2010–2019
Kuwakubali kwa Maofisa wa Kanisa
Aprili 2017


Kuwakubali kwa Maofisa wa Kanisa

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, Rais Monson ameomba kwamba sasa niwalete kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, na Urais Mkuu wa Makundi Saidizi wa Kanisa kwa ajili ya kura ya zenu za kuwakubali.

Imependekezwa kwamba tumkubali Thomas Spencer Monson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Dieter Friedrich Uchtdorf kama Mshauri wa Pili wa Urais wa Kwanza

Wale wote wanaokubali wanaweza kuonyesha.

Wale wanaopinga, kama wako, wanaweza kuonyesha pia.

Imependekezwa kwamba tumkubali Russell M. Nelson kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na wafuatao kama washiriki wa Akidi hiyo: Russell M. Nelson, Dallin H. Oaks, M. Russell Ballard, Robert D. Hales, Jeffrey R. Holland, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, na Dale G. Renlund.

Wale wanaokubali, wanaweza kuonyesha.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha ishara.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wale wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Tunatambua kwa shukrani huduma ya Mzee Bruce  D.Porter, rafiki yetu na mshirika, aliyefariki Disemba  28, 2016. Tungependa kutuma salamu za upendo na rambi rambi zetu za dhati kwa Dada Susan Porter, watoto wao, wajukuu wao. Tuna shukrani kuweza kuhudumia pamoja na mtu huyu mwema.

Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe Taylor  G. Godoy na John  C. Pingree  Jr. kama Sabini wa Eneo. Wale ambao wangependa kuonyesha shukrani zao kwa ndugu hawa kwa huduma yao, tafadhali onyesheni hivyo.

Inapendekezwa kwamba tuwapunzishe kwa shukrani za dhati, Akina dada Linda  K. Burton, Carole  M. Stephens, na Linda  S. Reeves kama Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Vile vile tunawapumzisha washiriki wa bodi kuu ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.

Wale wote ambao wangependa kuungana nasi kutoa shukrani kwa akina dada hawa kwa huduma yao bora, tafadhali waonyeshe ishara.

Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe Dada Jean B. Bingham kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Mkuu wa Msingi na Dada Bonnie H. Cordon kama Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Msingi.

Wale ambao wangependa kutoa shukrani kwa akina dada hawa wanaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono.

Imependekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini wa Eneo: Taylor G. Godoy, Joni L. Koch, Adilson de Paula Parrella, John C. Pingree Jr., Brian K. Taylor, na Taniela B. Wakolo.

Wale wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.

Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Imependekezwa kwamba tuwakubali Jean B. Bingham kuhudumu kama Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, pamoja na Sharon L. Eubank kama Mshauri wa Kwanza na Reyna I. Aburto kama Mshauri wa Pili.

Tena inapendekezwa kwamba tuwwakubali Bonnie H. Cordon sasa ahudumu kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Mkuu wa Msingi na Cristina B. Franco kama Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Msingi.

Wale wote wanaokubali, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha ishara.

Imependekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini wa Eneo: Luis R. Arbizú, David A. Benalcázar, Berne S. Broadbent, David L. Buckner, L. Todd Budge, Luciano Cascardi, Ting Tsung Chang, Pablo H. Chavez, Raymond A. Cutler, Fernando P. Del Carpio, José Luiz Del Guerso, Aleksandr A. Drachyov, I. Raymond Egbo, Carlos R. Fusco Jr., Jorge A. García, Gary F. Gessel, Guillermo I. Guardia, Marcel Guei, José Hernández, Karl D. Hirst, Ren S. Johnson, Jay B. Jones, Anthony M. Kaku, Paul N. Lekias, John A. McCune, Tomas S. Merdegia, Artur J. Miranda, Elie K. Monga, Juan C. Pozo, Anthony Quaisie, James R. Rasband, Carlos G. Revillo Jr., Martin C. Rios, Johnny F. Ruiz, K. Roy Tunnicliffe, na Moisés Villanueva.

Wale wote wanaokubali wanaweza kuonyesha.

Kama kuna yeyote anayepinga aonyeshe ishara.

Imependekezwa kwamba tuwakubali Viongozi Wakuu, Sabini wa Eneo, na Urais Mkuu wa Vikundi Saidizi kama ilivyo sasa.

Wote wanaokubali, tafadhali waonyeshe ishara.

Wale wanaopinga, kama kuna yeyote.

(Kura imepokelewa.) Tunawaalika wale wote ambao inawezekana kuwa wamepinga mapendekezo yoyote wanapaswa kuwasiliana na marais wao wa vigingi.

Kina kaka na kina dada, asanteni kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Sasa tunawaomba Viongozi Wakuu wa Sabini wapya na Urais Mkuu mpya Msingi kuchukua nafasi zao kwenye jukwaa. Rais Monson kawaida husema, “Ni safari ndefu.” Asanteni kina dada. Asanteni ndugu. Kwa taarifa zenu, Dada Franco sasa anahudumu misheni pamoja na mmewe huko Ajentina Amekubali, kama mnavyojua, na ataanza huduma yake rasmi wantakaporudi mwezi Julai.