2010–2019
Hata Sabini Mara Saba
Aprili 2018


Hata Sabini Mara Saba

Katikati ya maisha yenye vizuizi na yasiyokamili, sisi wote tunashukuru kwa nafasi za pili.

Makosa ni sehemu ya maisha. Kujifunza kupiga piano kwa ufundi mkubwa haiwezekani bila ya kufanya makosa mara elfu—huenda hata mara milioni. Kujifunza lugha ya kigeni, mtu lazima akumbane na aibu ya kufanya makosa mara elfu—huenda hata mara milioni. Hata wanamichezo mahiri duniani hufanya makosa.

“Mafanikio,” imeelezwa, “siyo kutokuwepo kwa kushindwa, bali ni kutoka kwenye kushindwa na kwenda kwenye kushindwa bila ya kupoteza matumaini.”1

Kwa uvumbuzi wake wa balbu, Thomas Edison inasemekana alisema, “Sikushindwa mara 1,000. Taa ya balbu ni uvumbuzi wa hatua 1,000.”2 Charles F. Kettering alikuita kushindwa “alama za vidole katika safari ya mafanikio.”3 Inawezekana, kila kosa tulifanyalo linakuwa somo katika hekima, tukibadilisha vizuizi kuwa ngazi za kupandia.

Imani thabiti ya Nefi ilimsaidia kutoka kwenye kushindwa hadi kwenye kushindwa tena hata mwishowe alipata mabamba ya shaba. Ilimchukua Musa majaribio 10 kabla hajapata mafanikio ya kutoroka Misri pamoja na Waisraeli.

Tunaweza kushangaa—iwapo wote Nefi na Musa walikuwa katika njia ya Bwana, kwa nini Bwana hakuingilia kati na kuwasaidia kupata mafanikio katika jaribio lao kwanza? Kwa nini Aliwaruhusu—na kwa nini Anaturuhusu sisi—kuteseka na kushindwa katika majaribio yetu ya kufanikiwa? Miongoni mwa majibu mengi muhimu ya swali hilo, haya ni machache:

  • Kwanza, Bwana anajua kwamba “mambo haya yote yatatupa [sisi] uzoefu, na yatakuwa kwa faida [yetu].”4

  • Pili, kuturuhusu sisi “kuonja uchungu, ili [sisi] tupate kujua kutunza chema.”5

  • Tatu, kuthibitisha kwamba “vita ni vya Bwana,”6 na ni kwa neema Yake tu kwamba tunaweza kukamilisha kazi Yake kuwa kama Yeye.7

  • Nne, kutusaidia sisi kuendeleza na kujiandaa kuwa na tabia kama za Kristo ambazo haziwezi “kusafishwa” isipokuwa kwa njia ya “upinzani”8 na “katika tanuru ya mateso.”9

Hivyo, mbele ya maisha yenye vizuizi na yasiyokamili, sisi wote tunashukuru kwa nafasi za pili.

Mnamo mwaka 1970, nikiwa mwaka wangu wa kwanza BYU, nilijiunga na kozi ya mwanzo za fizikia iliyofundishwa na Jae Ballif, profesa mahiri. Baada ya kumaliza kila kitengo cha kozi, alitoa mtihani. Kama mwanafunzi alipata C na angetaka maksi nzuri, Profesa Ballif aliwaruhusu wanafunzi kufanya mtihani mwingine ukijumuisha mambo yaleyale. Kama mwanafunzi anapata B kwenye jaribio la pili na alikuwa bado hajaridhika, aliweza kufanya mtihani kwa mara ya tatu na nne, na kuendelea. Kwa kunisaidia mimi kunipa nafasi ya pili, alinisaidia mimi kuendelea na mwishowe nikapata A katika darasa lake.

Picha
Profesa Jae Ballif

Alikuwa profesa mwenye hekima ajabu na mwenye upendo ambaye anawahuisha na kuwatia moyo wanafunzi wake kuendelea kujaribu—kufikiria ushindwaji kama mwalimu, si kama janga, na kutoogopa kushindwa lakini kujifunza kutokana na hilo.

Hivi karibuni nilimpigia simu mtu huyu muhimu miaka 47 baada ya kuchukua somo lake la fizikia. Nilimwuliza kwa nini alikuwa tayari kuwaruhusu wanafunzi warudie mara nyingi kuboresha maksi zao. Jibu lake: “Nilitaka kuwa upande mmoja na wanafunzi.”

Tukiwa tumeguswa na kufurahia nafasi ya pili baada ya makosa, au kushindwa kwa akili, tumesimama wote tukishangaa neema ya Mwokozi kwa kutupa nafasi ya pili katika kushinda dhambi, au kushindwa kwa moyo.

Hakuna aliye zaidi kwenye upande wetu zaidi ya Mwokozi. Anaturuhusu kurudia na kuendelea kurudia mitihani Yake. Kuwa kama Yeye kutahitaji nafasi za pili katika mapambano yetu ya kila siku pamoja na mwanadamu wa asili, kama vile kudhibiti shauku, kujifunza uvumilivu na kusamehe, kushinda ujasiri, na kuepuka dhambi, nikitaja machache tu. Iwapo kufanya kosa ni hali ya kibinadamu, ni kushindwa mara ngapi kunaweza kutuchukua sisi hadi hali yetu haiwi ya kibinadamu bali ya kiungu? Maelfu? Inawezekana milioni.

Kujua kwamba kuanguka kutakuwa ni hofu ya kila siku kwetu, Mwokozi alilipa deni ili kutupa fursa nyingi kadiri ilivyowezekana ili kushinda majaribio yetu ya duniani. Ukinzani ambao Yeye hurusu mara nyingi unaweza kuonekana wa kutisha na usiowezekana kabisa kuustahimili, lakini Yeye hatuachi bila tumaini.

