2015
Songa Mbele katika Imani
Aprili 2015


Endeleeni kwa Imani

Toka katika mkutano wa mafundisho, “Hatahivyo niliendelea ,” yaliyotolewa kwenye Chuo Kikuu cha Brigham Young tarehe 4 Februari, 2014. Kwa nakala nzima katika Kingereza, nenda speeches.byu.edu.

Masomo manne ya kutukuka ya kufanya uamuzi na Nefi yanaweza kupunguza hofu yako na kukuongezea kujiamini ili kusonga mbele.

Picha
composite of Nephi praying and a modern youth praying

Ufafanuzi kutokaRoho ya Maombi,na Claudio Roberto AquiarRamires

Ninyi vijana sasa mnaishi katika kile kinachoitwa “Muongo wa Maamuzi.” Mnafanya maamuzi mengi ya chaguzi muhimu za maisha yenu, kama vile “kwenda hekaluni, kutumikia misheni, kupata elimu, kuchagua taaluma, na kumchagua mwenza na kuunganishwa kwa maisha haya na kwa milele yote katika hekalu takatifu.”1

Ninaongea mahususi kwa wale wanaosumbuka na chaguzi muhimu moja au zaidi ya hizi ya chaguzi muhimu—wengine huenda wanapooza kwa woga wa kufanya maamuzi mabaya au kutaka kuimarishwa kuendelea kuwa na imani kwa uamuzi uliofanywa hapo awali.

Masomo manne ya kutukuka ya kufanya uamuzi na Nefi, kama yanafuatwa, yanaweza kupunguza woga wako na kuongeza kujiamini kwako kusonga mbele.

1. Tii Amri

Mstari wa mwisho wa kumbukumbu tukufu za Nefi zilifumbua maisha yake: “Kwani Bwana ameniamuru hivi, na ni lazima nitii” (2 Nephi 33:15).

Imani ya Nefi na upendo kwaajili ya Mwokozi inajionyesha kwenye utii wake katika amri za Mungu. Aliomba (ona 1 Nephi 2:16). Alisoma maandiko (ona 1 Nephi 22:1). Alitafuta na kufuata mwongozo toka kwa nabii aliye hai (ona 1 Nephi 16:23–24). Utii kama huo ulimruhusu Roho Mtakatifu kuwa na Nefi kwa nguvu katika maisha yake yote na kufuata ufunuo binafsi uliokuwa unaendelea.

Wewe pia lazima ukae karibu na Bwana kwa kutii amri za Mungu. Ninashuhudia kwamba utii endelevu katika mambo madogo kama ya kusoma maandiko, kusali daima, kuhudhuria ibada Kanisani, kufuata ushauri wa manabii walio hai, na kuwatumikia wengine kutakusaidia wewe kuwa na Roho—na ufunuo unaopatikana.

Ukamilifu siyo sharti kwa ufunuo binafsi. Sharti ni toba ya kila siku (ona Warumi 3:23). Kama toba yako ni ya kweli na kamilifu (ona M&M 58:42–43), nguvu ya utakaso ya Upatanisho itamleta Roho akuongoze katika maamuzi magumu ya maisha.

2. Songa Mbele katika Imani

Jiweke mwenyewe kwenye kandambili za Nefi. Baba yako anakuambia Bwana ameiamuru familia yako kuuacha utajiri na kuondoka kwenda nyikani. Hutopenda kujua juu ya safari yako na huko uendako?

Nafikiri Nefi angekuwa amesisimka kama Bwana angekuwa amefunua yale yajayo. Lakini hivyo sivyo Mungu alivyofanya kazi na Nefi, na sivyo atakavyofanya kazi na wewe.

Wakati familia ya Nefi ilipokuwa ikisafiri nyikani, miongozo ilikuja kwake pekee “kila mara” (1 Nefi 16:29; 18:1). Akiitafakari safari ya maisha yake kwa uhakika asingeweza kupewa nafsi iliyonyooka na uzoefu wa imani iliyojengeka ambayo ilimsaidia kuwa mtu mwenye tabia ya Kristo.

Picha
composite with illustration of Lehi loading the plates of Laban on a donkey and a modern girl reading the Book of Mormon

Kama unasubiri Mungu kukufunulia ni taaluma gani uisomee, nani wa kumuoa, kazi gani uikubali, wapi kwa kuishi, au kuendelea na masomo ya juu, na uzae watoto wangapi, huenda usingeweza kuondoka kwenye nyumba yako. Ninashuhudia kwamba ufunuo utakuja tu “Wakati fulani fulani.”

