Maandiko Matakatifu
Alma 41


Mlango wa 41

Katika ufufuko wanadamu huamka katika hali ya furaha isiyo na mwisho au huzuni isiyo na mwisho—Uovu haujawahi kuwa furaha—Watu wa tamaa za kimwili hawana Mungu ulimwenguni—Kila mtu hupokea tena kwenye Ufufuko tabia na sifa alizozichuma wakati akiwa duniani. Karibia mwaka 74 K.K.

1 Na sasa, mwana wangu, nina machache ya kusema kuhusu ufufuko ambao umezungumziwa; kwani tazama, wengine awamegeuza maandiko, na bwamepotelea mbali kwa sababu ya kitu hiki. Na ninaona kwamba akili yako imekuwa na wasiwasi kuhusu kitu hiki. Lakini tazama, nitakuelezea.

2 Ninakwambia, mwana wangu, kwamba mpango wa ufufuo ni wa lazima na haki ya Mungu; kwani ni lazima kwamba vitu vyote virudishwe kwenye kanuni zao. Tazama, ni lazima na haki, kulingana na uwezo wa kufufuka kwa Kristo, kwamba roho ya kila mtu irudishwe kwa mwili wake, na kila asehemu ya mwili sharti irudishwe vile ilivyokuwa.

3 Na ni lazima na ahaki ya Mungu kwamba binadamu bwahukumiwe kulingana na cvitendo vyao; na ikiwa vitendo vyao vilikuwa vizuri kwenye maisha haya, na nia za mioyo yao zilikuwa nzuri, ndipo pia itakuwa kwa siku ya mwisho, ditarudishwa kwa ile ambayo ni nzuri.

4 Na ikiwa vitendo vyao ni viovu awatarudishiwa uovu. Kwa hivyo, vitu vyote vitarudishwa kwa kanuni zao, kila kitu kwa asili ya umbo lake—bmwili wenye kufa utafufuliwa katika kutokufa, cvilivyoharibika kwa visivyo haribika—vikiinuliwa kwenye furaha disiyo na mwisho kurithi ufalme wa Mungu, au taabu isiyo ya mwisho kurithi ufalme wa ibilisi, moja kwa upande mmoja, na mwingine kwa upande mwingine—

5 Mmoja ameinuliwa kwenye furaha kulingana na nia yake ya furaha, au uzuri kulingana na mahitaji yake ya uzuri; na mwingine kwenye ubaya kulingana na nia yake ya ubaya; kwani kwa vile ametamani kutenda maovu siku yote hata hivyo atapata zawadi yake ya uovu wakati usiku utakapoingia.

6 Na hivyo iko kwenye upande mwingine. Ikiwa ametubu dhambi zake, na kuhitaji haki mpaka mwisho wa siku zake, hata hivyo atapata zawadi kwa haki.

7 aHawa ni watu ambao wamekombolewa na Bwana; ndiyo, hawa ndiyo wao ambao wametolewa nje, ambao wameokolewa kutoka kwa ule usiku wa giza la milele; na hivyo wanasimama au kuanguka; kwani tazama, wanajihukumu bwenyewe, kama watafanya mazuri au maovu.

8 Sasa, maagizo ya Mungu ahayabadiliki; kwa hivyo, njia imeandaliwa kwamba yeyote atakaye angetembea juu yake na kuokolewa.

9 Na sasa tazama, mwana wangu, usijihatarishe na kosa lingine amoja zaidi dhidi ya Mungu juu ya yale mambo ya mafundisho, ambayo wewe umejihatarisha sasa kwa kutenda dhambi.

10 Usidhani, kwa sababu imezungumzwa kuhusu ufufuo, kwamba utarudishwa kutoka kwenye dhambi hadi kwenye furaha. Tazama, nakwambia, auovu haujapata kuwa furaha.

11 Na sasa, mwana wangu, watu wote ambao wako kwa hali ya aasili, au ningesema, kwenye hali ya bkimwili, wako kwenye masumbuko ya uchungu na kwenye kifungo cha uovu; chawako na Mungu duniani, na wameenda kinyume cha asili ya Mungu; kwa hivyo, wako kwa hali ya kinyume cha furaha.

12 Na sasa tazama, je, maana ya neno kurudisha ni kuchukua kitu cha hali ya asili na kukiweka kwenye hali isiyo asili, au kukiweka katika hali kinyume cha asili yake?

13 Ee, mwana wangu, hili silo jambo; lakini maana ya neno kurudisha ni kurejesha tena uovu kwa uovu, au mwili kwa mwili, au uibilisi kwa uibilisi—uzuri kwa lile ambalo ni zuri; haki kwa kile ambacho ni haki; adilifu kwa kile ambacho ni adilifu; rehema kwa lile ambalo lina rehema.

14 Kwa hivyo, mwana wangu, ona kwamba unawarehemu ndugu zako; tenda yaliyo amazuri, toa bhukumu kwa haki, na cufanye mema kila mara; na ikiwa utafanya vitu hivi vyote ndipo utakapopokea zawadi yako; ndiyo, utapata drehema irudishwe kwako tena; utapata haki kurudishwa kwako tena; utapata hukumu ya haki kurudishwa kwako tena; na utapata zawadi nzuri kutolewa kwako tena.

15 Kwani yale ambayo unayoyapeleka nje yatarudi kwako tena, na kurudishwa kwenye asili yake tena; kwa hivyo, neno kurudisha humhukumu mwenye dhambi, na haimthibitishi hata kidogo.