Maandiko Matakatifu
2 Nefi 9


Mlango wa 9

Yakobo anaelezea kwamba Wayahudi watakusanywa katika nchi zao zote za ahadi—Upatanisho ni ukombozi wa mwanadamu kutokana na Anguko—Miili ya wafu itafufuka kutoka kaburini, na roho zao zitatoka jehanamu na peponi—Watahukumiwa—Upatanisho unaokoa kutokana na kifo, jehanamu, ibilisi na mateso yasiyo na mwisho—Wenye haki wataokolewa katika ufalme wa Mungu—Adhabu ya dhambi yaelezwa—Yule Mtakatifu wa Israeli ni mlinzi wa mlango. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, nimesoma vitu hivi ili mfahamu kuhusu yale amaagano ya Bwana aliyoagana na nyumba yote ya Israeli—

2 Kwamba amezungumza kwa Wayahudi, kwa kinywa cha manabii wake watakatifu, hata tangu mwanzo hadi chini, kizazi kwa kizazi, mpaka wakati ufike awatakaporejeshwa kwa lile kanisa la kweli na zizi la Mungu; wakati bwatakapokusanywa nyumbani kwenye cnchi zao za urithi, na wataimarishwa katika nchi zao zote za ahadi.

3 Tazameni, ndugu zangu wapendwa, nawazungumzia vitu hivi ili kwamba mshangilie, na amuinue vichwa vyenu juu milele, kwa sababu ya baraka ambazo Bwana Mungu atawateremshia watoto wenu.

4 Kwani najua kwamba wengi wenu, mmetafuta sana, kujua vitu vijavyo; kwa hivyo najua kwamba mnajua kuwa amiili yetu lazima izeeke na kufa; walakini, katika miili yetu tutamuona Mungu.

5 Ndiyo, najua kwamba mnajua kwamba atajidhihirisha kimwili kwa wale walio Yerusalemu, kule tulikotoka; kwani ni lazima iwe miongoni mwao; kwani ilimpasa aMuumba mkuu akubali kuwa chini ya mwanadamu katika mwili, na afe kwa wanadamu bwote, ili wanadamu wote wawe chini yake.

6 Kwani kifo kimewapata wanadamu wote, ili kutimiza ampango wa huruma wa Muumba mkuu, inahitajika lazima pawe na nguvu ya bufufuo, na inahitajika lazima ufufuo umfikie mwanadamu kwa sababu ya cmwanguko; na mwanguko ulitokana na kosa; na kwa sababu mwanadamu alianguka dalitengwa kutokana na uwepo wa Bwana.

7 Kwa hivyo, unahitajika uwe aupatanisho busio na kipimo—bila huu upatanisho usio na kipimo huu uharibifu hauwezi kuvaa kutoharibika. Kwa hivyo, hukumu ya ckwanza iliyompata mwanadamu lazima dingekuwa kwa muda usio na mwisho. Na kama ni hivyo, miili hii lazima ingelala chini kuoza na kurudi mavumbini ilipotoka, bila kufufuka tena.

8 Ee ahekima ya Mungu, bhuruma zake na cneema! Kwani tazama, kama dmiili haifufuki tena roho zetu lazima ziwe chini ya yule malaika ealiyeanguka kutoka uwepo wa Mungu wa Milele, na akawa fibilisi, bila kufufuka tena.

9 Na roho zetu lazima zingekuwa kama yeye, na tuwe mashetani, amalaika kwa ibilisi, bkutengwa na uwepo wa Mungu wetu, na kuishi na baba wa cuwongo, katika huzuni, kama yeye mwenyewe; ndiyo, kwa kile kiumbe dkilichodanganya wazazi wetu wa kwanza, ambaye ehujigeuza kuwa fmalaika wa nuru, na huvuruga watoto wa watu kuwa na gmakundi maovu ya siri na ya mauaji na kila aina ya kazi za siri za giza.

10 Ee jinsi gani ulivyo mkuu wema wa Mungu wetu, anayetutayarishia njia ya kuepuka kunaswa na huyu mnyama mwovu; ndiyo, huyo mnyama, akifo na bjehanamu, ambayo naita kifo cha mwili, na pia kifo cha roho.

11 Na kwa sababu ya njia ya aukombozi wa Mungu wetu, Mtakatifu wa Israeli, hiki bkifo, ambacho nimetaja, ambacho ni cha muda, kitaachilia wafu wake; kifo ambacho ni kaburi.

