2010–2019
Ujasiri katika Ushuhuda wa Kristo
Oktoba 2016


Jasiri katika Ushuhuda wa Kristo

Hatuwezi kukubali kuona ushuhuda wetu wa Baba na Mwana ukanganywae na kuchanganywa na vikwazo.

Uzima wa milele ni zawadi kubwa zaidi ya Mungu na hutolewa kwa wale “wanaotii amri za [Mungu] na kuvumilia hadi mwisho.”1 Kwa upande mwingine, uzima wa milele pamoja na Baba yetu wa Mbinguni unyimwa wale “ambao sio jasiri katika ushuhuda wa Yesu.”2 Kuna idadi ya vikwazo kwa ujasiri wetu ambavyo vinaweza kutuzuia sisi kufikia malengo ya uzima wa milele.3 Vikwazo vinaweza kuwa changamani; acha dhihirishe

Miaka mingi iliyopita baba yangu alijenga kibanda kidogo katika shamba la mifugo sehemu aliyolelewa. Taswira ya eneo la malisho ilikuwa ya kipekee. Wakati kuta zilipojengwa katika kibanda, nilitembelea huko. Nilishangazwa kwamba dirisha lilitazama moja kwa moja kwenye nguzo ya umeme iliyokuwa umbali mdogo toka kwenye nyumba. Kwangu mimi, ilikuwa ni kizuizi cha mwonekano mzuri.

Picha
Nguzo ya umeme upeo wa nje dirishani

Nilisema, “Baba, kwa nini uliwaacha waweke nguzo ya umeme mbele ya upeo wa macho yako toka dirishani?”

Baba yangu, mtu wa vitendo na mkimya, alielezea kwa hisia, “Quentin, nguzo hiyo ya umeme ni kitu kizuri kwangu kwenye shamba lote la mifugo!” Kisha akatoa maelezo yake. “Ninapoiangalia nguzo ile, nagundua kwamba, tofauti na wakati nilikulia hapa, sitahitaji kubeba maji kwenye vyombo toka mtoni hadi nyumbani ili kupikia, kunawa mikono, au kuoga. Sitahitaji kuwasha mishumaa au taa ya mafuta usiku ili nisome. Ninataka kuiona ile nguzo katikati ya upeo wa macho wa dirishani.”

Baba yangu alikuwa na mtazamo tofauti juu ya nguzo ya umeme kuliko niliokuwa nao. Kwake yeye ile nguzo iliwakilisha maendeleo katika maisha, lakini mimi ilikuwa ni kizuizi cha taswira nzuri. Baba yangu aliuthamini umeme, mwanga, na usafi zaidi taswira nzuri. Mara moja nikagundua kwamba nikiwa nafikiria nguzo ilikuwa ni kizuizi kwangu, ilikuwa na maana halisi, ishara yenye maana kwa baba yangu.

Kizuizi ni “kikwazo katika imani au ufahamu” au “kikwazo cha maendeleo.”4 Kujikwaa kiroho ni “kuanguka katika dhambi au uasi.”5 Kikwazo kinaweza kuwa kitu chochote ambacho kinatuvuruga sisi kufikia malengo mema.

Hatuwezi kukubali kuona ushuhuda wetu wa Baba na Mwana ukanganywae na kuchanganywa na vikwazo. Hatuwezi kuanguka katika mtego huo. Ushuhuda wetu Kwao unahitaji ubaki msafi na rahisi kama vile utetezi rahisi wa baba yangu wa nguzo ya umeme katika shamba la mifugo alikokulia.

Je, baadhi ya vikwazo gani ambavyo vinavyokanganya na kuchanganya ushuhuda wetu rahisi wa Baba na Mwana kutuzuia kuwa jasiri katika ushuhuda huo?

Kikwazo Kimoja ni Falsafa za Wanadamu

Tumejizatiti kwa kila aina ya elimu na kuamini “utukufu wa Mungu ni akili.”6 Lakini tunajua pia mkakati unaotumiwa na adui ni kuwaongoza watu mbali na Mungu na kuwafanya wajikwae kwa kusisitiza falsafa za wanadamu juu ya Mwokozi na mafundisho Yake.