Baba yetu wa mbinguni anataka sisi tukue, na hiyo inajumuisha kukuza uwezo wetu wa kujua mambo, kutoa hukumu, na kufanya maamuzi. Lakini pia anatualika kuleta maamuzi yetu Kwake kwa njia ya sala (ona M&M 9:7–9). Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amefundisha kwamba majibu ya maombi yetu yanakuja “katika moja wapo ya njia tatu.”2

Kuthibitisha Imani

“Kwanza,” Mzee Scott alisema, “unaweza kuhisi amani, ufariji, na uhakika ambao unathibitisha kwamba uamuzi wako ni sahihi.”3 Mke wangu, Christy, na mimi tumegundua kwamba uthibitisho kwa maamuzi yanayo athiri maisha yanaweza kuwasilishwa kupitia maandiko, mara nyingi baada ya ibada ya hekaluni.

Kwa mfano, baada ya kutafakari kwingi na kuomba, tuliamua kuiacha nyumba ya ndoto yetu huko Texas, tukakubali uhamisho wa kikazi, na kuhama na watoto sita kwenda Beijing, China. Lakini kwa kukata tamaa tulitamani uthibitisho wa kiroho kwa uhamisho kama huu. Uhakikisho mtakatifu ulikuja kwetu—katika hekalu—tukiwa tunasoma maneno haya katika Mafundisho na Maagano: “Ni mapenzi yangu kwamba unatakiwa usikawie siku nyingi katika sehemu hii; usifikirie mali yako. Nenda katika nchi za mashariki” (M&M 66:5–7).

Sauti ya Yesu Kristo katika maandiko, ikiambatana na hisia zenye nguvu toka kwa Roho Mtakatifu, ilithibitisha kwamba uamuzi wetu wa kuhamia kwenda China ulikuwa sahihi.

Mawazo yasiyotulia

Njia ya pili Baba wa Mbinguni anavyo jibu sala ni kupitia “hisia zisizotulia, mzubao wa mawazo, ikionyesha kwamba uchaguzi wako si sahihi.”4

Baada ya misheni yangu huko Taiwan, nilifikiri uanasheria wa kimataifa ungekuwa chaguo zuri la kazi. Wakati Christy na mimi tulivyofikiria kwamba uwezekano wa baadaye, tulielewa kwamba miaka mitano zaidi ya elimu ya gharama ilikuwa mbele yetu.

Uchumi wa Marekani ulikuwa umeshuka sana na akiba zetu za pesa zilikuwa kidogo, hivyo tukafikiria kwamba kujiunga na Jeshi la Anga ROTC litakuwa ni chaguo la busara ili kujilipia shule. Lakini nilipofanya mitihani iliyotakiwa na kujaza fomu, hakika hatukujisikia vizuri kufanya yale maamuzi. Hakuna mzubao wa mawazo au hisia zenye giza—ni ukosefu wa amani.

Kile kilicho jifanya maamuzi yasiyo na mantiki kifedha yalihuishwa, katika sehemu ndogo, kwa sababu ningekuwa mwanasheria mbaya!

Uaminifu Mtakatifu

Mungu anajibu maombi kwa njia ya tatu: hakuna jibu. “Wakati unapoishi kwa haki na uchaguzi wako unabaki vilevile katika mafundisho ya Mwokozi na unahitaji kutenda,” Mzee Scott alisema, “endelea kwa kuamini.”5

Jaribio la mwisho la Nefi la kupata mabamba ya shaba linaonyesha ni jinsi gani tunatakiwa kuendelea katika kuamini. Alirekodi:

“Na nikaongozwa na Roho, wala sikujua toka mwanzo vitu ambavyo ningefanya.

Hata hivyo nikaenda mbele” (1 Nephi 4:6–7).

Wakati utawadia kipindi cha muongo wako wa maamuzi wakati ambao huwezi kuahirisha zaidi na lazima kutenda. Nimejifunza kwanza, kama Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amefundisha, “tutapata mwongozo wa Roho pale tutakapofanya kila kitu tunachoweza, pale tutakapokuwa nje juani tukifanya kazi badala ya kukaa kivulini tukiomba kwa ajili ya mwongozo wa hatua ya kwanza ya kuchukua.”6

Kama ilivyokuwa kwa Nefi, Roho katika muda muafaka atathibitisha au kukuonya njia uliyochagua.

3. Ishi Kisasa

Kujitoa kwa Nefi kwenda nchi ya ahadi kunasimama kama kizuizi cha kaka zake Lamani na Lemueli. Walifanya uamuzi wa kwenda, lakini mioyo yao haikuondoka Yerusalemu. Nefi alikuwa akitengeneza upinde wake uliovunjika ili awinde kwa ajili ya chakula na kupasua mbao ili kutengeneza meli wakati kaka zake wakiwa wakicheka kwenye hema.

