Kitabu cha Alma Mwana wa Alma

Mlango wa 32

Alma anawafundisha walio masikini ambao mateso yao yamewanyenyekeza—Imani ni tumaini kwa lile ambalo halionekani ambalo ni kweli—Alma anatoa ushuhuda kwamba malaika huwahudumia wanaume, wanawake, na watoto—Alma analinganisha neno na mbegu—Lazima ipandwe na kulishwa—Ndipo inakua kuwa mti ambao kutoka kwake matunda ya uzima wa milele huvunwa. Karibu mwaka wa 74 kabla ya kuzaliwa Kristo.

1 Na ikawa kwamba waliendelea mbele, na kuanza kuhubiri neno la Mungu kwa watu, wakiingia kwenye masinagogi yao, na kwenye nyumba zao; ndio, na hata walihubiri neno kwenye mitaa yao.

2 Na ikawa kwamba baada ya kazi nyingi miongoni mwao, wakaanza kuwa na mafanikio miongoni mwa watu wa vyeo vya achini; kwani tazama, walitupwa nje ya masinagogi kwa sababu ya nguo zao hafifu—

3 Kwa hivyo hawakuruhusiwa kuingia katika masinagogi yao kumwabudu Mungu, wakichukuliwa kama uchafu; kwa hivyo walikuwa masikini; ndio, walichukuliwa na ndugu zao kama takataka; kwa hivyo walikuwa amasikini kulingana na vitu vya ulimwengu; na pia walikuwa masikini katika mioyo yao.

4 Sasa, Alma alipokuwa akifundisha na kuwazungumzia watu kwenye mlima Onida, kulitokea kikundi kikubwa kwake, cha wale ambao tulikuwa tukizungumza juu yao, ambao walikuwa amasikini moyoni, kwa sababu ya umasikini wao kulingana na vitu vya ulimwengu.

5 Na wakamjia Alma; na yule ambaye alikuwa anawaongoza akamwambia: Tazama, ni anini hawa ndugu zangu watafanya, kwani wanadharauliwa na watu wote kwa sababu ya umasikini wao, ndio, hata nasa na makuhani wetu; kwani bwametutupa nje ya masinagogi ambayo tuliyafanyia kazi kwa wingi kujenga kwa mikono yetu; na wametutupa nje kwa sababu ya umasikini wetu mkuu; na hatuna mahali pa kumuabudia Mungu wetu; na tazama, tutafanya cnini?

6 Na sasa Alma aliposikia haya, alipindua uso wake mara moja, na kumwangalia, kwa shangwe kubwa; kwani aliona kwamba amateso yao yalikuwa yamewafanya kwa kweli kuwa bwanyenyekevu, na kwamba walikuwa cwamejiandaa kusikiliza neno.

7 Kwa hivyo hakusema mengi kwa huo umati mwingine; lakini alinyoosha mbele mkono wake, na kupaza sauti kwa wale ambao aliwaona, ambao walikuwa kwa kweli wametubu, na akawaambia;

8 Ninaona kwamba ammenyenyekea moyoni; na ikiwa ni hivyo, heri kwenu.

9 Tazama ndugu yenu alisema, Tutafanya nini?—kwani tumetupwa nje ya masinagogi yetu, kwamba hatuwezi kumuabudu Mungu wetu.

10 Tazama ninawaambia, mnafikiri kwamba hamwezi akumuabudu Mungu isipokuwa kwenye masinagogi yenu pekee?

11 Na zaidi ya hayo, ningewauliza, mnafikiri kwamba lazima mmuabudu Mungu tu siku moja kwenye juma?

12 Nawaambia, ni vyema kwamba mmetupwa nje ya masinagogi yenu, ili muwe wanyenyekevu, na ili mjifunze ahekima; kwani ni lazima mjifunze hekima; kwani ni kwa sababu mmetupwa nje, kwamba mmedharauliwa na ndugu zenu kwa sababu ya bumasikini wenu mkuu, kwamba mioyo yenu imenyenyekea; kwani mnyenyekezwa kwa lazima.

13 Na sasa, kwa sababu mmelazimishwa kunyenyekea heri nyinyi; kwani mtu wakati mwingine, akilazimishwa kunyenyekea, hutafuta toba; na sasa kwa kweli, yeyote anayetubu atapata huruma; na yule ambaye anapata huruma na akuvumilia hadi mwisho huyo ataokolewa.

