2010–2019
Upendo Kamili Hutupa Hofu Nje
Aprili 2017


Upendo Kamili Hutupa Hofu Nje

Acha tuweka kando hofu yetu na badala yake tuishi kwa furaha, unyenyekevu, tumaini, na imani kakamavu kwamba Bwana yu pamoja nasi.

Akina kaka na kina dada wapendwa wangu, rafiki wapendwa, ni fursa na furaha ilioje kukutana kama Kanisa la ulimwenguni kote tukiwa kitu kimoja katika imani na upendo wetu kwa Mungu na watoto Wake.

Nashukuru kwa ajili ya uwepo wa nabii wetu mpendwa, Thomas  S. Monson Rais, daima tutayatia moyoni maneno yako ya maelekezo, ushauri, na hekima. Tunakupenda, Rais Monson na daima tunakuombea.

Miaka iliyopita, nilipokuwa nikihudumu kama rais wa kigingi katika Frankfurt, Ujerumani, dada mpendwa lakini asiye na furaha alinijia mwishoni wa mojawapo wa mikutano yetu ya kigingi.

“Si inasikitisha? alisema. “Lazima kumekuwa na watu wanne au watano waliokuwa wamelala fofofo wakati wa hotuba yako!”

Nikafikiria kwa dakika na kujibu, “Nina hakika kwamba usingizi kanisani ndiyo kati usingizi wote wenye afya sana.”

Mke wangu Harriet, alisikia mzungumzo hayo na baadaye kusema kwamba ilikuwa mojawapo wa majibu mazuri ambayo niliyotoa.

Mwamko Mkuu

Miaka michache iliyopita katika Amerika Kaskazini, kundi lililoitwa “Mwamko Mkuu” ambalo lilisambaa kote mikoani. Mojawapo wa madhumuni yake ya msingi yalikuwa ni kuwaamsha watu ambao walikuwa wanaokena kana wanamelala kuhusu mambo ya kiroho.

Kijana Joseph Smith alishawishika na mambo aliyoyasikia kutoka kwa wahubiri ambao walikuwa sehemu ya huu mwamko wa kidini wa siku zake. Ndiyo mojawapo wa sababu aliamua kutafuta kwa bidii mapenzi ya Bwana katika sala za faraghani.

Wahubiri hawa walikuwa na elimumwendo, mhemko katika mahubiri ambayo yalijulikana sana kwa msisitizo mkubwa juu ya vitishio vikali vya jehanamu ambavyo viliwangojea wenye dhambi.1 Hotuba zao haziwakuwafanya watu wasinzie—lakini zingeweza kusababisha ndoto chache za kutisha. Lengo lao na mfumo wao vilionekana kuwaogopesha watu ili waje kanisani.

Hofu kama Hila

Kihistoria, hofu mara nyingi imetumika kama njia ya kufanya watu wachukue uamuzi. Wazazi wameitumia kwa watoto wao, waajiri kwa waajiriwa, na wanasiasa kwa wapiga kura wao.

Wataalamu wa masoko huelewa nguvu ya hofu na mara nyingi huitumia. Hii ndio maana matangazo huonekana kubeba ujumbe unaodokeza kwamba kama tutakosa kununua chapa sahihi ya nafaka ya kifungua kinywa, au tukikosa mchezo wa video mpya au simu ya kigajani, tutakuwa katika hatari ya kuishi maisha ya taabu na tutakufa peke yetu na pasipo furaha.

Tunatabasamu katika hili na tunadhani kamwe hatutaangukia katika hila hiyo, lakini wakati mwingine tunafanya hivyo. Vibaya zaidi, wakati mwingine tunatumia njia kama hizo kuwafanya watu watende tunavyotaka.

Ujumbe wangu una malengo mawili kwa leo: La kwanza ni kutusihi kutazama kwa makini na kufikiria kiasi ambacho sisi tunatumia hofu kuwahamasisha wengine—ikiwemo sisi wenyewe. La pili ni kupendekeza njia bora zaidi.

