2010–2019
Mpango na Tangazo
Oktoba 2017


Mpango na Tangazo

Tangazo kwa familia, ni msisitizo wa Bwana wa ukweli wa injili tunaohitajikutuhimili katika changamoto za sasa kwa familia.

Kama ilivyo dhahiri katika tangazo letu kwa familia, waumini wa Kanisa la Yesu Kristo ka Watakatifu wa Siku za Mwisho wamebarikiwa na injili ya kipekee na njia tofauti za kuutazama ulimwengu. Tunashiriki na hata kufanya vyema katika shughuli nyingi za dunia, lakini katika baadhi ya masomo tunaacha kushiriki tukifuata mafundisho ya Yesu Kristo na Wanafunzi Wake, ya kale na ya sasa.

I.

Katika fumbo,Yesu aliwaelezea wale “ambao [hulisikia] neno” lakini “hawazai” neno lile “linaposongwa”na “shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali” (Mathayo 13:22).Baadaye,Yesu alimsahihisha Petro kwa kutothamini “mambo yanayokuwa ya Mungu, ila yale ya mwanadamu, “Kwani atafaidiwa nini mtu, akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?” (Mathayo 16:23, 26). Katika mafundisho Yake ya mwisho duniani, Aliwaambia Wanafunzi Wake, “Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, … ulimwengu huwachukia” (Yohana 15:19, pia ona Yohana 17:14, 16).

Vivyo hivyo, maandishi ya kale ya Mitume wa Yesu mara kwa mara hutumia taswira ya “ulimwengu” kuwakilisha upinzani kwa mafundisho ya injili. “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii” (Warumi 12:2), Mtume Paulo alifundisha,. “Maana hekima ya dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu” (1 Wakorintho 3:19). Na, “Angalieni,” alionya,“mtu asiwafanye mateka … kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” (Wakolosai 2:8).Mtume Yakobo alifundisha kwamba“kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu[.] …Yeyote basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu” (Yakobo 4:4).

Kitabu cha Mormoni mara nyingi hutumia taswira hii ya upinzani wa “ulimwengu.” Nefi alitoa unabii wa maangamizo ya mwisho ya “wale ambao wamejengwa ili wapate sifa machoni mwa ulimwengu, na wale wanaotafuta … vitu vya ulimwengu” (1 Nefi 22:23, pia ona 2 Nefi 9:30).Alma aliwalaani wale waliokuwa “wamejiinua …kwa vitu vya ulimwengu” (Alma 31:27). Ndoto ya Lehi huonyesha kwamba wale wanaotafuta kufuata fimbo ya chuma, neno la Mungu, watakumbana na upinzani wa ulimwengu. Wakazi wa “jengo kuu na pana” aliloona Lehi “walifanya mzaha na kunyoosha kidole” kwa “dharau” (1Nefi 8:26-27, 33). Katika ono lake lililotafsiri ndoto hii, Nefi alijifunza kwamba dhihaka hii na upinzani ulikuja kutoka kwa “umatiwa dunia, … ulimwengu na hekima yake,… kiburi cha ulimwengu” (1Nefi 11:34-36).

Picha
Picha ya Rais Thomas S. Monson

Nini maana ya tahadhari hizi za maandiko na amri kutokuwa wa “kidunia” au amri ya sasa ya “kuachana na ulimwengu”? (M&M 53:2). Rais Thomas S.Monson alifupisha mafundisho haya: “Lazima tuwe macho katika ulimwengu ambao umesogea mbali kutoka kwenye kile ambacho ni cha kiroho. Ni muhimu kwamba tukatae chochote ambacho hakikubaliani na maadili yetu, kukataa katika mchakato kusalimisha kile tunachotamani sana: uzima wa milele katika ufalme wa Mungu.”1

Mungu aliumba dunia hii kulingana na mpango Wake kuwapa watoto Wake wa kiroho mahali kupata uzoefu wa maisha ya kufa kama hatua muhimu kwa utukufu Anaotamani kwa watoto Wake wote. Wakati kuna falme tofauti na utukufu, lengo kuu la Baba yetu wa Mbinguni kwa watoto Wakeni kile Rais Monson alikiita “uzima wa milele katika ufalme wa Mungu,” ambao ni kuinuliwa katika familia. Hii ni zaidi ya wokovu. Rais Russel M. Nelson ametukumbusha, “katika mpango wa milele wa Mungu, wokovu ni suala binafsi, [lakini] kuinuliwa ni suala la familia.”2

Injili ya urejesho ya Yesu Kristo na tangazo la familia lenye mwongozo, ambalo nitalijadili baadaye, ni mafundisho muhimu kuongoza maandalizi yakuinuliwa.Kama vile tunavyopaswa kuishi kwa sheria ya ndoa na tamaduni zingine za ulimwengu uliofifia, wale wanaotafuta kuinuliwa lazima wafanye chaguzi binafsi katika maisha ya familia kulingana na njia ya Bwana ingawaje hiyo hutofautiana na njia ya ulimwengu.

