2010–2019
Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu
Aprili 2018


Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu

Katika siku zinazokuja, haitawezekana kunusurika kiroho bila ushawishi wa kuongoza, kuelekeza, na kufariji wa Roho Mtakatifu.

Ni heshima tukufu iliyoje kuadhimisha Pasaka pamoja nanyi siku hii ya Jumapili ya mkutano mkuu! Hakuna jambo ambalo lingefaa zaidi kuliko kuadhimisha tukio muhimu sana ambalo liliweza kutokea hapa duniani kwa kumwabudu kiumbe muhimu aliyewahi kutembea kwenye dunia hii. Katika hili, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunamwabudu Yeye ambae alianza Upatanisho Wake usio na mwisho katika Bustani ya Gethsemane. Alikuwa tayari kuteseka kwa ajili ya dhambi na udhaifu wa kila mmoja wetu, mateso ambayo yalimsababishia “kutokwa damu katika kila kinyweleo.”1 Alisulibiwa kwenye msalaba wa Kalvari2 na kufufuka siku ya tatu kama kiumbe wa kwanza kufufuka wa watoto wa Baba yetu wa Mbinguni. Ninampenda na ninashuhudia kwamba Yeye anaishi! Ni Yeye ndiye anayelielekeza na kuliongoza Kanisa Lake.

Bila Upatanisho usio na mwisho wa Mkombozi wetu, hakuna yeyote kati yetu angekuwa na matumaini ya wakati wo wote kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Bila Ufufuko Wake, kifo kingekuwa ndiyo mwisho. Upatanisho wa Mkombozi wetu ulifanya uwezekano wa uzima wa milele na kutokufa kuwa uhalisia kwa wote.

Ni kwa sababu misheni yake inayopita uwezo wa binadamu na ile amani anayowapatia wafuasi Wake ambayo mke wangu, Wendy, na mimi tulijisikia faraja mwishoni mwa tarehe 2 Januari, 2018, wakati tulipoamshwa na wito wa simu kutuambia kwamba Rais Thomas S. Monson amevuka ng’ambo ya pazia.

Picha
Rais Russell M. Nelson na Rais Henry B. Eyring

Jinsi gani tunamkosa Rais Monson! Tunaheshimu maisha yake na urithi wake. Jabali kiroho, ameacha alama isiyofutika juu ya wote waliomjua na juu ya Kanisa alilolipenda.

Siku ya Jumapili, Januari 14, 2018, katika chumba cha juu cha Hekalu la Salt Lake, Urais wa Kwanza uliundwa upya katika njia rahisi lakini mpangilio mtakatifu uliowekwaa na Bwana. Kisha katika kusanyiko la kiroho la jana, waumini wa Kanisa ulimwenguni kote waliinua mikono yao juu kuithibitisha kitendo cha awali kilichochukuliwa na Mitume. Kwa unyenyekevu nashukuru kwa kuunga kwenu mkono kukubali kwenu.

Pia nina shukrani kwa wale ambao mabegani mwao ninasimama. Imekuwa kwangu ni heshima kuhudumu katika akidi ya Mitume Kumi na Wawili kwa miaka 34 na kuwajua binafsi Marais 10 kati ya 16 waliotangulia wa Kanisa. Nilijifunza mengi kutoka kwa kila mmoja wao.

Pia nina deni kubwa kwa walionitangulia. Mababa wa mababu zangu wote wanane walioongoka katika Kanisa huko Ulaya. Kila mmoja wapo wa nafsi hizi hodari walitoa dhabihu ya kila kitu ili kuja Sayuni. Wakati wa vizazi vilivyofuatia, hata hivyo, sio wahenga wangu wote walibaki washiriki kikamilifu. Matokeo yake, sikulelewa katika nyumba ambayo injili ilikuwa kitovu chake.

Picha
Wazazi wa Rais Nelson
Picha
Familia Changa ya Rais Nelson

Ninawaheshimu sana wazazi wangu. Walifanya dunia iwe na maana kwangu na kunifundisha masomo ya maana sana. Siwezi kuwashukuru vya kutosha kwa maisha ya furaha nyumbani yaliyojengwa kwa ajili yangu na ndugu zangu. Na bado, hata nilipokuwa kijana, nilijua nilikuwa nakosa kitu fulani. Siku moja nilirukia treni na kwenda duka la vitabu la WSM kutafuta kitabu kuhusu Kanisa. Nilipenda kujifunza kuhusu injili.