Mtume Paulo alikuwa shahidi wa kweli wa Yesu Kristo kwa sababu ya uzoefu wa kimuujiza na wa kubadilisha maisha aliopata na Bwana7 Historia ya ajabu ya nyuma ya Paulo ilimwandaa kuishi na watu wa tamaduni nyingi. Alipenda “ukweli wa wazi” wa Wathesolanike na “huruma mwororo” ya Wafilipi.8 Awali alipata kuwa vigumu zaidi kuwaelewa Wagriki wasomi na wastaarabu. Katika Athens juu ya Areopago, alijaribu mbinu ya kifalsafa na ilikataliwa. Kwa Wakorintho, alidhamiria kuwafundisha “mafundisho ya kusulubiwa kwa Kristo.”9 Kwa kutumia maneno ya Mtume Paulo mwenyewe:

“Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu:

“Ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.”10

Baadhi ya matukio ya ajabu sana ya kimaandiko ya Mwokozi na misheni Yake yameainishwa katika 1 Wakorintho. Sura moja—15—imepata usikivu duniani kote kupitia maonyesho ya George Frideric Handel Masiya .11 Ina mafundisho ya kushangaza kumhusu Mwokozi. Katika sehemu ya tatu ya Masiya, mara baada ya “Kibwagizo cha Haleluya” maandiko yaliyotumiwa zaidi yanatoka katika 1 Wakorintho 15. Katika baadhi ya mistari hii, Paulo kwa uzuri anaelezea baadhi ya yale aliyotimiza Mwokozi:

“{Kwani] sasa Kristo amefufuka katika wafu, … limbuko lao waliolala.

“… Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

“Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. …

“U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? …

“Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.”12

Tunajua ukengeufu ulitokea kwa sehemu kwa sababu ya falsafa za mwanadamu ziliwekwa juu ya mafundisho ya msingi ya Kristo. Badala ya ujumbe rahisi wa Mwokozi, ukweli mwingi na mzuri ulibadilishwa au kupotea. Kwa kweli, Ukristo ulirithi baadhi ya tamaduni za kifalsafa za Kigriki ili kupatanisha imani zao na utamaduni wao uliokuwepo. Mwanahistoria Will Durant aliandika: “Ukristo haukuangamiza upagani; ulirithi. Akili ya Kigiriki, ikiwa inakufa, ilikuja kuingia katika maisha ya mhamo.”13 Kihistoria, na katika siku yetu wenyewe, baadhi ya watu hukataa injili ya Yesu Kristo kwa sababu, kwa maoni yao, haina ustaarabu wa usomi wa kutosha.

Mwanzoni mwa Urejesho, wengi angalao walikiri kuyafuata mafundisho ya Mwokozi. Nchi nyingi hujifikiria wenyewe kama mataifa ya Kikristo. Lakini hata hapo kale kulikuwa na unabii wa nyakati ngumu zaidi katika siku yetu.

Heber  C. Kimball alikuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa asili wa kipindi hiki na Mshauri wa Kwanza wa Rais Brigham Young. Alionya: “Muda unakuja wakati … itakuwa vigumu kuitofautisha sura ya Mtakatifu na ile sura ya adui wa watu wa Mungu. Kisha … angalia mchekecho mkubwa, kwani kutakuwa na muda wa mchujo, na wengi wataanguka.” Alimalizia kuna “JARIBIO linalokuja.”14

Katika siku yetu, ushawishi wa Ukristo katika nchi nyingi, ikijumuisha Marekani, umepungua sana. Bila ya imani za kidini, hakuna hali ya kuwajibika kwa Mungu. Kufuatana na hili, ni vigumu kuanzisha maadili ya wote kuhusu jinsi ya kuishi. Falsafa ambazo zinazoshikiliwa mara nyingi zinahitilafiana.