Tatizo la Hofu

Kwanza, ngoja tuzungumze tatizo la hofu Kwani, nani kati yetu hajawahi kushurutishwa na hofu kula vizuri, kufunga mkanda wa kiti kwenye gari, kufanya mazoezi zaidi, kutunza fedha, au hata kutubu dhambi?

Ni kweli hofu inaweza kuwa na ushawishi wa nguvu katika matendo na tabia zetu. Lakini uwezo huu huwa wa muda na hauna kina. Hofu mara chache ina nguvu ya kubadilisha mioyo yetu, na kamwe hatatubadili kuwa watu ambao hupenda mema na watiifu kwa Baba yetu wa Mbinguni.

Watu ambao wana hofu wanaweza kusema na kutenda vitu sahihi, lakini hawahisi vitu sahihi. Mara nyingi huhisi wasio na msaada na wenye kuchukia na hata wenye hasira. Baada ya muda hisia hizi hupelekea kutoamini, kutojali hata uasi.

Kwa bahati mbaya, huu mwenendo potovu katika maisha na uongozi hauko tu katika dunia ya kilimwengu. Hunihuzunisha sana ninaposikia waumini wa Kanisa ambao hutumia mamlaka yasiyo haki—iwe nyumbani kwao, miito yao ya Kanisani, kazini au kwenye mahusiano ya kila siku na wengine.

Mara nyingi, watu wanaweza kushutumu uonevu kwa wengine, lakini hawauoni ndani yao. Wakidai kushikiliwa kwa sheria zao za udhalimu, wakati wengine hawafuati sheria hizo zisizo na mpangilio, watu hao huwarudi kimaneno, kihisia na wakati mwingine hata kimwili.

Bwana amesema kwamba “wakati … tunatumia uthibiti au utawala au ulazimishaji juu ya nafsi za wanadamu, katika kiwango chochote kisicho cha haki, ... mbingu hujitoa zenyewe [na] Roho wa Bwana husikitika.”2

Nyakati zinaweza kutokea ambapo tunajaribiwa kuhalalisha vitendo vyetu kwa kuamini kuwa matokeo huhalalisha njia iliyotumika. Hata tunaweza kudhani kuwa kudhibiti, kutawala kwa hila, na ukali vitakuwa kwa ajili ya mazuri ya wengine. Sivyo, kwa kuwa Bwana ameweka wazi, “tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema,imani, upole, [na] kiasi.”3

Njia bora

Ninavyozidi kumjua Baba yangu wa mbinguni, ndivyo ninavyoona jinsi Yeye huwapa maongozi na kuwaongoza watoto Wake. Yeye hakarisiki, halipizi kisasi, wala hana chuki.4 Lengo lake—na kazi yake—ni kutufundisha, kutuinua, na kutuongoza katika ukamilifu Wake.5

Mungu alijielezea kwa Musa kama “mwenye rehema na hisani, mvumilivu na mwingi wa neema na ukweli.”6

Upendo wa Baba Yetu wa mbinguni kwetu sisi watoto Wake hupita sana uwezo wa uelewa.7

Je, hii humaanisha kuwa Mungu huruhusu au hatilii maanani tabia ambazo ni kinyume na amri Zake? Hapana, kiukweli Hapana!

Lakini anataka kubadili si tu tabia. Anataka kubadili asili yetu hasa. Anataka kubadili mioyo yetu

Anataka tufikie na kushikilia kwa nguvu fimbo ya chuma, kupambana na hofu zetu, na kishujaa kupiga hatua mbele na juu katika njia iliyosonga na nyembamba. Anataka hivi kwetu kwa sababu Anatupenda na kwa sababu hii ndio njia ya kuelekea kwenye furaha.

Kwa hiyo, ni namna gani Mungu huwahamasisha watoto Wake kumfuata katika siku zetu?

Mungu Alimtuma Mwanawe!