Leo ulimwengu una akina Lamani na Lemueli wengi. Lakini Mungu anahitaji wanaume na wanawake waliojidhatiti kama Nefi. Utapata uzoefu mkubwa kimaendeleo katika maisha unapojitoa kabisa katika maamuzi yako na kujitahidi kufanya vizuri zaidi katika hali yako ya sasa hata wakati una jicho linaloangalia baadae.

Nefi anaonesha kwa mfano ushauri wa busara wa Rais Thomas S. Monson: “Ndoto za mchana zilizopita na kutamani ya baadae inaweza kutoa faraja lakini haiwezi kuchukua nafasi ya kuishi katika maisha ya sasa. Hii ni siku ya nafasi yetu, na lazima tuishike.”7

4. Kuwa karibu na Nguvu za Wengine

Hata baada ya kutaka kuwa na Roho, tusonge mbele na uamuzi wetu, na tuwe tumejitoa kabisa, shaka zaweza kuendelea kujitokeza na kusababisha sisi kujiuliza uamuzi wetu. Katika hali kama hiyo familia iliyoaminika au rafiki anaweza kutoa ushauri na nguvu ya kuendelea kubaki kwenye njia. Ninashauri kwamba katika safari yake, mke wa Nefi akawa nanga yake ya kuaminika.

Shukrani kwa mke wa Nefi zikaja kwangu wakati nikitembelea Kumbukumbu za Historia ya Kanisa. Nilishangazwa na picha ya kuchorwa ya Nefi aliyokuwa amefungwa kwa nguvu kwenye mlingoti wa boti, akiwa amelowa sana kwa dhoruba kali.8

Kwenye upande wa Nefi walikuwa mke wake na mmoja wa watoto wake. Alikuwa anapitia tukio hilo hilo la dhoruba na changamoto kama Nefi, lakini macho yake yalikuwa na ujasiri na mikono yake ilikuwa inamlinda imezungushwa mabegani mwake. Katika wakati huo nilitambua kwamba nami pia nilikuwa nimebarikiwa kuwa na mwenza mwaminifu anayenipa nguvu wakati wa majaribu. Nilitumaini kwamba nami nilikuwa ni nguvu kwake.

Picha
composite of Nephite family and modern couple

Ndugu, kutunza na kuongeza nguvu za kiroho ulizozianzisha (au ambazo mtazianzisha) kama mmisionari au katika huduma nyingine za haki ni rasilimali nzuri kwako katika kuwa mume na baba mwema. Akina dada, kiwango cha kuhisi cha kiroho, imani, na ujasiri wa kumfuata Yesu Kristo ni miongoni mwa tabia zenu bora kama mke na mama.

Ninakualika kuwa aina ya mtu ambaye mwenza wako wa sasa au baadaye anaweza kutoa ushauri wenye busara na nguvu. Mwanamume muadilifu na mwanamke mstahiki, waliounganishwa katika milele yote kwenye hekalu, wanaweza kufanya mambo magumu kama wenza sawa.

Ninaahidi kwamba kama mtayatumia mafundisho mliyojifunza toka kwa Nefi na manabii wa sasa kuhusu kufanya maamuzi, mtaongozwa na ufunuo binafsi “kila mara.” Unapoendelea katika muongo wa uamuzi, ninaomba, kama alivyokuwa Nefi, kuwa na imani ya kusema:

“Na nikaongozwa na Roho, wala sikujua mapema vitu ambavyo ningefanya.

Hata hivyo niliendelea mbele” (1 Nefi 4:6–7).

Muhtasari

  1. Robert D. Hales, “Kwa Wenye Ukuhani wa Haruni: Kujiandaa kwa ajili ya Muongo wa Uamuzi,” Liahona, Mei 2007, 48.

  2. Richard G. Scott, “KutumiaKipawa cha Maombi Kutoka Juu,” Liahona, Mei 2007, 10; emphasis in original.

  3. Richard G. Scott, “Kutumia Kipawa cha Maombi Kutoka Juu,” 10.

  4. Richard G. Scott, “Kutumia Kipawa cha Maombi Kutoka Juu,” 10.

  5. Richard G. Scott, “Kutumia Kipawa cha Maombi Kutoka Juu,” 10.

  6. Dallin H. Oaks, “Katika Wakati Wake Mwenyewe, katika njia Zake Mwenyewe,” Liahona, Aug. 2013, 26.

  7. Thomas S. Monson, “Katika kutafuta Hazina,” Liahona, May 2003, 20.

  8. Ona Helpmeet, by K. Sean Sullivan, in “Kitabu cha Mormoni: A Worldwide View,” Liahona, Dec. 2000, 37.