Maandiko Matakatifu
Musa 6


Mlango wa 6

(Novemba–Desemba 1830)

Uzao wa Adamu watunza kitabu cha ukumbusho—Uzao wake wenye haki wahubiri toba—Mungu Anajionyesha mwenyewe kwa Henoko—Henoko anahubiri injili—Mpango wa wokovu ulifunuliwa kwa Adamu—Alipokea ubatizo na ukuhani.

1 Na aAdamu alisikiliza sauti ya Bwana Mungu, naye akawasihi wanawe kutubu.

2 Naye Adamu akamjua mke wake tena, naye akamzaa mwana, na akamwita jina lake aSethi. Na Adamu akalitukuza jina la Mungu; kwa maana yeye alisema: Mungu ameniwekea uzao mwingine, mahali pa Habili, ambaye Kaini alimwua.

3 Na Mungu akajidhihirisha mwenyewe kwa Sethi, naye hakuasi, bali akamtolea adhabihu ya kukubalika, kama ile ya ndugu yake Habili. Na kwake pia alizaliwa mwana wa kiume, naye akamwita jina lake Enoshi.

4 Na halafu watu hawa wakaanza akulilingana jina la Bwana, na Bwana akawabariki;

5 Na akitabu cha ukumbusho kikaandikwa, ambamo ndani yake kuliandikwa, katika lugha ya Adamu, kwa maana ilitolewa kwa wengi kwa kadiri walivyomlingana Mungu kuandika kwa roho wa bmwongozo;

6 Na kupitia wao watoto wao walifundishwa kusoma na kuandika, wakiwa na lugha iliyokuwa safi na isiyochafuliwa.

7 Sasa aUkuhani huu huu, ambao ulikuwepo mwanzoni, utakuwepo mwisho wa ulimwengu pia.

8 Sasa unabii huu Adamu aliusema, kama alivyoongozwa na aRoho Mtakatifu, na historia ya bnasaba ya cwatoto wa Mungu iliandikwa. Na hiki kilikuwa dkitabu cha vizazi vya Adamu, kikisema: Katika siku ile ambayo Mungu alipoumba mtu, kwa mfano wa Mungu alimuumba;

9 Katika amfano wa mwili wake yeye mwenyewe, baliwaumba mwanaume na mwanamke, na akawabariki, na kuwaita majina yao cAdamu, katika siku ile waliyoumbwa na kuwa dnafsi hai katika nchi iliyo emahali pa Mungu pa kuwekea miguu.

10 Na aAdamu aliishi miaka mia moja na thelathini, na akamzaa mwana kwa sura yake, kwa bmfano wake, akamwita jina lake Sethi.

11 Na siku za Adamu, baada ya kumzaa Sethi, zilikuwa miaka mia nane, na akazaa wana na mabinti wengi;

12 Na siku zote za Adamu alizoishi zilikuwa miaka mia tisa na thelathini, naye akafa.

13 Sethi akaishi miaka mia na mitano, naye akamzaa Enoshi, naye akatoa unabii katika siku zake zote, na kumfundisha mwanawe Enoshi njia za Mungu; kwa sababu hiyo Enoshi pia naye alitoa unabii.

14 Na Sethi aliishi, baada ya kumzaa Enoshi, miaka mia nane na saba, naye akazaa wana na mabinti wengi.

15 Na wanadamu wakawa wengi juu ya uso wa nchi. Na katika siku hizo Shetani alikuwa na autawala mkubwa miongoni mwa watu, na alighadhibika mioyoni mwao; na kutoka hapo vikazuka vita na umwagaji wa damu; na mkono wa mtu ukawa dhidi ya ndugu yake mwenyewe, katika kumletea mauti, kwa sababu ya matendo ya bsiri, wakitafuta mamlaka.

16 Siku zote za Sethi zilikuwa miaka mia tisa kumi na miwili, naye akafa.

17 Na Enoshi aliishi miaka tisini, na akamzaa aKanaani. Na Enoshi na mabaki ya watu wa Mungu wakatoka katika nchi hiyo, iliyoitwa Shuloni, nao wakaishi katika nchi ya ahadi, ambayo aliiita kwa jina la mwanawe mwenyewe, ambaye alimwita Kanaani.

18 Na Enoshi aliishi, baada ya kumzaa Kanaani, miaka mia nane na kumi na mitano, na akazaa wana na mabinti wengi. Na siku zote za Enoshi zilikuwa miaka mia tisa na mitano, naye akafa.

