2015
Amefufuka
Aprili 2015


Fasihi za Injili

Amefufuka

David O. McKay alizaliwa Septemba 8, 1873. Alitawazwa kuwa Mtume mnamo Aprili 9, 1906, akiwa na umri wa miaka 32, na Aprili 9, 1951, alikubaliwa kama Rais wa Tisa wa Kanisa. Ifuatayo ni dondoo kutoka katika hotuba aliyoitoa katika mkutano mkuu wa Aprili 1966. Kwa hotuba kamili, ona Conference Report, Apr. 1966, 55–59.

Imani thabiti katika Kristo ndiyo haja muhimu zaidi ya dunia ya leo.

Ikiwa muujiza ni tukio lisilo la kawaida ambalo nguvu iliyosababisha ina shinda hekima iliyo na kipimo cha binadamu, basi Ufufuko wa Yesu Kristo ni muujiza mkuu zaidi kwa wakati wote. Ndani yake kunafunuliwa ukuu wa Mungu na kutokufa kwa binasdamu.

Ufufuo ni muujiza, hata hivyo, katika maana tu kwamba upo nje ya ufahamu na uelewa wa binadamu. Kwa wale wote ambao wanaukubali kama kweli, ni ishara tu ya sheria sare ya maisha. …

Ithibitishe kama ukweli kwamba Kristo hakika aliuchukua mwili wake na kuonekana kama kiumbe aliyetukuzwa, aliyefufuliwa, na unajibu swali la wakati wote: “Kama mtu akifa, je, ataishi tena” (Ayubu 14:14).

Mashahidi wa Ufufuo

Picha
Two Apostles looking at the wounds in Jesus' hand and wrist.

Kwamba ufufuo halisi wa Kristo kutoka kaburini ulikuwa hakikisho kwa wanafunzi ambao walimjua Yeye kwa undani kwamba ni uhakika. Katika mawazo yao hapakuwa na shaka kabisa. Walikuwa mashahidi wa ukweli; walijua maana macho yao yaliona, masikio yao yalisikia, mikono yao iligusa uwepo wa mwili wa Mkombozi aliyefufuka.

Petro, Mtume mkuu, katika tukio wakati wale kumi na mmoja walipokutana ili kumchagua mmoja kuchukua nafasi ya Yuda Iskarioti, alisema, “Basi katika watu hawa lazima mmoja awe shahidi pamoja nasi juu ya kufufuka kwake” (Matendo 1:21–22).

Katika tukio jingine Petro alitangaza mbele ya adui zao, watu wale wale ambao walikuwa wamemuua Yesu msalabani; “Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake” (Matendo 2:22, 32).

Mashahidi wa Ziada

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linasimama na Petro, na Paulo, na Yakobo, na pamoja na Mitume wale wengine wote wa awali waliokubali Ufufuo si tu kama kuwa hakika kweli, lakini kama ukamilifu wa ujumbe mtukufu wa Kristo duniani.

Miaka elfu moja mia nane baada ya Yesu kufa msalabani, Nabii Joseph Smith alitangaza kwamba Bwana aliyefufuka alimtokea yeye, akisema: “Niliwaona Viumbe Wawili, ambao uangavu na utukufu wao ulishinda maelezo yote, wamesimama juu yangu angani. Mmoja wao akaniambia, akiniita mimi kwa jina na kusema, huku akimwonyesha yule mwingine—“Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikize Yeye!” (Joseph Smith—Historia 1:17). …

Ikiwa ushuhuda wa Joseph Smith ulisimama peke yake, ungekuwa, kama vile Kristo alivyosema kuhusu ushahuda wake wakati alipojisemea Mwenyewe, hauna maana yoyote, lakini Yesu alishuhudiwa na Mungu na Mitume. Na Joseph Smith alikuwa na mashahidi wengine [ambao] walithibitisha ushuhuda [wake], ukweli ambao ulijulikana kwao kutokana na malaika Moroni kujitokeza kwao. …

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho [pia] linatangaza ono tukufu la Nabii Joseph Smith:

“Na sasa, baada ya ushuhuda mwingi uliokwisha kutolewa juu yake, huu ni ushuhuda, wa mwisho wa zote, ambao tunautoa juu yake: Kwamba yu hai!” M&M 76:22).

Katika mwanga wa shuhuda kama hizi zisizoweza kukanushwa kama zilivyotolewa na Mitume wa kale—shuhuda zinazoanza miaka michache baada ya tukio lenyewe—katika mwanga wa ufunuo wa ajabu zaidi katika wakati huu wa Kristo aliye hai, inaonekana vigumu kweli kuelewa jinsi watu bado wanaweza kumkataa Yeye na wanaweza kuwa na shaka kuhusu kutokufa kwa mwanadamu.

Ni nini Tunachohitaji Leo

Imani thabiti katika Kristo ndiyo haja muhimu zaidi ya dunia ya leo. Ni zaidi ya hisia tu. Ni nguvu inayosababisha kutenda, na inapaswa iwe katika maisha ya binadamu nguvu ya kushawishi ya msingi zaidi ya zote. …

Ikiwa watu wangetenda tu mapenzi Yake, badala ya kutazamia bila tumaini katika kaburi iliyo giza na huzuni, wangegeuza macho yao yatazame mbinguni na kujua kwamba “Kristo amefufuka!” …

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linatangaza kwa ulimwengu wote kwamba Kristo ni Mwana wa Mungu, Mkombozi wa ulimwengu! Hakuna mfuasi wa kweli anayeridhika na kumkubali Yeye kama tu mleta mabadiliko mkubwa, mwalimu bora, au hata kama mtu mmoja mkamilifu. Mtu wa Galilaya—si kwa kuashiria, lakini hahika ni—Mwana wa Mungu aliye hai.

Hakika Kuzaliwa Upya

Hakuna mtu anayeweza kwa dhati kutumia katika maisha yake ya kila siku mafundisho ya Yesu wa Nazareti bila kuhisi mabadiliko katika maisha yake yote. Kifungu kuzaliwa tena kina maana ya ndani zaidi kuliko kile ambacho watu wengi hudhania kuwa. Ana furaha mtu yule ambaye kwa kweli amehisi nguvu yenye kuinua, kubadilisha inayokuja kutokana na ukaribu huu kwa Mwokozi, ujamaa huu kwa Kristo aliye hai. Ninashukuru kwamba ninajua ya kuwa Kristo ni Mkombozi wangu. …

Ujumbe wa Ufufuko ni wa faraja sana, wa utukufu zaidi ambao kamwe haujawahi kutolewa kwa mwanadamu, kwani wakati kifo kinapomchukua mpendwa mmoja kutoka kwetu, mioyo yetu inayohuzunika huinuliwa na tumaini na uhakika wa kiungu unaoelezwa katika maneno haya: “Hayuko hapa; kwani amefufuka!” [ona Mathayo 28:6; Marko 16:6].

Kwa moyo wangu wote najua kwamba Yesu ameshinda mauti, na kwa sababu Mkombozi wetu anaishi, ndivyo sisi pia.