Katika maisha haya ya kufa, hatuna kumbukumbu ya kile kilichotangulia kuzaliwa kwetu, na sasa tunapitia upinzani. Tunakua na kupevuka kiroho kwa kuchagua kutii amri za Mungu katika mfululizo wa chaguzi sahihi. Hizi hujumuisha maagano na ibada zinazohitajika na toba wakati chaguzi zetu ni mbaya. Kinyume chake, tunapokosa imani katika mpango wa Mungu na kutotii au kwa makusudi kujiondoa kwenye hatua zinazohitajika, tunaahirisha ukuaji na upevukaji huo. Kitabu cha Mormoni hufundisha, “Maisha haya ndiyo wakati wa watu kujitayarisha kukutana na Mungu” (Alma 34:32).

II.

Watakatifu wa siku za Mwisho wanaoelewa mpango wa Mungu wa wokovu wana mtazamo wa kipekee unaowasaidia kuona sababu ya amri za Mungu, asili isiyobadilika ya ibada zinazohitajika, na jukumu muhimu la Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Upatanisho wa Mwokozi wetu hutukomboa kutoka kwenye kifo na, kwa sharti la toba yetu, hutuokoa kutoka na dhambi. Kwa mtazamo huo, Watakatifu wa Siku za Mwisho wana vipaumbele na tamaduni za kipekee na wanabarikiwa kwa nguvu ya kuvumilia vurugu na maumivu ya maisha ya kufa.

Bila shaka, matendo ya wale wanaojaribu kufuata mpangowa Mungu wa wokovu yanaweza kuleta kutoelewana au hata mgongano kwa wanafamilia au marafiki ambao hawaamini kanuni zake. Mgongano huo daima huwa hivyo. Hata kizazi ambacho kimetafuta kufuata mpango wa Mungu kimekuwa na changamoto. Hapo kale, nabii Isaya aliwapa nguvu Waisraeli, ambao aliwaita “ninyi mnaoijua haki, … ambao nimeandika sheria yangu mioyoni mwao.” Kwao alisema, “Msiogope mzaha wa wanadamu, wala msiogope matusi yao” (Isaya 51:7, pia 2 Nefi 8:7). Lakini bila kujali sababu ya mgongano na wale wasioelewa au kuamini mpango wa Mungu, wale wanaoelewa daima wameamriwa kuchagua njia ya Bwana badala ya njia ya Ulimwengu.

III.

Mpango wa injili ambao kila familia inapaswa kufuata ili kujiandaa kwa uzima wa milele na kuinuliwa umefupishwa katika tangazo la kanisa la mwaka 1995, “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.”3 Maazimio yake, kwa kweli, yana muonekano tofauti na sheria za sasa, mila, na utetezi wa ulimwengu ambamo tunaishi. Katika siku yetu, tofauti zilizo dhahiri sana ni kukaa kinyumba bila ndoa, ndoa ya jinsia moja, na kulea watoto katika mahusiano hayo. Wale ambao hawaamini au kutamani kuinuliwa na wanashawishika sana na njia za ulimwengu huchukulia hili tangazo kwa familia kama maelezo ya sera inayopaswa kubadilishwa. Kwa kinyume chake, Watakatifu wa Siku za Mwisho wanakiri kwamba tangazo kwa familia hutoa maana ya aina ya mahusiano ya familia ambapo sehemu kuu ya muhimu ya maendeleo yetu ya milele huweza kutokea.

Tumeshuhudia kuongezeka kwa kasi ukubalifu wa jamii wa kuishi kinyumba bila ndoa na ndoa ya jinsia moja. Utetezi unaofanana wa vyombo vya mawasiliano, elimu, na hata mahitaji ya kazi huleta changamoto ngumu kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ni lazima tujaribu kuweka usawa katika mahitaji yanayoshindana ya kufuata sheria ya injili katika maisha yetu binafsi na mafundisho hata tunapotafuta kuonyesha upendo kwa wote.4 Kwa kufanya hivyo, wakati mwingine tunakumbana na, lakini hatupaswi kuogopa kile Isaya alichoita “mzaha wa wanadamu.”

