2010–2019
Ahadi Kuu Zaidi na za Thamani
Oktoba 2017


Ahadi Kuu Zaidi na za Thamani

Mpango mkuu wa furaha wa Baba yetu wa Mbinguni unajumuisha mafundisho, ibada, maagano, na ahadi kuu zaidi, za thamani ambazo tunaweza kuwa wapokeaji wa asili takatifu.

Mojawapo wa changamoto kubwa kila mmoja wetu hukumbana nayo kila siku ni kutoruhusu mahitaji ya hii dunia kutawala muda wetu na nguvu kiasi kwamba tunapuuza vitu vya milele vyenye umuhimu zaidi.1 Tunaweza kuchepushwa kwa urahisi sana kukumbuka na kuzingatia vipaumbele muhimu vya kiroho kwa sababu ya majukumu yetu mengi na ratiba zilizobana. Wakati mwingine tunajaribu kukimbia kwa kasi sana kiasi kwamba tunaweza kusahau ni wapi tuendako na ni kwa nini tunakimbia.

Mtume Petro anatukumbusha kwamba kwa wafuasi wa Yesu Kristo, “uweza Wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua Yeye aliyetuita kwa utukufu na wema.

“Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kuu zaidi, za thamani, ili kwamba kwa hizo tupate kuwa wapokeaji wa asili ya Uungu, tukikwepa uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.”2

Ujumbe wangu unasisitizia umuhimu wa ahadi kuu zaidi, za thamani zilizoelezwa na Petro kama ukumbusho halisi wa wapi tuendako katika safari yetu ya dunia na kwa nini. Pia nitajadili wajibu unaohusiana na siku ya Sabato, hekalu takatifu, na nyumba zetu katika kutusaidia kukumbuka ahadi hizi muhimu.

Naomba kwamba Roho Mtakatifu atamwelekeza kila mmoja wetu wakati tunapofikiri pamoja kweli hizi muhimu.

Utambulisho Wetu wa Kiungu

Mpango wa furaha wa Baba yetu wa Mbinguni unajumuisha mafundisho, ibada, maagano, na ahadi kuu zaidi, za thamani ambapo tunaweza kuwa wapokeaji wa asili takatifu. Mpango Wake unaelezea utambulisho wetu wa milele na njia itupasayo kufuata kujifunza, kubadilika, kukua, na, hatimaye, kukaa Naye milele.

Kama ilivyoelezewa katika “Familia: Tamko kwa Ulimwengu”:

“Wanadamu wote—wanaume na wanawake—wameumbwa katika mfano wa Mungu. Kila moja ni mwana au binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni, na, kama hivyo, kila moja ana asili takatifu na takdiri. …

“Katika ufalme kabla ya maisha ya dunia, wana na mabinti wa kiroho walimjua na kumwabudu Mungu kama Baba yao wa Milele na kukubali mpango Wake ambao ungewezesha watoto Wake kupokea mwili na kupata uzoefu wa dunia ili kukua kwa ukamilifu na hatimaye kutambua maisha yao matakatifu kama warithi wa maisha ya milele.”3

Mungu ameahidi watoto Wake kwamba kama watafuata mwongozo wa Mpango Wake na mfano wa Mwanawe Mpendwa, kutii amri, na kuvumilia katika imani hadi mwisho, basi kwa huruma ya Ukombozi wa Mwokozi, watapata uzima wa milele, zawadi ambayo ni kubwa kuliko zawadi zote za Mungu.”4 Uzima wa Milele ni ahadi kuu zaidi na ya thamani.

Kuzaliwa Upya Kiroho

Tunaelewa kiufasaha zaidi ahadi kuu zaidi na za thamani na kuanza kupata asili takatifu kwa kukubali kwa dhati wito kutoka kwa Bwana kuelekea utukufu na utu wema. Kama ilivyoelezwa na Petro, wito huu hutimizwa kwa kujitahidi kuachana na upotovu uliopo duniani.