19 Naye Kanaani aliishi miaka sabini, na akamzaa Mahalaleli; na Kanaani aliishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, na akazaa wana na mabinti. Na siku zote za Kanaani zilikuwa miaka mia tisa na kumi, naye akafa.

20 Na Mahalaleli aliishi miaka sitini na mitano, naye akamzaa Yaredi; na Mahalaleli aliishi, baada ya kumzaa Yaredi, miaka mia nane na thelathini, na akazaa wana na mabinti. Na siku zote za Mahalaleli zilikuwa mia nane na tisini na tano, naye akafa.

21 Na Yaredi aliishi miaka mia na sitini na miwili, naye akamzaa aHenoko; na Yaredi aliishi, baada ya kumzaa Henoko, miaka mia nane, na akazaa wana na mabinti. Na Yaredi alimfundisha Henoko katika njia zote za Mungu.

22 Na hii ni nasaba ya wana wa Adamu, aliyekuwa amwana wa Mungu, ambaye Mungu, mwenyewe, alizungumza naye.

23 Nao walikuwa awahubiri wa haki, na walinena na kutoa bunabii, na wakiwaitia watu wote, kila mahali, ckutubu; na dimani ilifundishwa kwa wanadamu.

24 Na ikawa kwamba siku zote za Yaredi zilikuwa mia tisa na sitini na miwili, naye akafa.

25 Na Henoko aliishi miaka sitini na mitano, na akamzaa aMethusela.

26 Na ikawa kwamba Henoko alisafiri katika nchi, miongoni mwa watu; na alipokuwa akisafiri, Roho wa Mungu akamshukia kutoka mbinguni, na kukaa juu yake.

27 Naye akasikia sauti kutoka mbinguni, ikisema: Henoko, mwanangu, toa unabii kwa watu hawa, na uwaambie—Tubuni, na hivyo ndivyo asemavyo Bwana: aNimekasirishwa na watu hawa, na hasira yangu kali inawaka dhidi yao; kwa kuwa mioyo yao imekuwa migumu, na bmasikio yao hayasikii vyema, na macho yao chayawezi kuona mbali;

28 Na kwa vizazi hivi vingi, hata tangu siku ile ambayo niliwaumba, awamepotoka, nao wamenikana Mimi, nao wamefuata ushauri wao wa gizani; na katika machukizo yao wenyewe wamebuni mauaji, na hawakuzishika amri, ambazo nilimpa baba yao, Adamu.

29 Kwa sababu hiyo, wamejiapia wenyewe, na kwa aviapo vyao, wamejiletea mauti juu yao wenyewe; na bjehanamu nimeitengeneza kwa ajili yao, kama hawatatubu;

30 Na hili ni tangazo, ambalo nimelitangaza katika mwanzo wa ulimwengu, kutoka kinywani mwangu mwenyewe, kutoka kuwekwa msingi wake, na kwa vinywa vya watumishi wangu, baba zenu, nimelitangaza hilo, hata kama litakavyopelekwa ulimwenguni, hadi miisho yake.

31 Na Henoko alipoyasikia maneno haya, akapiga magoti chini ya nchi, mbele za Bwana, na kunena mbele za Bwana, akisema: Kwa nini nimepata upendeleo mbele za uso wako, nami ni kijana mdogo, na watu wote wanichukia; kwa maana mimi asi mwepesi wa kusema; kwani mimi ni mtumishi wako?

32 Naye Bwana akamwambia Henoko: Enenda zako na ukafanye kama nilivyokuamuru wewe, na hakuna mtu atakayekurarua wewe. Fumbua akinywa chako, nacho kitajazwa, nami nitakupa maneno, kwa maana wenye mwili wote wako mikononi mwangu, nami nitafanya kama nionavyo kuwa vyema.

33 Uwaambie watu hawa: aChagueni leo hii, kumtumikia Bwana Mungu aliyewaumba ninyi.

34 Tazama Roho yangu i juu yako, kwa sababu hiyo maneno yako yote nitayahesabia kuwa haki; na amilima itakukimbia mbele yako, na bmito itageuka kutoka uelekeo wake; nawe utakaa ndani yangu, nami ndani yako; kwa hiyo ctembea pamoja nami.

35 Naye Bwana akamwambia Henoko, akisema: Jipake udongo macho yako, na uyaoshe, nawe utaona. Naye alifanya hivyo.

36 Naye akaona aroho zile ambazo Mungu aliziumba; na akaona pia vitu ambavyo havikuonekana kwa macho ya basili; na kutoka hapo ukaja usemi nao ukaenea katika nchi: Bwana amemwinua cmwonaji kwa watu wake.