Alimtuma Mwanawe wa Pekee, Yesu Kristo, kutuonyesha njia sahihi.

Mungu hutuhamasisha kupitia ushawishi, uvumilivu, utu wema upole na upendo usiokwisha.8 Mungu yuko upande wetu. Anatupenda, na tunapojikwaa, Antaka tusimame, na kujaribu tena na kuwa imara zaidi.

Yeye ni mnasihi wetu.

Ni tumaini letu kuu na la kuvutia.

Anatamani kutusisimua kwa imani

Anatuamini kuwa tutajifunza kutoka kwa makosa yetu na kufanya uchaguzi sahihi

Hii ndiyo njia bora!9

Je, maovu gani ya Ulimwengu?

Njia mojawapo ambayo tunawatawala wenzetu kwa hila ni kwa kuendelea kukaa katika uovu na hata kutia chumvi uovu duniani.

Hakika ulimwengu wetu umekuwa, na utaendelea, kutokuwa mkamilifu. Zaidi pia, watu wengi wasio na hatia wanateseka kwa sababu ya hali halisi na pia kukosekana kwa utu. Ubovu na uovu katika siku zetu ni wa kipekee na unatisha.

Lakini japo ya haya yote, nisingebadilisha kuishi katika kipindi hiki na kipindi kingine chochote katika historia ya ulimwengu. Tumebarikiwa kupita kiasi kuishi katika siku ya mafanikio yasiyo kifani, kuelimika na kufaidika. Zaidi ya yote, tumebarikiwa kuwa na utimilifu wa injili ya Yesu Kristo, ambayo hutupatia mtazamo wa kipekee juu ya hatari za kiulimwengu na kutuonyesha jinsi ya kuziepuka hatari hizi au kupambana nazo.

Nifikiriapo juu ya baraka hizi, ninataka kupiga magoti na kutoa sifa kwa Baba yetu wa Mbinguni kwa ajili ya upendo Wake usio na mwisho kwa watoto Wake.

Siamini Mungu anataka Watoto Wake kuwa na hofu au kuendelea na maovu ya ulimwengu huu. “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.”10

Ametupa sababu nyingi sana kufurahia. Sisi tunahitaji kuzitafuta na kuzitambua. Bwana kila mara anatukumbusha “usiogope” na “jipeni moyo”11 .na “msiogope, waumini wadogo”12

Bwana Atapigana Vita Vyetu

Kina kaka na kina dada, sisi ni “zizi dogo” la Bwana. Sisi ni Watakatifu wa siku za mwisho. Asili ya jina letu ni msismamo wa kutarajia kurudi kwa Mwokozi na kujiandaa wenyewe na ulimwengu kumpokea Yeye. Kwa hiyo, acha tumtumikie Mungu na kuwapenda wanadamu wenzetu. Acha tufanya hivi kwa imani ya asili, kwa unyenyekevu, kamwe tusidharau dini yoyote au kundi lolote la watu. Kina kaka na kiana dada, tunaamriwa kusoma neno la Mungu na kufuata sauti ya Roho, kwamba tuweze “kujua ishara za nyakati, na ishara za kuja kwa Mwana wa Mtu.”13

Sisi kwa hiyo, si mbumbumbu kuhusu changamoto za kiulimwengu au hatufahamu ugumu ya nyakati zetu. Lakini hii haimaanishi kwamba tujitwike mzigo wa hofu au kuwatwika wengine na hofu kila mara. Badala ya kukaa kwenye ukubwa wa changamoto zetu, si ingekuwa bora kuzingatia kwenye ukubwa usio na mwisho, uzuri na uhakika wa nguvu za Mungu wetu, kumwamini Yeye, na kujiandaa kwa moyo wa furaha kwa ujio wa Yesu Kristo?

