2010–2019
Chakula Chenye Uzima Kilichoshuka kutoka Mbinguni
Oktoba 2017


Chakula Chenye Uzima Kilichoshuka kutoka Mbinguni

Kama tunatamani kuishi katika Kristo na kumfanya Yeye aishi ndani yetu, basi utukufu ndio kile tunachotafuta,

Siku baada ya Yesu kimiujiza kulisha wale 5000 kule Galilaya na “mikate mitano tu ya shairi, na samaki wawili wadogo,”1 alizungumza kwa watu tena Kapernaumu. Mwokozi alitambua kwamba wengi hawakuvutiwa sana katika mafundisho Yake kama walivyovutiwa na kulishwa tena.2 Kulingana na hivyo basi, Yeye alijaribu kuwashawishijuu ya thamani kubwa mno ya “chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa.”3 Yesu alitangaza:

“Mimi ndimi chakula cha uzima.

“Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa.

“Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.

“Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”4

Maana ya Mwokozi aliyodhamiria ilipotea kabisa kwa wasikilizaji Wake ambao walielewa maelezo Yake kihalisi tu. Kurudi nyuma kimawazo, walishangaa, “Jinsi gani mtu huyu atatupa sisi mwili wake tuule?”5 Yesu alisisitiza kinagaubaga:

“Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana na Adamu na kuinywa damu yake, hauna uzima ndani yenu.

“Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

“Kwani mwili wangu ni nyama kweli, na damu yangu ni kinywaji kweli.”6

Kisha alieleza maana ya ndani sana ya sitiari Yake:

“Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.

“Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.”7

Bado wasikilizaji wake hawakushika nini Yesu alikuwa anasema, na “wengi … , waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? … [Na] Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena. ”8

Kula nyama yake na kunywa damu yake ni njia ya kuvutia ya kuelezea njia kikamilifu lazima tumlete Mwokozi ndani ya maisha yetu—ndani ya hali yetu kikweli—ili tuweze kuwa wamoja. Ni kwa jinsi gani hili hutokea?

Kwanza, tunaelewa kwamba katika kutoa dhabihu mwili Wake na damu Yake, Yesu alilipia dhambi zetu na alishinda kifo, yote kimwili na kiroho.9 Kwa wazi, kisha, tunapokea mwili Wake na kunywa damu Yake wakati tunapopokea kutoka Kwake nguvu na baraka za Upatanisho Wake.

Mafundisho ya Kristo yanaelezea nini kile ambacho lazima tufanye ili kupokea neema ya upatanisho.Ni kuamini na kuwa na imani katika Kristo, kutubu na kubatizwa, na kumpokea Roho Mtakatifu, “na kisha unakuja msamaha wa dhambi zako kwa moto na kwa Roho Mtakatifu.”10 Hili ndilo lango, la kufikia neema ya upatanisho wa Mwokozi na kwenye njia nyembamba iliyosonga ambayo inaelekea kwenye ufalme Wake.

“Kwa hivyo, kama mtasonga mbele [katika njia], mkila na kusherekea neno la Kristo, na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.

“… Tazama, hili ndilo fundisho la Kristo, na fundisho pekee na la kweli la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, ambao ni Mungu mmoja, bila mwisho.”11

Uashiriaji wa Sakramenti wa Chakula cha Bwana ni mzuri kutafakari. Mkate na maji vinawakilisha mwili na damu Yake ambaye ni Mkate wa uzimana maji yaliyo hai,12 kwa ukweli inatukumbusha kuhusu bei aliyolipa kutukomboa . Wakati mkate unapomegwa, tunakumbuka mwili wa Mwokozi uliochanika. Mzee Dallin H.Oaks wakati mmoja alisema kwamba “kwa sababu unakatwa na kumengwa, kila kipande cha mkate ni cha kipekee, kama vile watu binafsi ambao wanaupokea ni wa kipekee. Sisi wote tuna dhambi tofauti za kutubu. Sisi wote tuna mahitaji tofauti ya kuimarishwa kupitia Upatanisho wa Bwana Yesu Kristo, ambaye tunamkumbuka katika ibada hii.”13 Tunapokunywa maji, tunafikiria damu Yeye alimwaga Gethsemane na juu ya msalaba na nguvu zake za kutakasa.14 Tukijua kwamba “hakuna kitu kichafu kinachoweza kuingia kwenye ufalme wake,” tunaamua kuwa miongoni mwa “hao walioosha mavazi yao katika damu ya [Mwokozi], kwa sababu ya imani zao, na toba ya dhambi zao, na uaminifu wao mpaka mwisho,”15