37 Na ikawa kwamba Henoko akaenda katika nchi, miongoni mwa watu, akisimama juu ya vilima na mahali palipoinuka, na akalia kwa sauti kubwa, akiwashuhudia dhidi ya matendo yao; na watu wote awakaudhika kwa sababu yake.

38 Nao wakaja kumsikiliza, juu ya mahali palipoinuka, wakiwaambia walinda mahema: Kaeni hapa na myalinde mahema, wakati sisi tukienda huko kumwona mwonaji, kwani yeye hutoa unabii, na kuna jambo geni katika nchi; mtu wa mwituni amekuja miongoni mwetu.

39 Na ikawa wakati walipomsikia, hakuna mtu aliyeweka mkono wake juu yake; kwa maana woga uliwajia juu yao wote wale waliomsikia; kwa maana yeye alitembea pamoja na Mungu.

40 Na hapo akamjia mtu, ambaye jina lake lilikuwa Mahija, naye akamwambia: Tuambie wazi wazi wewe ni nani, na umetoka wapi?

41 Naye akawaambia: Nimetoka nchi ya Kanaani, nchi ya baba zangu, nchi ya haki hadi siku hii ya leo. Na baba yangu alinifundisha katika njia zote za Mungu.

42 Na ikawa, wakati nikisafiri kutoka nchi ya Kanaani, kwa bahari ya mashariki, nikaona ono; na lo, nikaona mbingu, na Bwana akanena nami, na akanipa amri; kwa hiyo, kwa ajili ya amri hii, ya kushika amri, ninayanena maneno haya.

43 Naye Henoko aliendeleza hotuba yake, akisema: Bwana aliyesema nami, huyo ndiyo Mungu wa mbinguni, naye ni Mungu wangu, na Mungu wenu, nanyi ni ndugu zangu, na kwa nini amnajishauri wenyewe, na kumkana Mungu wa mbinguni?

44 Mbingu hizo alizifanya; na adunia ni bmahali pake pa kuwekea miguu; na msingi wake ni wake. Tazama, yeye aliuweka, na jeshi la watu amelileta juu ya uso wake.

45 Na mauti yamekuja juu ya baba zetu; hata hivyo tunawajua, na hatuwezi kuwakana, na wote hata wa kwanza wao wote tunamjua, hata Adamu.

46 Kwa maana kitabu cha aukumbusho tumekiandika miongoni mwetu, kulingana na utaratibu uliotolewa kwa kidole cha Mungu; nacho kinatolewa katika lugha yetu wenyewe.

47 Na wakati Henoko alipokuwa akinena maneno ya Mungu, watu wakatetemeka, na hawakuweza kusimama mbele yake.

48 Naye akawaambia: Kwa sababu Adamu aalianguka, sisi tupo; na kwa kuanguka kwake bmauti yakaja; nasi tumefanywa washiriki wa dhiki na huzuni.

49 Tazama Shetani amekuja miongoni mwa wanadamu, naye ahuwajaribu ili wamwabudu yeye; na watu wamekuwa wenye btamaa, canasa, na duibilisi, nao wamefungiwa nje ya uwepo wa Mungu.

50 Lakini Mungu alifanya ijulikane kwa baba zetu kwamba watu wote lazima watubu.

51 Naye akamwitia baba yetu Adamu kwa sauti yake yeye mwenyewe, akisema: Mimi ndimi Mungu; niliyeufanya ulimwengu, na awatu bkabla hawajawa katika mwili.

52 Naye pia akamwambia: Kama utanigeukia, na kuisikiliza sauti yangu, na kuamini, na kutubu uvunjaji sheria wako wote, na akubatizwa, hata katika maji, katika jina la Mwanangu wa Pekee, aliyejaa bneema na kweli, ambaye ndiye cYesu Kristo, djina pekee litakalotolewa chini ya mbingu, ambalo kwalo ewokovu waweza kuja kwa wanadamu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, mkiomba mambo yote katika jina lake, na lolote mtakaloliomba, mtapewa.

53 Naye baba yetu Adamu akamwambia Bwana, na akasema: Ni kwa nini watu lazima watubu na kubatizwa katika maji? Na Bwana akamwambia Adamu: Tazama mimi animekusamehe uvunjaji wako wa sheria katika Bustani ya Edeni.

