2010–2019
Acha Roho Mtakatifu Aongoze
Aprili 2017


Acha Roho Mtakatifu Aongoze

Kwa jukumu takatifu, Anahuisha, anashuhudia, anafundisha, na kutushawishi kuenenda katika nuru ya Bwana.

Akina kaka na dada, mimi, kama ninyi nyote, ninatambua kuwa tunaona kuharakishwa kwa kazi ya Bwana kupitia kwa Rais Thomas S. Monson na ujumbe wake asubuhi hii. Rais Monson, tunakupenda, tunakukubali, na tunakuombea daima, “mpendwa nabii wetu.”1

Tumehisi uwepo wa Roho wa Bwana wikiendi hii. Iwe upo hapa katika ukumbi huu mkuu au unatazama nyumbani au mmekusanyika katika majengo ya kanisa katika sehemu za mbali za ulimwengu, mmepata nafasi ya kuhisi Roho wa Bwana. Roho huyo huthibitisha kwenye mioyo yenu na akili zenu ukweli uliofundishwa katika mkutano huu.

Fikiria maneno ya wimbo huu unaofahamika:

Acha Roho Mtakatifu Aongoze;

Acha atufundishe kilicho cha kweli.

Atashuhudia juu ya Kristo,

Angaza akili zetu kwa mtazamo wa mbinguni.2

Kutoka ufunuo wa siku za mwisho tunajua kwamba Uungu unajumuisha viumbe watatu na tofauti: Baba yetu wa Mbinguni; Mwanae Wapekee, Yesu Kristo; na Roho Mtakatifu. Tunajua kwamba “Baba ana mwili wa nyama na mifupa wenye kushikika kama wa mwanadamu; na Mwana vile vile; lakini Roho Mtakatifu hana mwili wa nyama na mifupa, bali ni mtu wa Kiroho. Kama isingekuwa hivyo, Roho Mtakatifu asingeweza kukaa ndani yetu.”3

Ujumbe wangu leo unalenga juu ya umuhimu wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Baba yetu wa Mbinguni alijua kwamba tungekumbana na changamoto, taabu, na machafuko; Alijua tungeshawishika na maswali, kukata tamaa, majaribu na udhaifu. Kutupa nguvu za kimwili na mwongozo wa kiroho, Alimtoa Roho, jina jingine Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu hutufunga sisi kwa Bwana. Kwa jukumu takatifu, Anahuisha, anashuhudia, anafundisha, na kutushawishi kuenenda katika nuru ya Bwana. Tuna jukumu takatifu kujifunza kugundua ushawishi Wake katika maisha yetu na kujibu.

Kumbuka ahadi ya Bwana: “Nitakupa Roho wangu, ambaye ataiangaza akili yako, ambayo itaijaza nafsi yako kwa shangwe.”4 Ninapenda hakikisho hilo! Shangwe inayojaza nafsi zetu huleta matarajio ya milele katika kutofautisha maisha ya siku hadi siku. Shangwe hiyo inakuja kama amani wakati wa shida au huzuni kubwa. Inaleta ufariji na ujasiri, kuufungua ukweli wa injili, na kukuza upendo wetu kwa Bwana na kwa watoto wote wa Mungu. Ijapokuwa uhitaji wa baraka za aina hiyo ni mkubwa, katika njia nyingi ulimwengu umewasahau na kuwaacha.

Kila wiki tunapopokea sakrament takatifu, tunaweka maagano ya “wakati wote kumkumbuka yeye,” Bwana Yesu Kristo, na dhabihu Yake ya upatanisho. Katika kutii agano takatifu, ahadi imetolewa kwamba “ili daima Roho wake apate kuwa pamoja [nasi].”5

Ni jinsi gani tunafanya hivyo?

Kwanza, tunajitahidi kuishi kwa kustahili Roho.

Roho Mtakatifu hukaa na wale ambao ni “waangalifu kumkumbuka Bwana Mungu wao siku hadi siku.”6 Kama vile Bwana alivyoshauri, lazima “tuyaweke kando mambo ya ulimwengu huu, na kuyatafuta mambo ya ulimwengu ulio bora,”7 kwani “Roho ya Bwana haishi kwenye mahekalu yasiyo matakatifu”8 Lazima kila mara tujaribu kutii sheria za Mungu, kusoma maandiko, kuomba, kuhudhuria hekalu, na kuishi kikweli makala ya imani ya kumi na tatu, “kuwa waaminifu, wakweli, wasafi, wakarimu, wema, na … kutenda mema kwa watu wote.”

Pili, lazima tukubali kupokea Roho.

Ndiyo, tazama, nitakujulisha wewe akilini mwako na katika moyo wako, kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye atakujia na ambaye atakaa moyoni mwako.9 Nilianza kujua haya nikiwa mmisionari kijana huko Scotch Plains, New Jersey. Siku moja Julai asubuhi mwenza wangu na mimi tulihisi kuongozwa kuangalia marejeo ya majina ya Temple Square. Tulibisha mlango wa nyumba ya Elwood Schaffer. Bi. Schaffer kwa upole alitukatalia.

