema, “Mimi sijui, Baba. Nifundishe wewe.”

Picha
Brynlee na baba yake

Katika mkutano mkuu wa zamani, Mzee JeffreyR. Holland alitangaza: “Hata iwe ni jinsi gani unavyofikiria umechelewa, iwe ni nafasi ngapi unafikiri umepoteza, iwe ni makosa kiasi gani unahisi umetenda,  … au umbali kiasi gani kutoka nyumbani na familia na Mungu unahisi umeondoka, ninashuhudia ya kwamba bado haujasafiri mbali kuliko mahali upendo wa Mungu unaweza kufika. Haiwezekani wewe kuzama chini zaidi ya kule nuru isiyokoma ya Upatanisho wa Kristo inang’aa.”4

Ee, jinsi gani nataka kila mmoja wa watoto wangu, wajukuu, na kila mmoja wenu—ndugu na dada zangu, kuhisi furaha na ukaribu wa Baba wa Mbinguni na wa Mwokozi wetu tunapotubu dhambi zetu na udhaifu wetu kila siku. Kila mtoto anayewajibika wa Baba wa Mbinguni anahitaji kutubu. Fikiria ni dhambi gani tunahitaji kutubu. Je, ni nini kinachotuzuia? Tunahitaji kujiboresha kwa njia gani?

Mimi najua, kama Rais Packer alivyoona na kushuhudia, kwamba, tunapotubu kwa kweli dhambi zetu hakika zinaondolewa—bila alama! Mimi binafsi nimehisi upendo, furaha, nafuu, na matumaini mbele za Bwana wakati nimetubu kwa dhati.

Kwangu mimi, miujiza kubwa katika maisha si kutawanywa kwa maji ya Bahari ya Shamu, kusongeza milima, au hata uponyaji wa mwili. Muujiza mkubwa hutokea tunapomkaribia Baba yetu wa Mbinguni katika maombi na kusihi kwa dhati ili kusamehewa na kisha kusafishwa kutokana na dhambi hizo kupitia dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi wetu. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.