2018
Pata Kumjua Yeye na Familia Yake
February 2018


Kanuni za Ualimu wa Kutembelea, Februari 2018

Pata Kumjua Yeye na Familia Yake

Ualimu wa kutembelea unahusu kupata kumjua kila dada na kumpenda kila dada ili tuweze kumsaidia kuimarisha imani yake na kutoa huduma.

Imani, Familia, Usaidizi

Rita Jeppeson na mwalimu wake mtembeleaji wamekuwa marafiki wazuri wakati ambapo walikuwa wakitembeleana na kushiriki kanuni za injili. Lakini kutembeleana kwao pia ni pamoja na kucheza michezo ya kuunda maneno pamoja. Ni kitu kinachompendeza Rita zaidi kuhusu mwalimu wake mtembeleaji kwa sababu anafahamu ya kwamba wao ni marafiki na matembezi hayo sio tu jambo la “kutia alama kuonyesha kukamilika” kwenye orodha. Kuna mambo mengi ambayo kina dada wanaweza kufanya wakati wa matembezi, kama vile kutembea pamoja au kungo’a magugu katika bustani huku watoto wakicheza.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema, “Jitazameni kama wajumbe wa Bwana kwa watoto Wake. … Tungetumaini … kwamba mtaanzisha, kipindi cha uhalisia, cha kiinjili juu ya kuwajali waumini, kuwaangalia waumini na kujaliana, mkishughulikia shida za kiroho na kimwili kwa njia yoyote inayoleta usaidizi.”1

Bwana kupitia Musa aliwaamuru wana wa Israeli kwamba “Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzaliwa kwenu, mpende kama nafsi yako (Mambo ya Walawi 19:34). Kina dada ambao tunawatembelea na kuwafundisha wanaweza kuwa “wageni” tunapoanza huduma yetu, lakini tunapopata kumjua pamoja na familia yake, hamu yetu itaongezeka “kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe miepesi” na kuwa “mioyo yetu iunganishwe pamoja kwa umoja na kwa upendo mmoja kwa mwingine” (Mosia 18:8, 21).

Reyna I. Aburto, Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, hukumbuka wakati alikuwa muumini mpya wa kanisa aliyetalikiwa karibuni. “Waalimu wangu wa kutembelea walikuja nyumbani kwangu,” alisema, “na walileta hisia njema za kujumuishwa na upendo katika moyo wangu.”2

Zingatia Hili

Katika familia za kina dada ambao wewe unawatembelea kuwafundisha, ni matukio gani muhimu yajayo ambayo unapaswa kuyajua na kuyakumbuka?

Muhtasari

  1. Jeffrey R. Holland, “Wajumbe wa Kanisa,” Liahona, Nov. 2016, 62.

  2. Reyna I. Aburto, “Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama Umekuwa Nini Kwangu?” Mkutano Mkuu wa Wanawake kule Brigham Young University, Mei 5, 2017, LDS.org.