Kuyaweka matumaini yetu imara tukiwa tunakumbana na changamoto za maisha, neema ya Mwokozi ipo tayari na wakati wote. Neema Yake ni “msaada mtukufu au nguvu, … nguvu ya kuwezesha ambayo inaruhusu wanaume na wanawake kujipatia uzima wa milele na kuinuliwa baada ya kutumia juhudi zao bora wenyewe.”10 Neema Yake na jicho Lake la upendo lipo juu yetu katika safari yetu yote akiwa anatutia moyo, anapunguza mizigo, kuimarisha, kututoa, kutulinda, kutuponya, na vinginevyo “kuwasaidia watu wake,” hata kama wanaanguka katika njia ndefu nyembamba na iliyosonga.11

Toba ni zawadi pekee ya Mungu ambayo inaturuhusu na kutuwezesha sisi kwenda kwenye kushindwa hadi kushindwa tena bila ya kukata tamaa. Toba sio mpango wake wa akiba katika tukio tunaloweza kushindwa. Toba ni mpango Wake, tukijua kwamba tutatubu. Hii ni injili ya toba, na kama Rais Russell M. Nelson anavyoona, itakuwa ni “mtaala wa kudumu.”12

Katika mtaala huu wa toba ya kudumu, sakramenti ndio njia ya Bwana ya kuleta muendelezo wa msamaha Wake. Kama tutaipokea kwa moyo uliyopondeka na roho iliyovunjika, Yeye anatuzawadia msamaha wa kila wiki tunapoendelea kutoka kwenye kushindwa hadi kushindwa tena tukiwa katika njia ya agano. Kwani “licha ya dhambi zao, moyo wangu umejaa huruma juu yao.”13

Lakini ni mara ngapi Yeye tatusamehe? Je, uvumilivu Wake ni wa muda gani? Wakati fulani Petro alimwuliza Mwokozi, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Hadi mara saba?”14

Picha
Petro na Yesu

Kwa kudhania, Petro alifikiri saba ilikuwa ni namba ya juu sana kusisitiza idadi ya juu ya kusamehe mara nyingi na ukarimu ule ungefikia mwisho. Katika kumjibu, Bwana alimwambia Petro asihesabu—asiweke kikomo cha kusamehe.

“Yesu alimwambia, Sikuambii, Hata mara saba: bali, Hata saba mara sabini.”15

Ni dhahiri kwamba, Mwokozi alikuwa haanzishi upeo wa mwisho wa 490. Hiyo italingana na kusema kwamba kula sakramenti kuna mwisho hadi mara 490 na kisha mara ya 491, mkaguzi wa mbinguni ataingilia na kusema, “Ninasikitika, kadi yako ya toba imekwisha muda wake—kuanzia sasa na kuendelea, utakuwa kivyako.”

Bwana alitumia hesabu ya sabini mara saba kama mfano wa Upatanisho Wake usio na mwisho, upendo Wake usiokoma, na neema Yake isiyo na mwisho. Ndio, na kila mara watu wangu watatubu, nitawasamehe makosa yao dhidi yangu.”16

Hiyo haimaanishi kwamba sakramenti inakuwa kibali cha kutenda dhambi. Hiyo ni sababu moja kirai hiki kijumuishwa katika kitabu cha Moroni: “Lakini mara walipotubu na kuomba msamaha, kwa kusudi halisi, walisamehewa.”17

Kusudi halisi linamaanisha kuwa na juhudi halisi na badiliko halisi. “Badiliko” ni neno la kanuni Mwongozo katika Maandiko hutumia kuelezea toba: “Badiliko la akili na moyo ambalo linaleta tabia mpya juu ya Mungu, mtu mwenyewe, na maisha kwa ujumla.”18 Aina hiyo ya badiliko inaleta ukuaji wa kiroho. Mafanikio yetu, hivyo, hayaendi toka kwenye kushindwa hadi kushindwa tena, bali kukua kutoka kwenye kushindwa na kwenda kwenye kushindwa bila ya kupoteza matumaini.

Kuhusu badiliko, fikiria uamuzi huu: “Vitu ambavyo havibadiliki vinabaki kama vilivyo.” Sehemu hiyo ya wazi haimaanishi kudharau akili zenu bali ni kauli ya busara ya Rais Boyd K. Packer, ambaye naye aliongeza, “Na tukishapita kwenye mabadiliko—tumeshavuka.19

Kwa sababu hatutaki kumaliza mpaka tuwe kama vile Mwokozi wetu alivyo,20 tunahitajika kusimama kila muda tuangukapo, kwa nia ya kukua na kuendelea bila kujali mapungufu yetu. Katika udhaifu wetu, Yeye anatuhakikishia sisi, “Neema yangu yakutosha: maana uwezo wangu hutimilika katika udhaifu.”21

Ni kwa muda wa picha au kukua kwa michoro tunaweza kugundua kukua kwetu. Vivyo hivyo, kukua kwetu kiroho mara nyingi hakukubaliki isipokuwa kupitia lensi ya nyuma ya maisha. Ingekuwa vyema mara kwa mara kufanya kipimo kupitia lensi hiyo ili kujua maendeleo yetu na kututia moyo ili tusonge mbele kwa “kuendelea kushirikiana katika Kristo, tukiwa na mwangaza kamili wa tumaini.”22

Nina furaha ya milele kwa ajili ya upendo wa kweli, subira, na uvumilivu wa Wazazi wa Mbinguni na Mwokozi, ambao wanaturuhusu sisi kupata nafasi za pili katika safari yetu ya kurudi katika uwepo Wao. Katika jina la Yesu Kristo, amina.