Alipoanza kufunga mlango, nilihisi kufanya kitu ambacho sijawahi kukifanya na sijakifanya tena toka siku hiyo! Niliweka mguu wangu mlangoni na kuuliza, “Kuna mtu mwingine yeyote ambaye angependa ujumbe wetu?” Binti yake wa miaka 16, Marti, alikuwa na shauku, na aliomba kwa ajili ya mwongozo siku moja kabla. Marti alikutana nasi, na wakati huo, mama yake alishiriki kwenye mazungumzo. Wote wawili walijiunga na Kanisa.

Picha
Mzee Rasband kama mmisionari

Kilichotokea baada ya ubatizo Marti, watu 136, wakiwemo wengi wa familia yake, wamebatizwa na kuweka maagano ya injili. Nina shukrani kubwa kiasi gani kwamba nilimsikiliza Roho na kuweka mguu wangu kwenye mlango siku ile ya joto la Julai. Marti na idadi ya familia yake wapo hapa leo.

Tatu, lazima tugundue Roho anapokuja.

Uzoefu wangu umekuwa kwamba Roho mara nyingi anawasiliana nasi kwa njia ya hisia. Unahisi katika maneno ambayo unayaelewa, ambayo yanaeleweka kwako, ambayo “yanakuongoza wewe.” Fikiria majibu ya Wanefi wakiwa wanamsikiliza Bwana akiomba kwa ajili yako. Na umati ulisikia na hulitoa ushuhuda; na mioyo yao ilifunguka na walisikia katika mioyo yao, maneno ambayo aliomba.10 Walihisi katika mioyo yao maneno ya sala Yake. Sauti ya Roho Mtakatifu ni nyororo na ndogo.

Katika Agano Jipya, Eliya alipambana na makuhani wa Baali. Makuhani walitarajia “sauti” ya Baali kushuka chini kama radi na kuteketeza dhabihu zao kwa moto. Lakini hapakuwa na sauti, wala moto.11

Wakati mwingine baadaye, Eliya aliomba. “Na, tazama, Bwana akapita, na kuvumisha upepo mkali ambao uliporomosha milima na kuvunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwemo kwenye upepo: na baada ya upepo likaja tetemeko, lakini Bwana hakuwemo kwenye tetemeko:

“Na baada ya tetemeko ukaja moto; lakini Bwana hakuwemo kwenye moto: na baada ya moto ikaja sauti nyororo tulivu.”12

Unaijua hiyo sauti?

Rais Monson amefundisha, “Tunapoendelea na safari ya maisha, acha tujifunze lugha ya Kiroho.”13 Roho anaongea maneno ambayo “tunahisi.” Hisia hizi ni pole, zinatenda kwa kugusa, kufanya kitu, kusema kitu, kujibu kwa njia fulani. Kama sisi ni wa kawaida au wa kutoweka maanani ibada yetu, hujitenga mbali na hupotezwa na mambo ya kidunia, tunajikuta tunapungua katika uwezo wetu wa kuhisi. Kuhusu Roho Mtakatifu, Nefi alimwambia Lamani na Lemueli, “Mmesikia sauti yake mara kwa mara; na amewazungumzia kwa sauti ndogo tulivu, lakini mlikuwa mmekufa ganzi, kwamba hamkupata maneno yake.”14

Mwezi Juni mwaka jana nilikuwa katika jukumu huko Amerika ya Kusini. Tulikuwa kwenye ratiba ngumu ya siku 10 tukitembelea Colombia, Peru, na Ecuador. Tetemeko kubwa liliua mamia ya watu, likijeruhi maelfu, likiharibu na kubomoa nyumba na jamii katika Miji ya Ecuador ya Portoviejo na Manta. Nilihisi kuongozwa kuongeza safari ya kuwatembelea waumini waishio katika miji ile. Barabara zikiwa zimebomoka, hatukuwa na uhakika kama tungefika kule. Hakika, tuliambiwa tusingeweza kufika kule, lakini mwongozo haukutoweka. Hata hivyo, tulibarikiwa na tuliweza kuitembelea miji yote miwili.

Kwa notisi fupi kama ile, nilitegemea viongozi wachache wenye ukuhani wangehudhuria mkutano ule ulioitishwa. Hata hivyo, tulifika katika kila kigingi na kukuta makanisa yamejaa hadi nyuma. Baadhi walikuwa wafuasi wa siku nyingi wa eneo, waanzilishi ambao walijiunga kwanza na Kanisa, wakiwahimiza wenzao kujiunga nao katika kuabudu na kuhisi Roho wa Bwana katika maisha yao. Waliokaa mstari wa mbele walikuwa ni waumini waliopoteza wapendwa wao na majirani kwenye tetemeko. Nilihisi kuongozwa kutawaza baraka za kitume juu ya wote ambao walihudhuria, moja ya kipaji nilichopewa. Japokuwa nilikuwa nimesimama mbele ya chumba, ilikuwa kama vile mikono yangu ilikuwa kwenye kichwa cha kila mmoja wao na nilihisi maneno ya Bwana yakibubujika.

