Maandiko Matakatifu
2 Nefi 25


Mlango wa 25

Nefi anautukuza unyoofu—Unabii wa Isaya utafahamika katika siku za mwisho—Wayahudi watarejea kutoka Babilonia, watamsulubu Masiya, na watatawanywa na kuadhibiwa—Watarudishwa wakimwamini Masiya—Atakuja kwanza miaka mia sita tangu Lehi aondoke Yerusalemu—Wanefi wanatii sheria ya Musa na kumwamini Kristo, aliye Mtakatifu wa Israeli. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Sasa mimi, Nefi, nasema machache kuhusu maneno ambayo nimeandika, ambayo yamenenwa na kinywa cha Isaya. Kwani tazama, Isaya alizungumza vitu vingi ambavyo vilikuwa avigumu kufahamika na watu wangu; kwani hawajui kuhusu mtindo wa kutoa unabii miongoni mwa Wayahudi.

2 Kwani mimi, Nefi, sijawafundisha vitu vingi kuhusu desturi za Wayahudi; akwani kazi zao zilikuwa kazi za giza, na matendo yao yalikuwa matendo ya machukizo.

3 Kwa hivyo, ninawaandikia watu wangu, kwa wale wote watakaopokea hapo baadaye vitu hivi ambavyo ninaandika, ili wajue hukumu za Mungu, kwamba zinashukia mataifa yote, kulingana na neno ambalo amenena.

4 Kwa hivyo, sikilizeni, Enyi watu wangu, ambao ni wa nyumba ya Israeli, na msikilize maneno yangu; kwani kwa sababu maneno ya Isaya sio wazi kwenu, walakini ni wazi kwa wale wote ambao wamejazwa na aroho ya bunabii. Lakini nawapatia unabii, kulingana na roho aliye ndani yangu; kwa hivyo nitatoa unabii kulingana na cunyofu uliokuwa na mimi tangu wakati nitoke Yerusalemu na baba yangu; kwani tazama, nafsi yangu inafurahia unyofu kwa watu wangu, ili wajifunze.

5 Ndiyo, na nafsi yangu inafurahia maneno ya aIsaya, kwani nilitoka Yerusalemu, na macho yangu yameona vitu vya bWayahudi, na ninajua kwamba Wayahudi wanafahamu vitu vya manabii, na hakuna watu wengine wanaofahamu vitu vilivyonenwa Wayahudi kama wao, ila tu kwamba wawe wamefundishwa desturi ya vitu vya Wayahudi.

6 Lakini tazama, mimi, Nefi, sijafundisha watoto wangu desturi za Wayahudi; lakini tazama, mimi, mwenyewe, nimeishi Yerusalemu, kwa hivyo najua kuhusu eneo karibu inayoizingira; na nimewatajia watoto wangu kuhusu hukumu za Mungu, ambazo azimefanyika miongoni mwa Wayahudi, kwa watoto wangu, kulingana na yale yote ambayo Isaya amezungumza, na siyaandiki.

7 Lakini tazama, ninaendelea na unabii wangu, kulingana na aunyofu wangu; ambamo kwayo najua kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kukosea; walakini, katika siku ambazo unabii wa Isaya utatimizwa watu watajua kwa hakika, wakati yatatimizwa.

8 Kwa hivyo, yana athamani kwa watoto wa watu, na kwa yule anayedhani kwamba hayana, kwa hawa nitawazungumzia zaidi, na kuyatilia mkazo kwa watu bwangu; kwani ninajua kwamba yatawafaidi sana katika csiku za mwisho; kwani katika siku hizo watayafahamu; kwa hivyo, ni kwa faida yao nimeyaandika.

9 Na kama vile kizazi kimoja miongoni mwa Wayahudi akimeangamizwa kwa sababu ya uovu, hata hivyo wameangamizwa kutoka kizazi hadi kizazi kulingana na maovu yao; na hakuna aliyeangamizwa bila bkuaguliwa na manabii wa Bwana.