Kwa bahati mbaya, hii pia hutokea kwa baadhi ya waumini wa Kanisa ambao hupoteza mwelekeo wao na wanashawishika mambo ya muda—mengi ambayo ni wazi si mema.

Sambamba na unabii wa Heber C. Kimball, Mzee Neal A. Maxwell alisema mwaka 1982: “Mchekecho mwingi utatokea kwa sababu ya kulegeza tabia za haki ambazo huenda bila toba. Wachache watakata tamaa badala ya kushikilia hadi mwisho. Wachache watadanganywa na wasaliti. Vivyo hivyo, wengine watachukizwa, wengi kwa kila kipindi watakuwa vikwazo!”15

Kikwazo kingine ni Kukataa Kuiona Dhambi katika Mwanga Wake Wenyewe

Moja ya mambo ya kipekee na ya kusumbua siku hizi ni kwamba watu wengi hujiingiza katika vitendo vya dhambi lakini hukataa kufikiria ni dhambi. Hawana majuto au nia ya kukiri tabia zao kwa kuziona kuwa zina makosa ya kimaadili. Hata baadhi ya wanaokiri imani katika Baba na Mwana wanachukulia kimakosa nafasi ambayo Baba wa Mbinguni mwenye upendo hafai kuweka madhara ya tabia ambayo ni kinyume na amri Zake.

Hii ilionekana ni nafasi iliyochukuliwa na Koriantoni, mwana wa Alma Mdogo katika Kitabu cha Mormoni. Alijihusisha na tabia mbaya ya kutenda kinyume na maadili na alikuwa akionywa na Alma. Tumebarikiwa kwamba nabii mkuu Alma, ambaye binafsi alikumbana na “giza nyingi [na] mwangaza wa ajabu,”16 aliandika agizo alilotoa. Katika mlango wa 39 wa Alma, tunasoma jinsi alivyomshauri mwana huyu kupitia njia ya toba na kisha kuelezea jinsi Kristo alivyokuja kuiondoa dhambi. Aliweka wazi umuhimu wa toba kwa Koriantoni kwa sababu “hakuna kitu kichafu kitakachorithi ufalme wa Mungu.”17

Alma 42 ina baadhi ya mafundisho makuu juu ya Upatanisho katika maandiko yote. Alma alimsaidia Koriantoni kuelewa kwamba si “haki kwamba wenye dhambi watupiliwe kwenye hali ya taabu.”18 Lakini alisema kwamba kuanzia Adamu, Mungu wa rehema ametoa “nafasi kwa ajili ya toba” kwa sababu bila toba, “mpango mkuu wa wokovu ungezuiliwa.”19 Alma pia alithibitisha kwamba mpango wa Mungu ni “mpango wa furaha.”20

Mafundisho ya Alma yanaelimisha sana: “Kwani tazama, haki hutekeleza madai yake yote, na pia huruma hudai yote yaliyo yake; na hivyo, hakuna ila tu waliotubu kwa ukweli watakaokolewa.”21 Ikionekana katika mwanga wake wa kweli, baraka tukufu za toba na kusikiliza mafundisho ya Mwokozi ni ukumbusho muhimu. Sio makosa kuwa wazi, kama Alma alivyokuwa kwa Koriantoni, kuhusu matokeo ya uchaguzi wa dhambi na ukosefu wa toba. Imeelezwa mara nyingi, “Sasa au baadaye kila mtu atakaa chini kwenye karamu ya matokeo.”22

Baraka za ajabu za selestia za Upatanisho wa Mwokozi ni kwamba kwa njia ya toba, matendo ya dhambi yanafutwa. Baada ya toba ya Koriantoni, Alma alimaliza kwa kusema, “Usiache vitu hivi vikusumbue mara nyingine, na ni dhambi zako tu zikusumbue, pamoja na taabu hiyo ambayo itakuleta wewe kwenye toba.”23