Tunaposonga mbele kwa kutii na imani katika Mwokozi, basi kwa sababu yaUpatanisho Wake na nguvu ya Roho Mtakatifu, “mabadiliko makuu [yanatokea] ndani yetu, au mioyoni mwetu, hata kwamba hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima.”5 “Tumezaliwa tena; ndio, wazaliwa wa Mungu, tumebadilishwa kutoka hali [yetu] ya kimwili na ya kuanguka, kwa hali ya utakatifu, tukiwa tumekombolewa na Mungu.”6 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”7

Mabadiliko mapana kama hayo katika asili yetu kwa kawaida hayatokei kwa haraka au mara moja. Kama Mwokozi, sisi pia “hatupokei utimilifu mwanzoni, bali [hupokea] neema juu ya neema.”8 “Kwani tazama, hivi asema Bwana Mungu: Nitawapatia watoto wa watu mstari juu ya mstari, amri juu ya amri, hapa kidogo na pale kidogo; na heri wale wanaosikiliza kanuni zangu, na kutii mashauri yangu, kwani watajifunza hekima.”9

Ibada za Ukuhani na maagano matakatifu ni muhimu katika hatua hii endelevu ya kuzaliwa upya kiroho; pia ni njia ambayo Mungu ameteua ambapo tunapokea ahadi zake kubwa mno na za thamani. Ibada ambazo zinapokelewa kwa kustahili na kukumbukwa daima hufungua njia za mbinguni ambazo nguvu za kiungu zinaweza kumiminika katika maisha yetu. Maagano ambayo yanaheshimiwa kwa uthabiti na kukumbukwa daima hutupa lengo na uhakika wa baraka katika dunia na hata milele.

Kwa mfano, Mungu anatuahidi, kulingana na uaminifu wetu, ushirikiano wa daima na mshiriki wa tatu ya Uungu, hata Roho Mtakatifu,10 kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo tunaweza kupokea na daima kutunza ondoleo la dhambi zetu,11 kwamba tupate amani katika dunia hii,12 kwamba Mwokozi amevunja vifungo vya mauti na kushinda kaburi kwa shangwe,13 na kwamba familia zinaweza kuwa pamoja kwa milele yote.

Inaeleweka, ahadi zote kuu zaidi na za thamani ambazo Baba wa Mbinguni anatoa kwa watoto Wake hazihesabiki au kuelezeka kiufasaha. Hata hivyo, hata sehemu ya orodha ya baraka zilizoahidiwa nilizowasilisha punde zinaweza kusababisha kila mmoja wetu “kusimama akistaajabu,”14 na “kuanguka chini na kumuabudu Baba”15 katika jina la Yesu Kristo.

Kukumbuka Ahadi

Rais Lorenzo Snow alionya, “Tumekuwa wepesi mno kusahau lengo kuu la maisha, sababu ya Baba wa Mbinguni kututuma hapa duniani, na pia wito mtakatifu tulioitwa; na hivyo, badala ya kuinuka juu ya vitu vidogo vya mpito … , mara nyingi tunajishusha chini kulingana na dunia pasipo kutumia msaada wa kiungu ambao Mungu alianzisha, ambao pekee unaweza kutuwezesha kushinda [hivyo vitu vya mpito].”16

Siku ya sabato na hekalu takatifu ni vyanzo viwili thabiti vya msaada wa kiungu ulioanzishwa na Mungu kutusaidia kuinuka juu ya usawa na upotovu wa dunia. Mwanzoni tunaweza fikiri kwamba malengo ya juu ya kutunza siku ya sabato na kuhudhuria hekaluni yanaendana lakini tofauti. Ninaamini, hata hivyo, kwamba malengo hayo mawili yanafanana kabisa na hufanya kazi pamoja kutuimarisha kiroho kama watu binafsi na katika nyumba zetu.

Siku ya Sabato.

