Maandiko Matakatifu
3 Nefi 11


Yesu Kristo alijidhihirisha kwa watu wa Nefi, wakati umati ulipokuwa umejikusanya pamoja katika nchi ya Neema, na akawahubiria; na hivi ndivyo alivyojidhihirisha kwao.

Kuanzia mlango wa 11.

Mlango wa 11

Baba anashuhudia kuhusu Mwana Wake Mpendwa—Kristo anatokea na kutangaza Upatanisho Wake—Watu wanapapasa alama za vidonda katika mikono na miguu na ubavu Wake—Wanapiga yowe Hosana—Anaanzisha utaratibu na namna ya ubatizo—Roho ya ubishi ni ya ibilisi—Mafundisho ya Kristo ni kwamba watu wanapaswa kuamini na wabatizwe na wapokee Roho Mtakatifu. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Na sasa ikawa kwamba kulikuwa na umati mkubwa uliokusanyika pamoja, wa watu wa Nefi, karibu na hekalu ambalo lilikuwa katika nchi ya Neema; na walistaajabu na kushangaa mmoja na mwingine, na walionyeshana mabadiliko amakubwa na ya ajabu ambayo yalikuwa yamefanyika.

2 Na walikuwa wanamzungumzia huyu Yesu Kristo, ambaye aishara zilikuwa zimetolewa kuhusu kifo chake.

3 Na ikawa kwamba wakati walipokuwa huko wakizungumza mmoja na mwingine, walisikia asauti kama iliyotokea mbinguni; na wakaelekeza macho yao kila upande, kwani hawakutambua hiyo sauti ambayo walisikia; na haikuwa sauti kali, wala ya makelele; walakini, na ingawa ilikuwa sauti bndogo tulivu, iliwapenya wale walioisikia hadi moyoni, mpaka kwamba hapakuweko na sehemu ya miili yao ambayo haikutetemeka; ndiyo, iliwatoboa mpaka kwenye roho yenyewe, na ikasababisha mioyo yao kuchomeka.

4 Na ikawa tena kwamba walisikia ile sauti, na hawakuitambua.

5 Na tena mara ya tatu wakasikia hiyo sauti, na wakafungua masikio yao kuisikiliza; na macho yao yakaelekea kule kulikotokea sauti; na walitazama kwa uthabiti kuelekea mbinguni, kule ambako sauti ilitokea.

6 Na tazama, mara ya tatu walielewa ile sauti ambayo walisikia; na ikawaambia:

7 Tazama aMwana wangu Mpendwa ninayependezwa bna yeye, ambaye ndani yake nimetukuza jina langu—msikilizeni yeye.

8 Na ikawa walipofahamu, walielekeza macho yao tena mbinguni; na tazama, awalimwona mtu akiteremka kutoka mbinguni, na alikuwa amevaa joho refu leupe; na akaja chini na kusimama katikati yao; na macho ya umati wote yaligeuka kumwangalia, na hawakufungua vinywa vyao, hata mmoja kwa mwingine, na hawakujua kilichomaanishwa, kwani walidhani ni malaika ambaye alionekana kwao.

9 Na ikawa kwamba alinyosha mkono wake mbele na kuzungumza kwa watu akisema:

10 Tazama, Mimi ni Yesu Kristo ambaye manabii walishuhudia atakuja ndani ya ulimwengu.

11 Na tazama mimi ni anuru na uzima wa ulimwengu; na nimekunywa kutoka kwa bkikombe kichungu ambacho Baba amenipatia, na nimemtukuza Bwana kwa ckujivika dhambi za ulimwengu ambamo ndani yake nimevumilia dmapenzi ya Baba katika vitu vyote kutoka mwanzo.

12 Na ikawa kwamba wakati Yesu alipokuwa amesema maneno haya, umati wote uliinama kwenye ardhi; kwani walikumbuka kwamba ilikuwa aimetabiriwa miongoni mwao kwamba Kristo atajidhihirisha kwao baada ya kupaa kwake mbinguni.

13 Na ikawa kwamba Bwana aliwazungumzia akisema:

14 Inukeni na mje kwangu, ili msukume mikono yenu na amuitie kwenye ubavu wangu, na pia kwamba mguse balama za misumari katika mikono yangu na katika miguu yangu, ili mjue mimi ni Mungu wa Israeli, na cMungu wa dulimwengu wote, na nimeuawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.

15 Na ikawa kwamba umati ulienda mbele, na kusukuma mikono yao ubavuni mwake, na wakaona alama za misumari katika mikono yake na katika miguu yake; na hivi walifanya wakienda mbele mmoja mmoja, mpaka walipoenda wote, na waliona na macho yao na kupapasa kwa mikono yao, na walijua ukweli na walishuhudia wenyewe kwamba ani yeye, ambaye manabii waliandika kwamba atakuja.