Kuangalia Zaidi ya Lengo ni Kikwazo

Nabii Yakobo aliwafananisha Wayahudi wa kale kama “watu wenye shingo ngumu” walidharau maneno yaliyokuwa wazi, “wakawaua manabii, na wakatafuta vitu ambavyo hawakuweza kuvifahamu. Kwa hivyo, kwa sababu ya upofu wao, upofu ambao ulitokana na kuangalia zaidi ya lengo, lazima waanguke.”24

Kukiwa na mifano mingi ya kuangalia zaidi ya lengo,25 ijulikanayo katika siku hizi ni siasa kali. Injili ya siasa kali ni wakati mtu mmoja huinua kanuni yoyote ya injili juu ya kanuni nyingine muhimu na kuchukua nafasi zaidi ya au kinyume na mafundisho ya viongozi wa Kanisa. Mfano mmoja ni wakati mtu anapotetea nyongeza, mabadiliko, au mkazo wa msingi kwenye kipengele kimoja cha Neno la Hekima. Mwingine ni maandalizi ya gharama kwa ajili ya “matukio siku za mwisho.” Katika mifano yote miwili, wengine wanahimizwa kupokea tafsiri za pembeni. “Kama tunaigeuza sheria ya afya au kanuni nyingine yoyote kwenda kwenye hali ya ushabiki wa kidini, tunaangalia zaidi ya alama.”26

Tukizungumzia mafundisho muhimu, Bwana alieleza, “Yeyote atangazaye zaidi au pungufu kuliko hili, huyo siye wangu.”27 Tunapoinua kanuni yoyote kwa namna ambayo inapunguza kujitoa kwetu kwenye kanuni nyingine muhimu au kuchukua nafasi tofauti na au inayozidi mafundisho ya viongozi wa Kanisa, tunaangalia zaidi ya alama.

Kwa nyongeza, baadhi ya waumini hukuza sababu, nyingi ya hizo ni nzuri, kwa hali bora kwa mafundisho ya msingi ya injili. Wanabadilisha kujitoa kwao kwenye jambo fulani kama jukumu lao la kwanza na kuliacha jukumu la Mwokozi na mafundisho Yake kama nafasi ya pili. Kama tunaweka kitu chochote juu ya kujitoa kwetu kwa Bwana, kama matendo yetu yanamtambua Yeye kama mwalimu mwingine tu na siyo Mwana mtukufu wa Mungu, hivyo tunatazama zaidi ya alama. Yesu Kristo ni alama!

Sehemu ya 76 ya Mafundisho na Maagano inaweka wazi kuwa “shujaa katika ushuhuda wa Yesu”28 ni mtihani rahisi, muhimu kati ya wale watakaorithi baraka za ufalme wa selestia na wale walio katika ufalme mdogo wa terestia. Kuwa jasiri tunahitaji kufokasi katika uwezo wa Yesu Kristo na sadaka Yake ya upatanisho ili kushinda kifo na, kwa njia ya toba, kutusafisha toka dhambini na kufuata mafundisho ya Kristo.29 Pia tunahitaji mwanga na elimu ya maisha na mafundisho ya Mwokozi ili kutuongoza katika njia ya agano, ikiwemo ibada takatifu ya hekalu. Lazima tuwe imara kwa Kristo, tukila neno lake, na kuvumilia hadi mwisho.30

Hitimisho

Kama tunahitaji kuwa jasiri katika ushuhuda wetu wa Yesu, lazima tuepuke vikwazo ambavyo vinatutega na kuzorotesha safari za wanaume na wanawake wengi wa kuheshimika. Acheni tujizatiti kuwa katika utumishi Wake daima. Tukiwa tunatafuta elimu, tunatakiwa kukwepa falsafa za wanadamu ambazo zinadidimiza dhamira yetu kwa Bwana. Lazima tuione dhambi katika mwanga wake wa kweli na kuupokea Upatanisho wa Mwokozi kwa njia ya toba. Tunatakiwa kuepuka kuangalia zaidi ya alama na kulenga kwa Yesu Kristo, Mwokozi na Bwana wetu, na kufuata mafundisho Yake.

