2010–2019
Ushahidi wa Mungu wa kuvutia: Kitabu cha Mormoni
Oktoba 2017


Ushahidi wa Mungu wa Kuvutia: Kitabu cha Mormoni

Kitabu cha Mormoni ni ushahidi wa Mungu wa kuvutia wa uungu wa Yesu Kristo, wito wa unabii wa Joseph Smith, na ukweli kamili wa Kanisa hili.

Kitabu cha Mormoni sio tu jiwe la msingi la dini yetu, lakini pia kinaweza kuwa jiwe la msingi la ushuhuda wetu ili wakati majaribio au maswali yasiyojibiwa yanapotukabili, kinaweza kushikilia ushuhuda wetu kwa usalama.Kitabu hiki ni uzito mmoja juu ya mizani ya kweli ambao huzidi uzito wa pamoja wa hoja zote za wakosoaji. Kwa nini? Kwa sababu kama ni cha kweli, basi Joseph Smith alikuwa nabii na hili ndilo Kanisa la urejesho la Yesu Kristo, bila kujali hoja yoyote ya kihistoria au nyingine kinyume chake. Kwa sababu hii, wakosoaji wana nia ya kupinga Kitabu cha Mormoni, lakini vikwazo wanavyokabiliana navyo ni vikuu kwa sababu kitabu hiki ni chakweli.

Kwanza, wakosoaji wanapaswa kuelezea jinsi Joseph Smith, kijana mkulima mwenye umri wa miaka 23 mwenye elimu ya chini, aliunda kitabu na mamia ya majina na mahali ya kipekee, pamoja na hadithi na matukio ya kina. Kwa hiyo, wakosoaji wengi hupendekeza kwamba alikuwa mbunifu mwerevu ambaye alitegemea vitabu mbalimbali na rasilimali nyingine za mitaa ili kuunda maudhui ya kihistoria ya Kitabu cha Mormoni. Lakini kinyume na madai yao, hakuna shahidi hata mmoja ambaye anadai kuwa alimwona Joseph na rasilimali hizo zilizotajwa kabla ya utafsiri kuanza.

Hata kama hoja hii ilikuwa kweli, haitoshi sana kuelezea kuwepo kwa Kitabu cha Mormoni. Mtu lazima pia ajibu swali: Joseph alisomaje nyenzo hizi zote zinazodaiwa, kuondoa mambo yasiyo na maana, kuweka wazi kweli tata kama vile,ni nani aliyekuwa mahali gani na wakati gani, na kisha kuitamka kwa kumbukumbu kamili? Kwa kuwa wakati Joseph Smith alipotafsiri, hakuwa na maelezo yoyote. Hakika, mke wake Emma alikumbuka hivi: “Hakuwa na muswada au kitabu cha kusoma. … Ikiwa alikuwa na kitu chochote cha aina hiyo, hangeweza kukificha kutoka kwangu.”1

Kwa hivyo Joseph alifanyaje kazi hii ya ajabu ya kutamka kitabu chenye ukurasa 500 na zaidi bila maelezo yoyote? Ili kufanya hivyo, haikufaa awe tu mbunifu mwerevu lakini pia angekuwa na kumbukumbu ya picha ya idadi kubwa sana. Lakini kama hii ni kweli, kwa nini wakosaaji wake hawakusisitiza talanta hii ya ajabu?

Lakini kuna zaidi. Majadiliano haya yanajumuisha tu maudhui ya kihistoria ya kitabu. Masuala ya kweli bado yamebakia: Je, Joseph alitoaje kitabu kinachonururisha kwa Roho, na alipata wapi mafundisho makubwa sana kama hayo, ambayo mengi yanafafanua au yanapingana na imani za Kikristo za wakati wake?

Kwa mfano, Kitabu cha Mormoni kinafundisha, kinyume na imani nyingi za Kikristo, kwamba Kuanguka kwa Adamu ilikuwa hatua nzuri kusonga mbele. Inafunua maagano yaliyotolewa wakati wa ubatizo, ambayo hajatajwa katika Biblia.

Kwa kuongezea, mtu anaweza kuuliza, Joseph alipata wapi ufahamu wenye nguvu kwamba kwa sababu ya Upatanisho wa Kristo, Yeye hawezi tu kututakasa bali pia kutukamilisha? Alipata wapi mahubiri ya ajabu juu ya imani katika Alma 32? Au mahubiri ya Mfalme Benyamini juu ya Upatanisho wa Mwokozi, labda mahubiri ya ajabu juu ya suala hili katika maandiko yote? Au fumbo la mzeituni na utata wake wote na utajiri wa kimafundisho? Ninaposoma fumbo hili, ni lazima nipate ramani ili kufuata uchangamani wake. Je! Sasa tunapaswa kuamini kuwa Joseph Smith alitoa tu mahubiri haya akilini mwake bila maelezo yoyote?

