2010–2019
Mwamuzi Mwenye Haki
Oktoba 2016


Mwamuzi Mwenye Haki

Kunayo njia moja tu ya kuhukumu hukumu ya haki, jinsi afanyavyo Yesu Kristo, na hiyo ni kuwa jinsi Yeye alivyo.

Katika maisha yake ya duniani, Yesu Kristo alikuwa hakimu mwenye upendo, mwenye busara isiyo ya kawaida, na mvumilivu. Anajulikana katika maandiko kama “hakimu mwenye haki” (2 Timotheo 4:8; Musa 6:57), na ushauri Wake kwetu pia ni kuwa “mhukumu hukumu yenye haki” (tazama Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 7:1–2 [katika Mathayo 7:1, tanbihi a]) na “weka imani yako katika Roho yule ambaye huongoza kufanya mema … [na] kuhukumu kwa haki” (M&M 11:12).

Ushauri huu kwa Wanefi Kumi na Wawili utatusaidia kuhumu jinsi Bwana anavyohukumu. “Nyinyi mtakuwa waamuzi wa watu hawa, kulingana na hukumu ambayo nitawapatia, ambayo itakuwa haki. Kwa hivyo mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Amin, nawaambia, hata vile nilivyo” (3 Nefi 27:27; imetiliwa mkazo). Mara nyingine sisi husahau kwamba wakati aliposhauri kuwa alivyo, ilikuwa katika muktadha wa jinsi ya kuhukumu kwa haki.

Hukumu Isiyo ya Haki

Picha
Mwokozi na Mafarisayo na waandishi

Mfano wa aibu wa hukumu isiyo ya haki unatoka kwa fumbo la kondoo aliyepotea wakati Wafarisayo na waandishi walimhukumu vibaya Mwokozi na walioketi naye kwa chakula cha jioni, wakisema “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.” (Luka 15:2)—wasitambue ukweli kwamba pia wao walikuwa wenye dhambi. Wakiwa na mioyo ya kushutumu, waandishi na Wafarisayo hawakuwahi fahamu furaha ya kumwokoa kondoo aliyepotea.

Picha
Mwokozi na mwanamke aliyefumaniwa na uzinzi

Ilikuwa pia ni “waandishi na Mafarisayo ” waliomleta “mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi”(Yohana 8:3) kwake Mwokozi kuona ikiwa angemhukumu kulingana na torati ya Musa (ona mstari wa 5). Mnafahamu kisa hicho, jinsi alivyowanyenyekeza kwa sababu ya hukumu yao ambayo haikuwa ya haki, “wakashitakiwa na dhamiri zao ” na wakaondoka “mmoja mmoja” (mstari wa 9; imetiliwa mkazo). Kisha alimwambia mwanamke yule, “Enenda zako; wala usitende dhambi tena. Na Mwanamke akamsifu Mungu kutoka wakati huo, na kuamini katika jina lake” (Tafsiri ya Joseph Smith, [katika Yohana 8:11 [katika Yohana 8:11, tanbihi c]).

Picha
Mwokozi akizungumza na mwanamke aliyefumaniwa na uzinzi

Mwanaume na Mwanamke wa asili ndani ya kila mmoja wetu yuko na mwelekeo wa kuwashutumu wengine na kuhukumu bila haki, au kujidai wenye haki. Iliwafanyikia pia Yakobo na Yohana, wawili kati ya Mitume wa Mwokozi. Walikasirishwa sana wakati watu wa kijiji ja Wasamaria walimkosea heshima Mwokozi (tazama Luka 9:51–54):

Picha
Mwokozi na wafuasi

“Walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; kama Eliya naye alivyofanya?

“Lakini, akawageukia, akawakanya, na akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.

“Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa.”(mistari ya 54–56).

“Mwamuzi wa wote” wa leo (M&M 107:74) wanapaswa kuepuka mvuto wa ghafla kama huo wa kushutumu, kama walivyofanya Yakobo na Yohana wakati huo. Mwamuzi mwenye haki atajibu kukiri kwa huruma na kuelewa. Kijana mwenye kukosa, kwa mfano, anapaswa kuondoka kwenye ofisi ya askofu akihisi upendo wa Mwokozi kupitia askofu na akiwa amezingirwa na furaha na uwezo wa uponyaji wa Upatanisho—kamwe asiaibishwe au kudharauliwa. Vingenevyo, askofu anaweza bila ya kufahamu akamfurusha kondoo aliyepotea zaidi nyikani (ona Luka 15:4).