Mtakatifu wa Siku za Mwisho aliyeongoka huamini kwamba tangazo kwa familia, lililotolewa karibu robo karne iliyopita na kutafsiriwa katika lugha nyingi, ni msisitizo wa Bwana wa ukweli wa injili tunaohitajikutupitisha katika changamoto za sasa kwa familia. Mifano miwili ni ndoa ya jinsia moja na kuishi kinyumba bila ndoa. Miaka 20 tu baada ya tangazo kwa familia, Mahakama ya Juu Marekani ilihalalisha ndoa ya jinsia moja, ikipindua maelfu ya miaka ya ndoa kuwa na mpaka kati ya mwanaume na mwanamke. Asilimia ya kutisha ya watoto wa Marekani waliozaliwa kwa mama ambaye hajaolewa na baba imekuja taratibu: asilimia 5 mwaka 1960,5 asilimia 32 mwaka 1965,6 na sasa ni asilimia 40.7

IV.

Tangazo kwa familia huanza kwa kutangaza “kwamba ndoa kati ya mwanaume na mwanamke imetakaswa na Mungu, na kwamba familia ni muhimu katika mpango wa Muumba kwa maisha ya milele ya watoto Wake.” Pia huthibitisha kwamba “jinsia ni hulka muhimu ya utambuzi wa milele wa maisha kabla ya, maisha ya dunia, na utambulisho na dhamira ya milele.” Linaendelea kutangaza “kwamba Mungu ameamuru kwamba nguvu takatifu za kuzaa ni lazima zitumike tu, kati ya mwanamume na mwanamke, ambao wameoana kihalali kama mme na mke.”

Tangazo linathibitisha muendelezo wa wajibu wa mume na mke kuongezeka na kuijaza dunia na wajibu wa dhati kupendana na kutunzana na kwa watoto wao: “Watoto wana haki ya kuzaliwa ndani ya muungano wa ndoa, na kuleleka na baba na mama ambao huheshimu viapo vya ndoa kwa uaminifu mkuu.” Kwa taadhima linaonya dhidi ya unyanyasaji wa mwenza au watoto, na linatamka kwa dhati kwamba “furaha katika maisha ya familia itapatikana kwa urahisi ikiwa imejegwa katika mafundisho ya Bwana Yesu Kristo.” Mwisho, linatoa mwito wa kuchukua“hatua za kiserikali zilizowekwa kuendeleza na kuimarisha familia kama kitengo muhimu cha jamii.”

Mnamo 1995, Rais wa Kanisana Mitume wengine 14 wa Bwana walitoa maelezo haya muhimu ya mafundisho. Kama mmoja wa hao Mitume saba tu ambao bado wanaishi, ninahisi kulazimika kushiriki kilicholeta tangazo kwa familia kwa maelezo ya wote wanaolizingatia.

Mwongozo uliotambulisha hitaji la tangazo kwa familia ulikuja kwa uongozi wa kanisa miaka 23 iliyopita. Ilikuwa mshangao kwa baadhi waliofikiri kanuni za kweli kuhusu ndoa na familia zilikuwa zikieleweka vizuri bila maelezo ya kujirudia.8 Hata hivyo, tulihisi uhakika na tulianza kazi. Mada zilitambulishwa na kujadiliwa na akidi ya mitume kumi na wawili karibu mwaka mzima. Lugha ilipendekezwa, kupitiwa upya, na kurudiwa. Kwa salatuliendeleakumsihi na Bwana kwa mwongozo Wakejuu ya kile tungesema na jinsi ya kukisema. Sote tulijifunza “mstari juu ya mstari, kanuni juu ya kanuni,” kama Bwana alivyoahidi (M&M 98:12).