Nimezungumza juu ya kupokea neema ya upatanisho wa Mwokozi kuondolea mbali dhambi zetu na doa la dhambi hizo ndani yetu. Lakini kimethali kula mwili Wake na kunywa damu Yake ina maana zaidi, na ni kuweka kwandani uborana tabia ya Kristo, kumweka kando mtu wa kawaida na kuwa watakatifu “kupitia upatanisho wa Kristo Bwana.16 Tunapopokea mkate na maji ya sakramenti kila wiki, tutafanya vyema kufikiri jinsi gani kiujazo na kikamilifukwa ukamilifu lazima tujumuishe tabia Yake na mpangilio wa maisha Yake yasiyo na dhambi ndani ya maisha yetu na utu wetu. Yesu asingeweza kulipia dhambi za wengine isipokuwa Yeye mwenyewe alikuwa hana dhambi. Kwa vile sheria haikuwa na dai lolote kwake, angeweza kujitolea Mwenyewe katika nafasi yetu kutosheleza sheria na kisha kutoa huruma. Kama tunavyokumbuka na kuheshimu dhabihu Yake ya upatanisho hatuna budi pia kutafakari maisha Yake yasiyo na dhambi.

Hii inapendekeza haja kupambana kwa nguvu upande wetu. Hatuwezi kuwa tumetosheka kubaki kama tulivyo lakini lazima twende mbele kwa uthabiti kuelekea “kipimo cha tabia ya Kristo mwishowe.”17 Kama baba ya Mfalme Lamoni katika Kitabu cha Mormoni, lazima tuwe tayari kuziacha dhambi zetu zote18 na kulenga kile Bwana anategemea kutoka kwetu, kibinafsi na kwa pamoja.

Sio muda mrefu uliopita, rafiki mmoja alinisimulia uzosefu aliokuwa nao wakati akihudumia kama Rais wa misheni. Alikuwa amefanyiwa upasuaji ambao ulihitaji wiki kadha za kurudisha nguvu. Wakati akipata afueni, alitenga muda wa kupekua maandiko.Alasiri moja alipokuwa anatafakari maneno ya Mwokozi katika sura ya 27 ya 3 Nefi, alielekea usingizini. Yeye kisha alielezea:

“Nilianza kuota ndoto ambayo nilioneshwa kwa uwazi, maisha na matukio ya maisha yangu. Nilioneshwa dhambi zangu, chaguzi mbaya, nyakati … niliwatendea watu kwa hasira, pamoja na kukosa kufanya mengi mazuri ambayo nilitakiwa niseme au kufanya. … [Marejeo] mapana … ya maisha yangu nilioneshwa kwa dakika chache tu, lakini ilionekana muda mrefu zaidi. Niliamka, kwa kushtuka na … mara moja nilipiga magoti pembeni mwa kitanda na nilianzakusali, kuomba msamaha, nikitoa hisia za moyo wangu jinsi ambavyo sijawahi kufanya hapo nyuma.

“Kabla ya ndoto, Sikujua kwamba [nilikuwa] na haja kubwa ya kutubu jinsi hiyo.Makosa yangu na udhaifu ghafla yalikuwa wazi na dhahiri kwangu na kwamba pengo kati ya mtu niliyekuwa na utukufu na uzuri wa Mungu lilionekana [kama] mamilioni ya maili. Katika sala yangu asubuhi ile, nilieleza shukrani zangu za ndani kwa Baba wa Mbinguni na kwa Mwokozi kwa moyo wangu wote kwa kile walichofanya kwa ajili yangu na kwa mahusiano niliyoyatunza ya mke wangu na watoto.Wakati nikiwa nimepiga magoti nilihisi pia upendo wa Mungu na huruma ambayo ilikuwa ya kugusika, licha ya hisia zangu kutostahili, …