Nidhamu

Hata hivyo, huruma haibatilishi haja ya nidhamu. Neno nidhamu linatokana na neno la Kilatino discere “kujifunza,” au discipulus, “mwanafunzi,” kumfanya mwanafunzi kuwa mwanafunzi na mfuasi.1 Kutuoa nidhamu kwa njia ya Bwana ni kufundisha kwa upendo na uvumilivu. Katika maandiko Bwana mara nyingi anatumia neno kurekebisha anapozungumzia nidhamu (ona, kwa mfano, Mosia 23:21; M&M 95:1). Neno kurekebisha linatokana na Kilatino castus, “castus,” linalomaanisha bikira au safi, na kurekebisha ili kusafisha.”2

Duniani, ni hakimu wa duniani anayeshutumu binadamu na kumfunga gerezani. Kwa kulinganisha, Kitabu cha Mormoni kinatufundisha kwamba wakati tunapotenda dhambi makusudi, tunakuwa “tunajihukumu wenyewe” (Alma 41:7) na kujipeleka sisi wenyewe katika gereza la kiroho. Jambo la kinaya ni kwamba mwamuzi wa wote katika kisa hiki yuko na funguo ambazo zinafungua milango ya gereza; “kwani pamoja na kuwarudi ninawatayarishia njia kwa ajili ya ukombozi wao katika mambo yote yatokanayo na majaribu” (M&M 95:1; mkazo umeongezewa). Uamuzi wa hakimu mwenye haki huwa wenye rehema, upendo, na wa kuokoa, sio kushutumu.

Kijana Joseph Smith alipewa nidhamu kwa muda miaka minne wa majaribio kabla ya kupokea yale mabamba ya dhahabu, “kwa sababu hujashika amri za Bwana.”3 Baadaye, wakati Joseph alipoteza zile kurasa 116 za muswada, alipewa nidhamu tena. Ingawaje Joseph alijuta kwa kweli, Bwana bado aliondoa fadhila zake kwa muda mfupi, kwa sababu “wale niwapendao pia huwarudi ili dhambi zao ziweze kusamehewa” (M&M 95:1).

Joseph alisema, “ malaika alifurahi aliponirejeshea ile Urim na Thumim na kusema kwamba Mungu alifurahishwa na uaminifu wangu, na unyenyekevu na kunipenda kwa toba yangu na bidii kenye sala.”4 Kwa sababu Bwana alitaka kumfundisha Joseph funzo muhimu, alihitaji dhabihu yenye kuponda moyo kutoka kwake—dhabihu ikiwa sehemu muhimu ya nidhamu.

Dhabihu

“Katika siku za kale, dhabihu ilikuwa na nia ya kufanya kitu au mtu fulani kuwa mtakatifu,”5 kuiunganisha na, katika hali ya kutegemeana, kwa ufafanuzi wa neno rekebisha—“kutakasa.” Vile vile, katika Israeli ya kale, msamaha ulipatikana kupitia kwa sadaka kwa ajili ya dhambi au hatia, au dhabihu.6 Dhabihu “haikuelekeza tu kwa ile dhabihu kubwa na ya mwisho” (Alma 34:14) lakini ilisaidia kuleta hisia ya dhati ya shukrani kwa ajili ya Upatanisho wa Mwokozi. Ukosefu wa nia ya kutoa dhabihu kama sehemu ya toba yetu kunadhihaki au dunisha dhabihu ya Kristo kuu kwa dhambi hiyo hiyo na kunapuuza mateso yake—ishara sugu ya kutokuwa na shukrani.

Kwa upande mwingine, kupitia kinaya nzuri ya dhabihu, kwa kweli tunapokea kitu chenye thamani ya milele—rehema yake na msamaha na hatimaye “yale yote Baba aliyonayo” (M&M 84:38). Kama sehemu ya mchakato wa toba, dhabihu pia huwa kama zeri ya uponyaji kusaidia kuchukua nafasi ya “majuto ya dhamiri” (Alma 42:18) na “amani katika dhamira” (Mosia 4:3). Bila dhabihu, mtu anaweza kupata ni vigumu kujisamehe, kwa sababu ya dhamira inayodumu ya jambo lililofichwa.7

Mzazi Kama Hakimu Mwenye Haki

Wakati wachache kati yetu wataitwa kuwa waamuzi wa wote, kanuni za uamuzi wa haki zinafaa kwetu sote, hasa kwa wazazi ambao wana nafasi kila siku kuzitumia kanuni hizi kwa watoto wao. Kumfundisha mtoto kwa ufanisi ni kiini cha uzazi mwema, na kutoa nidhamu kwa upendo ni kiini cha kuwa mwamuzi mwenye haki.

Rais Joseph F. Smith alifundisha, “Ikiwa watoto ni waasi na wagumu kudhibiti, kuwa mvumilivu nao hadi utakapoweza kuwashinda kwa upendo, … na kisha unaweza basi [kunyoosha] tabia zao upendavyo.”7

Ni umaizi kwamba katika kufundisha jinsi ya kupeana nidhamu, manabii wanaonekana siku zote kurejelea sifa za Kristo. Mafundisho na Maagano inatupa ushauri unaojulikana vyema kuhusu nidhamu:

“Hakuna nguvu au uwezo unaoweza au upaswao kudumishwa kwa njia ya ukuhani, isipokuwa tu kwa njia ya ushawishi, kwa uvumilivu, kwa upole na unyenyekevu, na kwa upendo usio unafiki;

“Kwa wema, na maarifa safi, ambayo yataikuza sana nafsi isiyo na unafiki, na isiyo na hila—

“Kukemea kwa ukali kwa wakati wake, utakapokuwa umeongozwa na Roho Mtakatifu; na halafu baadaye kuonyesha ongezeko la upendo” (M&M 121:41–43).