14 Na sasa, vile nilivyowaambia nyinyi, kwamba kwa sababu mlilazimishwa kunyenyekea mlibarikiwa, hamdhani kwamba wale ambao wanajinyenyekeza kwa ukweli wenyewe kwa sababu ya neno wamebarikiwa zaidi?

15 Ndio, yule ambaye anajinyenyekeza mwenyewe kwa ukweli, na kutubu dhambi zake, na kuvumilia hadi mwisho, huyo atabarikiwa—ndio, atabarikiwa zaidi ya wale ambao hulazimishwa kunyenyekea kwa sababu ya umasikini wao mwingi.

16 Kwa hivyo, heri wale ambao ahunyenyekea wenyewe bila kulazimishwa kunyenyekea; kwa usahihi zaidi, heri yule ambaye anaamini katika neno la Mungu, na anabatizwa bila ukaidi wa moyo, ndio, bila kushurutishwa kujua neno, au hata kulazimishwa kujua, kabla ya kuamini.

17 Ndio, kuna wengi ambao husema: ikiwa utatuonyesha aishara kutoka mbinguni, ndipo tutajua kwa hakika; halafu tutaamini.

18 Sasa ninauliza; hii ni imani? Tazama, nawaambia, Hapana; kwani ikiwa mtu anajua kitu hana sababu ya akuamini, kwani anakijua.

19 Na sasa, hulaaniwaje zaidi ya yule ambaye aanajua mapenzi ya Mungu na hayatimizi, kuliko yule ambaye huamini tu, au ana sababu ya kuamini, na kuanguka kwenye makosa?

20 Sasa, kwa kitu hiki lazima mhukumu. Tazama, nawaambia, kwamba ni sawa mkono mmoja hata vile ilivyo kwa mwingine; na itakuwa hivyo kwa kila mtu kulingana na vitendo vyake.

21 Na sasa nilivyosema kuhusu imani—aimani sio kuwa na ufahamu kamili wa vitu; kwa hivyo mkiwa na imani, bmnatumainia vitu ambavyo chavionekani, ambavyo ni vya kweli.

22 Na sasa, tazama, ninawaambia, na ningetaka kwamba mkumbuke, kwamba Mungu ni mwenye hekima kwa wote wanaoamini katika jina lake; kwa hivyo, anataka kwa mara ya kwanza, kwamba mwamini, ndio, hata katika neno lake.

23 Na sasa, yeye huwatolea wanadamu neno lake kwa malaika, ndio, asio tu kwa wanaume peke yao lakini pia kwa wanawake. Sasa hii si yote; bwatoto wadogo huwa na maneno wanayopewa mara nyingi, ambayo yanawafadhaisha werevu na wasomi.

24 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, kwa vile mnatamani kujua kutoka kwangu mtafanya nini kwa sababu mnasumbuliwa na kutupwa nje—sasa sitaki mfikirie kwamba ninamaanisha kutoa hukumu kwenu isipokuwa kulingana na yale ambayo ni kweli—

25 Kwani simaanishi kwamba nyinyi nyote mmelazimishwa kujinyenyekeza; kwani ninaamini kwa ukweli kwamba kuna wengine kati yenu ambao wangenyenyekea wenyewe, hata wawe kwa hali gani.

26 Sasa, vile nilivyosema kuhusu imani—kwamba haikuwa ufahamu kamili—hata hivyo ni kama maneno yangu. Hamwezi kujua ukweli wao kwanza, kwa ukamilifu, vile imani si ufahamu kamili.

27 Lakini tazama, ikiwa mtaamka na kuziwasha akili zenu, hata kwenye kujaribu juu ya maneno yangu na kutumia sehemu ya imani, ndio, hata ikiwa hamwezi ila akutamani kuamini, acha hamu hii ifanye kazi ndani yenu, hata mpaka mwamini kwa njia ambayo mtatoa nafasi kwa sehemu ya maneno yangu.

28 Sasa, tutalinganisha neno kwa ambegu. Sasa ikiwa mtatoa nafasi, ili bmbegu ipandwe ndani ya cmoyo wako, tazama, ikiwa itakuwa mbegu ya kweli, au mbegu nzuri, ikiwa hamtaitupa nje kwa dkutoamini kwenu, kwamba mtashindana na Roho ya Bwana, tazama, itaanza kuvimba ndani ya vifua vyenu; na wakati mtakaposikia huu mwendo wa kuvimba, mtaanza kusema ndani yenu—inawezekana kwamba hii ni mbegu nzuri, au kwamba neno ni nzuri, kwani linaanza kukua ndani ya nafsi yangu; ndio, inaanza kuangaza ekuelewa kwangu, ndio, inaanza kunipendeza mimi.

