2018
Kujenga Mahusiano ya Maana
August 2018


Picha
Ministering

Kanuni za Kuhudumu, Agosti 2018

Kujenga Mahusiano ya Maana

Uwezo wetu wa kuwajali wengine unaongezeka tunapokuwa na uhusiano mzuri pamoja nao.

Mwaliko wa kuwahudumia wengine ni fursa ya kujenga mahusiano ya kujali pamoja nao—aina ya uhusiano ambao ungewafanya kuwa huru kuomba au kukubali usaidizi wetu. Tunapokuwa tumefanya juhudi za kukuza aina hiyo ya uhusiano, Mungu anaweza kubadilisha maisha katika pande zote za uhusiano.

“Ninaamini kwa dhati hakuna badiliko la maana bila mahusiano ya maana,” alisema Dada Sharon L. Eubank, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Usaidizi wa Kina Mama. Na kwa matendo yetu ya huduma kuwa yenye mgeuzo katika maisha ya wengine, alisema, lazima “yawe na mizizi kwenye hamu ya dhati ya kuponya na kusikiliza na kushiriki na kuheshimu.”1

Mahusiano ya maana siyo mbinu za utekelezaji wa sera. Yamejengwa juu ya huruma, juhudi za dhati, na “upendo usio unafiki” (M&M 121:41).2

Njia za Kujenga na Kuimarisha Mahusiano

“Tunajenga [mahusiano] mtu mmoja baada ya mwingine,” alisema Mzee Dieter F. Uchtdorf Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.3 Tunapojitahidi kujenga mahusiano ya maana na wale tunaowahudumia, Roho Mtakatifu anaweza kutuongoza. Mapendekezo yafuatayo yamejikita katika mpangilio Mzee Uchtdorf aliotoa.4

  • Jifunze kuhusu wao.

    Rais Ezra Taft Benson (1899–1994) alifundisha, “Huwezi kuwatumikia vyema wale usiowajua vyema.” Alipendekeza kujua majina ya kila mwanafamilia na kujua matukio muhimu kama vile siku za kuzaliwa, baraka, ubatizo, na ndoa. Hii hutoa fursa ya kuandika ujumbe au kupiga simu kumpongeza mwanafamilia kwenye mafanikio maalumu au ufanikishaji.5

  • Tumieni muda pamoja.

    Uhusiano huchukua muda kukua. Tafuta fursa za kuendeleza mawasiliano. Utafiti unaonyesha kwamba kuwafanya watu wajue kwamba unajali ni muhimu kwa mahusiano bora.6 Watembelee mara kwa mara wale ambao umeitwa kuwahudumia. Zungumza nao kanisani. Tumia njia zozote za ziada zinazoleta maana—kama vile barua pepe, Facebook, Instagram, Twitter, Skype, kupiga simu, au kutuma kadi. Mzee Richard G. Scott (1928–2015) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alizungumza kuhusu nguvu ya maonyesho rahisi yenye ubunifu ya upendo na msaada: “Mara nyingi ningefunua maandiko yangu, … na kupata ujumbe wa upendo na wa kuunga mkono [mke wangu] Jeanene aliopachika kwa siri ndani ya kurasa. … Jumbe hizo za thamani … zimeendelea kuwa hazina ya thamani ya faraja na ushawishi.”7

    Pia, kumbuka kwamba uhusiano huchukua pande mbili. Unaweza kuonesha upendo na urafiki, lakini uhusiano hauwezi kukua mpaka onesho hilo liweze kukubaliwa na kurudishwa. Kama mtu mwingine anaonekana kutopokea, usilazimishe uhusiano. Mpe mtu huyo muda kuona juhudi zako za dhati, na kama itabidi, shauriana na viongozi wako kuhusu kama uhusiano wa maana bado unaonekana kuwezekana au kutowezekana.

  • Wasiliana kwa kujali.

    Kujenga mahusiano ya maana kunatuhitaji kwenda zaidi ya kijuujuu. Mawasiliano ya kijuujuu yamejaa mazungumzo madogo madogo kuhusu ratiba, hali ya hewa, na mambo mengine yasiyo ya muhimu sana, lakini hayajumuishi kushiriki hisia, imani, malengo, na shughuli ambazo ni muhimu kutengeneza mahusiano yenye maana zaidi. Baba wa Mbinguni ametengeneza aina hii ya maana zaidi ya mawasiliano kwa kushiriki hisia Zake na mipango na Mwana Wake (ona Yohana 5:20) na kwetu sisi kupitia manabii Wake (ona Amosi 3:7). Kwa kushiriki matukio ya siku kwa siku na changamoto za maisha na kila mmoja wetu kama tunavyoongozwa na Roho, tunapata ukubali wa kila mmoja tunapotafuta mvuto wa pamoja na uzoefu wa pamoja.

    Kusikiliza ni sehemu muhimu ya kuonyesha kwamba unajali.8 Unaposikiliza kwa makini, fursa yako ya kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo huongezeka unapopata uelewa na utambuzi kwenye mahitaji yao na wanapohisi kupendwa, kueleweka na salama.

  • Zithamini tofauti vile vile mifanano.