16 Na wakati walipokuwa wameenda wote na kujishuhudia wenyewe, walipaza sauti kwa toleo moja wakisema:

17 Hosana! Heri liwe jina la Mungu Aliye Juu Sana! Na waliinama chini miguuni mwa Yesu na akumwabudu.

18 Na ikawa kwamba alimzungumzia aNefi (kwani Nefi alikuwa miongoni mwa umati) na kumwamuru kwamba aje mbele.

19 Na Nefi akainuka na kwenda mbele na kusujudu mbele ya Bwana na kubusu miguu yake.

20 Na Bwana alimwamrisha kwamba ainuke. Na aliinuka na kusimama mbele yake.

21 Na Bwana akamwambia: Ninakupatia auwezo kwamba butabatiza hawa watu nikiwa nimeenda tena mbinguni.

22 Na tena Bwana aliita awengine, na akawaambia vile vile; na akawapatia uwezo wa kubatiza. Na akawaambia: Kwa njia hii mtabatiza; na bhakutakuwa na ugomvi miongoni mwenu.

23 Kweli nawaambia, kwamba yeyote atakayetubu dhambi zake kupitia amaneno yenu, na bkutaka kubatizwa katika jina langu, kwa njia hii mtawabatiza—Tazama, mtaenda chini na ckusimama majini, na katika jina langu mtawabatiza.

24 Na sasa tazama, haya ndiyo maneno ambayo mtasema, mkiwaita kwa jina, mkisema:

25 Nikiwa nimepewa amamlaka na Yesu Kristo, ninakubatiza wewe katika jina la bBaba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

26 Na hapo amtawatumbukiza katika maji, na kutoka tena nje ya maji.

27 Na kwa kufuata njia hii, mtabatiza katika jina langu; kwani tazama, kweli nawaambia kwamba, Baba, na Mwana wake, na Roho Mtakatifu wana aumoja; na niko ndani ya Baba, na Baba ndani yangu, na Baba na mimi tuna umoja.

28 Na kulingana na vile nimemwamuru hivyo ndivyo mtabatiza. Na hakutakuwa na augomvi miongoni mwenu, kama vile ilivyo hapa sasa; wala hakutakuwa na ugomvi miongoni mwenu kuhusu nukta za mafundisho yangu, kama vile ilivyokuwa.

29 Kwani amin, amin, nawaambia, yule ambaye ana aroho ya bubishi siye wangu, bali ni wa ibilisi, ambaye ni baba wa ubishi, na huchochea mioyo ya watu kubishana kwa hasira wao kwa wao.

30 Tazama, hili sio fundisho langu, kuchochea mioyo ya wanadamu kwa hasira, moja dhidi ya mwingine; lakini hili ndilo fundisho langu, kwamba vitu kama hivi viondolewe mbali.

31 Tazama, amin, amin, ninawaambia, nitatangaza kwenu amafundisho yangu.

32 Na haya ni amafundisho yangu, na ni mafundisho ambayo Baba amenipatia; na bninashuhudia mwenyewe kwa Baba, na Baba anashuhudia mwenyewe kwangu, na cRoho Mtakatifu anashuhudia kwa Baba na kwa Mimi, na ninashuhudia kwamba Baba huamuru watu wote, kila mahali, kutubu na kuniamini.

33 Na yeyote aaminiye ndani yangu na akubatizwa, bataokolewa; na hawa ndiyo cwatakaorithi ufalme wa Mungu.

34 Na yeyote asiyeamini ndani yangu na hajabatizwa, atahukumiwa.

35 Amin, amin, nawaambia, kwamba, hili ni fundisho langu, na ninashuhudia kutoka kwa Baba; na yeyote aanayeamini ndani yangu anaamini kwa Baba pia, na kwake Baba atanishuhudia, kwani atamtembelea bna moto na cRoho Mtakatifu.

36 Na hivyo ndivyo Baba atakavyoshuhudia kunihusu, na Roho Mtakatifu atashuhudia kwake Baba na Mimi, kwani Baba na Mimi na Roho Mtakatifu tu wamoja.

37 Na tena nawaambia, lazima mtubu na amuwe kama mtoto mdogo, na mbatizwe kwa jina langu, au hamtapokea vitu hivi kwa njia yoyote.

38 Na tena nawaambia, lazima mtubu na mbatizwe katika jina langu na muwe kama mtoto mchanga au hamtarithi ufalme wa Mungu kwa vyovyote.

39 Amin, amin, nawaambia, kwamba haya ni mafundisho yangu, na yeyote aatakayejenga juu ya mwamba wangu, na bmilango ya jehanamu haitamshinda.

40 Na yeyote atakayetangaza mengi au madogo kuliko haya, na kuyaimarisha kuwa mafundisho yangu, yeye anatokana na uovu, na hajajenga kwenye mwamba wangu; lakini hujenga kwenye msingi wa amchanga, na milango ya jehanamu husimama kupokea mtu kama huyu wakati mafuriko yakija na upepo hujipigisha juu yake.

41 Kwa hivyo muwaendee watu hawa, na mtangaze yale maneno ambayo nimezungumza, hadi mwisho wa dunia.