Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 131


Sehemu ya 131

Mafundisho ya Joseph Smith Nabii, yaliyotolewa huko Ramus, Illinois, 16 na 17 Mei 1843.

1–4, Ndoa ya selestia ni muhimu kwa kuinuliwa katika mbingu ya juu; 5–6, Jinsi watu wanavyotiwa muhuri kwa uzima wa milele inaelezwa; 7–8, Roho zote ni maada.

1 Katika utukufu wa aselestia kuna mbingu au daraja tatu;

2 Na ili kupata la ajuu zaidi, mwanadamu lazima aingie katika utaratibu huu wa ukuhani [ikimaanisha bagano jipya na lisilo na mwisho la ndoa];

3 Na kama hakufanya hivyo, hawezi kulipata.

4 Anaweza kuingia katika nyingine, lakini huo ndiyo mwisho wa ufalme wake; hawezi akuongezeka.

5 (17 Mei 1843.) Neno la aunabii lililo imara zaidi linamaanisha kujua kwamba mtu bametiwa muhuri kwa cuzima wa milele, kwa njia ya ufunuo na roho wa unabii, kwa kupitia uwezo wa Ukuhani Mtakatifu.

6 Haiwezakani kwa mwanadamu akuokolewa katika bujinga.

7 Hakuna kitu kisichoundwa na maada. aRoho yote ni maada, lakini ni angavu zaidi au safi, na yaweza kutambuliwa tu kwa macho yaliyo bsafi zaidi;

8 Hatuwezi kuiona; lakini wakati miili yetu itakaposafishwa tutaona kwamba yote ni maada.