Nilipokuja kuelewa Neno la Hekima, niliwataka wazazi wangu kuishi sheria ile. Kwa hiyo, siku moja nilipokuwa mdogo sana, nilikwenda kwenye chumba kilichokuwa chini ya nyumba yetu na kuvunja kwenye sakafu ya saruji kila chupa ya pombe! Nilitegemea baba yangu kuniadhibu, lakini hakusema neno lolote.

Nilipopevuka na kuanza kuelewa umuhimu wa mpango wa Baba wa Mbinguni, mara nyingi nilijiambia, “Sitaki tena zawadi yo yote ya Krismasi! Ninataka tu kuunganishwa kwa wazazi wangu.” Tukio hilo nililotamani sana halikutokea mpaka wazazi wangu walipopita umri wa miaka 80, lakini lilitokea. Siwezi kuelezea kikamilifu furaha ambayo nilihisi siku hiyo,3 na kila siku mimi huhisi furaha hiyo ya kufunganishwa kwao na mimi kufunganishwa nao.

Picha
Russell na Dantzel Nelson

Katika Mwaka 1945, wakati nikiwa shule ya tiba, Nilimwoa Dantzel White katika Hekalu la Salt Lake. Yeye na Mimi tulibarikiwa na mabinti wanane wazuri na mmoja tunu wa kiume. Leo familia yetu inayozidi kukua ni mojawapo ya furaha kuu ya maisha yangu.

Picha
Rais Nelson na Dada Nelson na mabinti wao
Picha
Rais Nelson na mwanawe

Katika mwaka wa 2005, baada ya takribani miaka 60 ya ndoa, kipenzi changu Dantzel aliitwa bila kutegemea nyumbani. Kwa muda, huzuni yangu ilikuwa karibu kudumaza. Lakini ujumbe wa Pasaka na ahadi ya kufufuka ulinisaidia.

Picha
Wendy na RussellNelson

Kisha Bwana alimleta Wendy Watson pembeni mwangu. Tuliunganishwa katika Hekalu la Salt Lake mnamo tarehe 6 Aprili 2006. Jinsi gani ninavyompenda! Yeye ni mwanamke asiye wa kawaida---baraka kubwa mno kwangu, kwa familia yetu na kwa Kanisa zima.

Kila moja ya baraka hizi imekuja kama matokeo ya kutafuta na kusikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu. Alisema Rais Lorenzo Snow, “Hii ni heshima kubwa kwa kila Mtakatifu wa Siku za Mwisho … kwamba ni haki yetu kuwa na ufunuo wa Roho kila siku ya maisha yetu.”4

Mojawapo ya mambo ambayo Roho amerudia kuyaleta katika akili yangu tangu wito wangu mpya kama Rais wa Kanisa ni jinsi Bwana alivyo tayari kufunua fikra na mapenzi yake. Heshima ya kupokea ufunuo ni moja ya karama kuu za Mungu kwa watoto Wake.

Kupitia mafunuo ya Roho Mtakatifu, Bwana atatusaidia katika utafutajii wetu wote wa haki. Katika chumba cha upasuaji, nimesimama karibu na mgonjwa—bila ya kuwa na uhakika jinsi ya kufanya upasuaji haujawahi kufanyika hapo awali—na nikapata mchoro wa Roho Mtakatifu akiuchora kiufundi katika akili zangu.5

Kuimarisha posa yangu kwa Wendy, Nilimwambia, “Ninaujua ufunuo na jinsi ya kuupokea.” Kwa heshima yake—na, nilivyokuja kujifunza, mfano wake halisi—tayari ametafuta na kupokea ufunuo wake mwenyewe kuhusu sisi, ambao ulimpa ujasiri wa kusema ndio.

Kama mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, Niliomba kila siku kwa ajili ya ufunuo na nilitoa shukrani kwa Bwana kila muda aliposema nami kwenye moyo wangu na akili.

Fikiria muujiza wake! Wito wo wote wa Kanisa, tunaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni na kupokea mwongozo na maelekezo, mnaonywa kuhusu hatari na kuvutwa mawazo, na kuwezeshwa kukamilisha vitu kiurahisi ambavyo hatukuweza kufanya sisi wenyewe. Kama hakika tutampokea Roho Mtakatifu na kujifunza na kutambua na kuelewa ushawishi wake, tutaongozwa katika mambo makubwa na madogo.

Hivi karibuni nilipokabiliana na kazi ya ngumu ya kuchagua washauri wawili, nilipatwa na mshangao jinsi ambavyo ningeweza kuchagua wawili tu kutokana na wanaume kumi na wawili ambao nawapenda na kuwaheshimu.