Baada ya Mungu kuumba vitu vyote, Alipumzika katika siku ya saba na kuamuru kwamba siku moja ya kila wiki kuwa muda wa kupumzika ili kusaidia watu kumkumbuka.17 Siku ya sabato ni Muda wa Mungu, muda mtakatifu maalumu umetengwa kumuabudu Yeye na kupokea na kukumbuka ahadi Zake kuu na za thamani.

Bwana ameelekeza katika kipindi hiki cha maongozi:

“Na ili ujilinde na dunia pasipo na mawaa, utakwenda kwenye nyumba ya sala na kutoa sakramenti zako katika siku yangu takatifu;

“Kwani amini hii ndiyo siku iliyoteuliwa kwako kupumzika kutoka katika kazi zako, na utoe dhabihu zako za shukrani kwa Aliye Juu sana.18

Hivyo basi, katika sabato tunamuabudu Baba katika jina la Mwana kwa kushiriki katika ibada na kujifunza kuhusu, kupokea, kukumbuka na kufanya upya maagano. Katika siku Yake tukufu, mawazo yetu, matendo, na mwenendo ni ishara kwa Mungu na kielelezo cha upendo wetu Kwake.19

Lengo la ziada la Sabato ni kukuza ono letu kutoka katika vitu vya ulimwengu kuelekea baraka za milele. Tukijiondoa wakati huu mtukufu kutoka katika shughuli nyingi za kawaida za maisha yetu yaliyobana, tunaweza “tazama kwa Mungu na kuishi”20 kwa kurudia na kukumbuka ahadi kubwa na za thamani ambapo tunakuwa wapokeaji wa asili takatifu.

Hekalu Takatifu

Bwana ameamuru watu Wake daima kujenga mahekalu, maeneo matakatifu ambapo watakatifu wanaostahili wanaweza kufanya maagizo na ibada takatifu za injili kwa wao binafsi na kwa wafu. Mahekalu ni sehemu takatifu zaidi kati ya sehemu zote za kuabudu. Hekalu kiuhalisia ni nyumba ya Bwana, sehemu takatifu maalumu ambayo imetengwa kwa ajili ya kumuabudu Mungu na kwa kupokea na kukumbuka ahadi Zake kuu na za thamani.

Bwana ameelekeza katika kipindi hiki, “Jipangeni wenyewe; tayarisheni kila kitu kilicho muhimu, na jengeni nyumba, hata nyumba ya sala, nyumba ya mfungo, nyumba ya imani, nyumba ya mafundisho, nyumba ya utukufu, nyumba ya utaratibu, nyumba ya Mungu.”21 Lengo kuu la kuabudu hekaluni ni kushiriki katika ibada na kujifunza kuhusu, kupokea, na kukumbuka, maagano. Tunafikiri, tunafanya, na tunavaa tofauti katika hekalu kuliko katika sehemu nyingine ambazo tunaweza kuwepo.

Lengo kuu la hekalu ni kuinua mtazamo wetu kutoka vitu vya dunia na kuelekea baraka za milele. Tukijiondoa kwa muda mfupi kutoka katika mazingira ya kidunia ambayo tunayaelewa, tunaweza “tazama kwa Mungu na kuishi”22 kwa kupokea na kukumbuka ahadi kubwa na za thamani ambapo tunakuwa wapokeaji wa asili takatifu.

Tafadhali kumbukeni kwamba siku ya Sabato na hekalu, kwa pamoja ni wakati mtukufu na sehemu takatifu maalumu ambayo imetengwa kwa kumuabudu Mungu na kupokea na kukumbuka ahadi Zake kuu na za thamani kwa watoto Wake. Kama ilivyoanzishwa na Mungu, malengo makuu ya vyanzo hivi viwili vya kiungu vya msaada ni sawa kabisa: ni kwa nguvu na kwa kurudia kuweka usikivu wetu kwa Baba wa Mbinguni, Mwanawe Mpendwa wa Pekee, Roho Mtakatifu, na ahadi zinazoambatana na ibada na maagano ya injili ya urejesho ya Mwokozi.