Baba yangu aliiona nguzo kama chanzo cha kutoa umeme, mwanga, na maji mengi kwa ajili ya kupikia na kuoshea. Iilikuwa ni jiwe kuu la kukanyagia ili kuboresha maisha yake.

Mwandishi mmoja alipendekeza kwamba vikwazo vinaweza kuwekwa katika jiwe kuu la kukanyagia kwenda kwenye tabia njema na Mbinguni.”31

Kwetu sisi, kuwa jasiri katika ushuhuda wa Yesu ni jiwe kuu la kukanyagia kuelekea kufuzu kwa huruma ya Mwokozi na ufalme wa selestia. Yesu Kristo ndilo jina pekee chini ya mbingu ambalo tunaweza kuokolewa.32 Ninatoa ushahidi wangu wa kweli wa uungu Wake na jukumu Lake katika mpango wa Baba. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Mafundisho na Maagano 14:7; ona pia Yohana 17:3.

  2. Mafundisho na Maagano 76:79.

  3. Ona True to the Faith: A Gospel Reference (2004), 52–53.

  4. Merriam-Webster’s Collegiate Dictionary, 11th ed. (2003), “stumbling block.”

  5. Merriam-Webster’s Collegiate Dictionary, “stumble.”

  6. Mafundisho na Maagano 93:36.

  7. Ona Matendo ya Mitume 9:1–9; 26:13–18.

  8. Ona Frederic W. Farrar, The Life and Work of St. Paul (1898), 319.

  9. Ona Farrar, The Life and Work of St. Paul 319–20.

  10. 1 Wakorintho 2:4–5.

  11. Ona George Frideric Handel, Messiah, ed. T. Tertius Noble (1912).

  12. 1 Wakorintho 15:20–22, 55, 57.

  13. Will Durant, The Story of Civilization, vol. 3, Caesar and Christ (1944), 595.

  14. Heber  C. Kimball, in Orson F. Whitney, Life of Heber C. Kimball (1945), 446.

  15. Neal A. Maxwell, “Be of Good Cheer,” Ensign, Nov. 1982, 68.

  16. Mosia 27:29.

  17. Alma 40:26.

  18. Alma 42:1. Katika mafundisho ya Watakatifu wa Siku za Mwisho, nafasi imetolewa kwa wanadamu wote ikijumuisha wale ambao hawatasikia kuhusu Kristo katika maisha haya, watoto ambao hufa kabla ya umri wa kuwajibika, na wale ambao hawana uelewa (ona Mafundisho na Maagano 29:46–50; 137:7–10).

  19. Alma 42:5.

  20. Alma 42:8.

  21. Alma 42:24. Note that the personal pronoun for justice is his (male) and the personal pronoun for mercy is her (female).

  22. Robert Louis Stevenson, katika Carla Carlisle, “A Banquet of Consequences,” Country Life Magazine, July 6, 2016, 48. Mrs. Carlisle credits Robert Louis Stevenson for the quote. Baadhi huwasifia wengine.

  23. Alma 42:29.

  24. Yakobo 4:14.

  25. Katika makala ambayo niliandika kwa magazeti ya Kanisa mwaka wa 2003, nilisisitizia maeno manne ambayo yanaweza kuanzisha upofu wa kidini na kujikwaa ambako Yakobo alielezea: kubadilisha falsafa za wanadamu kwa kweli za injili, injili ya msimamo mkali, vitendo vya umahiri kama mbadala wa kuweka wakfu kila siku, na kuinua sheria kushinda mafundisho.(ona“Looking beyond the Mark,” Liahona, Mar. 2003, 21–24).

  26. Quentin L. Cook, “Looking beyond the Mark,” Liahona, Mar. 2003, 22–24.

  27. Mafundisho na Maagano 10:68.

  28. Mafundisho na Maagano 76:79.

  29. Ona 2 Nefi 31:17–21.

  30. Ona 2 Nefi 31:20–21.

  31. Henry Ward Beecher, katika Tryon Edwards, A Dictionary of Thoughts (1891), 586.

  32. Ona 2 Nefi 31:21; Mosia 3:17.