2010–2019
Toba Siku Zote ni Chanya
Oktoba 2017


Toba Siku Zote ni Chanya

Mara tutakapoweka mguu kwenye njia ya toba, tunaalika nguvu ya kukomboa ya Mwokozi katika maisha yetu.

Miaka kadhaa iliyopita, Rais Gordon B. Hinckley alihudhuria mchezo wa mpira wa miguu wa vyuo. Alikuwa pale kutangaza kwamba uwanja ule wa michezo utaitwa kufuatia kocha wa muda mrefu, aliyependwa, ambaye yuko karibu kustaafu. Kwa vyovyote, timu ilitaka kushinda mchezo huu kwa heshima ya kocha wao. Rais Hinckley alialikwa kutembelea chumba cha mapumziko kushiriki maneno machache ya kutia moyo. Ikitiwa moyo na maneno yake, timu hio siku hiyo ilishinda mchezo huo na kumaliza msimu huo na rekodi ya ushindi.

Leo, ningependa kusema kwa wale wanaoweza kuwa na wasiwasi kwamba “hawashindi” katika maisha. Ukweli ni, kama inavyotarajiwa, kwamba sisi “wote tumetenda dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”1 Wakati kunaweza kuwa na misimu ya kutoshindwa katika mchezo, haipo kabisa katika maisha. Bali nashuhudia kwamba Mwokozi Yesu Kristo alifanya Upatanisho kamili na akatupa zawadi ya toba—njia yetu ya kurudi kwenye uangavu kamili wa matumaini na maisha ya ushindi.

TobaHuleta Furaha

Mara nyingi tunafikiri toba kama kitu cha kuhuzunisha na kuvunja moyo. Bali mpango wa Mungu ni mpango wa furaha, sio mpango wa taabu! Toba inatia moyo na kuadilisha.Dhambi ndiyo huleta huzuni2 Toba ni njia yetu ya kutorokea! Kama Mzee D. Todd Christofferson alivyoelezea: “Bila toba, hakuna maendeleo ya kweli au maendeleo maishani. … Ni kupitia tu toba tunapopata njia ya kufikia neema ya upatanisho wa Yesu Kristo na wokovu.Toba … inatuelekeza kwenye uhuru, matumaini, na amani.”3 Ujumbe wangu kwa wote—hususani kwa vijana—ni kwamba toba daima ni chanya.

Tunapozungumzia toba, hatuzungumzi tu kuhusu juhudi za kujiendeleza binafsi. Toba ya kweli ni zaidi ya hilo—inatiwa moyo na imani katika Bwana Yesu Kristo na uwezo Wake kusamehe dhambi.Kama Mzee Dale G. Renlund alivyotufundisha, “Bila Mkombozi, … toba inakuwa kwa kawaida badiliko nyonge la tabia.”4 Tunaweza kujaribu kubadili tabia zetu sisi wenyewe, lakini Mwokozi tu anaweza kuondoa madoa yetu na kuinua mizigo yetu, kutuwezesha kusaka njia ya utii pamoja na matumaini na nguvu. Furaha ya toba ni zaidi ya furaha ya kuishi maisha ya heshima.Ni furaha ya kusamehewa, ya kuwa safi tena, na ya kukaribia zaidi kwa Mungu. Mara utakapopata furaha hiyo, hakuna hata mbadala wa kadri utakaofaa.

Toba ya kweli inatuvutia sisi kufanya utii wetu kuwa sharti—agano, kuanza na ubatizo, na kurudiwa upya kila wiki wakati wa Meza ya Bwana, sakramenti. Hapo tunapokea ahadi kwamba tunaweza “daima kuwa na Roho wakepamoja [nasi]”5 pamoja na furaha na amani yote ambayo huja kutoka wenza Wake wa siku zote.Hili ni tunda la toba, na hii ndiyo inafanya toba iwe ya furaha!

TobaInahitaji Kuendelea

Ninapenda fumbo la mtoto mpotevu.6 Kuna kitu fulani chenye kutia uchungu kuhusu ule wakati ambao kimsingi mpotevu “Alijitambua” Akiwa amekaa ndani ya zizi la nguruwe, akiwaza angeweza “kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe,” mwishowe alielewa kwamba alikuwa amepoteza sio tu urithi wa baba yake bali pia maisha yake mwenyewe. Akiwa na imani kwamba baba yake angempokea—kama sio mwana basi kama mtumishi—aliamua kuweka uasi wake uliopita nyuma yake na kwenda nyumbani.

Mara kwa mara nimeshangaa kuhusu mwendo mrefu wa mwana kurudi nyumbani. Kulikuwa na muda ambao alisita na kufikiria,”Nitapokelewa vipi na baba yangu? Penginehata alitembea hatua chache nyuma kuelekea kwa nguruwe. Fikiria jinsi hadithi ingekuwa tofauti kama angesalimu amri na kuacha. Bali imani ilimfanya aendelee, na imani ilimfanya baba yake kumtazamia na kungoja kwa subira:

“Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.

“Na mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena.

“Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Leteeni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni: …

“Kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.”

Toba Ni kwa Kila Mtu

Akina kaka na akina dada, sisi wote ni wapotevu. Sisi wote tunatakiwa “kujitambua”—kwa kawaida zaidi ya mara moja—na kuchagua njia ambayo inaongoza kurudi nyumbani. Ni uchaguzi tunaofanya kila siku, maisha yetu yote.

