2010–2019
Mpango Mtukufu wa Baba Yetu
Aprili 2017


Mpango Mtukufu wa Baba Yetu

Kwa sababu ya npango mtakatifu wa Mungu, tunajua kwamba kuzaliwa na kifo ni tu matukio muhimu katika safari yetu hadi uzima wa milele pamoja na Baba yetu wa Mbinguni.

Mapema katika mafunzo yangu kama daktari, nilipata fursa ya kumsaidia mama kijana kujifungua mtoto wake wa kwanza. Alikuwa ametulia, mwenye kutazamia, na mwenye furaha. Wakati mtoto alipozaliwa, nilimpa mtoto wa thamani aliyemzaa. Kwa machozi ya furaha yakitiririka usoni mwake, alimchukua yule mtoto mpya kabisa mikononi mwake na akamchunguza kutoka kichwani mpaka vidoleni. Alimshika kwa karibu na kumpenda kama vile mama tu anavyoweza. Ilikuwa heshima kuwa kwenye chumba kile pamoja naye.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwanzo wa maisha kwa kila mmoja wetu. Lakini kuzaliwa kwetu ilikuwa kweli ndiyo mwanzo? Ulimwengu unaona kuzaliwa na kifo kama ndio mwanzo na mwisho. Lakini kwa sababu ya mpango mtakatifu wa Mungu, tunajua kwamba kuzaliwa na kifo ni tu matukio muhimu katika safari yetu hadi uzima wa milele pamoja na Baba yetu wa Mbinguni.1 Hizi ni sehemu muhimu za mpango wa Baba yetu—nyakati takatifu ambapo maisha ya duniani na mbinguni zinakatana. Leo, nikifikiria juu ya kile nilichojifunza kutokana kuangalia kuzaliwa na kifo kupitia miaka yangu mingi ya kazi ya udaktari na huduma ya Kanisa, nataka kushuhudia kuhusu mpango mtukufu wa Baba yetu.

Kabla hatujazaliwa,tuliishi na Mungu, Baba ya roho zetu. Sisi wote duniani kwa uhalisia ni makaka na madada katika familia yake,2 na kila mmoja wetu ni wa thamani Kwake. Tuliishi pamoja na Yeye kwa kipindi kirefu kisicho pimika kabla ya kuzaliwa duniani—kujifunza, kuchagua, na kujitayarisha.

Kwa sababu Baba wa Mbinguni anatupenda, Anatutaka tupate zawadi kubwa mno anayoweza kutoa, zawadi ya uzima wa milele.3 Hakuweza kiurahisi tu kutupa zawadi hii; ilitupasa tuipokee kwa kumchagua Yeye na njia Zake. Hii ilihitaji kwamba tuondoke kwenye uwepo Wake na kuanza safari ya ajabu na yenye changamoto, safari ya imani, ukuaji, na kuwa. Safari ambayo Baba yetu wa Mbinguni alitayarisha kwa ajili yetu inaitwa mpango wa wokovu au mpango wa furaha.4

Katika baraza kuu kabla ya kuja duniani Baba yetu alituambia kuhusu mpango Wake.5 Tulipouelewa, tulishangilia sana kiasi kwamba tulipiga kelele za shangwe na “nyota za asubuhi ziliimba pamoja”.6

Mpango ule umejengwa juu ya nguzo kubwa tatu: nguzo za milele.7

Nguzo ya kwamza ni Kuumbwa kwa dunia, kutayarishwa kwa safari yetu ya duniani.8

Nguzo ya pili ni Anguko la wazazi wetu wa kwanza wa duniani, Adamu na Hawa. Kwa sababu ya Anguko hili, baadhi ya vitu vya kupendeza tulipewa. Tuliweza kuzaliwa na kupokea mwili.9 Nitakuwa milele mwenye shukrani kwa mama yangu kwa kuwa leta kaka zangu na mimi katika ulimwengu na kutufundisha kuhusu Mungu.