Kinyume na hitimisho kama hilo, alama za vidole vya Mungu ziko kote katika Kitabu cha Mormoni, kama inavyothibitishwa na ukweli wake mkubwa wa mafundisho, hasa mahubiri yake mazuri juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo.

Ikiwa Joseph hakuwa nabii, basi ili kuzingatia ufahamu huu na mafundisho mengine mazuri ya umaizi wa mafundisho, wakosoaji lazima wafanye hoja kuwa alikuwa pia mwanatheolojia mwenye kipaji. Lakini ikiwa ilikuwa hivyo, mtu anaweza kuuliza: kwa nini Joseph ndiye aliyekuwa wa pekee katika miaka 1,800 kufuatia huduma ya Kristo kutoa mafundisho mapana na ya kufafanua sana? Kwa sababu ilikuwa ufunuo, sio uerevu, ndiyo ulikuwa chanzo cha kitabu hiki.

Lakini hata kama tukidhani kwamba Joseph alikuwa mbunifu na mwanatheolojia mwenye kipaji, mwenye kumbukumbu ya picha—talanta hizi peke yake hazitomfanya awe mwandishi mwenye ujuzi. Kuelezea kuwepo kwa Kitabu cha Mormoni, wakosoaji lazima pia waweke madai kwamba Joseph alikuwa mwandishi wa kawaida mwenye vipawa alipokuwa na umri wa miaka 23. Vinginevyo, alifumanisha vipi majina, maeneo, na matukio katika mshikamano mzima bila kuingiliana? Aliandikaje mikakati ya vita ya kina, kutunga mahubiri mazuri, na kutunga vifungu ambavyo vimesisitizwa, kukaririwa, kunukuliwa, na kuwekwa kwenye milango ya friji na mamilioni ya watu, virai kama vile, “mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu.” (Mosia 2:17) au “wanadamu wapo, ili wapate shangwe.” (2 Nefi 2:25). Hizi ni jumbe zilizo hai—jumbe zinazoishi na kupumua na kuhamasisha. Kupendekeza kuwa Joseph Smith katika umri wa miaka 23 alikuwa na ujuzi muhimu wa kuandika kazi hii ajabu katika mswada mmoja katika takriban siku 65 za kazi ni kinyume na hali halisi ya maisha.

Rais Russell M. Nelson, mwandishi mwenye uzoefu na mwenye ujuzi, alishiriki kwamba alikuwa na maandishi zaidi ya 40 hotuba ya hivi karibuni ya mkutano mkuu. Je! Sasa tunapaswa kuamini kwamba Joseph Smith, peke yake, aliandika Kitabu cha Mormoni chote katika mswada mmoja na mabadiliko machache ya kisarufi yakifanywa hapo baadaye?

Mke wa Joseph, Emma, alithibitisha ugumu wa kazi kama hiyo: “Joseph Smith [kama kijana] hangeweza kuandika wala kutamka barua sahihi na yenye maandishi kamili; acha hata kutamka kitabu kama Kitabu cha Mormoni.”2

Na hatimaye, hata kama mtu anakubali hoja zote zilizotajwa hapo mbeleni, zisizoaminika kama vile zilivyo, wakosoaji bado wanakabiliwa na kikwazo kingine kinachokuja. Joseph alidai kuwa Kitabu cha Mormoni kiliandikwa kwenye mabamba ya dhahabu. Madai haya yalipata ukosoaji mkali katika siku yake—kwa kuwa “kila mtu” alijua kwamba historia za kale ziliandikwa kwenye mafunjo au ngozi, hadi miaka baadaye, wakati mabamba ya metali yenye maandishi ya kale yalipovumbuliwa. Aidha, wakosoaji walidai kuwa matumizi ya saruji, kama ilivyoelezwa katika Kitabu cha Mormoni, ilikuwa zaidi ya ujuzi wa kiufundi wa Wamarekani hawa wa zamani—mpaka miundo ya saruji ilipopatikana katika Amerika ya kale. Wakosoaji sasa wanasema nini kwa uvumbuzi huu na mengine uvumbuzi usiyowezekana kama huu? Joseph, unaona, lazima pia alikuwa ni mtu wa kukisia mwenye bahati sana. Kwa namna fulani, licha ya matatizo yote dhidi yake, dhidi ya ujuzi wote wa kisayansi na wa kitaaluma, alikisia sahihi wakati wengine wote walikosea.

