2015
Yesu Amponya Mkoma
Aprili 2015


Wakati waa Maandiko

Yesu amponya Mwenye Ukoma

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Jifunze kuhusu Agano Jipya pamoja mwaka huu!

Fikiria wakati ulipokuwa mgonjwa. Je! Mtu alifanya jambo lolote la wema ili kukusaidia kujisikia vyema zaidi?

Katika Agano Jipya, tunasoma kuhusu jinsi Yesu alivyoonyesha ukarimu kwa watu waliokuwa wagonjwa. Siku moja mtu aliyekuwa na ugonjwa mkali wa ngozi unaoitwa ukoma alimwendea Yesu. Alijua kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya kila mtu aliyekuwa mgonjwa. Aliamini kuwa Yesu angemponya. Yesu akamgusa mkoma na akamwambia, “Nataka takasika!” (Marko 1:41). Mara Yesu alipokuwa amenena, yule mtu aliponywa.

Tunaweza kufuata nyayo za Yesu kwa kuwa wema na wenye upendo kwa wengine walio wagonjwa au wenye huzuni.