12 Na akifo hiki ambacho nimetaja, ambacho ni kifo cha kiroho, kitaachilia wafu wake; kifo cha kiroho ambacho ni bjehanamu; kwa hivyo, kifo na jehanamu lazima ziachilie wafu wao, na jehanamu lazima iachilie roho zake zilizo utumwani, na kaburi lazima liachilie miili yake iliyo utumwani, na miili na croho za wanadamu ditaunganishwa tena; na ni kwa nguvu za ufufuo za yule Mtakatifu wa Israeli.

13 Ee jinsi gani ulivyo mkuu ampango wa Mungu wetu! Kwani katika njia nyingine, bpeponi ya Mungu lazima iachilie roho za walio haki, na kaburi iachilie miili ya walio haki; na roho na mwili ckuunganishwa tena, na wanadamu wote wawe dwasioharibika, na wasiokufa, na wao ni nafsi zinazoishi, wakiwa na eufahamu fkamili kama sisi tulio na miili, ila tu ufahamu wetu utakuwa kamili.

14 Kwa hivyo, tutakuwa na aufahamu kamili wa bhatia zetu, na uchafu wetu, na cuchi wetu; na walio haki watakuwa na ufahamu kamili wa furaha yao, na dhaki yao, wakiwa ewamevishwa fusafi, ndiyo, hata kwa gjoho la haki.

15 Na itakuwa kwamba baada ya wanadamu wote kupita mauti haya ya kwanza na kupata uzima, jinsi vile wamekuwa wasiokufa, lazima watasimama mbele ya kiti cha ahukumu cha yule Mtakatifu wa Israeli; na kisha bhukumu itafika, na kisha lazima wahukumiwe kulingana na hukumu takatifu ya Mungu.

16 Na kwa hakika, kama Bwana anavyoishi, kwani Bwana Mungu amelizungumza, na ni aneno lake la milele, ambalo halikosi bkutimizwa, kwamba wale walio haki bado watakuwa haki, na wale walio cwaovu bado watakuwa dwaovu; kwa hivyo, wale ambao ni waovu ni eibilisi na malaika wake; na watatupwa kwenye moto usio na fmwisho, waliotayarishiwa; na mateso yao ni kama gziwa la moto na kiberiti ambacho ndimi zake zinapanda juu milele na daima bila mwisho.

17 Ee jinsi gani ilivyo kuu ahaki ya Mungu wetu! Kwani anatimiza maneno yake yote, na yametoka kinywani mwake, na sheria yake lazima itimizwe.

18 Lakini, tazama, awatakatifu, wale wateule wa yule Mtakatifu wa Israeli, wale ambao wamemwamini yule Mtakatifu wa Israeli, wale ambao wamevumilia bmisalaba ya ulimwengu, na kudharau aibu yake, cwatarithi dufalme wa Mungu, ambao walitayarishiwa etangu mwanzo wa dunia, na shangwe yao itakuwa tele fmilele.

19 Ee jinsi gani ilivyo kuu rehema ya Mungu wetu, yule Mtakatifu wa Israeli! Kwani ahuwakomboa watakatifu wake kutokana na yule mnyama bmwovu yaani ibilisi, na kifo, na cjehanamu, na lile ziwa la moto na kiberiti, ambalo ni mateso yasiyo na mwisho.

20 Ee jinsi gani ulivyo mkuu autakatifu wa Mungu wetu! Kwani banafahamu vitu vyote, na hakuna jambo lolote asilolijua.

21 Na anakuja ulimwenguni ili aawaokoe wanadamu wote kama watakubali sauti yake; kwani tazama, anapokea bmaumivu ya wanadamu wote, ndiyo, maumivu ya kila kiumbe kinachoishi, waume kwa wake, na watoto, ambao ni wa jamii ya cAdamu.

22 Na anakubali haya ili ufufuo uwafikie wanadamu wote, ili wote wasimame mbele yake katika siku ile kuu ya hukumu.

23 Na anawaamuru wanadamu wote kwamba lazima awatubu, na bwabatizwe katika jina lake, wakiwa na imani kamili katika yule Mtakatifu wa Israeli, au kama sivyo hawawezi kuokolewa katika ufalme wa Mungu.