Nyumba Zetu

Muhimu zaidi, nyumbani panapaswa kuwa muunganiko wa muda na mahali ambapo watu na familia hukumbuka kwa umakini zaidi ahadi kuu zaidi na za thamani za Mungu. Kuacha nyumba zetu kwenda kutumia muda wetu katika vikao vya Jumapili na kuingia eneo takatifu la hekalu ni muhimu lakini haitoshi. Mpaka tu tutakapoleta nyumbani mwetu roho na nguvu tunayopata kutoka katika hizo shughuli takatifu ndio tunaweza kuendeleza mtazamo wetu katika malengo makubwa ya dunia na kushinda upotovu uliopo duniani. Uzoefu wetu wa Sabato na hekalu lazima uwe kichocheo cha kiroho ambacho kinajaza watu na familia na nyumba zetu na ukumbusho endelevu wa masomo muhimu tuliyojifunza, na uwepo wa nguvu ya Roho Mtakatifu, na kuongoka kwa kina na endelevu kwa Bwana Yesu Kristo, na “matumaini thabiti kabisa”23 katika ahadi za Mungu za milele.

Siku ya Sabato na hekalu inaweza kutusaidia kuanzisha nyumbani mwetu “njia thabiti zaidi”24 endapo “tutakusanya pamoja sehemu moja vitu vyote katika Kristo, kote vilivyopo mbinguni, na vilivyopo duniani; hata katika Yeye.”25 Tunachokifanya majumbani mwetu na muda Wake mtukufu na tunachojifunza katika sehemu takatifu ni muhimu katika kuwa wapokeaji wa asili takatifu.

Ahadi na Ushuhuda

Tunaweza kiurahisi kushinda mambo ya kawaida na ya kujirudiarudia ya duniani. Kulala, kula, kuvaa, kufanya kazi, kucheza, kufanya mazoezi, na shughuli nyinginezo za desturi ni muhimu. Lakini hatimaye, tunachokuwa ni matokeo ya uelewa wetu na utayari kujifunza kutoka kwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu; sio tu mjumuisho wa shughuli za kila siku katika kipindi cha uhai wetu.

Injili ni zaidi ya vitu vya kazi za wazi tunavyopaswa kufanya kila siku ; lakini, ni uzi mzuri sana wa ukweli “umefungwa vizuri”26 na kusukwa pamoja, umeundwa kutusaidia sisi kuwa kama Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo, hata wapokeaji wa asili takatifu. Kweli, tumepofushwa “kwa kuangalia kupita alama”27 wakati huu ukweli muhimu wa kiroho unafunikwa na mahitaji, wasiwasi, na uholelaholela wa dunia.

Tukiwa wenye busara na kumualika Roho Mtakatifu kuwa kiongozi wetu,28 Nashuhudia Atatufundisha kile kilicho cha kweli. “Atashuhudia juu ya Kristo, [na] kuangaza fahamu zetu kwa muonekano wa mbinguni”29 tunapokuwa tukipambana kutimiza kudra yetu ya milele na kuwa wapokeaji wa asili takatifu.

Natoa ushuhuda wangu kwamba ahadi kuu zaidi na za thamani zinazoambatana na ibada zetu na maagano yetu ni za kweli. Bwana ametamka hivyo:

“Ninatoa kwenu maelekezo jinsi ya kuweza kutenda mbele zangu, ili iweze kugeuka kwenu kwa ajili ya wokovu wenu.

“Mimi, Bwana, ninafungwa wakati ninyi mnapofanya ninayosema; lakini msipofanya ninayosema, ninyi hamna ahadi.”30

Nashuhudia kwamba Baba yetu wa Mbinguni yu hai na ni muumbaji wa mpango wa wokovu. Yesu Kristo ndiye Mwanawe Mzaliwa wa Kipekee, Mwokozi wetu na Mkombozi wetu. Yu hai. Na Ninashuhudia kwamba mpango wa Baba na ahadi , Upatanisho wa Mwokozi, na ushirikiano wa Roho Mtakatifu unawezesha “amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”31 Juu ya kanuni hizi nashuhudia katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.