Wakati yote yamesemwa na kufanywa hatimaye, mtu anaweza kushangaa jinsi mtu anaweza kuamini kwamba mambo na nguvu hizi zote zinazodaiwa, kama ilivyopendekezwa na wakosoaji, umewekwa kwa uchangamano kwa njia ambayo ilimwezesha Joseph kuandika Kitabu cha Mormoni na hivyo kuendeleza hila ya kishetani. Lakini hii inaleta maana gani? Kwa kupinga moja kwa moja madai hayo, kitabu hiki kimewahimiza mamilioni kumkataa Shetani na kuishi maisha zaidi ya Kikristo.

Ingawa mtu anaweza kuchagua kuamini njia ya wakosoaji ya kufikiri, kwangu ni, mwisho wa kiakili na kiroho. Kuamini hivyo, itabidi nikubali dhana isiyodhihirishwa moja baada ya nyingine. Kwa kuongezea, itabidi nipuuze ushuhuda wa kila mmoja wa Mashahidi 11,3 ingawaje kila mmoja alibakia mkweli kwa ushuhuda wake hadi mwisho; Itabidi nikatae mafundisho ya Mungu yanayojaza ukurasa baada ya ukurasa wa kitabu hiki kitakatifu kwa ukweli wake wa milele; Itabidi nipuuze ukweli kwamba watu wengi, ikiwa ni pamoja na mimi, wamekuja karibu na Mungu kwa kusoma kitabu hiki kuliko kitabu kingine, na juu ya yote, itabidi nikatae minong’ono ya kuthibitisha ya Roho Mtakatifu. Hii itakuwa kinyume na kila kitu ambacho ninachojua kuwa ni kweli.

Mmoja wa marafiki zangu wazuri na werevu aliacha Kanisa kwa muda. Hivi karibuni aliniandikia juu ya kurudi kwake: “Mwanzoni, nilitaka Kitabu cha Mormoni kuthibitishwa kwangu kihistoria, kijiografia, kiisimu, na kiutamaduni. Lakini wakati nilibadilisha mtazamo wangu kwa yale ambayo kinafundisha juu ya injili ya Yesu Kristo na ujumbe Wake wa kuokoa, nilianza kupata ushuhuda wa ukweli wake. Siku moja nilipokuwa nikisoma Kitabu cha Mormoni katika chumba changu, nilisita na kupiga magoti chini na kutoa sala ya moyo na nikahisi pakubwa kwamba Baba wa Mbinguni alinong’onezea roho yangu kwamba Kanisa na Kitabu cha Mormoni vilikuwa bila shaka vya kweli. Kipindi changu cha miaka mitatu na nusu cha kuchunguza Kanisa upya kiliniongoza tena kwa moyo wote na kwa ushawishi wa ukweli wake.”

Ikiwa mtu atachukua wakati wa kusoma kwa unyenyekevu na kutafakari Kitabu cha Mormoni, kama vile rafiki yangu alivyofanya, na kutegea sikio kwa matunda matamu ya Roho, hatimaye atapokea ushuhuda unaohitajika.

Kitabu cha Mormoni ni mojawapo ya karama za Mungu zenye thamani kuu kwetu. Ni upanga na ngao—hutuma neno la Mungu kwenye vita ili kupigania mioyo ya waadilifu na hutumika kama mlinzi wa tao la ukweli. Kama Watakatifu, hatuna tu fursa ya kutetea Kitabu cha Mormoni bali pia nafasi ya kujihami—kuhubiri mafundisho yake matakatifu kwa uwezo na kutoa ushuhuda wa ushahidi wake mkuu wa Yesu Kristo.

Ninatoa ushuhuda wangu wa dhati kwamba Kitabu cha Mormoni kilitafsiriwa kupitia karama na uwezo wa Mungu. Ni ushahidi wa Mungu wa kusadikisha wa uungu wa Yesu Kristo, wito wa unabii wa Joseph Smith, na ukweli kamili wa Kanisa hili. Na kiweze kuwa jiwe la msingi la ushuhuda wetu, ili kiweze kusemwa kwetu, kama ilivyokuwa kwa Walamani walioongoka “hawakuanguka kamwe” (Alma 23:6). Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Emma Smith, katika “Last Testimony of Sister Emma,” Saints’ Herald, Okt. 1, 1879, 289, 290.

  2. Emma Smith, katika Daughters in My Kingdom, 290.

  3. Ona “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu,” na “Ushuhuda wa Mashahidi Wanane,” Kitabu cha Mormoni.