24 Na kama hawatatubu na kuamini katika ajina lake, na kubatizwa kwa jina lake, na bkuvumilia hadi mwisho, lazima wapate claana ya milele; kwani Bwana Mungu, yule Mtakatifu wa Israeli, amezungumza.

25 Kwa hivyo, ametoa asheria; na ambapo bhakuna sheria imetolewa hakuna adhabu; na pasipo adhabu hakuna hukumu; na pasipo hukumu rehema za yule Mtakatifu wa Israeli zinawadai, kwa sababu ya upatanisho; kwani wanakombolewa kwa nguvu zake.

26 Kwani aupatanisho unatimiza madai yake ya bhaki kwa wale ambao chawakupatiwa dsheria, kwamba wanakombolewa kutokana na yule mnyama mwovu, kifo na jehanamu, na yule ibilisi, na ziwa la moto na kiberiti, ambalo ni mateso bila mwisho; na wanarejeshwa kwa yule Mungu aliyewapatia epumzi, ambaye ni yule Mtakatifu wa Israeli.

27 Lakini ole kwa yule ambaye alipewa asheria, ndiyo, aliye na sheria zote za Mungu, kama sisi, na huzivunja, na yule anayepoteza siku za majaribio yake, kwani hali yake ni mbovu!

28 Ee ule ampango wa ujanja wa yule mwovu! Ee butupu, na ugoigoi, na upumbavu wa wanadamu! cWanapoelimika wanadhani kwamba wana dhekima, na hawasikii emawaidha ya Mungu, kwani wanaiweka kando, wakifikiria kwamba wanajua wenyewe, kwa hivyo, hekima yao ni ujinga na haiwafaidi. Na wataangamia.

29 Lakini kuelimika ni vyema ikiwa awatatii bmawaidha ya Mungu.

30 Lakini ole kwa amatajiri, ambao ni matajiri kwa vitu vya ulimwengu. Kwani kwa sababu wao ni matajiri wanachukia walio bmasikini, na wanawatesa wale wapole, na mioyo yao iko kwenye hazina yao; kwa hivyo, hazina yao ni mungu wao. Na tazama, hazina yao itaangamia nao pia.

31 Na ole kwa viziwi wale awasiosikia; kwani wataangamia.

32 Ole pia kwa wale walio vipofu wasioona; kwani nao pia wataangamia.

33 Ole kwa wale wasiotairiwa moyoni, kwani ufahamu wa maovu yao utawasonga katika siku ya mwisho.

34 Ole kwa aliye amdanganyifu, kwani atatupwa bjehanamu.

35 Ole kwa muuaji aanayeua akitaka, kwani batakufa.

36 Ole kwa wale wanaotenda aukahaba, kwani watatupwa jehanamu.

37 Ndiyo, ole kwa wale awanaoabudu masanamu, kwani ibilisi wa ibilisi wote huwafurahia.

38 Na, mwishowe, ole kwa wale wote wanaokufa katika dhambi zao; kwani awatamrejea Mungu, na kuona uso wake, na kubaki katika dhambi zao.

39 Ee, ndugu zangu wapendwa, kumbukeni uovu wa kumkosea yule Mungu Mtakatifu, na pia uovu wa kukubali ushawishaji wa yule amwovu. Kumbukeni, kufikiria bkimwili ni ckifo, na kufikiria kiroho ni duzima wa emilele.

40 Ee, ndugu zangu wapendwa, sikilizeni maneno yangu. Kumbukeni ukuu wa yule Mtakatifu wa Israeli. Msiseme kwamba nimezungumza vitu vigumu dhidi yenu; kwani mkifanya hivyo, mtaasi kinyume cha aukweli; kwani nimenena maneno ya Muumba wenu. Najua kwamba maneno ya kweli ni bmakali kwa uchafu wote; lakini walio haki hawayaogopi, kwani wanapenda ukweli na hawatingishwi.

41 Kisha, Ee ndugu zangu wapendwa, anjooni kwa Bwana, yule Mtakatifu. Kumbuka kwamba mapito yake ni matakatifu. Tazama, bnjia ya mwanadamu ni cnyembamba, lakini imenyooka mbele yake, na dmlinzi wa mlango ni yule Mtakatifu wa Israeli; na haajiri mtumishi yeyote pale; na hakuna njia nyingine yoyote isipokuwa kwa mlango; kwani hawezi kudanganywa, kwani Bwana Mungu ndilo jina lake.