29 Sasa tazama, si hii itaongeza imani yenu? Ninawaambia, Ndio; walakini haijakua kwa ufahamu kamili.

30 Lakini tazama, vile mbegu inavyovimba, na kumea, na kuanza kukua, ndipo mtasema kwamba mbegu ni nzuri; kwani tazama inavimba, na kumea, na kuanza kukua. Na sasa, tazama, si hii itaimarisha imani yenu? Ndio, itaimarishaa imani yenu: kwani mtasema tunajua kwamba hii ni mbegu nzuri; kwani tazama inachipuka na inaanza kukua.

31 Na sasa, tazama, mna hakika kwamba hii ni mbegu nzuri? Nawaambia, Ndio; kwani kila mbegu huzaa amfano wake.

32 Kwa hivyo kama mbegu inakua ni nzuri, lakini kama haikui, tazama si nzuri, kwa hivyo hutupiliwa mbali.

33 Na sasa, tazama, kwa sababu mmejaribu utafiti, na kupanda mbegu, na inavimba na kumea, na kuanza kukua, lazima mjue kwamba mbegu ni nzuri.

34 Na sasa, tazama, ufahamu wenu ni kamili? Ndio, aufahamu wenu ni kamili kwa kile kitu, na bimani yenu inalala; na hii kwa sababu mnajua, kwani mnajua kwamba neno limevimbisha nafsi zenu, na pia mnajua kwamba limemea, kwamba ufahamu wenu umeanza kuelimika, na cakili zenu zinaanza kupanuka.

35 Ee basi, si hii ni kweli? Nawaambia, Ndio, kwa sababu ni anuru; na chochote ambacho ni nuru, ni kizuri, kwa sababu kinaonekana, kwa hivyo lazima mjue kwamba ni nzuri; na sasa tazama, baada ya nyinyi kuonja nuru hii si ufahamu wenu ni kamili?

36 Tazama nawaambia, Hapana; wala msiweke kando imani yenu, kwani mmejaribu tu imani yenu kupanda mbegu kwamba mngejaribu utafiti kujua kama mbegu ilikuwa nzuri.

37 Na tazama, mti ukianza kukua, mtasema: Acha tuulishe kwa uangalifu mkuu, kwamba uweze kupata mizizi, kwamba upate kukua, na kututolea matunda. Na sasa tazama, ikiwa mtaulisha kwa uangalifu mwingi mtapata mizizi, na kukua, na kuleta matunda.

38 Lakini amkiuachilia mti ule, na msifikirie kuulisha, tazama hautapata mzizi wowote; na wakati joto la jua linawadia na kuuchoma, kwa sababu hauna mzizi hukaukia mbali, na mtaukata na kuutupa nje.

39 Sasa, hii sio kwa sababu mbegu haikuwa nzuri, wala sio kwa sababu tunda lake halingekuwa la kutamanika; lakini ni kwa sababu amchanga wenu ni kame, na hamwezi kuulisha mti, kwa hivyo hamwezi kupata tunda juu yake.

40 Na hivyo, ikiwa hamtalisha neno, mkingojea tu kwa imani kupata tunda juu yake, hamwezi mkachuna tunda la amti wa maisha.

41 Lakini ikiwa mtalisha neno, ndio, lisha mti unapoanza kukua, kwa imani yenu kwa bidii kuu, na auvumilivu, mkitumainia kupata tunda kwake, utamea mizizi; na tazama utakuwa mti butakaokua na kuzaa matunda yasiyo na mwisho.

42 Na kwa sababu ya abidii yenu na imani yenu na uvumilivu wenu kwa neno kwa kulilisha, kwamba limee ndani yenu, tazama, baadaye mtavuna bmatunda kwake, ambayo ni ya thamani sana, ambayo ni tamu kupita kiasi; na ambayo ni meupe kupita kiasi, ndio, na safi kupita kiasi; na mtakula hili tunda mpaka hata mshibe, kwamba hamtapata njaa, wala kuona kiu.

43 Kisha, ndungu zangu, mtavuna zawadi ya imani yenu, na bidii yenu, na subira, na uvumilivu, mkingojea mti kuwatolea matunda.