Picha
Mzee na Dada Rasband katika Amerika Kusini

Haikuishia hapo. Nilihisi kuongozwa kuongea nao kama alivyofanya Yesu Kristo alipowatembelea watu katika Amerika. “Akachukua watoto wao wachanga … na kuwabariki, na kuomba kwa Baba juu yao.”15 Tulikuwa Ecuador, tulikuwa kwenye kazi ya Baba yetu, na hawa walikuwa watoto Wake.

Nne, lazima tutende juu ya mwongozo wa kwanza.

Kumbuka maneno ya Nefi: “Na nikaongozwa na Roho, wala sikujua kimbele vitu ambavyo ningefanya.“Walakini niliendelea mbele.”16

Na kwa hivyo na sisi lazima. Lazima tuwe na kujiamini katika mwongozo wetu wa kwanza. Wakati mwingine tunatazama mambo kimantiki, tunashangaa iwapo tunahisi mwongozo wa kiroho au huenda ni mawazo yetu wenyewe. Wakati tunaanza kuhisi mara ya pili, hata mara ya tatu ya hisia zetu—na sisi wote tunafanya hivyo—tunamwondoa Roho; tunakuwa na shaka na ushauri wa kiroho. Nabii Joseph Smith alisema, “Kama utasikiliza kwenye ushawishi wa kwanza, utafanikiwa mara tisa kati ya kumi.”17

Sasa tahadhari: usitarajie mafataki kwa sababu ulimwitikia Roho Mtakatifu. Kumbuka, wewe upo kwenye kazi ya “sauti ndogo, tulivu.”

Nikiwa nahudumu kama rais wa misheni katika Jiji la New York , nilikuwa na baadhi ya wamisionari wetu katika mkahawa huko Bronx. Familia changa ikaja na kukaa karibu nasi. Walionekana walihitaji injili. Niliwatazama wamisionari wetu wakiwa wanaendelea kuwa pamoja nami, kisha waligundua ile familia ikimaliza chakula chao na kutoka nje. Kisha nikasema, “Wazee, kuna somo hapa leo. Mliiona familia nzuri imekuja katika mkahawa huu. Tungeweza kufanya nini?”

Mmoja wa wazee aliongea haraka. “Nilifikiria kusimama na kwenda kuongea nao. Nilihisi muashirio, lakini nilishindwa kuitikia.”

“Wazee,” nilisema, “lazima mara zote tutende wakati wa ushawishi wa kwanza. Muashirio huo uliohisi alikuwa Roho Mtakatifu!”

Ushawishi wa kwanza ni msukumo kutoka mbinguni. Wakati unapoidhinisha au kushuhudia kwetu, tunahitaji kugundua kama ulivyo na kamwe tusiache upite. Mara nyingi, ni Roho anayetusukuma kumfikia mtu, familia na marafiki hususani wenye shida. “Hivyo … sauti ndogo tulivu, ambayo hunong’ona na kupenya vitu vyote,”18 inatuonyesha nafasi ya kufundisha injili, kutoa ushuhuda wa Urejesho na Yesu Kristo, kutoa msaada na kuwaokoa wana wa thamani wa Mungu.

Ifikirie kuwa kama inavyoitwa “mwitikiaji wa kwanza.” Katika jamii nyingi, wahudumu wa kwanza kwenye janga, maafa, au msiba ni zimamoto, polisi, wahudumu Hufika na taa zikimulika, na ninaweza kuongeza, sisi tunawashukuru sana. Njia ya Bwana inaonekana lakini inahitaji maamuzi ya haraka. Bwana anajua mahitaji ya watoto Wake wote—na Anajua nani amejiandaa kusaidia. Kama tutamwacha Bwana ajue wakati wa maombi yetu ya asubuhi kwamba tupo tayari, Atatuita kwenda kuitikia wito. Kama tunaitikia wito, Atatuita kila wakati na tutajikuta wenyewe katika kile Rais Monson anachokiita “ujumbe wa Bwana.”19 Tutakuwa waitikiaji wa kwanza wa kiroho tukitoa msaada kutoka juu.

Kama tunakuwa makini kwenye ushawishi ambao unakuja kwetu, tutakua katika roho wa ufunuo na kupokea zaidi na zaidi Roho mwenye umaizi na mwongozo. Bwana amesema, “Weka imani yako katika Roho yule ambaye huongoza kufanya mema.”20

Naomba tuwekee umakini wito wa Bwana “changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza.”21 Anatuongoza kwa Roho Mtakatifu. Naomba tuishi karibu na Roho, tukitenda kwa haraka wakati wa ushawishi wa kwanza, tukijua unatoka kwa Mungu. Ninatoa ushahidi wa nguvu za Roho Mtakatifu za kutuongoza, kutulinda, na daima kuwa pamoja nasi, katika jina la Yesu Kristo, amina.