2018
Shauriana kuhusu Mahitaji Yao
Septemba 2018


Picha
ministering

Kanuni za Uhudumu, Septemba 2018

Shauriana kuhusu Mahitaji Yao

Huna haja ya kufanya hivi peke yako. Kushauriana kunaweza kuleta msaada unaouhitaji ili kuwasaidia wengine.

Mungu amekualika wewe kumhudumia mtu au familia katika kata yako au tawi kulingana na mahitaji yao. Ni kwa namna ipi unaweza kujua mahitaji hayo ni yapi? Kanuni ya kushauriana, ambayo imekuwa ni kitovu katika Kanisa ni ufunguo.

Baada ya kujadiliana kuhusu nini tunaweza kushauriana, tutachunguza:

  1. Kushauriana na Baba wa Mbinguni.

  2. Kushauriana na mtu na familia ambayo umepewa kuihudumia.

  3. Kushauriana na mhudumu mwenza.

  4. Na kushauriana na wengine waliopewa jukumu la kuhudumu katika familia ile ile au mtu yule yule unayemhudumia.

Kushauriana na viongozi wetu pia ni muhimu. Makala ya siku zijazo ya Kanuni za Kuhudumu katika Liahona zitafafanua kwa kina katika kushauriana na viongozi na pia kazi ya usahili wa wahudumu katika mchakato huo.

Tunachoshauriana

Kuelewa mahitaji ni muhimu katika kuhudumiana sisi kwa sisi. Lakini ni katika hali ipi mahitaji haya yanaweza kuwa na je, kuna kitu kingine cha zaidi tofauti na mahitaji ambacho ni lazima tukitambue?

Mahitaji yanaweza kuja katika hali tofauti. Wale tunaowatumikia wanaweza kukumbana na changamoto ambazo ni za kihisia, kifedha, kimwili, kielimu, na zaidi. Mahitaji mengine ni ya kipaumbele zaidi kuliko mengine. Baadhi tutaweza kuwa na uwezo kuwasaidia; wengine inaweza kutulazimu kutoa msaada sisi wenyewe. Katika juhudi zetu ili kusaidia mahitaji ya kimwili, tusisahau kuwa wito wetu kuhudumu hujumuisha kuwasaidia wengine kuendelea katika njia ya agano, kujiandaa kwa ajili ya na kupokea ibada za muhimu za kikuhani kwa ajili ya kuinuliwa.

Kwa nyongeza katika kushauriana kuhusu mahitaji ya mtu au familia, hatuna budi kutafuta kujifunza kuhusu uwezo wao. Je, ni nini wasichohitaji kusaidiwa? Ni uwezo gani na vipawa vipi walivyonavyo ambavyo vingeweza kubariki wengine? Ni kwa namna ipi wao wanafaa kipekee katika kusaidia kuujenga ufalme wa Mungu? Kuelewa uwezo wa mtu kunaweza kuwa ni muhimu kama kuelewa mahitaji yake.

Kushauriana na Baba wa Mbinguni

Moja kati ya kanuni kuu za imani yetu ni kwamba Baba wa Mbinguni huzungumza na watoto Wake (ona Makala ya Imani 1:9). Tuanapopokea jukumu jipya la kumhudumia mtu fulani, hatuna budi kushauriana na Baba wa Mbinguni katika sala, tukitafuta umaizi na uelewa katika mahitaji na uwezo wao. Mchakato huo wa kushauriana kupitia sala lazima uendelee katika kipindi chote cha uhudumu kwetu.

Kushauriana na watu binafsi na familia

Ni kwa namna gani na kwa wakati gani tunawatazama watu binafsi na familia ambazo tumeitwa kuzitumikia kunaweza kutofautiana kutokana na hali, lakini kushauriana moja kwa moja na mtu binafsi au familia ni muhimu katika kujenga mahusiano na uelewa wa mahitaji yao, ikijumuisha namna gani wanataka kusaidiwa. Baadhi ya maswali yanaweza kusubiri mpaka pale uhusiano wenye tija umejengeka. Wakati kukiwa hakuna njia moja sahihi ya kufanya hivyo, fikiria yafuatayo:

  • Tafuta ni kwa namna ipi na wakati upi wangependa uwasiliane nao.

  • Jifunze kuhusu vitu wavipendavyo na asili yao.

  • Njoo na mapendekezo ya jinsi unavyoweza kusaidia, na waulize mapendekezo yao.

Wakati tukijenga uaminifu, fikiria kujadili kuhusu mahitaji ya mtu binafsi au familia. Uliza maswali kama ulivyotiwa msukumo na Roho Mtakatifu.1 Kwa mfano:

  • Ni changamoto zipi wanazokumbana nazo?