42 Na kwa yeyote anayebisha, kwake yeye atamfungulia; na kwa wenye ahekima, na walioelimika, na wale walio matajiri, ambao bwanajidai kwa sababu ya elimu yao, na hekima yao, na utajiri wao—ndiyo, hao ndiyo anaochukia; na wasipoacha vitu hivi, na wajichukue kama cwajinga mbele ya Mungu, na dkunyenyekea, hatawafungulia.

43 Lakini vitu vya wenye hekima na walio werevu avitafichwa kwao milele—ndiyo, furaha ile iliyotayarishiwa watakatifu.

44 Ee, ndugu zangu wapendwa, kumbukeni maneno yangu. Tazama, navua mavazi yangu, na kuzisukasuka mbele yenu; Naomba kwamba Mungu wa wokovu wangu anitazame na jicho lake linaloona akila mahali; kwa hivyo, mtajua katika siku ile ya mwisho, wakati wanadamu wote watakapo hukumiwa kulingana na kazi zao, kwamba Mungu wa Israeli alishuhudia kwamba bnilijitoa mzigo wa maovu yenu kutoka nafsi yangu, na kwamba nasimama kwa usafi mbele yake, na kwamba damu yenu chaiko juu yangu.

45 Ee, ndugu zangu wapendwa, acheni dhambi zenu; jifungueni aminyororo ya yule atakayewafunga; njooni kwa yule Mungu aliye bmwamba wa wokovu wenu.

46 Tayarisheni nafsi zenu kwa siku ile ya autukufu ambapo wale walio watakatifu watahudumiwa kwa haki, hata siku ile ya bhukumu, kwamba msitetemeke kwa woga; na kwamba msikumbuke chatia yenu ya uovu katika ukamilifu, na mlazimishwe kulia: Takatifu, takatifu ni hukumu zako, Ee Bwana Mungu dMwenyezi—lakini najua hatia yangu; nilivunja sheria yako, na makosa yangu ni yangu; na ibilisi amenipata, na kwamba mimi ni mawindo kwa huzuni yake mbovu.

47 Lakini tazameni, ndugu zangu, je, ni lazima niwafahamishe huu ukweli wa kutisha wa vitu hivi? Je, ningesumbua nafsi zenu kama mawazo yenu yangekuwa mema? Ningekuwa wazi kwenu kulingana na udhahiri wa kweli kama mngepata uhuru wa dhambi?

48 Tazama, kama mngekuwa watakatifu ningewazungumzia kuhusu utakatifu; lakini kwa vile ninyi sio watakatifu, na mnanitegemea mimi kama mwalimu, lazima aniwafundishe kuhusu matokeo ya bdhambi.

49 Tazama, nafsi yangu inachukia dhambi, na moyo wangu unafurahishwa na haki; na anitalisifu jina takatifu la Mungu wangu.

50 Njooni, ndugu zangu, kila mmoja aliye na kiu, njooni kwenye amaji; na yule asiye na pesa, njoo ununue na ule; ndiyo, njooni mnunue mvinyo na maziwa bila bpesa na bei.

51 Kwa hivyo, msitumie pesa zenu kwa yale yasiyo na thamani, wala anguvu zenu kwa yale yasiyotosheleza. Mnisikilize kwa makini, na mkumbuke yale maneno ambayo nimezungumza; na mje kwa yule Mtakatifu wa Israeli, na bmle yale yasiyoangamia, wala kuharibiwa, na mruhusu nafsi zenu zifurahie unono.

52 Tazameni, ndugu zangu wapendwa, kumbukeni maneno ya Mungu wenu; muombeni bila kukoma kwa mchana, na amshukuru jina lake takatifu kwa usiku. Acheni mioyo yenu ishangilie.

53 Na tazameni jinsi gani yalivyo makuu amaagano ya Bwana, na jinsi gani ulivyo mkuu ufadhili wake kwa watoto wa watu; na kwa sababu ya ukuu wake, na neema yake na brehema, ametuahidi kwamba uzao wetu hautaangamizwa kabisa, kimwili, lakini kwamba atawahifadhi; na katika vizazi vya baadaye watakuwa ctawi takatifu kwa nyumba ya Israeli.

54 Na sasa, ndugu zangu, ningewazungumzia zaidi; lakini kesho nitawaelezea maneno yangu yaliyosalia. Amina.