54 Kuanzia hapa ukaenea msemo miongoni mwa watu, kwamba aMwana wa Mungu amefanya bupatanisho kwa ajili ya hatia ya asili, ambayo dhambi za wazazi haziwezi kujibiwa juu ya vichwa vya cwatoto, kwa maana wao ni safi tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu.

55 Na Bwana akamwambia Adamu, akisema: Kadiri watoto wako watakavyotungwa mimba katika dhambi, vivyo hivyo wakati watakapoanza kukua, adhambi hutunga katika mioyo yao, nao huonja buchungu, ili wapate kujua kutunza chema.

56 Na imetolewa kwao kujua mema na maovu; kwa sababu hiyo wao awanajiamulia wenyewe, na nimekupa sheria na amri nyingine.

57 Kwa hiyo wafundishe watoto wako, kwamba watu wote, kila mahali, lazima awatubu, au vinginevyo hawataweza kuurithi ufalme wa Mungu, kwa maana hakuna kitu kilicho bkichafu kinachoweza kukaa huko, au ckukaa mbele zake; kwani, katika lugha ya Adamu, dMtu wa Utakatifu ndilo jina lake, na jina la Mwanawe wa Pekee ni eMwana wa Mtu, hata Yesu Kristo, fMwamuzi wa haki, ambaye atakuja wakati wa meridiani.

58 Kwa hiyo ninakupeni amri, kuyafundisha mambo haya kwa uhuru kwa awatoto wenu, mkisema:

59 Kwamba kwa sababu ya uvunjaji wa sheria limekuja anguko, ambalo laleta mauti, na kadiri ninyi mlivyozaliwa katika ulimwengu kwa maji, na damu, na aroho, ambavyo nilivifanya, na hivyo kuwa bvumbi la nafsi iliyo hai, hata hivyo lazima cmzaliwe tena katika ufalme wa mbinguni, kwa dmaji, na kwa Roho, na kuoshwa kwa damu, hata damu ya Mwanangu wa Pekee; ili mpate kutakaswa kutokana na dhambi zote, na ekufurahia fmaneno ya uzima wa milele katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao, hata gutukufu katika mwili usiokufa;

60 Kwa maana kwa amaji mnazishika amri; na kwa Roho mnahesabiwa bhaki, na kwa cdamu ninyi dmnatakaswa;

61 Kwa hiyo imetolewa kukaa ndani yenu; ushuhuda wa mbinguni; yule aMfariji; mambo ya amani ya utukufu usiokufa; ukweli wa mambo yote; kile ambacho huhuisha vitu vyote, kile ambacho hufanya vitu vyote kuwa hai; kile kinachojua vitu vyote, na chenye uwezo wote kulingana na hekima, huruma, ukweli, haki, na hukumu.

62 Na sasa, tazama, ninawaambia: Huu ndiyo ampango wa wokovu kwa watu wote, kupitia damu ya bMwanangu wa Pekee, ambaye atakuja wakati wa meridiani.

63 Na tazama, vitu vyote vina mfano wake, na vitu vyote vimeumbwa na vimefanywa ili akunishuhudia Mimi, vitu vyote vilivyo vya kimwili, na vile vya kiroho; vitu vilivyoko mbinguni juu, na vitu vilivyo juu ya nchi, na vitu vilivyo ndani ya nchi, na vitu vilivyo chini ya nchi, vyote juu na chini: vitu vyote vinanishuhudia Mimi.

64 Na ikawa kwamba, Bwana aliposema na Adamu, baba yetu, kwamba Adamu alilia kwa Bwana, naye akanyakuliwa na aRoho wa Bwana, naye akachukuliwa ndani ya maji, na kulazwa chini bmajini, na kutolewa kutoka majini.

65 Na hivyo akawa amebatizwa, na Roho wa Mungu akamshukia juu yake, na hivyo akawa aamezaliwa kwa Roho, na akawa amehuishwa katika utu wa bndani.

66 Naye akasikia sauti kutoka mbinguni, ikisema: Wewe aumebatizwa kwa moto, na kwa Roho Mtakatifu. Huu ndiyo bushuhuda wa Baba, na Mwana, na kutoka sasa na hata milele;

67 Na wewe ni kwa amfano wake yeye ambaye hana mwanzo wa siku au mwisho wa miaka, kutoka milele yote hadi milele yote.

68 Tazama, wewe u ammoja ndani yangu, mwana wa Mungu; na hivyo wote wapate kuwa bwana wangu. Amina.