Kama watu Wake wa maagano, hatuhitaji kusitishwa na hofu kwa sababu ya kile ambacho kinaweza kutokea. Badala yake tunaweza kuendelea mbele kwa imani, ujasiri, nia ya dhati na tumaini kwa Mungu tunapokaribia changamoto na nafasi zilizo mbele yetu.14

Hatutembei katika njia ya ufuasi peke yetu. “Bwana Mungu wako … anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.”15

“Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.”16

Tukitokewa na tishio, acha tupate ushujaa wetu, imani ya kutosha na tuwe na imani katika ahadi kwamba “hakuna silaha ambayo itafanyika dhidi [yetu] itafanikiwa.17

Tunaishi nyakati za hatari na ghasia? Bila shaka tunaweza.

Mungu Mwenyewe amesema “Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”18

Je, unaweza kutumia imani kuamini na kutenda ipasavyo? Je, tunaweza kuishi kulingana na ahadi zetu na maagano matakatifu? Je, tunaweza kushika amri za Mungu hata katika hali zenye changamoto? Bila shaka tunaweza!

Kwa sababu Mungu ameahidi, “Mambo yote yatafanyika kwa pamoja kwa faida yenu, kama ninyi mnatembea wima.”19 Kwa hiyo, acha tuweke kando hofu yetu na tuishi kwa furaha, tumaini, na imani kakamavu kwamba Bwana yu pamoja nasi.

Upendo Kamili Hutupa Hofu Nje

Rafiki zangu wapendwa, kaka zangu na dada zangu wapendwa katika Kristo, kama tutajikuta tunaishi katika hofu au woga, au kama tutajikuta kuwa maneno yetu, mtazamo wetu na matendo yetu yanasababisha hofu kwa wengine, mimi ninaomba kwa nafsi yote kwamba tutakombolewa kutokana na hofu hii kwa kiuasumu teule cha uungu cha hofu: upendo safi wa Kristo, kwani “pendo lililo kamili huitupa nje hofu.20

Upendo mkamilifu wa Kristo hushinda majaribu ya kudhuru, kuonea au kukandamiza, au udhalimu.

Upendo kamili wa Kristo huruhusu unyenyekevu, heshima na ujasiri mkuu kama wafuasi wa Mwokozi wetu mpendwa. Upendo kamili wa Kristo hutupatia ujasiri mkuu wa kupita hofu zetu na kuweka imani yetu yote katika nguvu na uzuri wa Baba yetu wa Mbinguni, na Mwanawe, Yesu Kristo.

Nyumbani kwetu, sehemu zetu za kazi, miito yetu kanisani, na katika mioyo yetu, acha tubadilishe hofu kwa upendo kamili wa Kristo. Upendo wa Kristo utabadlisha hofu kwa imani!

Upendo wake utatuwezesha kutambua, kuamini, na kuwa na imani katika uzuri wa Baba yetu wa Mbinguni, mpango Wake mtakatifu, injili Yake, na amri Zake.21 Kumpenda Mungu na wanadamu wenzetu kutageuza utiifu wetu katika amri za Mungu kuwa baraka na si mzigo. Upendo wa Kristo utatusaidia kuwa wakarimu kidogo zaidi, wenye kusamehe zaidi, wenye kujali zaidi, na wenye kujitolea zaidi kwa kazi Yake.

Tunapojaza mioyo yetu na upendo wa Kristo, tutaamshwa kuwa upya kiroho na tutatembea kwa furaha, kwa kujiamini, na kuwa macho, hai katika nuru na utukufu wa Mwokozi wetu mpendwa, Yesu Kristo.

Ninashuhudia, pamoja na Mtume Yohana, “Hakuna hofu katika upendo wa [Kristo].”22 Akina ndugu na kina dada, marafiki wapendwa, Mungu anawajua kikamilifu, Yeye anawapenda kikamilifu. Anajua nini kilicho mbele yenu Yeye anawataka “msiogope, ila muamini tu23 na “kukaa katika upendo wake [kamili].”24 Haya ndiyo maombi yangu na baraka zangu katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. George Whitehead and Jonathan Edwards ni mifano miwili mikubwa ya wahubiri wa namna hii.

