Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 110


Sehemu ya 110

Maono yaliyoonyeshwa kwa Joseph Smith Nabii na Oliver Cowdery katika hekalu huko Kirtland, Ohio, 3 Aprili 1836. Wakati ulikuwa ni ule wa mkutano wa siku ya Sabato. Historia ya Joseph Smith inaeleza: “Wakati wa alasiri, niliwasaidia Marais wengine katika kugawa Chakula cha Bwana kwa Kanisa, baada ya kupokea kutoka kwa Mitume Kumi na Wawili, ambao ilikuwa zamu yao kuongoza kwenye meza takatifu kwa siku hii. Baada ya kufanya huduma hii kwa ndugu zangu, nilirejea kwenye mimbari, pazia likiwa limeshushwa, na nikapiga magoti, pamoja na Oliver Cowdery, kwa sala ya unyenyekevu na kimya kimya. Baada ya kumaliza kusali, ono lifuatalo lilifunguliwa kwetu sote wawili.”

1–10, Bwana Yehova atokea katika utukufu na kulikubali Hekalu la Kirtland kama nyumba Yake; 11–12, Musa na Elia kila mmoja anatokea na kukabidhi funguo za nyakati zao; 13–16, Eliya anarudi na kukabidhi funguo za kipindi chake kama ilivyoahidiwa na Malaki.

1 aPazia liliondolewa kutoka akilini mwetu, na bmacho yetu ya ufahamu yakafunguliwa.

2 Tulimwona Bwana akiwa amesimama kwenye jukwaa la mimbari, mbele yetu; na chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa dhahabu safi, katika rangi kama ya kaharabu.

3 aMacho yake yalikuwa kama mwale wa moto; nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama theluji safi; buso wake ulingʼara kupita mngʼaro wa jua; na csauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi yakimbiayo, hata sauti ya dYehova, akisema:

4 Mimi ni akwanza na mwisho; Mimi ni yeye aliye bhai, Mimi ni yule aliyeuawa; Mimi ni cmtetezi wenu kwa Baba.

5 Tazama, dhambi zenu azimesamehewa; nanyi ni wasafi mbele zangu; kwa hiyo, inueni vichwa vyenu na kufurahi.

6 Na acha mioyo ya ndugu zenu na ifurahi, na acha mioyo ya watu wangu wote ifurahi, ambao, kwa nguvu zao, awameijenga nyumba hii kwa ajili ya jina langu.

7 Kwani tazama, animeikubali bnyumba hii, na jina langu litakuwa humu; nami nitajionyesha kwa watu wangu kwa rehema katika nyumba hii.

8 Ndiyo, anitajitokeza kwa watumishi wangu, na kusema nao kwa sauti yangu mwenyewe, kama watu wangu watashika amri zangu, na ikiwa bhawataichafua cnyumba hii takatifu.

9 Ndiyo mioyo ya maelfu na makumi ya elfu itafurahia kwa furaha kuu kwa matokeo ya abaraka zitakazomwagwa, na kwa bendaomenti ambayo watumishi wangu wamepewa katika nyumba hii.

10 Na umaarufu wa nyumba hii utaenea hadi nchi za kigeni; na huu ni mwanzo wa baraka ambazo azitamwagwa juu ya vichwa vya watu wangu. Hivyo ndivyo. Amina.

11 Baada ya aono hili kufungwa, mbingu zilitufungukia tena; na bMusa akatokea mbele yetu, na kutukabidhi cfunguo za dkukusanyika kwa Israeli kutoka pande nne za dunia, na kuongozwa kwa makabila kumi kutoka nchi ya ekaskazini.

12 Baada ya hili, aElia alitokea, na kutukabidhi bkipindi cha cinjili ya Ibrahimu, akisema kwamba kupitia sisi na uzao wetu vizazi vyote baada yetu sisi vitabarikiwa.

13 Baada ya ono hili kufungwa, ono jingine kubwa na tukufu likatukia juu yetu; kwani aEliya nabii, baliyechukuliwa mbinguni bila ya kuonja mauti, alisimama mbele yetu, na kusema:

14 Tazama, wakati umetimia kikamilifu, ambao ulinenwa kwa kinywa cha Malaki—ukishuhudia kwamba yeye [Eliya] lazima atatumwa, kabla ya kuja kwa siku ile iliyo kuu na ya Bwana—

15 aKuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na ya watoto iwaelekee mababu, dunia yote isije ikapigwa kwa laana—

16 Kwa hiyo, funguo za kipindi hiki zimekabidhiwa mikononi mwenu; na kwa hili ninyi mpate kujua kwamba asiku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana i karibu, hata milangoni.