“Naweza kusema sijawahi kuwa vile tangu siku hiyo. …Moyo wangu ulibadilika. … Kile kilichofuata ni kwamba nilikuwa zaidi na maono kuelekea wengine, na nafasi kubwa zaidi ya upendo, iliyounganika na hisia ya umuhimu wa kuhubiri injili.…Ningeweza kutoa maelezo kwa ujumbe wa imani, matumaini na toba, na karama za toba zilizopatikana katika Kitabu cha Mormoni [jinsi] ambavyo haijawahi kutokea kabla.”19

Ni muhimu kutambua kwamba ufunuo dhahiri wa huyu mtu mwema wa dhambi zake na mapungufu yake hayakumkatisha tamaa au kumfanya kufa moyo. Ndio, alihisi mshtuko kidogo na majuto. Alihisi hali kali ya haja ya kutubu. Alinyenyekezwa, hata hivyo alihisi shukrani, amani, na matumaini kwa sababu ya Yesu Kristo,” mkate wa uhai ulioshuka chini kutoka Mbinguni.”20

Rafiki yangu alizungumza juu ya pengo aliloona katika ndoto yake kati maisha yake na utukufuwa Mungu, Utukufu ndiyo neno sahihi. Kula mwilina kunywa damu ya Kristo maana yake kufuatilia utukufu. Mungu anaamrisha, “muwe watakatifu, kwani mimi ni mtakatifu. “21

Enoki alitushauri, “Kwa hiyo wafundishe watoto wako, kwamba watu wote, kila mahali, lazima watubu, au vinginevyo hawataweza kuurithi ufalme wa Mungu, kwa maana hakuna kitu kilicho kichafu kinachoweza kukaa huko, au kukaa mbele zake; kwani, katika lugha ya Adamu, Mtu wa Utakatifu ndilo jina lake, na jina la Mwanawe wa Pekee ni Mwana wa Mtu, hata Yesu Kristo, Mwamuzi wa haki, ambaye atakuja wakati wa meridiani.”22 Kama kijana, nilishangaa kwa nini katika Agano Jipya Yesu kila mara anatajwa (na hata anajitaja Mwenyewe) kama Mwana wa Mtu wakati kikweli ni Mwana wa Mungu, lakini maelezo ya Enoki yanaweka wazi kwamba marejeo haya ni kwa kweli utambuzi wa Uungu wake na utukufu—Yeye ni Mwana wa Mtu wa Utukufu, Mungu Baba.

Kama tunatamani kuishi katika Kristo na kumfanya Yeye aishi ndani yetu,23 kisha utukufu ni kile tunachokitafuta, yote mwili na roho.24 Tunautafuta katika hekalu ambako kumeandikwa “Utukufu kwa Bwana.”Tunautafuta katika ndoa zetu, familia, na nyumba zetu, Tunautafuta kila wiki tunapofurahia siku takatifu ya Bwana.25 Tunautafuta hata katika kila kitu cha maisha ya kila siku: mazungumzo yetu, mavazi yetu, mawazo yetu. Kama Rais Thomas S. Monson anavyoesema, “Sisi ni mazao ya vyote tunavyosoma, vyote tunavyoona, vyote tunavyosikia na vyote tunavyofikiri.”26 Tunatafuta utukufu wakati tunapochukua msalaba wetu kila siku.27

Dada Carol F. McConkie, ameona: ”tunatambua wingi wa majaribio, majaribu, na taabu ambazo zinaweza kutuvuta mbali kutoka vyote vile ambavyo ni adilifu na vyenye utukufu mbele ya Mungu. Lakini uzoefu wetu wa maisha ya kufa unatupa nafasi ya kuchagua utukufu. Mara nyingi ni dhabihu tunazofanya kutii maagano yetu ambayo yanatutakasa na kutufanya watakatifu.”28 Na kwenye “dhabihu tunazofanya”, ningeongeza huduma tunayotoa.

