Misaada ya Kujifunza
Utangulizi


Uteuzi kutoka Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia

Zifuatazo ni sehemu zilizo chaguliwa za Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia ya Toleo la King James (TJS). Bwana alimwongoza Nabii Joseph Smith kuurejesha ukweli kwenye maandiko ya Biblia ya King James ambayo yalipotea au kubadilishwa tangu pale maneno ya kwanza yalipoandikwa. Ukweli huu uliorejeshwa ulifafanua mafundisho na kuboresha uelewa wa maandiko.

Kwa sababu Bwana alimfunulia Joseph kweli fulani ambazo mwandishi wa kwanza aliziandika, Tafsiri ya Joseph Smith ni tofauti na tafsiri ya Biblia nyingine yoyote ulimwenguni. Kwa maana hiyo, neno tafsiri linatumika katika mapana na katika njia tofauti kuliko kawaida, kwa maana tafsiri ya Joseph ilikuwa ni ufunuo zaidi ya tafsiri ya kawaida kutoka lugha nyingine.

Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia ya Mfalme James ina mahusiano pamoja au ni imetamkwa katika sehemu za Mafundisho na Maagano (ona sehemu za 37, 45, 73, 76, 77, 86, 91, na 132). Pia, kitabu cha Musa na Joseph Smith—Mathayo ni dondoo kutoka kwa Tafsiri ya Joseph Smith.

Kwa maelezo zaidi juu ya Tafsiri ya Joseph Smith, ona “Tafsiri ya Joseph Smith (TJS)” katika Mwongozo wa Maandiko.

Kielelezo kifuatacho kinaonesha mifano ya uteuzi kutoka Tafsiri ya Joseph Smith:

Picha
Sampuli

TJS, Mathayo 4:1, 5–6, 8–9. Linganisha na Mathayo 4:1, 5–6, 8–9; mabadiliko ya aina hiyo hiyo yamefanywa katika Luka 4:2, 5–11

Yesu anangozwa na Roho Mtakatifu, siyo na Shetani.

1 Kisha Yesu akaongozwa na Roho, kwenda nyikani, ili kuwa pamoja na Mungu.

5 Kisha Yesu akachukuliwa hadi mji mtakatifu, na Roho akamkalisha juu ya kinara cha hekalu.

6 Kisha ibilisi akamjia na kusema, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini, kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake, na mikononi mwao watakuchukua, usije wakati wowote ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

8 Na tena, Yesu alikuwa katika Roho, naye akamchukua mpaka mlima mrefu mno, na akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wake.

9 Naye ibilisi akamjia tena, na kusema, Haya yote nitakupa, ukianguka na kunisujudia.

Maelezo haya yaliyo katika herufi nzito ni fungu la maneno katika tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia ya King James. Kwa sababu tafsiri yake imeyarejesha maneno kwenye maandishi ya Biblia, namba za mistari zinaweza kuwa tofauti na toleo unalotumia.

Marejeo mtambuko huonyesha kifungu katika Biblia yako ambacho unapaswa kukilinganisha na tafsiri ya Joseph Smith.

Maelezo haya yanaelezea ni mafundisho gani Joseph Smith alifafanua kwa tafsiri yake.

Haya ni maandiko kama yalivyotafsiriwa na Joseph Smith. (Italiki zimeongezawa kuonesha tofauti kutoka tafsiri za simulizi za Mfalme James.)