Maandiko Matakatifu
Makala ya Imani 1


Makala ya Imani
ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Mlango wa 1

1 aTunaamini katika bMungu, Baba wa Milele, na katika cMwanawe, Yesu Kristo, na katika dRoho Mtakatifu.

2 Tunaamini kwamba wanadamu wataadhibiwa kwa ajili ya adhambi zao wenyewe, na siyo kwa ajili ya buvunjaji sheria wa Adamu.

3 Tunaamini kwamba kwa njia ya aUpatanisho wa Kristo, wanadamu wote wanaweza bkuokolewa, kwa ckutii dsheria na ibada za eInjili.

4 Tunaamini kwamba kanuni na aibada za kwanza za Injili ni: bkwanza, Imani katika Bwana Yesu Kristo; pili, cToba; tatu, dUbatizo kwa kuzamishwa kwa ajili ya eondoleo la dhambi; nne, Kuwekewa fmikono kwa ajili ya gkipawa cha Roho Mtakatifu.

5 Tunaamini kwamba mwanadamu ni lazima aaitwe na Mungu, kwa bunabii, na kwa kuwekewa cmikono na wale walio katika dmamlaka, ili ekuhubiri Injili na kuhudumu katika fibada zake.

6 Tunaamini katika amuundo ule ule ambao ulikuwepo katika Kanisa la Asili, yaani, bmitume, cmanabii, dwachungaji, walimu, ewainjilisti, na kadhalika.

7 Tunaamini katika avipawa vya bndimi, cunabii, dufunuo, emaono, fuponyaji, gfasiri za ndimi, na kadhalika.

8 Tunaamini aBiblia kuwa ni bneno la Mungu ilimradi imetafsiriwa kwa cusahihi; pia tunaamini dKitabu cha Mormoni kuwa ni neno la Mungu.

9 Tunaamini yale yote Mungu aaliyoyafunua, na ambayo sasa anayafunua, na tunaamini kwamba bado Yeye batayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu.

10 Tunaamini katika akukusanyika kiuhalisi kwa Israeli na katika urejesho wa bMakabila Kumi; kwamba cSayuni (Yerusalemu Mpya) itajengwa katika ya bara la Marekani; kwamba Kristo datatawala yeye mwenyewe juu ya dunia; na, kwamba dunia itafanywa eupya na kupokea futukufu wake wa gkipepo.

11 Tunadai ahaki ya kumwabudu Mungu Mwenyezi kulingana na bmwongozo wa cdhamiri zetu sisi wenyewe, na tunawaruhusu watu wote haki hiyo, na dwaabudu namna, mahali, au chochote watakacho.

12 Tunaamini katika kuwa chini ya wafalme, marais, watawala, na waamuzi, katika kutii, kuheshimu, na kuzishika asheria.

13 Tunaamini katika kuwa awaaminifu, wakweli, bwasafi, wakarimu, wema, na katika ckufanya mema kwa watu wote; naam, twaweza kusema kwamba tumefuata dmaonyo ya Paulo—Tunaamini mambo yote, etunatumaini mambo yote, tumestahimili mambo mengi, na tunatumaini kuwa tutaweza fkustahimili mambo yote. Kama kuna kitu chochote kilicho gchema, chenye kupendeza, au chenye taarifa njema au chenye kustahili sifa, tunayatafuta mambo haya.

Joseph Smith.