Maandiko haya yanatufundisha kukemea “utakapokuwa umeongozwa na Roho Mtakatifu,” sio unapoongozwa na hasira. Roho Mtakatifu na hasira hawalingani, kwa sababu “yule ambaye ana roho ya ubishi siye wangu, lakini ni wa ibilisi, ambaye ni baba wa ubishi, na huchochea mioyo ya watu kubishana na hasira” (3 Nefi 11:29). Rais George Albert Smith alifundisha kwamba “mambo yasiyokuwa mema mara nyingi hayasemwi chini ya msukumo wa Bwana. Roho wa Bwana ni roho mwenye wema; ni roho mwenye uvumilivu; ni roho wa hisani na upendo na ustahimili na uvumilivu. …

… Lakini ikiwa tutakuwa na roho wenye kutafuta makosa … katika njia haribifu, ambayo kamwe haiji kwa kuongozwa na Roho wa Baba yetu wa Mbinguni na daima ni haribifu.

“…Wema ni uwezo ambao Mungu ametupa kufungua mioyo migumu na kudhibiti nafsi kaidi.”9

Utambulisho wa Kweli wa Watoto Wetu

Wakati ambapo Mwokozi aliwatembelea Wanefi, alifanya jambo la ajabo na watoto:

Picha
Mwokozi na Watoto Wanefi

“Na ikawa kwamba aliwafundisha na kuwahudumia watoto wa umati … , na aliwapatia uwezo wa kuongea, na waliwazungumzia baba zao vitu vikubwa na vya ajabu. …

“… Na waliona na kusikia watoto hawa; ndio, hata watoto wachanga walifungua vinywa vyao, na kuongea vitu vya kustaajabisha” (3 Nefi 26:14, 16).

Pengine zaidi ya kufungua vinywa vya watoto wachanga, Bwana alikuwa akifungua macho na masikio ya wazazi wao waliokuwa wamestaajabu. Wazazi hao walikuwa wamepewa zawadi ya ajabu ya kutazama katika milele na kuona utambulisho wa ukweli na kimo cha maisha ya kabla ya dunia cha watoto wao. Je, hilo halingebadilisha milele jinsi ambavyo wazazi wanavyowaona na kuwatunza watoto wao? Ninapenda mageuzo haya ya dondoo hii ya Goethe: “Jinsi unavyomwona [mtoto] ndivyo unavyomtunza, na jinsi unavyomtunza ndivyo atakavyokuwa.”,9 Kukumbuka utambulisho wa kweli wa mtoto ni zawadi ya utabiri ambao kwa uungu unatia msukumo mtazamo wa mwamuzi mwenye haki.“

Hitimisho

RaisThomas S. Monson ametufundisha, “Kamwe usiruhusu shida ya kutatuliwa kuwa muhimu zaidi ya mtu anayepaswa kupendwa.”11 Ni muhimu sana kiasi gani kanuni hii ilivyo katika kuwa waamuzi wenye haki, hasa na watoto wetu.

Kunayo njia moja tu ya kuhukumu hukumu ya haki, jinsi afanyavyo Yesu Kristo, na hiyo ni kuwa jinsi Yeye alivyo. Kwa hivyo, “mnapaswa kuwa watu [pamoja na wanawake] wa aina gani? Amin, nawaambia, hata vile nilivyo” ((3 Nefi 27:27). Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona “disciple,” etymonline.com.

  2. Ona Merriam-Webster’s Collegiate Dictionary, 11th ed. (2003), “chasten.”

  3. Karen Lynn Davidson and others, eds., Histories, Volume 1: Joseph Smith Histories, 1832–1844, vol. 1 of the Histories series of The Joseph Smith Papers (2012), 83.

  4. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 71; emphasis added.

  5. Guide to the Scriptures, “Sacrifice,” scriptures.lds.org.

  6. Ona Bible Dictionary, “Sacrifices.”

  7. Dhabihu tunayotoa kwenye altari ya meza ya sakramenti kila wiki ni moyo uliovunjika na roho iliyopondeka (ona 2 Nefi 2:7; 3 Nefi 9:20; Mafundisho na Maagano 59:8). Moyo uliovunika ni moyo wa toba; roho iliyopendeka ni roho ya utiifu (see D. Todd Christofferson, “When Thou Art Converted,” Liahona, May 2004, 12).

  8. Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith (1998), 299.

  9. Teachings of Presidents of the Church: George Albert Smith (2011), 225, 226, 228; emphasis added.

  10. Inahusishwa na Johann Wolfgang von Goethe, brainyquote.com.

  11. Thomas S. Monson, “Finding Joy in the Journey,” Liahona, Nov. 2008, 86.