Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 69


Sehemu ya 69

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii huko Hiram, Ohio, 11 Novemba 1831. Ukusanyaji wa mafunuo ulio kusudiwa kwa uchapishaji wa awali ulikuwa umekwisha pitishwa kwenye mkutano maalum wa 1–2 Novemba. Ilipofika 3 Novemba ufunuo uliopo hapa ndani unaoonekana kama sehemu ya 133, baadae ukaitwa Kiambatisho, uliongezwa. Oliver Cowdery mwanzoni alikuwa ameteuliwa kubeba miswada ya amri na mafunuo yaliyo kusanywa kwenda Independence, Missouri, kwa ajili ya kupiga chapa. Pia alikuwa achukue fedha zilizokuwa zimechangwa kwa ajili ya kulijenga Kanisa huko Missouri. Ufunuo huu unamwelekeza John Whitmer kuongozana na Oliver Cowdery na pia unamwelekeza Whitmer kusafiri na kukusanya taarifa za kihistoria katika wito wake kama mwanahistoria wa Kanisa na mtunza kumbukumbu.

1–2, John Whitmer atafuatana na Oliver Cowdery kwenda Missouri; 3–8, Yeye pia atahubiri na kukusanya, atanakili kumbukumbu, na kuandika habari za kihistoria.

1 Nisikilizeni, asema Bwana Mungu wenu, kwa ajili ya mtumishi wangu aOliver Cowdery. Siyo hekima kwangu kwamba lazima akabidhiwe amri na fedha ambazo atazibeba kwenda nchi ya Sayuni, isipokuwa mtu mmoja aende pamoja naye mtu ambaye atakuwa mkweli na mwaminifu.

2 Kwa hiyo, Mimi, Bwana, ninapenda kuwa mtumishi wangu, aJohn Whitmer, aende pamoja na mtumishi wangu Oliver Cowdery;

3 Na pia kwamba naye ataendelea katika kuandika na kutengeneza ahistoria ya mambo yote muhimu ambayo atayaona na kuyafahamu yahusuyo kanisa langu;

4 Na pia kwamba atapokea aushauri na msaada kutoka kwa mtumishi wangu Oliver Cowdery na wengineo.

5 Na pia, watumishi wangu walio nchi za ngʼambo yawapasa kutuma taarifa za ausimamizi wao katika nchi ya Sayuni;

6 Kwani nchi ya Sayuni itakuwa makao na mahali pa kupokea na kufanya mambo haya yote.

7 Hata hivyo, mtumishi wangu John Whitmer atasafiri mara nyingi kutoka mahali hadi mahali, na kutoka kanisa hadi kanisa, ili aweze kupata maarifa kwa urahisi—

8 Akihubiri na kuelezea, akiandika, kunakili, kuchagua, na kupata mambo yote yatakayokuwa kwa faida ya kanisa, na kwa vizazi vinavyo chipukia vitakavyokua katika nchi ya aSayuni, kuimiliki kutoka kizazi hata kizazi, milele na milele. Amina.