Kwa sababu najua kwamba wazo zuri lipo juu ya msingi wa taarifa, kwa maombi nilikutana uso kwa uso na kila Mtume.6 Na kisha nikajitenga peke yangu katika chumba cha faragha katika hekalu na nilitafuta mapenzi ya Mungu. Ninashuhudia kwamba Bwana alinielekeza kumchagua Rais Dallin H. Oaks na Rais Henry B. Eyring kuhudumu kama washauri wangu katika Urais wa Kwanza.

Katika njia kama hiyo, ninashuhudia kwamba Bwana alinipa mwongozo wa kiungo kwa wito wa Mzee Gerrit W. Gong na Mzee Ulisses Soares ili kutawazwa kuwa Mitume Wake. Ninawakaribisha kwenye huduma hii ya kipekee ya undugu.

Tunapokutana kama baraza la Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, vyumba vyetu vya mikutano vinakuwa vyumba vya ufunuo. Roho ni dhahiri yupo. Tunapokabiliana na mambo chamgamani, njia ya kufurahisha inafunguka wakati kila Mtume kwa uhuru anaelezea mawazo na mtazamo wake. Ingawa tunaweza kutofautiana katika mitazamo ya awali, upendo tunaouhisi sisi kwa sisi ni dhabiti. Umoja wetu unatusaidia kutambua mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Kanisa Lake.

Katika mikutano yetu, walio wengi kamwe hawaamui! Tunasikilizana kimaombi na kuzungumza sisi wenyewe mpaka tunapoukuwa tumekubaliana. Kisha tunapokuwa tumefikia uamuzi kamili, nguvu yenye kutuunganisha ya Roho Mtakatifu ni msisimko wa ute wa mgongo! Tunapata uzoefu wa kile Nabii Joseph Smith alichokijua wakati alipofundisha, “Kwa muungano wa hisia tunapata nguvu na Mungu.”7 Hakuna mshiriki wa Urais wa Kwanza au Akidi ya wale Kumi na Wawili kamwe ataweza kuacha maamuzi kwa ajili ya Kanisa la Bwana uwe uamuzi wake mzuri mwenyewe.

Wakina kaka na dada zangu, tunawezaje kuwa wanaume na wanawake—watumishi wa kama Kristo—ambao Bwana anatuhitaji tuwe? Je, tunawezaje kupata majibu kwa maswali ambayo yanatutatanisha? Kama uzoefu unaopita uwezo wa binadamu wa Joseph Smith katika Kisitu Kitakatifu unatufundisha cho chote, ni kwamba mbingu zipo wazi na kwamba Mungu anazungumza na watoto Wake.

Nabii Joseph Smith aliweka mpangilio kwa ajili yetu sisi ili kuufuata katika kujibu maswali yetu. Akivutiwa kwa ahadi ya Yakobo kwamba kama tunapungukiwa na hekima na tuombe dua kwa Mungu, kijana Joseph alipeleka swali lake moja kwa moja kwa Baba wa Mbinguni.8 Alitafuta ufunuo binafsi, na utafutaji wake ulifungua kipindi hiki cha mwisho cha maongozi ya Mungu.

Kwa namna hii, utafutaji wako utafungua nini kwa ajili yako? Ni hekima gani unayopungukiwa? Je, unaona hitaji gani muhimu kwako kujua au kuelewa? Fuata mfano wa Nabii Joseph Smith. Tafuta sehemu ya ukimya ambako utakwenda mara kwa mara. Jinyenyekeze mbele ya Mungu. Mimina moyo wako kwa Baba yako wa Mbinguni. Mgeukie Yeye kwa ajili ya Majibu na faraja.

Omba katika jina la Yesu Kristo kuhusu matatizo yako, hofu zako, udhaifu wako—ndio, mahitaji ya moyo wako. Na kisha sikiliza! Andika mawazo ambayo yanakuja kwenye akili yako. Andika hisia zako na zifuatilie kwa vitendo ambavyo unashawishiwa kufanya. Unaporudia njia hii siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi, mwaka baada ya mwaka, “utakua katika kanuni za ufunuo.”9

Je, ni kweli Mungu anataka kuongea na wewe? Ndiyo! “Kama vile mwanadamu asivyoweza kunyoosha mkono wake dhaifu kuusimamisha mto Missouri katika mkondo wake uliokusudiwa… ili kumzuia Mwenyezi asimwage chini maarifa kutoka mbinguni juu ya vichwa vya Watakatifu wa Siku za Mwisho.”10

Hupaswi kushangaa kuhusu nini ni kweli.11 Hupaswi kushangaa nani unaweza kumwamini kiusalama. Kupitia ufunuo binafsi, unaweza kupokea ushahidi wako mwenyewe kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu, kwamba Joseph Smith ni nabii, na kwamba hili ni Kanisa la Bwana. Bila kujali nini wengine wanaweza kusema au kufanya, hakuna hata mmoja anayeweza kamwe kuutoa ushahidi iliobebwa kwenye moyo wangu na akili kuhusu nini ni kweli.