Mungu pia alitupa haki ya uadilifu ya kujiamulia—uwezo na heshima ya kuchagua na kujitendea sisi wenyewe.10 Ili kutusaidia sisi kuchagua vyema, Baba wa Mbinguni alitupa amri. Kila siku, tunaposhika amri Zake, tunamwonyesha Mungu kwamba tunampenda, na Yeye hubariki maisha yetu.11

Akijua kwamba siku zote tusingechagua vyema,—au kwa maneno mengine tungefanya dhambi,—Baba alitupa nguzo ya tatu: Mwokozi Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Kupitia mateso Yake, Kristo alilipa bei ya vyote kifo cha kimwili na dhambi.13 Yeye alifundisha: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”13

Yesu Kristo aliishi maisha makamilifu, siku zote akitii amri za Baba Yake. Alitembea katika barabara za Palestina,akifundisha kweli za milele, akiponya wagonjwa, akisababisha vipofu waone, na kufufua wafu.”14 Yeye “alikwenda kila mahali akifanya mema”15 na aliwasihi wote kufuata mfano wake.”16

Mwishoni mwa maisha yake ya hapa duniani, alipiga magoti na aliomba,a kisema:

“Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako uniondolee kikombe hiki: walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. …

“Naye, kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hali yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.”17

Kristo anatusaidia kuelewa vyema ukubwa wa mateso Yake wakati alipomwambia Nabii Joseph Smith:

“Mimi, Mungu, nimeteseka mambo haya kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wasiteseke kama watatubu;

“Lakini kama hawatatubu lazima wateseke hata kama Mimi;

“Mateso ambayo yaliyosababisha Mimi mwenyewe, hata Mungu, mkuu kuliko yote, kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutoka damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka mwili na roho.”18

Pale katika Bustani ya Gethsenane, alianza kulipa gharama ya dhambi zetu na magonjwa yetu, maumivu yetu na udhaifu wetu.19 Kwa sababu alifanya hivyo, kamwe hatutakuwa peke yetu katika udhaifu huo kama tukichagua kutembea pamoja Naye. “Alikamatwa na kuhukumiwa kwa mashitaka ya uongo, kutiwa hatiani kuridhisha kundi la watu wenye fujo, na kuhukumiwa kifo juu ya msalaba wa Kalvari.” Juu ya msalaba alitoa maisha Yake kwa ajili ya dhambi za binadamu wote katika zawadi kuu ya uwakilishi kwa niaba ya wote ambao wataishi wakati wowote katika dunia.”20

Alitangaza:

“Tazama, Mimi ni Yesu Kristo ambaye manabii walishuhudia atakuja ndani ya ulimwengu.

“Na tazama mimi ni nuru na uzima wa ulimwengu ; na nimekunywa kutoka kwa kikombe kichungu ambacho Baba amenipatia, na nimemtukuza Baba kwa kujivika dhambi za ulimwengu.”21

Kisha, siku ya kwanza ya wiki,22 Alifufuka kutoka kaburini akiwa na mwili mkamilifu uliofufuka, kamwe hautakufa tena milele. Na kwa sababu alifanya hivyo, ili nasi pia.

Nashuhudia kwamba Kristo kweli alifufuka kutoka kaburini. Lakini ili kufufuka kutoka kaburini, kwanza ilibidi afe. Na kwa hivyo na sisi lazima.

Kingine cha baraka kuu katika maisha yangu imekuwa kuhisi ukaribu wa mbinguni wakati wa nyakati hizo ninapokaa pembeni mwa kitanda cha watu wakati wanapofariki. Mapema asubuhi moja miaka mingi iliyopita, niliingia chumba cha hospitali cha mjane mwaminifu Mtakatifu wa Siku za Mwisho aliyekuwa na saratani. Wawili kati ya mabinti zake walikuwa wamekaa pamoja naye. Wakati nilipokwenda pembeni mwa kitanda chake, kwa haraka niligundua kwamba hakuwa tena anateseka kwa sababu ndio kwanza amekufa.