Picha
Picha ya Rais Gordon B. Hinckley

Wakati wa mchakato huu wa ufunuo, nyaraka ya pendekezo iliwasilishwa kwa Urais wa Kwanza, ambao husimamia na kutangaza rasmi mafundisho na kanuni ya Kanisa. Baada ya urais kufanya marekebisho zaidi, tangazo juu ya familia lilitangazwa na Rais wa Kanisa, Gordon B. Hinckley. Katika mkutano wa wanawake wa September 23, 1995, alitambulisha tangazo kwa maneno haya: “kwa hila nyingi zinazorithishwa kama ukweli, kwa uwongo mwingi kuhusiana na viwango na thamani, kwa ushawishi mkubwa na ulaghai kuchafua ulimwengu taratibu, tumehisi kuonya na kuonya kabla.”9

Ninashuhudia kwamba tangazo juu ya familia ni maelezo ya ukweli wa milele, mapenzi ya Bwana kwa watoto Wake. Limekuwa ni msingi wa mafundisho na utamaduni wa kanisa kwa miaka 22 iliyopita na itaendelea hivyo siku za baadaye. Lifikirie hivyo, lifundishe, liishi, na utabarikiwa unapojitahidi kusonga mbele hata kwenye uzima wa milele.

Miaka 40 iliyopita, Rais Ezra Taft Benson alifundisha kuwa “kila kizazi kina majaribu yakena nafasi yake ya kusimama na kujithibitisha.”10 Ninaamini mtazamo wetu na matumizi ya tangazo kwa familia ni moja ya majaribu hayo kwa kizazi hiki. Ninaomba kwa ajili ya Watakatifu wa Siku za Mwisho wote kusimama imara katika jaribu hilo.

Ninafunga kwa mafundisho ya Rais GordonB. Hinckley aliyonena miaka miwili baada ya tangazo kwa familia kutangazwa. Alisema “Ninaona sikunjema za usonikatika ulimwengu usio na uhakika. Kama tutashikilia maadili yetu, kama tutajenga juu ya urithi wetu, kama sisi tutaenenda kwa utiifu mbele za Bwana, kama tutaiishi tu injili, tutabarikiwa katika njia ya kipekee. Tutachukuliwa kama watu wa kipekee ambao wamegundua funguo ya furaha ya kipekee.”11

Ninashuhudia juu ya ukweli na umuhimu wa milele wa tangazo kwa familia, lililofunuliwa na Bwana Yesu Kristo kwa Mitume Wake kwa kuinuliwa kwa watoto wa Mungu (ona Mafundisho na Maagano 131:1–4), katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Thomas S. “Simameni Mahali Patakatifu,” Liahona, Nov. 2011, 83.

  2. Russell M. Nelson, “Wokovu na Kuinuliwa,” Liahona, Mei 2008, 7, 10.

  3. Ona “Familia:Tangazo kwa ulimwengu Tangazo kwa Ulimwengu,” Liahona, Nov. 2010, 129.

  4. Ona Dallin H. Oaks, “Love and Law,” Liahona, Nov. 2009, 26–29.

  5. Ona “‘Disastrous’ Illegitimacy Trends,” Washington Times, Dec. 1, 2006, washingtontimes.com.

  6. Ona Stephanie J. Ventura and others, “Report of Final Natality Statistics, 1996,” Monthly Vital Statistics Report, June 30, 1998, 9.

  7. Ona Brady E. Hamilton and others, “Births: Provisional Data for 2016,” Vital Statistics Rapid Release, June 2017, 10.

  8. Rais Mkuu wa Wasichana alisema miaka 20 baadae: “Hatukutambua vyema wakati huo, jinsi ambavyo tungehitaji sana matangazo haya ya msingi katika ulimwengu wa sasa kama vigezo ambavyo tungetumia kupima kila fundisho jipya la kidunia linalotukabili kutoka kwa vyombo vya habari, intaneti, wasomi, televisheni na filamu, na hata wabunge. Tangazo juu ya familia limekuwa kiwango chetu cha kupimia filosofia za dunia, na ninashuhudia kwamba kanuni zilizomo katika kauli hii ni za kweli leo kama zilivyokuwa wakati zilipotolewa kwetu sisi na nabii wa Mungu takribani miaka 20 iliyopita” (Bonnie L. Oscarson, “Walinzi wa Tangazo kwa Familia,” Liahona, May 2015, 14–15).

  9. Gordon B. Hinckley, “Stand Strong against the Wiles of the World,” Ensign, Nov. 1995, 100.

  10. Ezra Taft Benson, “Our Obligation and Challenge,” regional representatives’ seminar, Sept. 30, 1977, 2; unpublished typescript, quoted in David A. Bednar, “On the Lord’s Side: Lessons from Zion’s Camp,” Liahona, July 2017, 19.

  11. Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley (2016), 186; see also “Look to the Future,” Ensign, Nov. 1997, 69.