Ninawasihi kujinyosha zaidi ya uwezo wenu wa kiroho wa sasa ili kupokea ufunuo binafsi, kwani Bwana ameahidi kwamba “Ikiwa utaomba, nawe utapokea ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa, ili uweze kujua siri na mambo ya amani—yale ambayo huleta shangwe, yale ambayo huleta uzima wa milele.”12

Kuna mengi zaidi Baba yako wa Mbinguni anataka wewe uyajue. Kama Mzee Neal A. Maxwell alivyofundisha, “Kwa wale wenye macho ya kuonea na masikio ya kusikilizia, ni wazi kwamba Baba na Mwana wanatoa siri za ulimwengu!”13

Hakuna kinachofungua mbingu kama vile muungano wa usafi uliozidishwa, utii kamili, kutafuta kwa bidii, kufurahia kila siku maneno ya Kristo katika Kitabu cha Mormoni,14 na muda wa kufanya kila siku kazi ya hekalu na historia ya familia.

Kuwa na uhakika, kunaweza kuwa na muda, wakati unahisi kama kwamba mbingu zimefungwa. Lakini ninaahidi kwamba kadiri mnavyoendelea kuwa watiifu,mkionesha shukrani kwa kila baraka Bwana anazowapa, na kwa subira mnapoheshimu ratiba ya Bwana, mtapewa elimu na uelewa mnaoutafuta. Kila baraka Bwana alizonazo kwa ajili yenu—hata miujiza—itafuata. Hicho ndio kile ufunuo binafsi utafanya kwa ajili yenu.

Mimi nina matumaini mema kuhusu baadaye. Itajazwa na nafasi kwa kila mmoja wetu kuendelea, kuchangia, na kupeleka injili kwa kila pembe ya dunia. Lakini mimi pia sio mshamba kuhusu siku zilizo mbele yetu. Tunaishi katika ulimwengu ambao ni changamani na unaozidishwa na ugomvi. Upatikanaji siku zote wa njia za mawasiliano za kijamii na mzunguko wa taarifa za habari masaa 24 zinatushambulia na ujumbe usio koma. Kama tunatakiwa kuwa na matumaini yo yote ya kupekuwa kupitia sauti nyingi sana na falsafa za watu ambazo zinashambulia ukweli, lazima tujifunze kupokea ufunuo.

Mwokozi na Mkombozi wetu, Yesu Kristo, atafanya baadhi ya kazi Zake kubwa kati ya sasa na wakati atakapo kuja tena. Tutaona dalili za ajabu ambazo Mungu Baba na Mwanae, Yesu Kristo, wataongoza dunia hii katika ukuu wa enzi na utukufu. Lakini katika siku zijazo, haitawezekana kunusurika kiroho bila uzoefu wa kuongoza, kuelekeza, kufariji na daima wa Roho Mtakatifu.

Wapendwa kaka na dada zangu, ninawasihi muongeze uwezo wenu wa kiroho wa kupokea ufunuo. Wacha Jumapili ya Pasaka iwe muda wa udhihirisho katika maisha yako. Chagua kufanya kazi ya kiroho iliyotakiwa kufurahia karama za Roho Mtakatifu na kuisikia sauti ya Roho mara kwa mara zaidi na kwa uwazi zaidi.

Pamoja na Moroni, ninawasihi kwenye Sabato hii ya Pasaka, “kuja kwa Kristo, na kuchukuwa kila karama nzuri ,”15 kuanzia na karama ya Roho Mtakatifu, karama ambayo inaweza na itabadili maisha yako.

Sisi ni wafuasi wa Yesu Kristo. Ukweli muhimu sana Roho Mtakatifu siku zote atashuhudia kwenu ni kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu anayeishi. Yeye yu hai! Yeye ndiye Mwombezi wetu kwa Baba. Mfano wetu, na Mkombozi wetu. Kwenye Jumapili hii ya Pasaka, tunaadhimisha dhabihu Yake ya kulipia dhambi, Ufufuko Wake halisi, na Uungu Wake.

Hili ni Kanisa Lake, lililorejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith. Nashuhudia hayo, kwa kuonesha hisia zangu za upendo kwa kila mmoja wenu, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.