Tunajua kwamba “wakati [sisi] tunapowatumikia wanadamu [wenzetu] [sisi] tunamtumikia tu Mungu [wetu].“29 Na Bwana anatukumbusha kwamba huduma kama hiyo ni muhimu katika maisha yake na tabia: “Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa; bali kutimika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.”30 Rais Marion G. Romney kwa busara alielezea: “Huduma siyo kitu tunachovumiliakatika dunia hii ili tuweze kupata haki ya kuishi katika ufalme wa selestia. Huduma ni uzi ambao maisha yaliyotukuka ambao kwao ufalme wa selestia umetengenezwa.”31

Zakaria alitabiri kwamba katika siku yautawala wa milenia wa Bwana katika njuga za farasi zitandikwa maneno, “Utakatifu kwa Bwana”32 Katika roho ile, Watakatifu waanzilishi katika mabonde haya walibandika kumbukumbu ile, “Utukufukwa Bwana,” ilionekana kama ya kawaida au mambo ya ulimwengu huu na vilevile yale ambayo yanahusishwa moja kwa moja na desturi za kidini.Yalikuwa yameandikwa kwenye vikombe na masahani ya sakranenti, nakuchapwa kwenye hati za kutawazwa kwa wale Sabini, na bango la Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.“Utukufu kwa Bwana” pia yalitokea kwenye madirisha ya maonesho ya Taasisi ya Ushirika ya Biashara ya Sayuni, duka kubwa la ZCMI.Yalipatikana kwenye kichwa cha nyundo na ngoma. “Utukufu kwa Bwana” yalikalibiwa kwenye vitasa vya milango ya nyumba ya Rais Brigham. Marejeo haya ya utukufu katika hali inayoonekana yasiyo ya kawaida au sehemu zisizotegemewa yanaweza kuonekana yasiyofaa, lakini yanaashiria jinsi ambavyo yalivyosambaa kote na daima malengo yetu juu ya utukufu yanatakiwa yawe.

Picha
Kikombe cha Sakramenti
Picha
Sahani ya Sakramenti
Picha
Dirisha la ZMCI
Picha
Nyundo
Picha
Ngoma
Picha
Kitasa cha mlango

Kushiriki mwili wa Mwokozi na kunywa damu Yake ina maana kuondoa kwenye maisha yetu chochote kisichowiana na tabia ya kikristo na kufanya sifa zake ziwe zetu. Hii ni maana kubwa ya toba, sio tu kuacha dhambi ya zamani bali pia “kugeuka kwa moyo na mapenzi kwa Mungu”33 kusonga mbele. Kama ilivyotokea kwa rafiki yangu katika ndoto yake ya ufunuo, Mungu atatuonesha mapungufu yetu na kasoro, bali pia atatusaidia kugeuza unyonge kuwa uthabiti34 Kama tutaomba kwa uaminifu, “Nini bado nimepungukiwa?”35 Hatatuacha tukisie, bali kwa upendo Atajibu kwa ajili ya furaha yetu. Na atatupatia tumaini.

Ni juhudi inayotumia nguvu sana, na ingetisha na kuogofya kama katika mapambano yetu kwa ajili ya utukufu tungekuwa peke yetu. Ukweli mtukufu ni kwamba hatupo peke yetu. Tuna upendo wa Mungu, neema ya Kristo, faraja na mwongozo wa Roho Mtakatifu, na urafiki wa Watakatifu wenzetu katika mwili wa Kristo. Na tusiwe tumetosheka na pale tulipo, lakini wala tusikatishwe tamaa. Huu ni wimbo rahisi, bali wimbo makini unaotuhimiza.

Tenga muda kuwa mtakatifu, dunia iko mbio;

Tumia muda mwingi faraghani ya Yesu pekee.

Kwa kumtafuta Yesu, tutakuwa kama Yeye.

Rafikiyo katika tabia yako mfano wake utauona.36

Natoa ushuhuda wa Yesu Kristo, “Mkate wa uzima ulishuka chini kutoka Mbinguni,”37 na kwamba “yoyote aulaye mwili [Wake], na anywae damu [Yake], ana uzima wa milele,”38 katika jina la Yesu Kristo, amina.