    “Baadhi … wanaamini kwamba Kanisa linataka kutengeneza kila muumini kutoka kwenye tabia moja—kwamba kila mmoja anapaswa kutazama, kuhisi, kufikiri, na kutenda kama wengine wote,” alisema Mzee Uchtdorf. “Hii ingepinga uwezo wa Mungu, ambaye alimuumba kila mtu tofauti na ndugu yake. …

    “Kanisa linasitawi tunapotumia utofauti huu na kumtia moyo kila mtu kukuza na kutumia talanta zetu kuinua na kuimarisha wafuasi wenzetu.”9

    Kuwapenda wengine jinsi Mungu anavyotupenda sisi kunahitaji kwamba tujaribu kuwaona wengine jinsi Mungu anavyowaona. Rais Thomas S. Monson (1927–2018) alifundisha, “Lazima tukuze uwezo wa kuwaona [wengine] si kama walivyo hivi sasa lakini kama wanavyoweza kuwa.”10 Tunaweza kuomba kwa ajili ya msaada ili kuwaona wengine jinsi Mungu anavyowaona. Tunapowatendea wengine kulingana na uwezekano wao wa kukua, wanaweza kuonyesha uwezo unaohitajika.11

  • Watumikie.

    Kuwa mwepesi kuona mahitaji ya wale unaowahudumia na kuwa tayari kutoa muda wako na talanta, iwe wakati wa uhitaji au kwa sababu tu unajali. Unaweza kuwa pale kutoa faraja, msaada, na usaidizi unaohitajika kunapokuwa na dharura, ugonjwa, au hali ya haraka. Lakini katika mahusiano mengi sisi ni wenye kuonyesha hisia. Mungu alitupatia uhuru wa kuchagua ili kwamba tutende kuliko kutendewa (ona 2 Nefi 2:14). Kama vile Mtume Yohana alivyofundisha kwamba sisi twampenda Mungu kwa maana Yeye alitupenda sisi kwanza (ona 1 Yohana 4:19), wakati wengine wanapohisi upendo wetu wa kweli kupitia matendo yetu ya huduma, inaweza kulainisha mioyo na kuongeza upendo na uaminifu.12 Hii hutengeneza mzunguko wa kwenda juu wa matendo ya ukarimu ambayo yanaweza kujenga mahusiano.

Kuhudumu kama Mwokozi Alivyofanya

Yesu Kristo alijenga mahusiano ya maana na Wafuasi Wake (ona Yohana 11:5). Aliwajua (ona Yohana 1:47–48). Alitumia muda pamoja nao (ona Luka 24:13–31). Mawasiliano Yake yalikwenda zaidi ya kijuujuu (ona Yohana 15:15). Alitambua vyema tofauti zao (ona Mathayo 9:10) na kuona nguvu yao (ona Yohana 17:23). Yeye alimtumikia kila mtu, japokuwa alikuwa Bwana wa wote, anasema Hakuja kutumikiwa bali kutumikia (ona Marko 10:42–45).

Wewe utafanya nini kujenga mahusiano imara na wale ulioitwa kuwatumikia?

Muhtasari

  1. Sharon Eubank, katika “Matendo ya Kibinadamu Lazima Yawe na mizizi katika Uhusiano, Sharon Eubank Anasema,” mormonnewsroom.org.

  2. Ona “Kanuni za Kuhudumu: Nyosha Mkono kwa Huruma,” Liahona, Julai 2018, 6–9.

  3. Dieter F. Uchtdorf, “Kwa Vitu Vyenye Umuhimu Zaidi,” Liahona, Nov. 2010, 22.

  4. Ona Dieter F. Uchtdorf, “Kwa Vitu Vyenye Umuhimu Zaidi,” 22.

  5. Ona Ezra Taft Benson, “Kwa Waalimu wa Nyumbani wa Kanisa,” Ensign, Mei 1987, 50.

  6. Ona Charles A. Wilkinson na Lauren H. Grill, “Kuonyesha Upendo: Msamiati wa Jumbe zenye Upendo,” katika Kutengeneza Mahusiano: Masomo katika Mawasiliano ya kimahusiano, ed. Kathleen M. Galvin, 5th ed. (2011), 164–73.

  7. Richard G. Scott, “Baraka za Milele za Ndoa,” Liahona, Mei 2011, 96.

  8. Ona “Kanuni za Kuhudumu: Vitu Vitano Wasikilizaji Wazuri Huvifanya,” Liahona, Juni 2018, 6–9.

  9. Dieter F. Uchtdorf, “Vichwa vya Habari Vinne,” Liahona, Mei 2013, 59.

  10. Thomas S. Monson, “Waone Wengine jinsi Wanavyoweza Kuwa,” Liahona, Nov. 2012, 69.

  11. Ona Terence R. Mitchell na Denise Daniels, “Motisha,” katika Handbook of Psychology, vol. 12, ed. Walter C. Borman na wengine (2003), 229.

  12. Ona Edward J. Lawler, Rebecca Ford, na Michael D. Large, “Unilateral Initiatives as a Conflict Resolution Strategy,” Social Psychology Quarterly, vol. 62, no. 3 (Sept. 1999), 240–56.