  • Je, ni malengo gani binafsi na ya kifamilia ambayo wanayo? Kwa mfano, je, wanataka kuwa bora zaidi katika kuwa na jioni ya familia nyumbani kila mara, au kuwa bora zaidi katika kujitegemea?

  • Ni kwa namna gani tunaweza kuwasaidia katika malengo na changamoto zao?

  • Ni ibada zipi za injili ambazo zinakuja katika maisha yao? Tunawezaje kuwasaidia kujiandaa?

Kumbuka kutoa msaada maalum, kama vile, “Ni usiku gani wa wiki hii tunaweza kukuletea chakula?” Pendekezo lisilo dhahiri, kama, “Tufahamishe kama kuna kitu chochote tunaweza kufanya,” halisaidii sana.

Kushauriana na Mhudumu mwenza

Kwa sababu wewe na mhudumu mwenza mnaweza msiwe pamoja kila mara wakati mnapokutana na mtu binafsi au familia, ni muhimu kuratibu na kushauriana kwa pamoja wakati mkitafuta msukumo wa kiungu kama wahudumu wenza. Haya ni baadhi ya maswali ya kufikiria:

  • Ni kwa jinsi gani na mara ngapi mtawasiliana kama wahudumu wenza.

  • Ni kwa namna gani kila mmoja wenu anaweza kutumia uwezo binafsi katika kuhudumia familia au mahitaji ya mtu binafsi.

  • Ni vitu gani mmejifunza, ni uzoefu upi mliokuwa nao, na msukumo upi mmeupata tangu wakati wa mwisho mlipoongelea kuhusu familia au mtu binafsi?

Kushauriana na Wengine Waliopewa Jukumu

Inaweza kuwa vizuri kila baada ya muda fulani kuongea na wengine ambao wamepewa jukumu la kuhudumia familia au mtu yule yule ambaye mnamhudumia.

Wasiliana ili Kutatua Changamoto

Mzee Chi Hong (Sam) Wong wa Sabini alitumia tukio kutoka Marko 2 katika siku zetu kufafanua jinsi gani kushauriana kwa pamoja kuliwawezesha watu wanne kupata jinsi gani ya kumwezesha mtu mwenye kupooza kufika katika uwepo wa Yesu.

“Ingeweza kuwa kama hivi,” alisema Mzee Wong. Watu wanne walikuwa wanatimiza jukumu kutoka kwa Askofu wao kumtembelea nyumbani kwake mtu mwenye kupooza. … Katika baraza la kata la hivi karibuni, baada ya kushauriana kwa pamoja juu ya mahitaji ya kata, askofu alikuwa ametoa majukumu ya ‘kwenda kuokoa.’ Hawa wanne walipewa kazi ya kumsaidia mtu huyu mwenye kupooza. …

“[Walipofika katika jengo ambalo Yesu alikuwemo,] watu walikuwa wamejaa sana chumbani. Hawakuweza kuingia kupitia mlangoni. Nina uhakika walijaribu kila kitu walichoweza kukifikiria, lakini hawakuweza kupita. … Walishauriana kwa pamoja nini cha kufanya—namna wangewezaje kumfikisha mtu yule kwa Yesu Kristo ili aponywe. … Walikuja na mpango—si mpango rahisi, lakini waliutekeleza.

“… ‘Waliitoboa dari pale alipokuwapo: na wakiisha kuivunja, wakaliteremsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza’ (Marko 2:4). …

“… ‘Naye Yesu, alipoona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako’ (Marko 2:5).”2

Mwaliko wa Kutenda

Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alihimiza, “Shaurianeni pamoja, tumieni kila zana inayopatikana, tafuteni mwongozo wa Roho Mtakatifu, mwombeni Bwana kwa ajili ya uthibitisho Wake, na kisha kunjeni mikono ya mashati yenu na mwende kufanya kazi.

“Ninawapa ahadi: kama mtafuata mpangilio huu, mtapokea mwongozo maalum wa nani, nini, lini, na wapi pa kutumikia katika njia ya Bwana.”3

Muhtasari

  1. Ona Hubiri Injili Yangu Mwongozo kwa ajili ya Huduma ya Kimisionari (2004), 183.

  2. Chi Hong (Sam) Wong, “Rescue in Unity,” Liahona, Nov. 2014, 14–15.

  3. Dieter F. Uchtdorf, “Providing in the Lord’s Way,” Liahona, Nov. 2011, 55.