Mara kwa mara tunahusisha toba na dhambi za kusikitisha ambazo zinahitaji“mabadiliko makubwa.”7 Lakini toba ni kwa ajili ya wote—wale wanaotangatanga katika “njia zilizokatazwa na wamepotea”8 vilevile wale ambao “wameingia katika njia nyembamba na iliyosonga” na sasa wanahitaji ku “kusonga mbele.”9 Toba inatuweka sehemu zote mbili kwenye njia sahihi na kutuweka kwenye njia sahihi. Ni kwa wale ambao ndiyo kwanza wanaanza kuamini, wale ambao waliamini wakati wote, na wale ambaowanaohitaji kuanza tena kuamini. Kama Mzee David A. Bednar alivyofundisha: “Wengi wetu tunaelewa kwamba Upatanisho ni kwa ajili ya wenye dhambi. Sina uhakika, hata hivyo, kama tunajua na kuelewa kwamba Upatanisho pia ni kwa watakatifu—kwa wanaume na wanawake wema ambao ni watiifu, wastahiki, na … kujitahidi kuwa wazuri zaidi.”10

Hivi karibuni nilitembelea kituo cha mafunzo cha wamisionari wakati kundi la wamisionari wapya kabisa walipowasili. Nilivutiwa sana nilipokuwa nawaangalia na kugundua nuru katika macho yao. Walionekana waangavu mno na wenye furaha na wenye shauku.Kisha wazo likanijia: “Wamepata uzoefu wa imani mpaka toba. Hii ndio sababu wamejawa na furaha na matumaini.”

Sifikirii kwamba hiyo ina maana wale wote walikuwa na makosa makubwa huko nyuma, bali nafikiria walijua jinsi ya kutubu; walikuwa wamejifunza kwamba toba ni chanya, na walikuwa tayari na walikuwa wenye hamu kushiriki ujumbe huu wa furaha pamoja na ulimwengu.

Hicho ndicho kile kinachotokea wakati tunapohisi furaha ya toba. Fikiria mfano wa Enoshi. Alikuwa na muda wake mfupi sana “kujitambua”, na baada ya hapo “hatia ilifagiliwa mbali,” moyo wake uligeuka mara moja kwenye ustawi wa wengine. Enoshi alitumia maisha yake yote akiwaalika watu wote kutubu na “alifurahia katika hilo zaidi ya yote ya ulimwengu,”11 Toba inafanya hayo; inageuza mioyo yetu kuelekea binadamu wenzetu, kwa sababu tunajua kwamba furaha tunayosikia ni kwa ajili ya kila mtu.

Toba ni Jambo la Kusaka Maisha Yote.

Nina rafiki aliyekulia katika familia ya Watakatifu wa Siku za Mwisho wasio shiriki kikamilifu. Wakati alipokuwa kijana mkubwa, yeye pia “alijitambua” na akaamua kujitayarisha kwa ajili ya misheni.

Alikuwa mmisionari mahiri. Siku yake ya mwisho kabla ya kurudi nyumbani, rais wa misheni alimsaili na kumwomba atoe ushuhuda wake. Alifanya hivyo, na baada ya kukumbatiana na machozi, yule rais alisema, “Mzee, unaweza kusahau au kukana chochote ulichoshuhudia sasa hivi ndani ya miezi kama hutaendelea kufanya mambo ambayo yalijenga ushuhuda wakokwanza.”

Rafiki yangu baadaye aliniambia kwamba ameomba na kusoma maandiko kila siku tangu aliporudi kutoka misheni yake. Kuwa daima “unarutubishwa na neno zuri la Mungu” kumeweka “katika njia sahihi.”12

Nyinyi mnaojitayarisha kwa misheni na nyinyi mnaorudi, chukueni tahadhari! Haitoshi tuu kupata ushuhuda; mnatakiwa kuudumisha na kuuimarisha. Kama kila mmisionsri anavyojua, kama unaacha kupiga pedali baisikeli, itaanguka, na kama unaacha kulisha ushuhuda wako, utafifia. Kanuni hii hii inatumika kwenye toba—ni ya kusaka maisha yote, sio uzoefu wa mara moja katika maisha.

Kwa wote wanaotafuta msamaha—vijana, vijana wakubwa waseja, wazazi, mababu, na ndio, hata mababu wa mababu zetu—ninawaalika mje nyumbani. Sasa ni wakati wa kuanza. Usicheleweshe siku yako ya toba.13

Kisha, utakapokuwa umefanya uamuzi ule, endelea kufuata njia. Baba yetu anangojea, ana hamu ya kukupokea. Mikono yake imenyooshwa“siku mzima” kwa ajili yako.14 Zawadi hii inastahili jitihada.

Kumbuka maneno haya kutoka kwa Nefi: “Kwa hivyo, lazima msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo, mkiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote. Kwa hivyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherekea neno la Kristo, na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.”15

Wakati mwingine safari itaonekana ndefu—hata hivyo, ni safari kuelekea maisha ya milele. Bali inaweza kuwa safari ya furaha kama tukiifuatilia na imani katika Yesu Kristo na matumaini katika Upatanisho Wake. Ninashuhudia kwamba mara tutakapoweka mguu kwenye njia ya toba, tunaalika nguvu ya kukomboa ya Mwokozi katika maisha yetu. Nguvu ile itaimarisha miguu yetu, pamoja na maono yetu, na kuongeza uamuzi wetu wa kuendelea kusonga mbele, hatua kwa hatua, mpaka siku ile tukufu hatimaye wakati wa kurudi nyumbani yetu ya milele na kumsikia Baba yetu Mbinguni akituambia, “Vyema sana”16 Katika jina la Yesu Kristo, amina