10 Kwa hivyo, walikuwa wameelezewa kuhusu maangamizo yatakayowajia, mara tu baada ya baba yangu alipotoka Yerusalemu; walakini, walishupaza mioyo yao; na kulingana na unabii wangu awameangamizwa, ijapokuwa wale bwaliopelekwa utumwani huko Babilonia.

11 Na sasa haya nazungumza kwa sababu ya roho iliyo ndani yangu. Na ingawaje wamehamishwa watarejea tena, na kumiliki nchi ya Yerusalemu; kwa hivyo, awatarudishwa tena katika nchi yao ya urithi.

12 Lakini, tazama, watakuwa na vita, na uvumi wa vita; na wakati siku inafika ambayo aMzaliwa Pekee wa Baba, ndiyo, hata Baba wa mbingu na dunia, atajithirihisha mwenyewe kwao katika mwili, tazama, watamkataa, kwa sababu ya maovu yao, na ugandamizo wa mioyo yao, na ugumu wa shingo zao.

13 Tazama, awatamsulubu; na baada ya kulazwa katika bziara kwa muda wa siku ctatu datafufuka kutoka kwa wafu, na uponyaji katika mabawa yake; na wale wote watakaoamini kwa jina lake wataokolewa katika ufalme wa Mungu. Kwa hivyo, nafsi yangu inafurahia kutoa unabii kumhusu, kwani enimeona siku yake, na moyo wangu unatukuza jina lake takatifu.

14 Na tazama itakuwa kwamba baada ya aMasiya kufufuka kutoka kwa wafu, na kujithirihisha kwa watu wake, kwa wengi kadiri watakavyoliamini jina lake, tazama, Yerusalemu bitaangamizwa tena; kwani ole kwa wale wanaopigana dhidi ya Mungu na watu wa kanisa lake.

15 Kwa hivyo, aWayahudi bwatatawanywa miongoni mwa mataifa yote; ndiyo, na cBabilonia pia itaangamizwa; kwa hivyo, Wayahudi watatawanywa na mataifa mengine.

16 Na baada ya wao kutawanywa, na Bwana Mungu kuwapiga kwa mataifa mengine kwa muda wa vizazi vingi, ndiyo, hata chini kutoka kizazi hadi kizazi mpaka watashawishiwa akumwamini Kristo, Mwana wa Mungu, na upatanisho, ambao ni kwa wanadamu wote bila kikomo—na wakati ile siku itakapofika kwamba watamwamini Kristo, na kumwabudu Baba katika jina lake, na mioyo mweupe na mikono safi, na wasimtazamie Masiya mwingine, kisha, katika ule wakati, siku itafika ambapo itakuwa lazima waamini vitu hivi.

17 Na Bwana atanyoosha mkono wake tena mara ya pili akuwarudisha watu wake kutoka kwa hali yao ya kupotea na kuanguka. Kwa hivyo, ataendelea kutenda kazi bkuu na maajabu miongoni mwa watoto wa watu.

18 Kwa hivyo, atawaletea maneno yake, amaneno yale byatakayowahukumu katika siku ya mwisho, kwani yatapewa kwao kwa lengo la ckuwasadikisha kuhusu Masiya wa kweli, aliyekataliwa nao; na kuwasadikishia kwamba hawana haja tena kumtazamia Masiya mwingine aje, kwani hakuna mwingine atakayekuja, ila tu awe dMasiya wa bandia atakayewadanganya watu; kwani kuna Masiya mmoja tu anayezungumziwa na manabii, na huyo Masiya ndiye yule atakayekataliwa na Wayahudi.