Katika wakati ule wa kifo, chumba kilikuwa kimejaa amani. Mabinti zake walikuwa na huzuni ya faraja, lakini mioyo yao ilijazwa na imani. Walijua kwamba mama yao hakuwa ameondoka lakini amerudi nyumbani.23 Hata katika wakati wetu wa huzuni mzito, katika nyakati ambapo muda unasimama kimya na maisha yanaonekana sio ya haki, tunaweza kupata faraja katika Mwokozi wetu kwa sababu Yeye aliteseka pia.24 Ilikuwa heshima kwangu kuwa katika chumba kile.

Tunapokufa, roho zetu zinaondoka kutoka kwenye miili yetu na tunakwenda hatua inayofuata ya safari yetu, ulimwengu wa kiroho. Ni sehemu ya kujifunza, kutubu, msamaha, na kuwa25 ambako tunangoja Ufufuko.26

Siku moja kubwa hapo baadaye, kila mtu aliyewahi kuzaliwa atafufuka kutoka kaburini. Roho zetu na miili yetu vitaungana tena katika hali zake kamilifu. Kila mmoja wetu atafufuliwa, “wote wazee na vijana, … wote wanaume na wanawake, wote waovu na wenye haki,” na “ kila kitu kitarejeshwa kwenye umbo lake kamili.”27

Baada ya Ufufuko tutakuwa na baraka kubwa kabisa ya kuhukumiwa na Mwokozi wetu, aliyesema:

“Nitawaleta watu wote kwangu, ili waweze kuhukumiwa kulingana na vitendo vyao.

“Na itakuwa kwamba yeyote atakayetubu na kubatizwa katika jina langu atajazwa; na ikiwa atavumilia hadi mwisho, tazama, yeye hatahukumiwa kuwa na hatia mbele ya Baba yangu kwenye ile siku wakati nitakaposimama kuhukumu ulimwengu.”28

Na kisha, kupitia Kristo na Upatanisho Wake, wote wanao chagua kumfuata Yeye kupitia imani, toba, ubatizo, kumpokea Roho Mtakatifu, na kuvumilia mpaka mwisho,29 wataona kwamba mwisho wa safari yao ni kupokea hatima yao ya kiungu kama warithi wa uzima wa milele.”30 Watarudi kwenye uwepo wa Baba yao ili kuishi pamoja Naye milele. Na tuchague vyema.

Kuna mengi zaidi ya sisi kuwepo kuliko tu kile kinachotokea kati ya kuzaliwa na kifo. Ninakualikeni njooni na tumfuate Kristo.31

Ninawaalika waumini wote wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kila siku, “mje kwa Kristo, na mkamilishwe ndani yake, na mjinyime ubaya wote, … [ili] kupitia kumwagika kwa damu ya Kristo, … ninyi [mpate] kuwa watakatifu, pasipo doa.”32

Ninawaalike wale ambao bado si waumini wa Kanisa mje na msome Kitabu cha Mormoni na kuwasikiliza wamisionari. Njooni, na muwe na imani na tubuni dhambi zenu. Njooni, mbatizwe na kupokea Roho Mtakatifu. Njooni, muishi maisha yaliyojaa Kristo. Mnapokuja Kwake na kushika amri Zake, mimi ninawaahidi mtapata amani na azma katika uzoefu huu wa duniani yenye vurugu na “uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”33

Kwa wale wote ambao mmepata ukweli huu na kwa sababu yoyote ile mmetanga, ninawaalikeni mrudi. Rudini leo. Baba yetu Mwokozi wanawapenda. Nashuhudia kwamba Kristo ana nguvu za kujibu maswali yenu yote, kuwaponya maumivu na huzuni yenu, na kuwwasamehe dhambi zenu. Mimi najua hili ni kweli. Mimi najua kwamba vitu hivi vyote ni kweli? Yesu Kristo yu hai. Hili ni Kanisa Lake. Katika jina la Yesu Kristo, amina.