2015
Kwa sababu ya Joseph
Aprili 2015


Kwa sababu ya Joseph

Tambua njia sita za maisha yako yalivyo (au yanaweza kuwa) tofauti kwa sababu ya Nabii Joseph Smith.

Picha
Painting of a young boy kneeling looking up at a grove of trees. At the center of the painting is a young boy (age 14) kneeling. His hands are resting on his thighs and he looks up at a light source above his head. The boy wears grey trousers (with suspenders) and grey vest and an off-white shirt. The shirt has a collar and two button placket at the front and the sleeves are rolled. The young boy had blond hair that is slightly rumpled. The background his a grove of trees, almost all with no leaves. There are some low saplings immediately behind the boy. The foreground has rocks, twings and small plants sprouting. "Walter Rane 04" appears in the lower right corner in red.

Joseph Smith alikufa zaidi ya miaka 170 iliyopita. Aliishi miaka 38 tu, akitumia zaidi ya muda huo katika sehemu za kujificha ambazo huenda wewe pengine huwezi kuzipata popote isipokuwa kwenye ramani yenye maelekezo ya kina. Na huenda pengine una mazoea na vitu vingi alivyovifanya katika maisha yake. Lakini umewahi kufikiria jinsi yanavyo kuathiri wewe binafsi? Wakati njia hizo ni nyingi kuzihesabu, unaweza kuanza na hizi sita.

Kwa sababu ya Joseph Smith:

1. Unaelewa Mungu na Yesu Kristo ni nani haswa.

Hata kama haingekuwa kwa Joseph Smith, bado ungeamini katika Mungu Baba na katika Yesu Kristo. Ungekuwa na ushuhuda wa Biblia. Lakini fikiria kiasi gani kwa undani na ametajirisha zaidi uelewa wako ni kwa sababu ya kile Joseph Smith alirejesha—ujasiri, ushuhuda uliokubalika wa Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu. Kwa mfano, unajua kitu ambacho watu wengi wa ulimwengu hawakijui: kwamba Mwokozi mfufuka alijidhihirisha huko Marekani—akithibitisha, kwa maneno Yake, kwamba Yeye si tu “Mungu wa Israeli, [bali pia] ni Mungu wa ulimwengu wote” (3 Nephi 11:14).

Fikiria jinsi ushuhuda wako wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo unavyo imarishwa kwa ushahidi wa nguvu wa manabii kama Nefi, Alma, na Moroni—bila kumsahau Joseph Smith mwenyewe, aliyetangaza: “Anaishi! Kwani tulimwona yeye, hata katika mkono wa kuume wa Mungu” (M&M 76:22–23). Katika siku ambayo imani kwa Mungu na Yesu Kristo inapingwa na mara nyingi kutelekezwa, ni baraka za aina gani ya kuwa na mwanga huu wa ziada!

2. Unajua kwamba wewe ni mwana wa Mungu—na hivyo ndivyo kila mmoja.

Picha
Youth in the Philippines are walking in a line and laughing and holding hands.

Pengine ukweli muhimu sana aliorejesha Joseph Smith kilikuwa ni ukweli kuhusu uhusiano wetu na Mungu.1 Yeye ni Baba yetu halisi. Umeshawahi kuacha kufikiria kuhusu vitu ambavyo vinatokana na ukweli ule? Inabadilisha jinsi unavyojiona mwenyewe: bila kujali ulimwengu unafikiria nini juu yako, unajua kwamba wewe ni mtoto mpendwa wa Mungu, ukiwa na sifa zake ndani yako. Inabadilisha jinsi unavyo waona wengine: ghafla kila mmoja—kila mmoja—ni kaka au dada yako. Inabadilisha jinsi unavyo yaona maisha yenyewe: furaha zake zote na majaribu ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kukusaidia wewe kuwa kama Yeye alivyo. Hakuna kitu kibaya kwenye nyimbo unazoimba kwenye darasa la watoto!2

3. Familia yako yaweza kuwa ya milele.

Picha
Family posing together on a street in Hong Kong.

Kwa nini watu wengi wanachanganyikiwa kuhusu umuhimu wa ndoa na familia? Huenda ni kwa sababu hawajui mafundisho, yaliyo rejeshwa kupitia Joseph Smith, kwamba ndoa na familia vimetawazwa na Mungu na vimepangwa kuwa vya milele (ona M&M 49:15; 132:7). Hizi siyo desturi zilizotengenezwa na mwanadamu ambazo jamii yetu imekuwa nazo—ni sehemu ya mpango wa milele wa mbinguni. Na asante kwa funguo za ukuhani na ibada za hekalu ambazo zilirejeshwa kupitia Joseph Smith, familia yako ya milele inaweza kuanzia hapa duniani.

4. Unayo njia ya kufikia ukuhani na baraka zake.

Picha
Filipino church members during a sacrament meeting.

Kwa sababu Mungu alirejesha ukuhani Wake kupitia Joseph Smith, unaweza kubatizwa, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Unaweza kutafuta baraka za ukuhani wa uponywaji, faraja, na mwongozo. Unaweza kufanya maagano matakatifu ambayo yanakuunganisha na Mungu. Na unaweza kuyarudia maagano upya kila wiki wakati unapokula sakramenti. Kupitia ibada za ukuhani, nguvu za Mungu zinaingia katika maisha yako (ona M&M 84:20–21). Hakuna kati ya hili linalowezekana bila ya kazi iliyokamilishwa kupitia Joseph Smith.

5. Upo huru kutokana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya.

Picha
Two young men in DR Congo playing basketball.

Au angalau unaweza kuwa kama unatii ufunuo wa Joseph uliopokelewa huko nyuma mwaka 1833—zamani kabla tumbaku haijagundulika kitabibu kuwa inasababisha saratani ya mapafu na pombe ilihusishwa na ugonjwa wa ini. Wakati unapokuwa na nabii akifunua hekima za Mungu, kwa nini usubiri hekima za ulimwengu zikufikie? Neno la Busara linaonyesha kwamba Mungu hazijali roho zetu pekee bali pia kuhusu miili yetu (ona M&M 89). Baada ya yote, kama vile ufunuo kwa Joseph Smith ulivyoelezea, kuwa na mwili kunatufanya sisi zaidi—siyo kidogo—kuwa kama Baba yetu wa Mbinguni, ambaye pia ana mwili wa nyama na mifupa (ona M&M 130:22).

6. Unaweza kujua ukweli wewe mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu.

Picha
A young Polynesian woman kneeling in prayer beside her bed.

Wakati kijana Joseph alipokwenda kwenye Kichaka Kitakatifu mwaka 1820, imani ya kawaida miongoni mwa makanisa mengi ilikuwa kwamba ufunuo ulikuwa ni kitu cha kale. Ono la Kwanza la Joseph linathibitisha kuwa si kweli. Mbingu ziko wazi—na si kwa manabii pekee. Yeyote mwenye swali anaweza kupata jibu kupitia unyenyekevu, kutafuta kwa dhati (ona M&M 42:61; 88:63). Kwa mfano, unaweza kujua mwenyewe kwamba Joseph Smith alikuwa ni Nabii wa Mungu kwa njia ile ile aliyotumia Joseph: kwa kumwuliza Mungu Mwenyewe.

Orodha hii ni mwanzo tu. Ungeweza kuongeza nini? Maisha yako yanatofauti gani kwa sababu ya Joseph Smith?

Muhtasari

  1. Ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 37–44.

  2. Ona “Mimi ni Mwana wa Mungu,” Hymns, no. 301.