19 Kwani kulingana na maneno ya manabii, aMasiya atakuja baada ya miaka bmia sita tangu baba yangu atoke Yerusalemu; na kulingana na maneno ya manabii, na pia neno la cmalaika wa Mungu, jina lake litakuwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

20 Na sasa, ndugu zangu, nimezungumza wazi ili msikosee. Na jinsi aishivyo Bwana Mungu aaliyewatoa Israeli kutoka nchi ya Misri, na akampatia Musa uwezo kwamba baponye mataifa baada ya wao kuumwa na cnyoka wenye sumu, kama wangemtazama nyoka ambaye aliinuliwa mbele yao, na pia akampa uwezo kwamba agonge dmwamba na maji yatokee; ndiyo, tazama nawaambia, kwamba jinsi vile hivi vitu ni kweli, na jinsi Bwana Mungu aishivyo, hakuna ejina lingine ambalo limetolewa chini ya mbingu ila tu awe huyu Yesu Kristo, ambalo nimelizungumzia, ambalo kwamba mwanadamu anaweza kuokolewa.

21 Kwa hivyo, kwa sababu hii Bwana Mungu ameniahidi kwamba hivi vitu ambavyo aninaandika vitawekwa na kuhifadhiwa, na kutolewa kwa uzao wangu, kutoka kizazi hadi kizazi, ili ahadi atimiziwe Yusufu, kwamba uzao wake bhautaangamia kamwe kadiri dunia itakavyosimama.

22 Kwa hivyo, hivi vitu vitaendelea kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kadiri dunia itakavyokuwepo; na vitaendelea kulingana na njia na mapenzi ya Mungu; na mataifa yatakayovimiliki ayatahukumiwa kwavyo kulingana na maneno ambayo yameandikwa.

23 Kwani tunajitahidi kuandika, akuwashawishi watoto wetu, na pia ndugu zetu, kumwamini Kristo, na kupatanishwa na Mungu; kwani tunajua kwamba ni kwa bneema kwamba tunaokolewa, baada ya ckutenda yote tunayoweza.

24 Na, ingawa tunamwamini Kristo, atunatii sheria ya Musa, na kutazama mbele kwa uthabiti kwa Kristo, hadi sheria itakapotimizwa.

25 Kwani, ni kwa kusudi hili asheria ilitolewa; kwa hivyo sheria bimekufa kwetu, na tumefanywa hai katika Kristo kwa sababu ya imani yetu; lakini bado tunatii sheria kwa sababu ya amri.

26 Na atunazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa bunabii kumhusu Kristo, na tunaandika kulingana na unabii wetu, ili cwatoto wetu wajue asili ya kutegemea dmsamaha wa dhambi zao.

27 Kwa hivyo, tunazungumza kuhusu sheria ili watoto wetu wajue mauti ya sheria; na wao, kwa kujua mauti ya sheria; watatazama mbele kwa ule uhai ulio katika Kristo, na wafahamu ni kwa kusudi gani sheria ilitolewa. Na baada ya sheria kutimizwa katika Kristo, kwamba wasishupaze mioyo yao dhidi yake wakati sheria itakapotakiwa kuwekwa kando.

28 Na sasa tazama, watu wangu, ninyi ni watu wa ashingo ngumu; kwa hivyo, nimewazungumzia kwa uwazi, ili msielewe vibaya. Na maneno ambayo nimezungumza yatabaki kama bushuhuda dhidi yenu; kwani yanatosha ckumfundisha mtu yeyote njia iliyo sawa; kwani njia iliyo sawa ni kuamini katika Kristo na kutomkana kwani kwa kumkana unawakana pia manabii na sheria.

29 Na sasa tazama, nawaambia kwamba njia iliyo sawa ni kuamini katika Kristo, na kutomkana; na Kristo ndiye Mtakatifu wa Israeli; kwa hivyo lazima msujudu mbele yake, na mmwabudu kwa auwezo wenu wote, akili, na nguvu, na nafsi zenu zote; na mkifanya hivi, hamtatengwa kwa njia yoyote.

30 Na, kadiri itakavyohitajika, lazima utii matendo na amasharti ya Mungu hadi sheria aliyopewa Musa itakapotimizwa.