  2. Mafundisho na Maagano 121:37

  3. Wagalatia 5:22–23.

  4. Wakati fulani, Mwokozi alitaka kuingia kijiji cha Wasamaria, lakini watu walimkataa Yesu na hawangetaka kumpokea katika kijiji chao. Wawili kati ya wafuasi Wake, walikerwa sana na hiki na wakauliza, “Bwana wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize, … ?” Yesu akajibu kwa angalizo hili: “Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo. Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa.”1982

  5. Ona Musa 1:39; ona pia Waefeso 3:19.

  6. Kutoka 34:6.

  7. Ona Waefeso 3:19.

  8. Ona Mafundisho na Maagano 121:41. Hakika Mungu hutarajia sisi, Watoto wake hapa duniani kuwa namna hii kati yetu, Yeye—mkamilifu akiwa na maadili ya kila aina—angekuwa mfano wa tabia hiyo.

  9. Kusanyiko kuu la Mbinguni ni tukio mahususi la kuonyesha tabia ya Mungu. Pale, Baba Yetu wa Mbinguni alielezea mpango wake kwa ajili ya ukuaji wetu wa milele. Mambo mahususi ya mpango huo yalijuisha uhuru wa kuchagua, uttifu, na ukombozi kupitia Upatanisho wa Kristo. Lusifa, hata hivyo alipendekeza namna tofauti. Alngehakikisha kuwa wote wangetii—na hakuna ambaye angepotea Njia pekee ya kufikia hili ni kwa kupitia kutokuwa na usawa na ulazimishaji. Lakini Baba Yetu mpendwa wa mbinguni hangeruhusu mpango huo. Alithamini uhuru wa kuchagua wa Watoto Wake Alijua lazima tutatenda makosa kwa namna fulani kama kweli ingepasa tujifunze. Na ndio maana alimtoa Mwokozi mabaye dhabihu yake ya milelelingeweza kutuosha dhambi na kuturuhusu kuingia katika ufalme wa Mungu.

    Wakati Baba Yetu wa mbinguni aliona wengi wa watotot wake wakishawishiwa na Lusifa, je aliwalazimisha kufuata mpango wake? Je aliwatisha au kuwaogopesha wale ambao walichagua chaguo hilo la kutisha? Hapana. Mungu wetu mwenye nguvu hakika angeweza kuzuia uasi huu. Angelazimisha mapenzi yake juu ya waasi na kuwafanya wakubali. Lakini badala yake aliwaruhusu watoto Wake wachague wao wenyewe.

  10. 2 Timotheo 1:7.

  11. Ona, kwa mfano, Yoshua 1:9; Isaya 41:13; Luka 12:32; Yohana 16:33; 1 Petro 3:14; Mafundisho na Maagano 6:36; 50:41; 61:36; 78:18.

  12. Luka 12:32.

  13. Mafundisho na Maagano 68:11

  14. Ushauri wa Musa kwa watu wake bado unafaa: “Msiogope. … Mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo” (Exodus 14:13, New King James Version).

  15. Kumbukumbu la Torati 31:6.

  16. Kutoka 14:14, Toleo jipya King James .

  17. Isaya 54:17.

  18. Yohana 16:33.

  19. Mafundisho na Maagano 90:24; ona pia 2 Wakorintho 2:14; Mafundisho na Maagano105:14.

  20. 1 Yohana 4:18.

  21. Na tukumbuke kuwa Mwokozi hakuja “ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”(Yohana 3:17). Kwa kweli, “Hafanyi chochote ila tu kwa manufaa ya ulimwengu; kwani anapenda ulimwengu, hata kwamba anatoa maisha yake ili awavute wanadamu wote kwake.” (2 Nefi 26:24).

  22. 1 Yohana 4:18; ona pia 1 Yohana 4:16.

  23. Marko 5:36.

  24. Yohana 15:10.